Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Sostenes Lyimo, akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godious
Kahyarara, na wasaidizi wake wakati walipotembelea katika Banda la Maonesho lamMfuko huo kwenye Viwanja vya Sabasaba
jana.
Kahyarara, na wasaidizi wake wakati walipotembelea katika Banda la Maonesho lamMfuko huo kwenye Viwanja vya Sabasaba
jana.
Picha na Mafoto Blog
Afisa Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Janeth Ezekiel,
akizungumza na mwananchi aliyefika kwenye Banda lao la Maonesho katika
Viwanja vya Sabasaba wakati akimwelekeza jambo kuhusu mafao ya Mfuko huo.
akizungumza na mwananchi aliyefika kwenye Banda lao la Maonesho katika
Viwanja vya Sabasaba wakati akimwelekeza jambo kuhusu mafao ya Mfuko huo.
Afisa
Mwandamizi na Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo,
akimfafanulia jambo mmoja kati ya wananchi waliofika katika Banda la
Mfuko huo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye
Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Mwananchi akitoa maoni yake katika mashine maalum baada ya kupata huduma kwenye Banda la
Maonesho la Mfuko wa Pensheni wa PPF, Maonesho ya KImataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Maonesho la Mfuko wa Pensheni wa PPF, Maonesho ya KImataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwananchi akitoa maoni yake katika mashine maalum baada ya kupata huduma kwenye Banda la
Maonesho la Mfuko wa Pensheni wa PPF, Maonesho ya KImataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Maonesho la Mfuko wa Pensheni wa PPF, Maonesho ya KImataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mwajuma
Msina, akimkabidhi Kitambulisho Mwanachama Mohamed Hassan (23) aliyejiunga na
huduma ya ‘Wote Scheme’ wakati alipotembelea kwenye Banda la Maonesho la Mfuko
huo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya
Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Msina, akimkabidhi Kitambulisho Mwanachama Mohamed Hassan (23) aliyejiunga na
huduma ya ‘Wote Scheme’ wakati alipotembelea kwenye Banda la Maonesho la Mfuko
huo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya
Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIRKI DHIFA YA KITAIFA NA MGENI WAKE RAIS KAGAME.
Raiswa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia)
akigonganisha bilauri na Mke wa Rais wa Rwanda, Mama Jeannette Kagame
katika kusherehekea Dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia mgeni wake Rais wa
Rwanda Paul Kagame (katikati) Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Kagame
alikuwa nchini kwa ziara ya Kikazi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kulia)
akigonganisha bilauri na Rais wa Rwanda Paul Kagame, katika kusherehekea
Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa
ajili ya mgeni wake Rais Kagame.
Dhifa hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku.
Dhifa hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia)
akifurahia jambo na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati)
akiwa amesima kutoa heshima wakati wa Dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia
mgeni wake Rais Kagame (kulia kwake). Kulia ni Makamu wa Rais Samia
Suluhu Hassan. Wa pili
kulia ni Mke wa Tanzania Mama Janet Magufuli na kushoto ni Mke wa Rais wa Rwanda, Jeannette Kagame.
kulia ni Mke wa Tanzania Mama Janet Magufuli na kushoto ni Mke wa Rais wa Rwanda, Jeannette Kagame.
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa tatu kushoto)
akiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim (wa pili kushoto),
Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman (wa tatu kulia) Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na
Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Rwanda, Louise Mushikiwabo (kulia).
Waziri
Mkuu Mstaafu Jiji Mstaafu Joseph Sinde Warioba akimsikiliza Naibu Spika
wa Bunge la Jamhuri Dkt. Tulia Ackson wakiwa kwenye Dhifa
ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa mgeni
wake Rais Kagame. Dhifa hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (kulia) akizungumza na Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida wakiwa kwenye Dhifa ya
Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya
mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame aliyetembelea Tanzania kwa ziara
ya Kikazi.
WAZIRI WA KAZI ATEMBELEA BANDA LA NSSF KATIKA MAONYESHO YA SABASABA 2016
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (kulia) akipokelewa na Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara mara baada ya kuwasili katika banda la Shirika hilo.
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara mara baada ya kuwasili katika banda la Shirika hilo.
Meneja
Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifashi ya Jamii
(NSSF), Eunice Chiume akisalimiana na Waziri Jenista Mhagama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama akisalimiana naOfisa Uhusiano wa NSSF, Devota.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (wa pili kulia), akipata maelezo
kutoka kwa Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kulia), wakati alipotembelea banda la NSSF kwenye maonyesho ya Biashara ya 40 ya
Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Prof. Godius Kahyarara.
kutoka kwa Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kulia), wakati alipotembelea banda la NSSF kwenye maonyesho ya Biashara ya 40 ya
Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Prof. Godius Kahyarara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (katikati), akiwa katika banda la NSSF.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (katikati), akipata maelezo kutoka kwa Meneja Kiongozi Masoko na
Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kulia), wakati alipotembelea banda la NSSF kwenye maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya
Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara.
Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kulia), wakati alipotembelea banda la NSSF kwenye maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya
Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama akiangalia Kadi ya mwanachama aliyejiunga na NSSF.
Meneja
Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kushoto), akitoa
maelezo kuhusu huduma za bima zinazotolewa na NSSF kwa Waziri wa Nchi
Ofisi ya waziri Mkuu, Jenista Mhagama. Kulia ni Mtaalam wa Bima, Peter
Isack.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagamaakizungumza na waandishi wa habari.
WANAKIBAHA 10,000 KUPATA TIBA BURE YA MACHO NA KINYWA
Baadhi
ya wakazi wa Mji wa Kibaha wakipata huduma ya upimaji wa macho na
miwani bure katika kituo cha afya mkoani kutoka kwa madaktari bingwa
raia wa Marekani ,mpango ambao umeratibiwa na mbunge wa Jimbo la Mji wa
Kibaha Sylvestry Koka.
Mbunge
wa Jimbo la Mji wa Kibaha Mjini, Sylvestry Koka akizungumza na
madaktari bingwa wa magonjwa ya macho na kinywa kutoka nchini Marekani
katika kituo cha afya cha mkoani,muda mfupi kabla ya wataalamu hao
kuanza kutoa huduma ya upimaji macho na ugawaji wa miwani bure mpango
ambao umeratibiwa na mbunge huyo .
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
——————————————————–
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
ZAIDI ya wakazi 10,000 katika Mji
wa Kibaha mkoani Pwani,wanatarajiwa kupata huduma ya tiba ya
macho,miwani na kinywa bure katika kituo cha afya Mkoani kwa muda wa
siku mbili .
Tiba hizo zinatolewa bure chini ya
mpango ulioratibiwa na mbunge wa jimbo la mji wa Kibaha Silvesrty Koka
pamoja na madaktari bingwa kutoka nchini Marekani .
