PRESIDENT John Magufuli has told Cuban business people to invest in the country’s sugar industry as well as medicine and diagnostic tools production.
Kaimu Kamishna
Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela,
akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu
yanayofanyika Jijini Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo @BMG
Serikali imeshauriwa kutoa ushirikiano kwa watetezi wa haki
za binadamu ili kurahisisha utendaji kazi wao badala ya kuwaona
watetezi hao kama wachochezi katika jamii na wakati mwingine kuwafungulia mashitaka.
Ushauri huo
umetolewa hii leo Jijini Mwanza na Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa
Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, kwenye mafunzo
ya siku tatu kwa
watetezi wa haki za binadamu kutoka mikoa mbalimbali nchini.
Amesema katika baadhi ya maeneo kama Loliondo mkoani Arusha kwenye mgogoro
wa ardhi kati ya wananchi na mwekezaji, watetezi wa haki za binadamu
wamechukuliwa kama wachochezi na kufunguliwa mashitaka jambo linalosababisha
baadhi yao kushindwa kutekeleza majukumu yao na wengine kuacha kabisa shughuli
za utetezi.
Akifungua Mafunzo hayo, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya
Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, amesema serikali itaendelea
kuwaelimisha wachimbaji wadogo ili waifahamu vyema sheria ya madini namba 4 ya mwaka 2010
ili kupunguza migogoro iliyopo na kwamba imetenga zaidi ya hekta elfu 12 kwa ajili ya
wachimbaji wadogo wadogo wa madini.
Pia amesema serikali imetenga shilingi bilioni 6.6 kwa ajili
ya ruzuku kwa wachimbaji wadogo na kuwahimiza kujiunga kwenye vikundi ili
wapatiwe ruzuku hiyo.
Baadhi ya
washiriki wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuimarisha utendaji wao wa
kazi jambo litakalowasaidia kutimiza vyema wajibu wao katika jamii bila
kuonekana wachochezi huku pia wakiwa katika upande salama dhidi ya
maisha yao.
Kaimu Kamishna
Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela,
akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu
yanayofanyika Jijini Mwanza.
Kaimu Kamishna
Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela,
akizungumza na wanahabari nje ya Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu
yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza na Wanahabari nje ya ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Miongoni mwa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Washiriki wa Semina
Mwonekano kwenye semina
Picha ya pamoja
Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya
Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga (kulia),
akimkabidhi cheti, Mpoki Mwasunga, baada ya kuhitimu mafunzo ya udereva
ya mwezi mmoja katika chuo cha udereva cha Nyato's kilichopo Majohe
Bomba mbili Manispaa ya Ilala Dar es Salaam leo. Wahitimu 19 ambao ni
walemavu walihitimu mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa shule hiyo Wilfred Nyato (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Usalama
Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter
Mashishanga, akiangalia alama ya usalama barabarani. Kushoto ni
Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya
Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu, Kabateke Jutoram
na Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani
nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero.
Wahitimu wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mshairi, Kiiza Amani akitoa burudani kwenye hafla hiyo.
Mkuu
wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi
(ASP), Peter Mashishanga (katikati), akihutubia kwenye hafla hiyo.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati
ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu, Kabateke Jutoram
na Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama
barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero.Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero, akitoa neno kwenye mkutano huo.
Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga (kushoto), akimkabidhi cheti, mhitimu, Subira Semsimbazi.
Hapa James Hizza akipokea cheti chake.
Sikujua Mbwembwe, akikabidhiwa cheti chake.
Wahitimu wakionesha vyeti vyao.
Stafu Sajeni, Enock Machunde akitoa darasa kwa hitimu hao kuhusu sheria za usalama barabarani.
Koplo, Faustina Ndunguru, akizungumza kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
WATU Jamii ya walemavu ambao ni maderava
wa vyombo vya moto wametakiwa kujitokeza kwenye shule mbalimbali za
udereva ili kupata mafunzo ya udereva ikiwa pamoja na kupata leseni
kabla ya kutumia vyombo hivyo.
Wito huo umetolewa Dar es Salaam leo na
Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa kipolisi wa Ilala,Peter Mashishanga
wakati akiwatunuku vyeti walemavu 19 ambao wa mefunzo ya mwenzi mmoja
katika shule ya udereva ya Nyato's iliyopo Majohe Bomba mbili Manispaa
ya Ilala.
