Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya
Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga (kulia),
akimkabidhi cheti, Mpoki Mwasunga, baada ya kuhitimu mafunzo ya udereva
ya mwezi mmoja katika chuo cha udereva cha Nyato's kilichopo Majohe
Bomba mbili Manispaa ya Ilala Dar es Salaam leo. Wahitimu 19 ambao ni
walemavu walihitimu mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa shule hiyo Wilfred Nyato (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Usalama
Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter
Mashishanga, akiangalia alama ya usalama barabarani. Kushoto ni
Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya
Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu, Kabateke Jutoram
na Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani
nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero.
Wahitimu wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mshairi, Kiiza Amani akitoa burudani kwenye hafla hiyo.
Mkuu
wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi
(ASP), Peter Mashishanga (katikati), akihutubia kwenye hafla hiyo.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati
ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu, Kabateke Jutoram
na Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama
barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero.
Mkurugenzi wakitengo
cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu
Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero, akitoa neno kwenye mkutano huo.
H
Mkuu
wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi
(ASP), Peter Mashishanga (kushoto), akimkabidhi cheti, mhitimu, Subira
Semsimbazi.
Hapa James Hizza akipokea cheti chake.
Sikujua Mbwembwe, akikabidhiwa cheti chake.
Wahitimu wakionesha vyeti vyao.
Stafu Sajeni, Enock Machunde akitoa darasa kwa hitimu hao kuhusu sheria za usalama barabarani.
Koplo, Faustina Ndunguru, akizungumza kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
WATU Jamii ya walemavu ambao ni maderava
wa vyombo vya moto wametakiwa kujitokeza kwenye shule mbalimbali za
udereva ili kupata mafunzo ya udereva ikiwa pamoja na kupata leseni
kabla ya kutumia vyombo hivyo.
Wito huo umetolewa Dar es Salaam leo na
Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa kipolisi wa Ilala,Peter Mashishanga
wakati akiwatunuku vyeti walemavu 19 ambao wa mefunzo ya mwenzi mmoja
katika shule ya udereva ya Nyato's iliyopo Majohe Bomba mbili Manispaa
ya Ilala.
Alisema kuwa ipo haja ya walemavu ambao
wanamiliki vyombo vya moto na kuendesha vyombo hivyo kabla hawajaingia
barabarani ni vema wakapata mafunzo ya kujuwa alama,kanuni na sheria za
usalama barabarani.
"Ni muhimu kwa kundi hili ambalo leo
mmepata vyeti vya kuhitimu mafunzo ya udereva kwenda kuwa mabalozi kwa
wengine ambao hawajapata fursa ya kupata mafunzo kama nyie kwenda
kuwahamasisha ili wajiunge katika vyuo vya udereva ikiwamo chuo hiki
cha Nyato's ambacho kimeaza mpango wa kutoa mafunzo haya kwa nchi nzima
kwa kushirikiana Kamati ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye
Ulemavu."alisema Mashishanga
Aidha aliwaeleza wahitimu hao kuwa
wahakikishe wanakwenda kupata majaribio kwa wa kufunzi wa kikosi cha
Usalama barabarani ili wapate leseni zitakazo wafanya waweze kuendesha
vyombo vya vya moto.
Kwaupande wake Mkurugenzi wakitengo cha
Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa
Polisi (ASP),Mossi Ndozero alisema kuwa ni muhimu kwa wahitimu hao
kwenda kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa pamoja na kuvaa
kofia ngumu,na kutozidisha abiria.
Naye Mkurugenzi wa shule hiyo Wilfred
Nyato alishukuru kwa ushirikiano uliopo kati ya Jeshi hilo na taasisi
yake ambapo pia ametoa ofa ya kusoma bure kwa mlemavu Thomas Kone
ambaye hivi karibuni alipata msaada wa bajaji kutoka kwa Rais Dk. John
Magufuli.