Awali akizungumza kabla ya kuanza
kwa zoezi hilo juzi,Koka alisema lengo lake ni kuwasaidia wananchi
wanaosumbuliwa na matatizo hayo katika jimbo hilo.
Aidha alielezea kuwa mbali ya tiba hizo kutolewa bure pasipo
malipo pia jumatatu (July 4)baadhi ya wauguzi pamoja na baadhi ya
madaktari watapatiwa mafunzo mbalimbali juu ya tiba za macho
yatakayowawezesha kuendelea kutoa huduma hiyo kwa wananchi.
“Natambua juhudi za serikali
katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya bora hivyo nikaamua
kuwaomba wataalamu wa magonjwa hayo nchini Marekani kuja kusaidia kutoa
huduma hizi”
“Falsafa ya “hapa kazi tu” haiwezi
kutekelezwa endapo hakuna mwenye kuwa na afya nzuri,hivyo imani yangu
ni kuwa baada ya wananchi waliokuwa na matatizo ya kiafya ikiwemo macho
na meno watakapopata huduma hii watatekeleza kwa vitendo agizo la Raisi
John Magufuli la kufanyakazi”alisema Koka.
Koka alielezea kuwa afya ni kitu muhimu kwa binadamu kuliko kitu chochote hata mali kwani unaweza kuwa na utajiri mkubwa lakini kama huna afya bora huwezi kufanya lolote.
Alisema ni jukumu lake kusimamia kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa jimbo lake katika sekta mbalimbali ikiwa ni sanjali na afya,elimu,miundombinu na mengineyo mengi.
Koka alielezea kuwa afya ni kitu muhimu kwa binadamu kuliko kitu chochote hata mali kwani unaweza kuwa na utajiri mkubwa lakini kama huna afya bora huwezi kufanya lolote.
Alisema ni jukumu lake kusimamia kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa jimbo lake katika sekta mbalimbali ikiwa ni sanjali na afya,elimu,miundombinu na mengineyo mengi.
Hata hivyo Koka alisema ataendelea
kuzitafutia ufumbuzi kero zinazokabili sekta ya afya ili kuwaondolea
adha wananchi jimboni hapo.
Kwa upande wake daktari wa macho
katika kituo cha afya mkoani ,Makonde Kilumbi alisema kumekuwa na
ongezeko la idadi ya wagonjwa wanaosumbuliwa na tatizo la macho na
ugonjwa wa presha ya macho .
Alisema ugonjwa wa presha ya macho
kwa sasa umekuwa ni tatizo linalowakumba watu wengi na ugonjwa wa mtoto
wa jicho ambapo wamekuwa wakipokea wagonjwa 150 hadi 200 kituoni hapo.
Dk.Kilumbi alisema chanzo kikubwa cha matatizo ya macho ni vumbi,mazingira machafu na hali ya kijiografia.
Akizungumza kwa niaba ya Madaktari kutoka nchini Marekani, mmoja wa wataalamu hao,Profesa Conrad Shayo alisema kutokana na hali halisi waliyoiona kuna kila sababu ya serikali kuweka mkakati mathubuti wa kukabiliana na matatizo hayo.
Baadhi ya wakazi waliofika kupata huduma hizo,akiwemo Nancy Godfrey,Cecilia Kimario walimshukuru Koka kwa kuwezesha mpango huo kuwafikia kwani wengi wao wanasumbuliwa na tatizo hasa la macho.
Akizungumza kwa niaba ya Madaktari kutoka nchini Marekani, mmoja wa wataalamu hao,Profesa Conrad Shayo alisema kutokana na hali halisi waliyoiona kuna kila sababu ya serikali kuweka mkakati mathubuti wa kukabiliana na matatizo hayo.
Baadhi ya wakazi waliofika kupata huduma hizo,akiwemo Nancy Godfrey,Cecilia Kimario walimshukuru Koka kwa kuwezesha mpango huo kuwafikia kwani wengi wao wanasumbuliwa na tatizo hasa la macho.
Mgeni Msafiri alimpongeza mbunge
huyo na kuomba aendelee kusimamia changamoto zinazokabili vituo vya
afya,zahanati jimbo humo ikiwa ni pamoja na madawa na vifaa tiba.
Mgeni alisema sekta ya afya bdo
ina changamoto nyingi hivyo kuna kila sababu ya kupigania kero zilizopo
ili ziweze kupungua kama sio kumalizika na kubaki historia.
MATUKIO KATIKA PICHA JIJINI DAR ES SALAAM
Magari
mawili aina ya Toyota Rav4 yakiwa yamegongana katika makutano ya
barabara ipitayo Benki ya NMB Bank House na Shirika la Bima la Taifa
(NIC) mtaa wa Samora 03 July, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Gari
la kufagia barabara la Kampuni ya Green Waste Pro. Ltd likisafisha moja
ya barabara ipitayo Benki ya NMB Bank House na Shirika la Bima la Taifa
(NIC) mtaa wa Samora 03 July, 2016 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)
TAARIFA KAMILI KUHUSU MSIBA WA ALIYEKUWA MBUNGE WA JIMBO LA KILINDI, BEATRICE SHELUKINDO
Familia
ya Bwana William H. Shelukindo, Inasikitika kutangaza kifo cha Bibi
Beatrice Matumbo Shelukindo kilichotokea siku ya Jumamosi 2/7/2016 huko
Arusha.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu 8 Galu Street, Ada Estate, Dar es salaam na huko Arusha.
Mazishi yatafanyika siku ya Jumatano Tarehe 6/07/2016 alasiri Mjini Arusha.
Bwana ametoa Bwana, ametoa Jina la Bwana lihimidiwe.
MA DC WATANO WALA KIAPO LINDI
hapa wakuu wa wilaya wakiendelea kula kiapo.
Mkuu
wa mkoa wa Lindi Mh Godfrey Zambi amewaapisha wakuu wa wilaya tano za
mkoa huo na hii ni picha ya pamoja mara baada ya kiapo
————————————
Na Mathias Canal, Lindi
Mkuu
wa mkoa wa Lindi Mh Godfrey Zambi amewaapisha wakuu wa wilaya tano za
mkoa huo huku kila mmoja akiahidi utendaji uliotukuka katika kukabiliana
na changamoto zinazowakabili wananchi husika.
Hafla
hiyo imefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa ambapo mkuu huyo
amewasisitiza viongozi hao kuhakikisha suala la upatikanaji wa madawati
linazaa taswira chanya kwa kuhakikisha madawati yanatimia kama ambavyo
agizo la rais lilitolewa hivi karibuni la kuhakikisha wanafunzi wanaketi
katika madawati pasipo kuwa na mbanano.
