Wednesday, August 24, 2016

WATOTO WALIOZALIWA WAKIWA WAMEUNGANA MWILI WAFARIKI DUNIA NCHINI SYRIA

Watoto wachanga wa mwezi mmoja walioungana mwili waliohamishwa kutoka kitongoji cha wasi kilichozingirwa na wanajeshi nchini Syria na kupelekwa Jijini Damascus wamefariki dunia.

Mapacha hao Nawras na Moaz walikuwa wameungana kifuani na mioyo yao ikiwa katika eneo moja.

Serikali ya Syria iliruhusu kuondolewa kwa mapacha hao katika eneo la waasi na kupelekwa hospitali Agosti 12, baada ya madaktari kapaza sauti zao ili kunusuru maisha yao.

No comments :

Post a Comment