Mkurugenzi
wa Idara ya Rasilimali Watu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania
Ltd, Hassan Dewji akizungumza wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana
waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni
ya MeTL Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
katika ukumbi wa Alliance Francaise.(Habari picha na Modewjiblog).
Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akizungumzia
idara yake ya masoko inavyofanya kazi wakati wa Kongamano la Ajira kwa
Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika
makampuni ya MeTL Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.
Mtaalamu
wa kilimo wa kampuni ya MeTL Group, Bw. George Mwamakula akizungumza
wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata
fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group, lililofanyika
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance
Francaise.
Mtaalamu
wa masuala ya fedha wa MeTL Group, Bi. Hasina Ahmed akizungumza wakati
wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa
ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group, lililofanyika jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.
Mtaalamu
wa idara ya uzalishaji wa nyuzi na nguo ya MeTL Group, Bw. Clement
Munisi akizungumza wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza
vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL
Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika
ukumbi wa Alliance Francaise.
Mtaalamu
kutoka kitengo cha mauzo wa MeTL Group, Bw. Yusuf Ali, akizungumza
kwenye Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata
fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group, lililofanyika
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance
Francaise.
Mtaalamu
wa idara ya uzalishaji na matengenezo wa MeTL Group, Bw. Vijay Raghavan
akizungumza kwenye Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao
watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group,
lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa
Alliance Francaise.
Washiriki
wakiuliza maswali juu uendeshaji wa vitengo mbalimbali vya makampuni ya
MeTL Group wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo
ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group,
lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa
Alliance Francaise.
Mkurugenzi
wa Idara ya Rasilimali Watu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania
Ltd, Hassan Dewji akijibu maswali yaliyoulizwa na washiriki wa
kongamano hilo.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer (katikati)
akikabidhi box la zawadi kwa mmoja wa washiriki aliyejishindia kwenye
mchezo wa kuokota majina wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana
waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni
ya MeTL Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
katika ukumbi wa Alliance Francaise. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya
Rasilimali Watu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd, Hassan
Dewji.
Na Mwandishi Wetu
Safari
ya Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) kutoa
ajira kwa Watanzania 100,000 hadi mwaka 2021 imeanza kufanyika kupitia
Job Affairs ambapo limewapa nafasi wasomi mbalimbali nchini kutumia
sehemu hiyo kuonyesha uwezo wao, na kati yao wasomi 25 wakipata nafasi
ya kujiunga na familia ya zaidi ya wafanyakazi 28,000 wa kampuni ya MeTL
Group.
Wakizungumza
na waandishi wa habari baada ya kufanyika kwa kongamano hilo, wasomi
mbalimbali waliipongeza kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited
kwa kufanya kongamano la Job Affairs kwani licha ya kutoa nafasi za
kazi lakini pia limewasaidia kujijengea uwezo mpya ambao hawakuwa nao
awali.
Mmoja
wa wasomi hao, Dennis Mtani alisema kupata nafasi ya kuhudhuria
kumewajengea jambo lipya kuhusu jinsi ya kuomba nafasi za kazi hadi kuwa
wafanyakazi bora katika kampuni.
Alisema
kutokana na ukubwa wa kampuni ya Mohammed Enterprises kwa bara la
Afrika ni matarajio yao kuwa wamejifunza jambo ambalo hata kama
hawatapata nafasi za kazi basi watabaki na uwezo ambao utawasaidia kujua
jinsi ya kuomba nafasi katika makampuni mengine ya kimataifa.
“Tumekuja
katika kongamano hili wengine hata CV walikuwa hawajui jinsi ya
kuandika ili kuomba nafasi na kuajiriwana na kutokana na ukubwa wa hii
kampuni kwa nchi za Afrika tumepata elimu ambayo inaweza kutusaidia
kwenda kufanya kazi kwa makampuni mengine,” alisema Mtani.
Nae
Monica Mziray alisema alijumuika katika kongamano hilo ili kujaribu
kutafuta nafasi ya kujiunga na kampuni ya Mohammed Enterprises kwani
anaamini ni kampuni kubwa ambayo anaamini ana ndoto za kuifanyia kazi na
ambayo inawajali wafanyakazi wake.
