Wednesday, August 24, 2016

HOTUBA YA MHE. BALOZI AUGUSTINE PHILIP MAHIGA, (MB) WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI WAKATI WA KUMKARIBISHA MHE. DKT. ALI MOHAMED SHEIN, RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI WAKATI WA UFUNGUZI WA KONGAMAMO LA TATU LA DIASPORA (3RD DIASPORA CONFERENCE) ZANZIBAR


Balozi Mahiga

Mhe. Dkt Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi; Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

Mhe. Zubeir Ali Maulid, Spika wa Baraza la Wawakilishi;

Mhe. Omar Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar;

Mhe. Issa Haji Ussi Gavu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;

Waheshimiwa Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;

Mhe. Said Hassan Said, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;

Waheshimiwa Wabunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar;

Waheshimiwa Makatibu Wakuu wa Serikali zote mbili;

Waheshimiwa Mabalozi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma na Binafsi;

Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa;

Ndugu WanaDiaspora na Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana.

ASSAALAM ALEYKUM,

Napenda kuchukua nafasi hii na kutoa shukrani za dhati kwa Mhe. Dkt Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuwa mwenyeji wetu na kukubali kuwa mgeni rasmi katika kongamano hili la Tatu la Diaspora. Uwepo wako katika Kongamano hili ni ishara kubwa ya mapenzi ya dhati uliyonayo kwa Diaspora na kutambua umuhimu wa mchango wao katika kuleta maendeleo ya nchini.
 

Vilevile, nawashukuru sana waandaji wa Kongamano hili kwa ujumla wao pamoja na wadhamini wetu ambao isingekuwa wao tusingeweza kufanikisha shughuli hii. Shukrani za pekee ziwaendee Kamati ya Mapokezi, kwa mapokezi mazuri tangu tulipowasili hapa visiwani Zanzibar, ninawashukuru sana na kuwapongeza kwa kazi nzuri.
Napenda kuchukua nafasi hii pia kuwapa pole kwa safari ndugu zetu wa Diaspora waliosafiri masafa marefu kutoka kila kona ya dunia kuja kuhudhuria Kongamano hili muhimu. Sina shaka mtafurahia ukarimu wa visiwani na huduma mbalimbali mtakazo zipata katika kipindi chote mtakacho kuwepo hapa Zanzibar. Karibuni sana mjisikie mko nyumbani maana mtu kwao ndio ngao.

Mhe. Rais,
Mabibi na Mabwana,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilianzisha Idara ya Diaspora mwaka 2010 kwa lengo la kuwatambua Watanzania wanaoishi ughaibuni na kuwahamasisha katika kuchangia maendeleo ya nchi kwa kutumia mitaji, ujuzi na elimu wanayoipata wakiwa nje ya nchi kwa manufaa ya Taifa lao.

Tangu ilipoanzishwa Idara, kumekuwa na jitihada mahsusi za kuwahamasisha na kuwashirikisha Diaspora katika kuchangia maendeleo ya nchi. Kwa kuanzia, Wizara yangu imekuwa ikiratibu makongamano ya Diaspora ndani na nje ya nchi, na hatimaye Kongamano hili la tatu linalofanyika hapa nchin

No comments :

Post a Comment