Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika anayeshughulikia Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje
Calleb Weggoro, Ikulu jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika anayeshughulikia Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje
Calleb Weggoro,kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Bi.Tonia Kandiero, Ikulu jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika anayeshughulikia Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje
Calleb Weggoro mara baada ya kumaliza mazungumzo, Ikulu jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika anayeshughulikia Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje
Calleb Weggoro (kushoto) na kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika Bi.Tonia Kandiero, Ikulu jijini Dar Es Salaam.
NA MWANDISHI MAALUM
Benki ya Maendeleo ya
Afrika (AfDB) imeihakikishia Serikali kuwa itaendelea kuisaidia Tanzania katika
kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo uimarishaji wa miundombinu ya barabara
katika kuelekea kwenye Taifa la uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Kauli hiyo imetolewa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika anayeshughulikia kanda ya Afrika
Mashariki, Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro alipokutana na kufanya mazungumzo na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan 24-Aug-16 ofisini kwake, Ikulu, Dar es salaam.
Dkt. Weggoro alisema
amefurahishwa na jinsi serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi kupitia
Mpango wa Ushirikiano kati ya Sekta Binafasi na sekta za Umma (PPP) katika utekelezaji
wa miradi mbalimbali na anaamini ushirikiano huo utakuwa na manufaa kwa Taifa.
Mkurugenzi huyo alimweleza Mheshimiwa
Makamu wa Rais kuwa katika Mkakati wa
Kitaifa wa 2016-2020 ulioandaliwa na Benki hiyo umeonesha maeneo matano mapya
ambayo yatapewa kipaumbele katika kusaidia nchi za Afrika.
Ametaja maeneo hayo kuwa ni
pamoja na masuala ya nishati, chakula, viwanda, utangamano wa nchi za Afrika na
kuboresha maisha ya wananchi hasa vijana na wanawake kwa kuwawezesha kiuchumi
kwa kuwapatia ajira.
Katika mazungumzo hayo
Makamu wa Rais aliishukuru benki hiyo kwa misaada yake ambayo imeiwezesha
serikali kutimiza azma yake ya kuleta maendeleo kwa wananchi wake kwenye nyanja
za kiuchumi na kijamii.
"Ni matumaini yangu
kuwa katika huu mkakati mpya benki itakuwa tayari kuisadia Tanzania na nchi
nyingine za kanda ya Afrika Mashariki, maana sote tunahitaji kusonga mbele
kimaendeleo," alisema Mheshimiwa Samia.
Katika msafara huo Dkt.
Weggoro alifuatana na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo ya AfDB Tonia Kandiero
ambaye alisema msaada wa benki hiyo katika kuimarisha miundombinu ya barabara
ni jambo la msingi na akaelezea kufurahishwa kwake jinsi serikali
inavyotekeleza miradi hiyo kwa ufanisi.
No comments :
Post a Comment