Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa, (kushoto),
akisikiliza maswali kutoka kwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mh.
Freeman Mbowe, wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, kwenye kikao cha 3 cha Mkutano wa 4 wa Bunge la 11 mjini
Dodoma, Septemba 8, 2016. (PICHA NA HASSAN SILAYO WA MAELEZO)
Waziri MkuuMajaliwa akijibu sehemu ya maswali aliyoulizwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akisalimiana na Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzania
Bungeni na Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe (MB) kwenye kikao cha 3 cha Mkutano wa 4 wa Bunge la 11 mjini
Dodoma, Septemba 8, 2016 ambapo Waziri Mkuu
alikuwa akijibu maswali ya papo kwa hapo.
Waziri Mkuu, akishukuru wakati
alipopongezwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Micehzo, Nape
Nnauye, marabaada ya kujibu kwa usahihi maswali hayo
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye
Ulemavu), Dkt. Abdallah Possi, akijibu swali bungeni ambapo alisema kuwa serikali ipo tayari kushirikiana
na raia katika kuhakikisha inakabiliana na biashara haramu ya Madawa ya Kulevya.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Suzan Kolimba akijibu swali
bungeni ambapo alisema serikali ipo katika mazungumzo na serikali ya China kwa
ajili ya kuboresha zao la Tumbaku.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni akijibu swali bungeni ambapo alisema Wizara imetenga
Shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kuboresha hali ya Magereza nchini.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongea na wabunge na kuviasa vyama vya siasa vyenye
tabia ya kufukuza wabunge kuacha hivyo kwani haviwatendei haki wapiga kura na
ni gharama kwa serikali
No comments :
Post a Comment