Tuesday, September 13, 2016

ASILIMIA 85 YA WAKAZI WA JIJI LA NAIROBI KUKOSA MAJI KWA SIKU MBILI

DC IKUNGI AITAKA KAMPUNI YA SHANTA GOLD MINE KUWALIPA FIDIA WANANCHI WALIOFANYIWA TATHIMINI ILI KUPISHA UCHIMBAJI WA DHAHABU

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa kikao cha pamoja kilichohudhuriwa na Wawakilishi wa kampuni ya Shanta Gold Mine Ltd, Wananchi wawakilishi kutoka Kijiji Cha Mlumbi na Uongozi wa kikosi kazi

Wananchi wawakilishi kutoka Kijiji Cha Mlumbi na Uongozi wa kikosi kazi wakijadili jambo nje ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya kabla ya kuingia kwenye kikao
Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd Philbert Rweyemamu akielezea namna ambavyo watawalipa wananchi 67 ndani ya wiki hii

MAJALIWA AKUTANA NA MABALOZI NA WAFANYABIASHARA KUWAOMBA WACHANGIE MAAFA KAGERA

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Wafanyabishara na Mabalozi wa Nchi Mbalimbali hapa nchini kuwaomba wachangie katika kujenga na kukarabati miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Alikutana nao Ikulu jijini Dar es salaam Septemba 13, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 100 kutoka kwa Charge d' Affairs wa ubalozi wa China nchini, Bw. Haodong Gou wakati alipokutana na wafanyabiashara na mabalozi wa nchi mbalimbali hapa nchini na kuwaomba wasaidie kuchangia ujenzi na ukarabati wa miundombinu iliyoathiriwa na tetemeko laardhi mkoani Kagera. Mkutano huo ulifanyika Ikulu jijini Dar es salaam Septemba 13, 2016.Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Suzan Kolimba. (Picha na Odisi ya Waziri Mkluu)

No comments :

Post a Comment