Zambi
amewataka wakuu hao wa wilaya kusimamia vyema utekelezaji wa ilani ya
chama cha mapinduzi ccm ili kukamilisha ahadi zilizoahidiwa na rais wa
jamhuri ya muungano wa tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati wa
kampeni zilizoanza Agosti na kumalizika Octoba mawaka jana.
Mkuu
wa Wilaya ya Nachingwea Rukia Akhibu Muwango amesema atasimamia na
kudhibiti suala la watumishi hewa na kulifanya kuwa zoezi endelevu ili
wilaya hiyo iweze kusonga mbele kwa muktadha wa mafanikio ya ajira kwa
vijana na watu wenye elimu lakini nafasi zao zilishikiliwa na watu
wasiokuwa halali (watumishi hewa).
Mkuu
huyo ameahidi kukutana na makundi mbalimbali Wilayani humo ili kupata
picha halisi ya namna hatua zimefikiwa za kuhakikisha wanafunzi wanasoma
kwa ufanisi mkubwa namafanikio zaidi kwa maana ya kufauli na kufikia
mpaka chuo kikuu.
Muwango
amesema amekuwa mtumishi erikali kwa muda mrefu hivyo kwa kiasi kikubwa
anazifahamu changamoto za wananchi hususani matatiuzo ya upatikanaji wa
maji, afya, elimu na miundombinu.
Wilaya
ya lindi ni moja kati ya wilaya zilizopo mkoani lindi zinazojihusisha
zaidi na kilimo kuliko masomo Muwango amesema kuwa atahakikisha
anaanzisha kamati ya maendeleo ya Elimu ya wilaya ambapo Kamati hiyo
itakuwa na wataalam na watu maarufu wa Wilaya ya Nachingwea na kamati
hiyo itajiwekea mikakati ya uboreshaji Elimu, hivyo mkuu wa Wilaya
atatashirikiana na wataalamu wa Halmashauri kuona mikakati hiyo
inafanikiwa.
Pamoja
na hayo mkuu huyo pia amesema kuwa anataraji kuanzishaTuzo ya Mkuu wa
wilaya kwa wanafunzi watakaofanya vizuri kila kata ambapo Vigezo
watakubaliana na kamati hiyo.
Wakuu
wa Wilaya wengine walioapishwa katika hafla hiyo ni pamoja na mkuu wa
Wilaya ya Ruangwa Joseph Joseph Mkirikiti, Mkuu wa Wilaya ya Liwale
Sarah Vicent Chiwamba, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga, Mkuu wa
Wilaya ya Kilwa Christopher Emil Ngumbiagai
MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YANUNUA 620 KWENYE KILELE CHA SHEREHE ZA MIAKA 5 YA KUZALIWA KWA GS1 NA KUADHIMISHA SIKU YA TWCC
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizindua kampeni ya NUNUA 620 (msibomilia)
katika ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa wengine pichani ni Mwenyekiti wa
Bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara na Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (kushoto) kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa jijini Dar es Salaam
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye bango la GS1 mara baada ya kuzindua
kampeni ya NUNUA 620 kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania Bi. Fatma Kange .
Wanawake
kutoka Majukwaa mbali mbali ya Wanawake nchini wakishangilia kwa
kujumuika na Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan (katikati) baada ya kuzindua kampeni ya NUNUA 620
kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa wakati maonyesho ya 40 ya Biashara
ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimsikiliza Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles
Mwijage wakati wa kutembelea maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa
maarufu kama Sabasaba.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiangalia moja ya jiko lililotengenezwa Tanzania na rafiki wa
mazingira wakati alipotembelea mabanda mabali mbali kwenye maonyesho ya
40 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiangalia kabati lililotengenezwa kwa mbao ya mnazi wakati
alipotembelea moja la banda la wajasiriamali kuotoka Zanzibar wakati wa
maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba jijini
Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumzana fundi wa kushona nguo mwenye ulemavu wa macho (asiyeona)
ambaye anafahamika kama Mtaalamu wa kushona Tanzania Ndugu Abdallah
Nyangalio, kulia ni Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles
Mwijage wakati wa maonyesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es
salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiangali moja ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wanawake
wakati wa maonyesho ya kimataifa ya biashara
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiangalia ubunifu wa hali ya juu ya gauni la kanga kwenye moja ya
mabanda ya wajasiamali wa Kitanzania wakati wa maonyesho ya 40 ya
Biashara ya Kimataifa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiongozana na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna
Mkapa
NAIBU SPIKA, DKT. TULIA ACKSON AFUNGUA KIKAO CHA UONGOZI CHA CHAMA CHA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA AFRIKA
(Picha na Ofisi ya Bunge)
Jumuiya Shia Wamkabidhi Madawati Rais Dk.Shein
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Mohamed
Raza Daramsi wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na
Viongozi na Mashekhe wa jumuiya hiyo kwa ajili ya kukabidhi msaada wa
madawati 100 kwa ushirikiano na familia ya Rais wa Jumuiya,msaada huo
utaowanufaisha wanafunzi wa Skuli mbali mbali za Zanzibar
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma akitoa shukurani kwa
Uongozi wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir wakati ulipofika Ikulu
Mjini Zanzibar leo kukabidhi madawati 100 kwa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia)
ikiwa ni katika kuimarisha sekta ya Elimu hapa Zanzibar
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(wa pili kulia) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mashekhe wa Jumuiya
ya Khoja Shia Ithna-asheir (kulia) Sheikh Shaaban Hussein,Sheikh
Maulana Dhishan Haidar na Rais wa Jumuiya hiyo Mhe, Mohamed Raza
(kushoto) wakati walipofika ikulu Mjini Zanzibar kukabidhi msaada wa
madawati 100 kawanafunzi wa Zanzibar,
Rais
wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Raza (kushoto) akitoa maelezo
kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
Mohamed Shein (kulia aliyekaa) wakati Jumuiya hiyo ilipofika Ikulu Mjini
Zanzibar leo kukabidhi madawati 100 kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar
ikiwa ni katika katua za kuimarisha sekta ya Elimu nchini.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(wa pili kulia)akikabidhiwa madawati 100 kutoka kwa Viongozi wa jumuiya
ya Khoja Shia Ithna-asheir na familia ya Rais wa Jumuiya hiyo Mohamed
Raza walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,msaada huo kwa ajili ya
wanafunzi wa Zanzibar,
[Picha na Ikulu.]
———————————————
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
amesema kuwa nia na malengo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika
kuimarisha sekta ya elimu ni makubwa hivyo kujitokeza kwa wanannchi na
taasisi mbali mbali kuiunga mkono sekta hiyo ili izidi kuimarika ni
jambo la faraja.
