Julita N Mongi, mwanachama mpya wa PSPF
kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari, PSS, akionyesha kitambulisho
chake cha uanachama alichokabidhiwa dakika 5 tu baada ya kujaza fomu.
Huduma hiyo inatolewa kwenye banda la PSPF lililoko jengo la Wizara ya
Fedha kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa, viwanja vya
Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Julai 3, 2016.
Wananchi wengi wamejitokeza kujiunga na Mfuko huo na kudhihirisha kuwa
ni chaguo la wengi. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Julita akikabidhiwa kadi yake na Afisa Masoko wa PSPF, Magira Werema
Mstaafu ambaye kwa sasa ni Mkulima wa Turian, Mzee Gabriel E. Kiogwe (84), akijaza za kujiunga na mpango wa PSS
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF,
Abdul Njaidi, akimkabidhi kadi ya uanachama, Mwanachama mpya, Mzee
Gabriel E. Kiogwe (84) dakika 5 baada ya kujaza fomu za kujiunga
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, akimpiga picha Mwanachama mpya Scola Malinga
Njaidi akimkabidhi kadi Scola Malinga, baada ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari, PSS
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF,
Abdul Njaidi akiwapatia maelezo ya kina ya faida za kujiunga na
uanachama kwenye Mfuko huo, wafanyakazi wa wizara ya Fedha, ambapo baada
ya maelezo hayo walijiunga na kuwa wanachama kupitia mpangio wa
uchangiaji wa hiari, PSS.
Joyce Kakore, akijaza fomu za kujiunga na mpango huo
Joyce Kakore, wa wizara ya Fedha,
(kulia), akikabidhiwa kadi ya kujiunga na uanachama PSPF, kupitia mpango
wa PSS. Anayemkabidhi ni Afisa Uhusiano Mwandamizi, wa Mfuko huo, Abdul
Njaidi
Afisa Matekelezo wa PSPF, Penzila
Kaisi, (kulia), akimpatia maelezo Mwanachama wa Mfuko huo aliyefika
kwenye banda la PSPF, ili kujua hali ya michango yake
Afisa wa PSS wa PSPF, SophiaMbilikira, (kushoto), akimsikiliza mwanachama wa PSPF aliyetembelea banda la Mfuko huo
Mwanachama mpya wa PSPF, kupitia PSS, Lillingani S. Juma akionyesha kadi yake
Julita N Mongi akijaza fomu
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF,
Abdul Njaidi, (kulia) na Afisa Uwekezaji wa Mfuko huo Hawa Kivina,
(wapili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wanachama wapya wa
Mfuko huo dakika chache baada ya kukabidhiwa kadi zao
Afisa Masoko wa PSPF, Magire Werema, (kushoto), akimkabidhi kadi ya uanachama wa PSPF, mwanachama mpya, Grace M Malya
Grace M Malya akiwa amembeba mtoto wake, akionyesha kadi yake ya uanachama baada ya kukabidhiwa
Wananchi wa kila kada wakipatiwa maelezo na maafisa wa PSPF kwenye banda la Mfuko huo
Afia Uhusiano Mwandamizi, wa PSPF, Abdul Njaidi akimkabidhi kadi ya uanachama mwanachama mpya Catherine D Mhina |
Afisa uwekezaji wa PSPF, Hawa Kivina,
(kushoto), akimpatia maelezo Mwanachama wa Mfuko huo, Meneja
Mawasiliano, Mamlaka ya Udhibiti Makampuni ya Bima Tanzania, Eliezer
Rweikiza, juu ya mikopo ya nyumba
Hadji Jamadari, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa PSPF, akichapisha vitambulisho vya wanachama wapya papo hapo na kuwakabidhi
Catherine D Mhina, akionyesha kadi yake
Rais Paul Kagame na mwenyeji wake Rais
John Pombe Magufuli, wakipungia mkono wananchi waliojawa na furaha mara
baada ya kuzinduz rasmi maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar
es Salaam kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini
Dar es Salaam, Julai 1, 2016. Imeelezwa na wachambuzi wa mambo kuwa
ziara hii ya Rais Kagame hapa Tanzania, ni ya kihistoria ambayo imezidi
kujenga mwanzo mpya baina ya mataifa haya mawili jirani, baada ya
"mchafuko wa hali ya hewa" mwaka uliopita kufuatia kutokea kwa
kutoelewana baina ya rais Kagame na rais wa awamu ya nne, Jakaya
Kikwete. Rais Kagame katika hotuba yake aliyoitoa kwa kirefu kwa lugha
ya Kiswahili murua, alionyesha kufurahishwa mno na mapokezi na moyo wa
upendo ambao Rais Magufuli na Watanzania kwa ujumla waliouonyesha kwake
hadi akafikia kusema, "Ninaona niko nyumbani". Rais Kagame pia katika
hotuba yake alimalizia kwa kibwagizo cja "Hapa Kazi tu", kauli mbiu ya
Rais Magufuli.(PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Mama Jannet Kagame (kushoto) na
mwenyeji wake Mama Jannet Magufuli, walipotembelea maonyesho ya biashara
