Tuesday, August 23, 2016

MAUAJI YA UTATA DHIDI YA POLISI YAREJEA TENA, ASKARI WANNE WAPIGWA RISASI MBANDE, JIJINI DAR ES SALAAM



NA K-VIS MEDIA
MAUAJI ya kitatanishi dhidi ya askari wa Jeshi la Polisiyamerejea tena naaba ya polisi wannee kuuawa kwa kupigwa risasi huko Mbande, wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam majira ya usiku kwenye tawi la benki ya CRDB.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akiwa amevalia magwanda ya polisi alifika eneo la tukio akifuatana na polisi wa Kanda Maalumya Dar es Salaam, Simon Siro na kuthibitisha vifo hivyo.
Alisema, wavamizi hao waliokuwa na nia ovu, walitumia usafiri wa pikipiki na walifika eneo la tukio wakati askari wakibadilishana lindo majiraya saa 1 na saa 2 usiku wa Agosti 23, 2016, wavamizi walifyatua risasi na kuwauwa askari hao, alisema Waziri Nchembakwa huzuni.
Vyanzo vya habari vinasema, wauaji wametoroka na bunduki moja ya polisi aina ya (Sub-Machinegun-SMG), lakini jambo la kustaajabisha, hawakuingia ndani ya benki hiyo.
Jambo hilo ndilo linalostaajabisha mashuhuda wa tukio hilo na kutafsiri kuwa ni mauaji ya makusudi dhidiya polisi, alisemashuhuda mmoja.
“Nitoe pole kwa IGP na familia za marehemu, tayari vijana wameingia kazini na msako unaendelea kila kona kuhakikisha wauaji haowanatiwa mikononimwa vtyombovya do,” alisema Waziri Nchemba.
Jambo la kutia shaka, wauaji hawakuingia ndaniya benki, kwani baada ya kutekeleza shambulio hilo waliondoka.
Mwanzoni mwa mwaka huu, kumeshuhudia matukio ya mauaji ya polisi kwenye maeneo kadhaa ya nchi, ambapo silahapia ziliporwa. Hata hivyo polisi walifanikiwa kutuliza wimbi hilo la mauaji kwa kufanya opereshenikubwa na tayari imewatia mbaroni baadhi ya wanaotekeleza mauaji hayo.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (mwenye kombati), akimjulia hali mmoja wa askariwaliojeruhiwa kwenye shambulio hilo
 Waziri akiwa na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SimonSiro (kushoto), kwenye eneo la tukio usiku wa kuamkia leo Agosti 24, 2016
  Waziri akitafakari na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SimonSiro (kushoto), kwenye eneo la tukio usiku wa kuamkia leo Agosti 24, 2016

No comments :

Post a Comment