Dk.
Shein aliyasema hayo wakati wa mazungumzo kati yake na viongozi na
Masheikh wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir wakiongoza na Rais wa
Jumuiya hiyo Mohammed Raza waliofika Ikulu mjini Zanzibar kumkabizi Rais
msaada wa madawadi yaliotolewa na uongozi huo pamoja na familia ya Rais
wa Jumuiya hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar.
Katika
maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
inathamini na imekuwa ikichukua juhudi za makusudi katika kuhakikisha
sekta ya elimu inaimarika na ndio maana Rais wa Kwanza wa Zanzibar mara
baada ya ukombozi alitangaza elimu bure.
Dk.
Shein alisema kuwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Zanzibar
ina historia kubwa ya elimu ya dini na dunia kwani ndio nchi iliyokuwa
ya mwanzo kuwa na elimu ya dini mnamo miaka 1890 na elimu ya dunia
kuanzia mwaka 1905 kwa kuanzisha skuli licha ya kuwa elimu hiyo ya dunia
waliipata watu wachache.
“Tumefarajika
sana, tunajiona hatupo peke yetu tupo na wenzetu katika kulitafutia
ufumbuzi suala hili, madawati ni muhimu kwa ajili ya wanafunzi
wetu…..ipo siku Zanzibar itakuwa haina shida ya madawati” alisema Dk.
Shein.
Aidha,
Dk. Shein alieleza kufarajika kwake na mwanzo mzuri uliooneshwa na
Jumuiya hiyo pamoja na familia ya Mohamed Raza kwa kutoa mchango wa
madawati hayo ambayo yatasaidia katika kuimarisha sekta ya elimu hapa
nchini kwa kuwasaidia wanafunzi kupata vikalio vya uhakika maskulini.
Mapema
Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Zanzibar, Mohammed Raza
alimueleza Dk. Shein kuwa Jumuiya yake imetoa msaada wa madawati 50 na
mtoto wake Hassan Mohammed Raza ametoa madawati 50 yenye thamani ya Tsh.
milioni 12 kwa ajili ya wanafunzi wa skuli za Zanzibar huku akiahdi
kuwa misaada hiyo itakuwa endelevu.
Katika
maelezo yake Raza alisema kuwa msaada huo una lengo la kuunga mkono
azma ya Dk. Shein ya kuhakikisha suala la upatikanaji wa madawati
linapatiwa ufumbuzi hapa nchini hali ambayo ilimpelekea Rais kuunda
Kamati ya Kitaifa ya watu 12 ikiongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria
ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Haroun Ali Suleiman.
Rais
huyo wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir ambaye pia ni Mwakilishi wa
Jimbo la Uzini alisema kuwa Jumuiya yake itaendelea kutoa misaada katika
sekta zote za maendeleo ikiwemo elimu, afya na nyenginezo huku akiahidi
kuwa atahakikisha kwa kushirikiana na Waziri wa Elimu anachukua juhudi
kusafiri hadi nje ya Zanzibar kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi suala
hilo.
Nao
Masheikh kutoka Jumuiya hiyo wakiongozwa na Sheikh Maulana Dhishan
Haidar walitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Dk. Shein kwa uongozi wake
mahiri sambamba na juhudi zake za kuendelea kusimamia amani na utulivu
hapa Zanzibar.
Viongozi
hao walieleza azma yao ya kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar pamoja na kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Shein katika
kuimarisha sekta mbali mbali hapa nchini.
“Zanzibar
imeweza kupata maendeleo…watu wake wanapendana….amani na utulivu
umeimarika kwa kiasi kikubwa haya yote yanatokana na uongozi bora wa Dk.
Shein”,alisema Maulana Haidar.
Nae
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma alitoa pongezi na
shukurani kwa Jumuiya na Familia ya Mohammed Raza kwa kutoa msaada huo
wa madawati ambayo yatawasaidia wanafunzi wa hapa Zanzibar katika kuweza
kujipatia elimu bora kwa ufanisi zaidi.
Waziri
Pembe alisema kuwa Wizara kwa upande wake inatoa shukurani kubwa na
inathamini mchango huo na kueleza kuwa kwa vile Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar ina nia nzuri juu ya jambo hilo anamatumaini makubwa kuwa
mafanikio yatapatikana.
Waziri
huyo wa Elimu alitumia fursa hiyo kupongeza juhudi zinazochukuliwa na
Dk. Shein katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo sekta
ya elimu na kuwaomba wananchi na taasisi nyengine kuendelea kutoa
michango yao ya vifaa hivyo kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar.
Hivi
karibuni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliwasilisha rasimu ya
uchangiaji na upatikanaji wa madawati maskulini ili kuweza kupunguza
upatikanaji wa madawati katika skuli za Zanzibar katika Baraza la
Wawakilishi.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
PPF YAIBUKA KIDEDEA KUNDI LA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII MAONYESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM 2016
Rais
wa Rwanda Paul Kagame, (wapili kulia) akiwa na mwenyeji wake Rais John
Pombe Magufuli, (wakwanza kulia), akimkabidhi tuzo ya msindi wa kwanza
kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na makampuni ya Bima, Mkurugenzi
Mkuu wa PPF, William Erio, wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya 40 ya
Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 1, 2016. Wapili kushoto ni Waziri wa
Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.
AHEAD AFRICA SOLUTION WASHIRIKI MAONESHO YA SABASABA
Afisa
Masoko wa Kampuni ya AHEAD AFRICA SOLUTION, Bi Zainabu Juma
akimuelekeza mmoja wa wananchi jinsi yakutumia moble application mpya
wakati wa Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.
Kwa mujibu wa Bi,Zainabu amesema hodi ni mtandao mpya kwaajili ya kutangaza biashara na kupata matukio mbalimbali.
Alisema mtu yoyote anaweza akaingia katika simu yake akajisajili kwakuandika
Maafisa
wa Kampuni ya AHEAD AFRICA SOLUTION wakiwa kwenye picha ya pamoja
Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja
vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.
MADC WAPYA MKOANI TANGA WATAKIWA KUSIMAMIA SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA UMAKINI MKUBWA
Mkuu wa wilaya mpya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella leo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi |
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Mhandisi Mwanaisha Rajabu akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martne Shigella |
Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Abdallah Issa akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga leo. |
Mkuu wa wilaya Mpya wa Handeni Mkoani Tanga,Godwin Gondwe akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella |
Msama awatahadharisha wauza CD Feki
Na Mwandishi Wetu
———————–
KAMPUNI
ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam imewatahadharisha wanaouza
kazi feki za wasanii mbalimbali hapa nchini kuachana na mfumo huo kwa
sababu kuanzia mwezi huu watawakamata wanaofanya biashara hiyo ndani ya
mwezi mmoja.