ya kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 1, 2016. (PICHA NA K-VIS
MEDIA/KAHLFAN SAID)
Mama Jannet Kagame (kushoto) na mwenyeji wake Mama
Jannet Magufuli, walipotembelea maonyesho ya biashara ya kimataifa ya
Dar es Salaam, Julai 1, 2016. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KAHLFAN SAID)
Rais Kagame akikagua gwaride la JWTZ wakati wa mapokezi yake uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere. (PICHA NA IKULU)
Mapokezi katika zulia jekundu Ikulu ya Dar es Salaam. (PICHA NA IKULU)
Rais Magufuli akiteta jambo na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame.(PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Rais Magufuli akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha mgeni wake, Rais Paul Kagame wa Rwanda.Rais Kagame akihutubia wakati akizindua maonyesho hayo viwanja vya Mwalimu Nyerere.(PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Rais Kagame akihutubia wakati akizindua maonyesho hayo viwanja vya Mwalimu Nyerere.(PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Rais Kagame akihutubia wakati akizindua maonyesho hayo viwanja vya Mwalimu Nyerere.(PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Mama Jannet Kagame akijitambulisha. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Marais wakipungia mkoni wananchi (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Wimbo wa Afrika Mashariki ukipigwa viwanja vya Sabasaba (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu), Jenista Mhagama (kulia) akipokelewa na Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara mara baada ya kuwasili katika banda la Shirika hilo.
Meneja
Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifashi ya Jamii
(NSSF), Eunice Chiume akisalimiana na Waziri Jenista Mhagama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunga, Kazi, Ajira Vijana na Wenye ulemavu, Jenista Mhagama akisalimiana naOfisa Uhusiano wa NSSF, Devota.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Kazi, Ajira Vijana na Wenye
ulemavu, Jenista Mhagama (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Meneja
Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kulia), wakati
alipotembelea banda la NSSF kwenye maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa
katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Kazi, Ajira Vijana na Wenye ulemavu, Jenista Mhagama (katikati), akipata maelezo kutoka kwa Meneja
Kiongozi Masoko na
Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kulia), wakati alipotembelea banda la
NSSF kwenye maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya
Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara.
Waziri Jenista Mhagama akiangalia Kadi ya mwanachama aliyejiunga na NSSF.
Meneja
Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kushoto), akitoa
maelezo kuhusu huduma za bima zinazotolewa na NSSF kwa Waziri Jenista
Mhagama. Kulia ni Mtaalam wa Bima, Peter Isack.
Waziri Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia)akikabidhiwa
madawati 100 kutoka kwa Viongozi wa jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir na
familia ya Rais wa Jumuiya hiyo Mohamed Raza walipofika Ikulu Mjini Zanzibar
leo,msaada huo kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(wa pili kulia) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mashekhe wa Jumuiya
ya Khoja Shia Ithna-asheir (kulia) Sheikh Shaaban Hussein,Sheikh Maulana
Dhishan Haidar na Rais wa Jumuiya hiyo Mhe, Mohamed Raza (kushoto)
wakati walipofika ikulu Mjini Zanzibar kukabidhi msaada wa madawati 100
kawanafunzi wa Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Mohamed
Raza Daramsi wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na Viongozi
na Mashekhe wa jumuiya hiyo kwa ajili ya kukabidhi msaada wa madawati 100
kwa ushirikiano na familia ya Rais wa Jumuiya,msaada huo utaowanufaisha
wanafunzi wa Skuli mbali mbali za Zanzibar
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma akitoa
shukurani kwa Uongozi wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir wakati
ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kukabidhi madawati 100 kwa Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) ikiwa
ni katika kuimarisha sekta ya Elimu hapa Zanzibar
No comments :
Post a Comment