Wajumbe
wa Kamati ya Maendeleo kwa Afrika katika Bnge la Korea Kusini
wakiwasili katika uwanja mdogo wa ndege uliopo katika Hifadhi ya Taifa
ya Serengeti.
Meneja
Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA,Victor Ketance akipokea
ugeni wa wajumbe kutoka Bunge la Korea Kusini walipotembelea Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kutizama eneo la uwekezaji wa kituo cha
kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) William Mwakilema akipokea ugeni wa
wajumbe kutoka Bunge la Korea Kusini walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti kwa ajili ya kutizama eneo la uwekezaji wa kituo cha kisasa
cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) William Mwakilema
akisalimiana na wadau wa utalii,Zainabu Ansel ,Mkurugenzi wa kampuni ya
Utalii ya Zara(katikati) na Mkurugenzi wa Kibo Safari's Willy
Chamburo.(kushoto) waliokuwepo uwanjani hapo.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Kibo Safari's ,Willy Chamburo (katikati) akizungumza
jambo na kiongozi wa ugeni wa Korea Kusini Won Yul Chui (kushoto) baada
ya kukutana katika uwanja mdogo wa ndege uliopo Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti .kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
William Mwakilema.
Wajumbe
wa Kamati ya Maendeleo ya Afrika katika Bunge la Korea Kusini wakitia
saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kuangalia eneo lililotengwa kwa ajili ya
ujenzi wa kituo cha kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema (kushoto)
akizungumza na Wajumbe wa kamati ya Maendeleoo ya Afrika ya Bunge la
Korea Kusini waliofika katika Hifadhi hiyo kwa ajili ya ufuatiliaji wa
maenedeleo ya kuanza kwa mradi wa ujenzi wa kituo cha kisasa cha Taarifa
katika Hifadhi hiyo.
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,William Mwakilema akiongoza
Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini walioko katika kamati ya
Maendeleo ya Afrika kutembelea maeneo kutakapo jengwa kituo cha kisasa
cha taarifa.
Moja
ya eneo lilipo sasa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo
inatumika kutoa taarifa kwa njia ya picha za video za Hifadhi hiyo.
Ujumbe
wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini wakitizama picha ya Hayati Baba wa
Taifa ,Mwl Julius K. Nyerere akiwa na rafiki yake Prof,Dkt Bernhard
Grzimek huku wakipata maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema.
Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini wakipata maelezo katika
michoro ya kituo cha kisasa cha taarifa katika Hifadhi ya taifa ya
Serengeti.
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema akitoa zawadi
kwa wajumbe wa Bunge la Korea Kusini mara baada ya kutembelea eneo
kutakapo jengwa kituo cha kisasa cha taarifa katika hifadhi hiyo.
Wajumbe
wa Bunge la Korea Kusini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi na watumishi wa Shirika la Hifadhhi za Taifa (TANAPA ) na
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Na
Dixon Busagaga wa Michuzi blog Kanda ya Kaskazini.
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Mhe Rosemary Staki Senyamule akizungumza na viongozi wa Kijiji na Kata ya Gonja Maore na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa Wilaya
baada ya kushiriki bega kw abega na wananchi katika upangaji wa
matofali kwenye tanuu tayari kwa kuchomwa ili kukamilisha ujenzi wa
miradi mbalimbali wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule akishiriki shughuli za maendeleo kwa kufyeka baadhi ya vichaka
NA
MATHIAS CANAL, KILIMANJARO
Mkuu
wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule ametenga
Siku moja katika Juma ili kushiriki shughuli za maendeleo kwa kushirikiana na
wananchi.
Huu
ni utaratibu ambao Mkuu huyo wa Wilaya ameuanzisha kwa muktadha wa kuchochea
ari katika utendaji Kazi na uwajibikani kwa kila mwananchi ili kuimarisha na
kusukuma kwa vitendo juhudi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Joseph Pombe Magufuli kwa vitendo na utekelezaji wa utendaji kazi ili kuakisi
dhana nzima ya serikali hii ya awamu ya tano ya Hapa Kazi Tu
MKUU mpya wa Wilaya ya Arusha, Gabriel
Damian Daqarro akizungumza muda mfupi baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo na
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Bw. Daqarro amabye alikuwa ofisi ya
Rais, anaanza majukumu hayo mapya akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Mkuu wa
mkoa Gamboaliyepandishwa cheo kufuatia kufutwa kazi kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa
huo Felix Tibenda Kijiko, wiki iliyopita.
Daqarro akila kiapo
Mkuu wa mkoa Gambo, akisaini kiapo, wakati wa zoezi la kuapishwa kwa mkuu mpya wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro (kulia)
Baadhi ya waliohudhuria hafla ya kiapo
Picha ya pamoja
No comments :
Post a Comment