Akizungumza
jana, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alisema wametoa siku
30 kwa wanaofanya biashara hiyo kuachana nayo kabla hawajawashukia.
“Tunatoa
siku 30 kwa wanaofanyabiashara ya kazi feki za wasanii, hiyo biashara
waachane nayo kwa sababu inapoteza pato la Taifa,” alisema Msama.
Msama
alisema kwa kuanzia watapita nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa na mkoa
kwa mkoa ili kusaka computer zinazotumika kuiba kazi za sanaa.
Msama
alisema ili kufanikisha kazi hiyo wanashirikiana na Jeshi la Polisi,
Wizara ya Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo sambamba na Kampuni ya
Msama Promotions ili kufanikisha zoezi hilo ambalo litakuwa ni la
kusafisha tatizo hilo.
Aidha Msama alisema ili kukomesha zoezi hilo wakikuta kazi feki kwenye duka wanabeba mzigo mzima wa kazi za sanaa.
Naye
Inspekta Jenera wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu alisema jamii inatakiwa
kutoa ushirikiano na Polisi katika jambo hilo ambalo linaumiza nguvu
kazi ya Taifa.
IGP
Mangu alisema wananchi wanatakiwa kutoa taarifa kwa Polisi ili kazi
ifanyike inavyotakiwa kwa lengo la maendeleo ya wasanii ambao wanasaka
namna ya kuendeleza maisha yao.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame akabidhi tuzo kwa washindi Sabasaba
Rais
wa Rwanda, Paul Kagame (wa pili kulia) akimkabidhi tuzo ya Mshindi wa
Tatu Sekta ya Mawasiliano na Tehama (ICT) Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni
ya Simu Tanzania (TTCL), Prof. Tolly Mbwette (kushoto) kwenye maonesho
ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba
jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli
na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage (wa pili kushoto)
———————————————————
Na. Immaculate Makilika, MAELEZO
RAIS
wa Serikali ya Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame amewakabidhi tuzo kwa
Wizara, taasisi za Serikali, kampuni, nchi washiriki pamoja na mashirika
yaliyoshinda katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa.
Rais
Paul Kagame alikabidhi tuzo hizo jana, wakati alipokuwa akifungua
maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Mwl Nyerere
maarufu kama Sabasaba, vilivyopo katika barabara ya Kilwa jijini Dar es
salaam.
Wizara
na taasisi za Serikali, kampuni pamoja na mashirika mbalimbali
yalishiriki maonesho hayo kwa kushindana katika kuonesha bidhaa bora na
kueleza huduma nzuri wanazotoa, ambapo baadae Rais Paul Kagame
aliwakabidhi washindi hao tuzo mbalimbali.
Baadhi
ya washindi hao walioganywa katika makundi mbalimbali ni pamoja na,
kundi la bidhaa za kilimo nafasi ya mshindi wa tatu ilishikwa na
kampuni ya farm equip Tanzania limited, nafasi ya mshindi wa pili
ilishikwa na kampuni Asas dairies na nafasi ya mshindi wa kwanza
ilishikwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA
JKT).
Katika
kundi la usindikaji wa vyakula na huduma za vinywaji, nafasi ya mshindi
wa tatu ilishikwa na kampuni ya Bakhresa Group, ikifuatiwa na kampuni
ya P&P, na nafasi ya mshindi wa kwanza ilishikwa na kampuni ya
Afri tea and coffe blenders limited.
Kwa
upande wa taasisi za kifedha, nafasi ya mshindi wa tatu ilishikwa na
benki ya TIB, ikifuatiwa na Benki ya CRDB huku Benki Kuu ya Tanzania
(BOT) ikishika nafasi ya kuwa mshindi wa kwanza. Vilevile katika kundi
la Mifuko ya hifadhi ya jamii nafasi ya mshindi wa tatu ilishikwa na
mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF, nafasi ya mshindi wa pili
ilishikwa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF na nafasi ya mshindi wa kwanza
ikiwa ni Mfuko wa Pensheni wa PPF.
Kwa
upande wa nchi za kigeni zilizoshiriki maonesho hayo ya 40 tuzo
zilienda kwa nchi za Rwanda iliyoshika nafasi ya mshindi wa tatu,
Ujerumani ikishika nafasi ya mshindi wa pili huku nafasi ya mshindi wa
kwanza ikiwa ni nchi ya Afrika Kusini. Aidha, washindi wa jumla
walioshiriki katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Sabasaba
ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kilichoshika nafasi ya mshindi
wa tatu , ikifuatia Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja Chuo cha Cha
Ufundi Stadi (VETA) kilichoshika nafasi ya mshindi wa kwanza.
Baada
ya kuwakabidhi tuzo hizo na kufungua rasmi maonesho hayo ya 40 ya
biashara ya kimataifa Rais Kagame alitoa wito kwa washiriki wa maonesho
hayo ya 40, kushirikiana ili kubuni mawazo mapya ya biashara ikiwa ni
pamoja na kutambua fursa zilizopo katika soko la pamoja la Jumuiya ya
Afrika ya Mashariki, katika kukuza biashara zao na kusaidia ukuzaji wa
uchumi wa pamoja katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
CCM Z’BAR YAENDELEA KUFANYA UHAKIKI WA MALI ZAKE.
Na Is-haka Omar, Zanzibar.
——————–
CHAMA
cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewataka wananchi wanaoishi katika
maeneo yanayomilikiwa na chama hicho kuhakikisha wanafunga mikataba
rasmi ili kuepuka usumbufu wakati maeneo hayo yatakapohitajika kwa
ajili ya shughuli za kichama.
Kimesema
kuna baadhi ya wananchi waliopewa maeneo ya kuishi kwa muda kwa nia ya
kuwasaidia na badala yake wameyageuza kuwa makaazi yao ya kudumu jambo
ambalo sio sahihi.
Akizungumza
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ndg. Vuai Ali Vuai kwa nyakati
tofauti katika mwendelezo wa ziara ya kuhakiki mali na maeneo mbali
mbali yanayomilikiwa na CCM huko Mbweni Mkoa wa Magharibi Kichama.
Alisema
chama kinaendelea na zoezi la kuhakiki mali zake kutokana na kuongezeka
kwa vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa
waaminifu wanaotengeneza hati na mikataba bandia ya kujimilikisha mali
za chama hicho kinyume na utaratibu.
Ndg.
Vuai alifafanua kwamba katika hatua za kupunguza kero hizo chama
kimeamua watu wote ambao wamepewa kibinadamu sehemu za kuishi ama
kufanya biashara kwa muda katika maeneo yanayomilikiwa na CCM wafunge
mikataba rasmi ili chama kiweze kunufaika na rasilimali zake.
