Thursday, September 8, 2016

MAKAO MAKUU YA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA KANDA YA KUSINI, LAZINDULIWA MKOANI MTWARA


Jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara ambalo limezinduliwa leo hii Septemba 8, 2016 na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Kamishna wa Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda mara baada ya kuwasili kwenye halfa fupi ya uzinduzi wa jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa halfa fupi ya uzinduzi wa jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara
  Kamishna wa Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Umma Jaji Mstaafu Salome Kagandaakihutubia kwenye hafla hiyo
 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ofisi ya Rais Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki akihutubia kwenye hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara 

                                  

 Watoto wanafunzi wa Darasa la kwanza kutoka Shule ya msingi ya Zinga wakiwa wanaweza kusoma vitabu wakiwa na miezi sita tuu ya darasani kupitia Programu ya Room to read
 Watoto wa Darasa la kwanza Shule ya Msingi ya Zinga iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani wakiwa wanajifunza matamshi ambapo mpaka sasa wanaelewa vizuri na hizi ni juhudi kubwa zinazofanywa na Shirika la Room to Read.Watoto wa Darasa la kwanza Shule ya Msingi ya Zinga iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani wakiwa wanajifunza matamshi ambapo mpaka sasa wanaelewa vizuri na hizi ni juhudi kubwa zinazofanywa na Shirika la Room to Read.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Zinga Msafiri Tolla akielezea namna walivyoweza kunufaika na Programu ya Room to Read ambapo amelishukuru shirika hilo na ameeleza mafanikio waliyo yapata kutokana na kujengewa Maktaba na Darasa ikiwa ni pamoja na kuwa imesaidia kupunguza upungufu wa Madarasa, katika Maktaba imeweza kusaidia kiwango cha usomaji kwa wanafunzi na kufanya wanafunzi wengi kupenda kusoma shuleni hapo, na imewawezesha hata wanajamii wanayo izunguka shule kuwa na utaratibu wa kujisomea katika Maktaba hiyo, mwisho alisema kuwa kwa sasa wanafunzi wanaweza kujisomea wenyewe bila matatizo
Afisa Elimu Taaluma Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Bi. Ester Lumato akielezea umuhimu wa Shirika la Room to Read ambapo katika shule ya Msingi Zinga walianza kufanya nao kazi kuanzia mwaka 2015,alisema miaka ya nyuma iliyopita taaruma ilikuwa chini lakini baada ya kuanza kufanya kazi na Room to Read kiwango hicho cha taaluma kimeongezeka zaidi. Ameongeza kuwa zamani mwanafunzi alikuwa anamaliza darasa la Saba hajui kusoma wala kuandika lakini kwa sasa wanamaliza wakiwa wanajua hayo yote kwa sababu ya shirika hilo kutoa Maktaba na Vitabu vya kutosha, mwisho alitoa wito kwa Mashirika mengine kujitoa kama Room to Read


Kamishna wa polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP, Simon Nyankoro Sirro
KAMISHNA wa Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam, CP, Simon Nyankoro Sirro,  anatoa rai kwa wakazi wa Jiji la Dar Es salaam na wageni wanaoingia jijini wakitokea mikoani  kupuuza  taarifa za sauti  zinazozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Polisi wanawakamata ovyo watu wanaolala kwenye nyumba za kulala wageni.

Taarifa hizo za uvumi  zinazoendelea kuzagaa  kwenye mitandao ya Kijamii kama WHATSAPP, TELEGRAM na pia zimechapishwa kwenye baadhi ya magazeti kwamba Askari Polisi wanawakamata watu  ovyo mchana wakiwa kwenye nyumba za kulala wageni  kwa madai ya kukamata kwa makosa ya uzembe na uzururaji na pia kutimiza kauli ya Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ‘HAPA NI KAZI TU’.

Kimsingi niwatoe hofu raia wema kuwa tunaendelea na oparesheni za kuwasaka watuhumiwa wa makosa mbalimbali yakiwemo wanaofanya biashara ya nyumba za kulala wageni kinyume cha sheria (guest bubu), mjambazi na wahalifu wengine wa makosa mbalimbali.

 Aidha taarifa za kuaminika zimebaini kuwa baadhi ya nyumba za kulala wageni zimekuwa zikitumika kuhifadhi magenge ya wahalifu, dada poa na kaka poa, hivyo Jeshi la Polisi tunawajibika kufuatilia na kuwakamata wahalifu.

Niwajibu wa Polisi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye nyumba za kulala wageni, Hoteli, migahawa, Vilabu vya vileo,  kumbi za starehe zinazokesha na zisizokesha na watakaobainika kuvunja sheria, hatua kali za kisheria dhidi yao zitachukuliwa. Sheria ya Mwenendo ya makosa ya jinai kifungu cha 60(1) (sura ya 77 iliyofanyiwa marekebisho 2002) kinampa nguvu askari kufanya ukaguzi wa maeneo yote yaliyotajwa hapo juu na kumkamata mtu yeyote anayetiliwa shaka akienda kinyume na utaratibu wa biashara hizo.

Sambamba na hayo nawatahadharisha wafanyabiashara wote wa nyumba za kulala wageni wafuate taratibu za kupokea wageni kwa kuandika kwenye vitabu, kuandika namba za vitambulisho vyao na sehemu wanayotoka, na pale watakapomtilia mashaka mteja yeyete watoe taarifa kituo chochote cha polisi.

Pia wenyeviti wa serikali za mitaa na wajumbe wa nyumba kumi wanawajibika kuwatambua wageni wote wanaoingia kwenye himaya zao na kuwachukulia hatua stahiki ili kuimarisha usalama katika jiji letu la  Dar Es salaam.

DAR ES SALAAM BILA UHALIFU INAWEZEKANA, TUSHIRIKIANE KUISAFISHA JIJI LETU

S.N.SIRRO - CP
 KAMISHNA WA POLISI
KANDA MAALUM

DAR ES SALAAM


Japanese Ambassador to Tanzania, H.E. Masaharu Yoshida,(partly hiden-1st-L), Major General Projest Rwegasira, (3rd–R),  Permanent Secretary, Ministry of Home Affair Mr. Michael Dunford, (2nd-R), WFP Tanzania Country Representative, pose for a photo to signify the handing over ceremony of the food for refugees at Dar es Salaamport

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKIWA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama (kushoto) akisalimiana na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (kulia) na Mbunge wa Arusha Mjini , Godbless Lema bungeni mjini Dodoma Septemba 8, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza swali kutoka kwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuuu Septemba 8, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma Septemba 8, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Bungara (kulia) na katikati ni Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 8, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, KassimMajliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina kwenye viwanja vya Bunge jini Dodoma Septemba 8, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments :

Post a Comment