“Nimefanya
kazi na kampuni zingine lakini niliacha sababu nataka kampuni ambayo
inanilia vizuri na inanipa kitu na mimi naipa kitu, nilisoma historia ya
Mohammed Enterprises, nimeona ni kampuni kubwa Afrika, nimeona bidhaa
zake na naona inaweza niongezea kitu,” alisem Mziray.
Aidha
akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Mkurugenzi wa Kitengo
cha Rasilimali wa Mohammed Enterprises, Hassan Dewji aliwambia
washiriki ambao wametoka katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu,
kwamba Idara ya Rasilimali Watu ya MeTL imekua ikitoa ajira, mafunzo ya
kukuza vipaji kwa watanzania wa kada mbalimbali ili kuchukua nafasi za
juu katika Makampuni shiriki ya MeTL.
Kuhusu
kongamano hilo la kazi alisema linalengo la kupata wasomi wenye taaluma
mbalimbali kutoka kwa vijana wa Kitanzania. Kwamba Idara ya Rasilimali
Watu imelenga kupata wahitimu katika nyanja za Uhasibu wa fedha,
Rasilimali watu, Masoko, Uhandisi, Kilimo na Viwanda vya nguo lakini pia
vijana wasomi watapewa mafunzo kwa kipindi cha wiki 52 huku wakiwa
wanalipwa na watakapomaliza mafunzo watapewa ajira na kuingizwa katika
mfumo wa uwajibikaji.
“Kundi
la Makampuni ya MeTL limepata umadhubuti wake kutokana na kuwa na
utamaduni wa kuhakikisha kwamba wanakuwa karibu na wafanyakazi wake na
kuwajali. Wafanyakazi wa Idara ya Rasimali Watu wamekua wakiandaa
mafunzo kuboresha elimu ya wafanyakazi, maarifa na utaalamu,
“Ushiriki
wa wafanyakazi ni sehemu ya maono ya wafanyakazi wa Idara ya Rasilimali
Watu katika kundi hili la makampuni. Kampuni hii huhakikisha kwamba
wafanyakazi wanapata mapumziko, kujitengeneza upya, wanakuwa na siku ya
familia, siku ya michezo na kwamba shughuli hizo zinafanywa kwa
mpangilio ili kuwezesha kuwepo kwa utamaduni wa familia moja
inayofanya kazi kwa kushirikiana kwa kiwango cha juu,” alisema Dewji.
Mfanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA), akizibua mtaro wakati wa zoezi la kuzibua mifumo ya maji taka mjini humo |
Tope zilizokuwa zimetuama katika mifereji ya kusafirisha maji taka katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi zikiondolewa.
Licha
ya kuwepo na kampuni iliyopewa kandarasi ya usafi katika kituo kikuu
cha mabasi cha mjini Moshi bado changamoto ya kuziba kwa mifereji ya
kusafirisha maji taka imekuwepo .
Wafanyakazi
wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA)
walishiriki kuzibua na kuondosha taka zote zilizokuwepo katika mifereji
hiyo.
Kitengo
cha maji taka cha Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini
Moshi kilihusika zaidi kuhakikisha hakuna mfereji utakao kuwa umebaki na
taka.
Baadhi ya wafanyabiashara katika kituo hicho kikuu cha mabasi walijitokeza pia katika kusaidia kufanya usafi .
Wafanyakazi
wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kukailisha zoezi la usafi katika
kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.
WATENDAJI WASHAURIWA KUANDAA MIRADI YA KUFIKIA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO
Mkufunzi
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Dar Salaam, dkt. Kenneth Mdadila
akiendesha mafunzo ya Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji
katika Sekta ya Umma.
Washiriki
wakifuatilia wakimsikiliza mkufunzi (hayupo pichani) moja ya mada
katika mafunzo ya Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji
katika Sekta ya Umma.
Naibu
Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango, Mhandisi Happiness Mgalula
akitoa hotuba wakati akifungua mafunzo ya Usimamizi na Utayarishaji wa
Miradi ya Uwekezaji katika Sekta ya Umma mjini Dodoma, Kulia ni mkufunzi
wa mafunzo hayo, dkt. John Mduma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na
kushoto ni Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla kutoka
Tume ya Mipango dkt. Lorah Madete.
No comments :
Post a Comment