Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe magufuli akimuapisha
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kapilimba
Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016
KABLA
ya kuteuliwa na Rais John Pombe Magufuli hivi karibuni, Kukaimu ukurugenzi wa Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Kapilimba, (pichani), alikuwa Mkurugenzi wa Udhibiti
Majanga wa BENKI Kuu ya Tanzania, ambako alifanya kazi kuanzia mwaka 2011,
kabla ya kufanya kazi hiyo, Dkt. Kapilimba alikuwa Meneja wa Udhibiti Mfumo wa
Majanga, Benki Kuu ya Tanzania, nafasi aliyoshikilia kutoka mwaka 2009 hadi 2011
alipopandishwa cheo kuwa Mkurugenzi wa Udhibiti Majanga Benki Kuu ya Tanzania.
Kabla
ya kuwa Meneja udhibiti mfumo (System Risk), Dkt. Kapilimba alifanya kazi kama
Mshauri wa Information Technology (IT), wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania,
kuanzia mwaka 2008 hadi 2009.
Dkt.
Kapilimba pia amewahi kuwa Mhadhiri na mkuu wa Idara ya Computer na Mifumo ya
Habari, Chuo Cha Masomo ya Kitaaluma cha Manchester nchini Uingereza.(MCPS). Pia
lifanya kazi ya uhadhiri kwa muda (Part time), Usanifu wa Computer, (Computer Architecture),
Chuo Kikuu Cha Salford nchini Uingereza.
Dkt.
Kapilimba ana PhD ya Sayansi ya Computer kutoka Chuo Kikuu cha Canterbury
nchini Uingereza, MSc. Katika Sayansi ya Computer kutoka Chuo Kikuu Cha Salford
nchini Uingereza, BSc.(Ed.) Hons katika Mahesabu, Fizikia na Elimu, kutoka Chuo
Kikuu Cha Dar es Salaam.
Lakini
pia Msomi huyo aliyebobea kwenye mifumo ya computer, ni mwanachama wa Mashirika
mbalimbali vya Kitaaluma, ikiwa ni pamoja na Charter IT, cha Chama cha Sayansi
cha Uingereza (British Computer Society), (MBCS CITP, pia cha Uingereza,
Taasisi ya Uchambuzi na Programu (MIAP), cha Uingereza, na Taasisi ya Uhandisi
wa Umeme na Vifaa vya Umeme (IEEE), cha Marekani.
Chanzo:-MetricStream
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe magufuli na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan pamoja na Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Masaju na Katibu Mkuu kiongozi Mhandisi
John Kijazi katika picha ya pamoja na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama
baada ya kuapishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa
Taifa Dkt Modestus Francis Kapilimba Ikulu jijini Dar es salaam leo
Agosti 24, 2016
(PICHA NA IKULU)
No comments :
Post a Comment