“
Watu waliopewa kwa dharura sehemu za kuishi na kufanya biashara kama
hatujawapa mikataba rasmi inayotambulikana kisheria, ambayo ni
kielelezo cha kumtambulisha nani mmiliki halali wa maeneo hayo baadae
inaweza kuwa fursa ya kufanya utapele na kusababisha usumbufu na lawama
kwa chama.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA ZIARA YA RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wakati wa dhifa ya Kitaifa
aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Rwanda Paul Kagame akizungumza na wageni mbalimbali katika dhifa ya
kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Waziri Mkuu mstaafu Salim Ahmed Salim Ikulu jijini Dar es Salaam
mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa
Rwanda Paul Kagame.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi Ikulu jijini
Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa
aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akijadiliana jambo na Mawaziri wakuu wastaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba
na Salim Ahmed Salim Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya
kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul
Kagame, Kulia ni mke wa Rais Mama Janeth Magufuli.
Kijana
Omar Abdalah Ramadhan akimsalimia kwa furaha Rais Dkt. John Pombe
Magufuli katika viwanja vya maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kijana
Omar Abdalah Ramadhan akimsalimia kwa furaha mama Janeth Magufuli mara
baada ya Rais wa Rwanda Paul Kagame kuondoka kwenye viwanja vya maonesho
ya sabasaba jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YANYAKUA TUZO MBILI KATIKA MAONESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM 2016 – SABASABA
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi
(katikati) akikabidhi tuzo mbili za ushindi ilizoshinda Wizara yake
katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwa
viongozi wa Kamati ya Maonesho ya Wizara hiyo jana tarehe 01 Julai, 2016
katika viwanja vya Sabasaba. Tuzo hizo ni Mshindi wa Kwanza katika
kundi la Wizara na Taasisi za Serikali na Mshindi wa pili katika kundi
la Mshindi wa Jumla wa Maonesho hayo. Tuzo hizo zilikabidhiwa na Rais wa
Rwanda Mhe. Paul Kagame aliyekuwa Mgeni Rasmi akiongozana na mwenyeji
wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa tano
kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waoneshaji wa Wizara yake muda
mfupi baada ya kupokea tuzo mbili za ushindi katika Maonesho
ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam jana tarehe 01 Julai,
2016 katika viwanja vya Sabasaba. Tuzo hizo ni Mshindi wa kwanza katika
Kundi la Wizara na Taasisi za Serikali na Mshindi wa Pili katika Kundi
la Mshindi wa Jumla.
Baadhi
ya Waoneshaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakifurahia ushindi wa
tuzo hizo. Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii ni moja ya mabanda
yanayovutia zaidi katika Maonesho ya Sabasaba ya mwaka huu 2016, kwa
kuwa na mchanganyiko wa mambo mbali mbali yanayoelimisha kuhusu uhifadhi
wa Maliasili, Malikale na Utalii. Katika banda hilo zipo pia fursa za
kuwaona wanyama hai kama vile Simba, Nyati, Chui, Mamba, Ndege
mbalimbali n.k. Kwa upande wa Utalii wa Ndani zipo fursa za kutembelea
hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa gharama nafuu ya Tsh. 10,000 kwa watoto
na Tsh. 20,000 kwa watu Wazima ikiwa ni nauli ya kwenda na kurudi, Aidha
kwa wale watakaopenda kulala itawagharimu Tsh. 50,000.
Baadhi ya Waoneshaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakifurahia tuzo hizo katika banda la Wizara hiyo.
Taswira ya tuzo hizo.
(Picha na Hamza Temba – Wizara ya Maliasili na Utalii)
MKURUGENZI MKUU NSSF AJIONEA MIRADI YA SHIRIKA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA 2016
Muonekano
wa Banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), katika
Maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.
Ofisa Masuala ya Bima wa NSSF, Peter Isack akitoa ufafanuzi kwa kuhusu majukumu ya kitengo chake kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kushoto), wakati mkurugenzi huyo alipotembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Sabasaba.
Ofisa Uwekezaji wa NSSF, Moringe Nyerere akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kushto), juu ya viwanja vinavyouzwa na NSSF vilivyopo eneo la Kiluvya.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Prof. Godius Kahyarara (kulia), akiangalia michoro ya nyumba ambayo ni
sehemu ya miradi ya shirika hilo. Wa pili kulia ni Ofisa Uwekezaji wa
NSSF, Moringe Nyerere.
Msimamizi wa Mradi wa Mtoni Kijichi, Mohames Kimbe akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (wa pili kulia), kuhusu mradi wa nyumba za Kijichi. Kulia ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Salim Kimaro na Juma Kintu kutoka Idara ya Uhusiano.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (wa pili kulia), akiangalia mradi wa Mtoni Kijichi.
Ofisa Mauzo wa NSSF, Abbas Ramadhan akitoa maelezo kuhusu mradi wa nyumba wa Kijichi.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi, Salim Kimaro (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa NSSF, Aman Marcel wakimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara kifaa maalum kinachotumiwa na wanachama kutoa maoni yao kuhusu huduma zinazotolewa na shirika hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda la NSSF.
Ofisa wa Masuala ya Bima
TTCL Yatwaa Ushindi wa Tatu Sekta ya Mawasiliano na Tehama
Rais
wa Rwanda, Paul Kagame (wa pili kulia) akimkabidhi tuzo ya Mshindi wa
Tatu Sekta ya Mawasiliano na Tehama (ICT) Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni
ya Simu Tanzania (TTCL), Prof. Tolly Mbwette (kushoto) kwenye maonesho
ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba
jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli
na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage (wa pili kushoto)
Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (kulia) akipata
maelezo kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa TTCL wanaoshiriki kwenye
maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere
sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kulia
ni baadhi ya wateja na wageni anuai wanaotembelea banda la kampuni ya
Simu Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara
viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kulia
ni baadhi ya wateja na wageni anuai wanaotembelea banda la kampuni ya
Simu Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara
viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (kulia) akipata maelezo
kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa TTCL wanaoshiriki kwenye maonesho ya
40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini
Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wakipiga picha na kufurahia
tuzo mbili walizozitwaa katika kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya
Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wakipiga picha na kufurahia tuzo
mbili walizozitwaa katika kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara
viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam. Pamoja na
Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Prof. Tolly Mbwette (kulia)
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wakipiga picha na kufurahia
tuzo mbili walizozitwaa katika kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya
Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu ala kiapo
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu ala kiapo cha kuitumikia
Wilaya hiyo kwa uadilifu, ubunifu na utu kwa kila mwananchi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu
Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng Methew Mtigumwe akiwa na wakuu wa wilaya wapya wa mkoa huu baada ya kuapishwa.