Alisema kuwa ipo haja ya walemavu ambao
wanamiliki vyombo vya moto na kuendesha vyombo hivyo kabla hawajaingia
barabarani ni vema wakapata mafunzo ya kujuwa alama,kanuni na sheria za
usalama barabarani.
"Ni muhimu kwa kundi hili ambalo leo
mmepata vyeti vya kuhitimu mafunzo ya udereva kwenda kuwa mabalozi kwa
wengine ambao hawajapata fursa ya kupata mafunzo kama nyie kwenda
kuwahamasisha ili wajiunge katika vyuo vya udereva ikiwamo chuo hiki
cha Nyato's ambacho kimeaza mpango wa kutoa mafunzo haya kwa nchi nzima
kwa kushirikiana Kamati ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye
Ulemavu."alisema Mashishanga
Aidha aliwaeleza wahitimu hao kuwa
wahakikishe wanakwenda kupata majaribio kwa wa kufunzi wa kikosi cha
Usalama barabarani ili wapate leseni zitakazo wafanya waweze kuendesha
vyombo vya vya moto.
Kwaupande wake Mkurugenzi wakitengo cha
Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa
Polisi (ASP),Mossi Ndozero alisema kuwa ni muhimu kwa wahitimu hao
kwenda kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa pamoja na kuvaa
kofia ngumu,na kutozidisha abiria.
Naye Mkurugenzi wa shule hiyo Wilfred
Nyato alishukuru kwa ushirikiano uliopo kati ya Jeshi hilo na taasisi
yake ambapo pia ametoa ofa ya kusoma bure kwa mlemavu Thomas Kone
ambaye hivi karibuni alipata msaada wa bajaji kutoka kwa Rais Dk. John
Magufuli.
Nyato alisema kuwa kimeazisha mpango wa
kutoa mafunzo ya udereva kwa kushirikiana na kamati ya Taifa ya
usalama kwa watu wenye ulemavu kwa lengo la kukabiliana na matukio ya
ajali za barabarani.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemthibitisha Bw. Gerson Partinus Msigwa, (pichani) kuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya
Rais, (Directorate of Presidential Communication - DPC).
Taarifa iliyotolewa leo Jumatano
Agosti 31,2016 na Katibu Mkuu Ikulu Bw. Peter Ilomo imeeleza kuwa Bw. Gerson
Partinus Msigwa amethibitishwa kuanzia leo tarehe 31 Agosti, 2016 kushika
wadhifa huo.
Kabla ya uthibitisho huo, Bw. Gerson Partinus Msigwa alikuwa
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, katika Ofisi ya Rais Ikulu
kuanzia tarehe 17 Novemba, 2015.
Awali kabla
ya kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa alikuwa
mtangazaji wa Televisheni ya Taifa TBC mkoani Ruvuma
Gerson Msigwa akiwa na Mke wake Catherine Nyoni kwenye moja ya hafla
Akiwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano
Ikulu, Msigwa (wapili kulia), akimsaidia mtangazaji wa ITV, kuripoti
wakati wa ziara ya Rais John Pombe Magufuli hivi karibuni wilayani Chato
Msigwa wakati akiwa mtangazaji wa TBC, akifanya moja ya mahojiano
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha ACP Sida Mohamed Himid kuwa Naibu Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ,
anayeshuhulikia Idara Maalum za SMZ,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa
Ikulu Mjini Unguja leo Agosti 31, 2016. (PICHA
NA IKULU YA ZANZIBAR)
Rais Shein akimkabidhi vitendea kazi ACP Sida
Rais akisaini kiapo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein (kushoto) akimuapisha Nd,Hassan Khatib Hassan kuwa Naibu Katibu
Mkuu, Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,atayeshuhulikia
masuala ya Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,katika hafla iliyofanyika
ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Baadhi ya Mawaziri wa Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi katika taasisi mbali mbali
walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
Mohamed Shein,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid (kulia) na Jaji
Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria
katika hafla ya kuapishwa Viongozi wa Taasisi mbali mbali za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Makamanda Wakuu wa Vikosi vya SMZ walihudhuria katika hafla ya kuapishwa
Viongozi wa taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi, walioteuliwa na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo
No comments :
Post a Comment