…………………………………..
Na matias cana,singida
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu ala kiapo cha kuitumikia
Wilaya hiyo kwa uadilifu, ubunifu na utu kwa kila mwananchi, Kiapo hicho
kimejidhihirisha mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng Methew Mtigumwe.
Muda mchache baada ya kiapo hicho mkuu huyo ameshiriki hafla fupi ya
kukaribishwa na Chama Cha Mapinduzi katika ofisi za Chama hicho katikati
ya mji wa Singida.
Mtaturu
amesema kuwa ana dhamira ya dhati kuhakikisha wananchi wanapata
maendelea shirikishwa hususani katika kuimarisha sekta ya elimu, afya,
miundombinu na kukemea Rushwa ambayo inarudisha nyuma Taifa.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa Mtaturu amesema kuwa
ushirikiano baina ya serikali na wananchi wa Ikungi itakuwa turufu kubwa
katika kuhakikisha wilaya inakomaa zaidi kimaendeleo.
“Naenda
kusaidiana nao ili kuhakikisha wilaya ina komaa zaidi kimaendeleo na
watu wake kuondokana na uduni wa kipato walionao wananchi, wananchi wana
uwezo wa kufuga na kulima vizuri jambo ambalo linaashiria kuwaondoa
wananchi kwenye wimbi la umasikini”
Amesema
Mtaturu Kuhusu wananchi wa Ikungi kukataa kuchangia shughuli za
maendeleo kufuatia pingamizi lilichagizwa na mbunge wa jimbo hilo
Mtaturu amesema kuwa Utaratibu wa kuchangia maendeleo upo katika dunia
nzima nchi mbalimbali za ulaya na kwingineko zimekuwa zikichangia
shughuli za maendeleo nchini Tanzania kwa ajili ya wananchi masikini
lakini wananchi
tunaosaididiwa kuondokana na wimbi hilo tunapaswa pia kuchangia shughuli za
maendeleo.
tunaosaididiwa kuondokana na wimbi hilo tunapaswa pia kuchangia shughuli za
maendeleo.
Amesema
wananchi wa Ikungi hawapaswi kutumika kisiasa huu ni muda,wa kufanya
kazi ili tusikubali maendeleo yetu kurudishwa nyuma na wanasiasa au watu
wachache wenye mtazamo wa kisiasa zaidi kuliko maendeleo.
“Huko
nyuma kulikuwa na watu wanajitolea kufanya shughuli za mikono kwa
kuchangia mawe, tofali au mchanga hivyo mchango huo ulikuwa muhimu zaidi
japo asilimia kubwa ya watanzania wanadhani mchango ni pesa pekee”
Ameongeza
Mtaturu Katika halfa hiyo pia Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng Methew
Mtigumwe amemuapisha mkuu wa Wilaya ya Mkalama Bw Jackson Jonas Masaka,
Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw Elius Chollo John Tarimo, na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Bw Emmanuely Jumanne Luhahula
Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw Elius Chollo John Tarimo, na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Bw Emmanuely Jumanne Luhahula
Aidha
mkuu wa Wilaya ya Manyoni hakuapishwa kutokana na kuwa nje ya nchi
kikazi tangu alipoteuliwa. Katika hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa Singida
amewataka wakuu wote wa Wilaya walioapishwa kuhakikisha wanasimamia
vizuri
katiba na sheriaza nchi sawia na kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka
2015-2020.
katiba na sheriaza nchi sawia na kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka
2015-2020.
“Nawaomba mkasimamie uadiligu, uaminifu, kufanya kazi kwa
weledi na kuhakikisha wanapinga rushwa kwa nguvu zote, lakini nataka
niwakumbushe hadi kufikia jana tarehe 30 Hakuna Halmasahauri ambayo imefanikiwa
kukusanya mapato na kufikia asilimia 80 hivyo nendeni mkahakikishe watu
wanalipa kodi stahiki ili kukuza pato la kila wilaya na kunusuru Halmashauri
zetu kufutwa”
weledi na kuhakikisha wanapinga rushwa kwa nguvu zote, lakini nataka
niwakumbushe hadi kufikia jana tarehe 30 Hakuna Halmasahauri ambayo imefanikiwa
kukusanya mapato na kufikia asilimia 80 hivyo nendeni mkahakikishe watu
wanalipa kodi stahiki ili kukuza pato la kila wilaya na kunusuru Halmashauri
zetu kufutwa”
Amesema Mtigumwe Mkuu huyo Amewapongeza wadau mbalimbali katika
Wilaya hiyo kwa kujitolea kuchangia madawati elfu arobaini mpaka sasa na
kuubakisha mkoa huo ukiwa na upungufu wa madawati kati ya 1500 katika mkoa huo.
Imetolewa na Ofisi ya muda ya Mkuu wa Wilaya (Ikungi) Julai 1, 2016
Wilaya hiyo kwa kujitolea kuchangia madawati elfu arobaini mpaka sasa na
kuubakisha mkoa huo ukiwa na upungufu wa madawati kati ya 1500 katika mkoa huo.
Imetolewa na Ofisi ya muda ya Mkuu wa Wilaya (Ikungi) Julai 1, 2016
POLISI, WANANCHI RASMI KATIKA MAPAMBANO
Mkuu
wa Polisi wilaya ya Arusha (SSP) Emmanuel Tille akiongea na viongozi wa
kata ya Moivaro tarafa ya Suye pamoja na askari wa vikundi vya ulinzi
shirikishi wakati wa uzinduzi wa vikundi vinne vya kata hiyo.
Diwani
wa kata ya Moivaro Rick Moiro akiongea na askari wa vikundi vya ulinzi
shirikishi toka kwenye baadhi ya mitaa ya kata yake mara baada ya
uzinduzi wa vikundi hivyo.
Mkuu
wa Polisi wilaya ya Arusha (SSP) Emmanuel Tille akiwakagua askari wa
vikundi vya ulinzi shirikishi kutoka mitaa ya Ngurumausi, Oldonyommasi,
Moivaro Kati na Shangarao.
Baadhi
ya viongozi wa kata ya Moivaro pamoja na askari wa vikundi vipya vya
ulinzi shirikishi wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Polisi wilaya ya
Arusha (SSP) Emmanuel Tille hayupo pichani.
Mmoja
wa wahitimu wa askari wa ulinzi shirikishi katika kata ya Moivaro
akikabidhiwa kitambulisho cha kazi kutoka kwa Mkuu wa Polisi wilaya ya
Arusha (SSP) Emmanuel Tille.
—————————
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Ikiwa jeshi la Polisi linaendeleza
harakati za kupambana na uhalifu ili kupunguza matukio ya namna hiyo,
wananchi wa kata ya Moivaro tarafa ya Suye halmashauri ya jiji la Arusha
hawapo mbali na jitihada hizo hivyo kuamua kujitokeza kwa moyo mmoja
kupinga uhalifu kwa kuanzisha vikundi vinne vya ulinzi shirikishi kutoka
mitaa ya Ngurumausi, Oldonyommasi, Moivaro Kati na Shangarao.
Akizindua vikundi hivyo ambavyo
vimewezeshwa na wadau walioongozwa na Jeff Mligha ambao walijitolea
vifaa mbalimbali vya ulinzi zikiwemo tochi, Mkuu wa Polisi wilaya ya
Arusha Mratibu Mwandamizi wa Polisi Emmanuel Tille kwa niaba ya Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha alisema kwamba matarajio ya wananchi katika
kata hiyo ya Moivaro ni makubwa na ana imani watakuwa wanalala na kuamka
salama hivyo kuwataka walinzi hao wawe na nidhamu kwenye kazi yao.
“Kazi ya ulinzi ina miiko yake;
kitu cha kwanza ni nidhamu ya hali ya juu. Mimi mwenyewe mpaka nafikia
hatua hii ni kwa sababu ya nidhamu na nawataka ninyi muige mfano wangu,
ninachosema hapa ni pamoja na kuwahi kazini, kutunza siri pasipo
kuwazunguka wenzako pamoja na kufuata maelekezo ya wakubwa wa vikundi
vyenu” Alisisitiza Tille.
Alisema japokuwa askari hao
wapatao 42 wamepewa mafunzo lakini kupitia Wakaguzi wa Polisi wa Tarafa
na askari kata wataendelea kuwapa mafunzo mara kwa mara ili waweze
kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria, huku akiwaonya wasijichukulie
sheria mkononi.
Aliwataka wananchi wanapopata
taarifa watoe kwa viongozi wa Polisi mara moja ili ziweze kufanyiwa kazi
kwa haraka na hatimaye kufikia malengo ya kupunguza uhalifu ndani ya
jiji la Arusha, huku akiwataka watendaji wa kata na Wakaguzi wa tarafa
wahakikishe askari wa kata wanakuwa katika maeneo yao kila siku hali
ambayo itawasaidia kubaini maeneo tete.
Akiongea katika uzinduzi huo
Diwani wa kata hiyo Rick Moiro alivitaka vikundi hivyo kufuata taratibu
za kazi na kupambana na uhalifu hasa vijana wanaojihusisha na madawa ya
kulevya aina ya bangi huku akiomba Jeshi la Polisi litoe ushirikiano wa
karibu na vikundi hivyo pindi tu wanapoomba msaada.
Naye Afisa Mtendaji wa kata hiyo
Bi. Editha Kisangia alisema kwamba mbali na hali ya uhalifu kuwa ya
kawaida katika eneo hilo lakini hatarajii kutokea kwa changamoto kutoka
kwa baadhi ya wananchi kushindwa kuchangia vikundi hivyo kwani faida
wataiona baada ya kuanza kufanya kazi.
Wakaguzi wa Polisi wanaoongoza
tarafa tatu za halmashauri ya jiji la Arusha toka mwaka 2013 ni pamoja
na Frimina Massao tarafa ya Suye, Winibrita Moshi tarafa Elerai na
Shabani Shabani tarafa ya Themi.
PPF YAIBUKA YAIBUKA KIDEDEA KUNDI LA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII
Rais
wa Rwanda Paul Kagame, (wapili kulia) akiwa na mwenyeji wake Rais John
Pombe Magufuli, (wakwanza kulia), akimkabidhi tuzo ya msindi wa kwanza
kundi la Mifuko
ya Hifadhi ya Jamii na makampuni ya Bima, Mkurugenzi Mkuu wa PPF,
William Erio, wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar
es Salaam Julai 1, 2016. Wapili kushoto ni Waziri wa Viwanda na
Biashara, Charles Mwijage.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele (wakwanza kulia) akiungana na wafanyakazi
enzake kusherehekea tuzo ambayo Mfuko umepata wakati wa uzinduzi wa
maonyesho hayo ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.
Afisa wa PPF anayeshughulikia huduma kwa Wanachama Mohammed Siaga,akionyesha tuzo hiyo
Wafanyakazi wa PPF wakishangilia ushindi huo mbele ya banda lao
Kikundi cha sarakasi cha Butterfly charejea kutoka India
Wasanii
wa Kikundi cha Butterfly Arts Group kilichokuwa kinafanya maonesho ya
sarakasi nchini India, Kulia ni kiongozi wa kikundi hicho Selemani
Pembe, Mwanaidi Abdallah, Abdallah Mkumba<hamidi Mbwana na Salem
Mbugio.
——————————————————–
Na Mwandishi wetu
KIKUNDI cha sarakasi cha Butterfly Arts Group kimerejea nchini juzi kutoka India kufanya maonesho ya sanaa ya sarakasi.
Katibu wa kikundi cha Butterfly
Arts Group, Selemani Pembe alisema jana Dar es Salaam kuwa katika ziara
yao ya kikazi nchini India iliyodumu kwa mwaka mmoja ilikuwa na
mafanikio makubwa ambapo wasanii wote sita wa kikundi hicho wamepata
mafunzo ya kutosha ya kufanya maonesho ya sarakasi.
Pembe ambaye pia ni mwalimu wa
Sarakasi nchini aliyewahi kuongoza vikundi vya sanaa vya DDC Kibisa,
Muungano Culture Troup, Makutano Dancing Troup, Ujamaa Ngoma Troup
alisema katika kipindi chote cha kuonesha sanaa ya sarakasi wamegundua
kuna utofauti mkubwa kati ya sanaa za maonesho za Tanzania na India.
Alisema wacheza sarakasi wa India
wanatumia vifaa vya kufunga juu ya jukwaa na kubembea juu kwa juu
tofauti na hapa nchini ambapo hakuna kumbi za kufunga vifaa maalum kwa
ajili ya kuonesha sarakasi hizo.
Pembe alisema pamoja na kasoro
hizo sarakasi ya Tanzania imekubalika sana nchini India hasa staili ya
kujenga maumbo (Pyramid, kujenga minara mbalimbali na kucheza ngoma za
asili.
Alisema maonesho mengine
yanayowavutia wanamichezo nchini India ni mchezo wa Limbo ambao
mwanasarakasi anapita katikati ya moto chini ya bomba maalum ambalo
limewashwa moto mkubwa na mchezo mwingine ni ule wa kupanda bomba kwa
staili mbalimbali mithili ya nyani.
Alisema katika kipindi cha mwaka
mmoja walikuwa wakifanya maonesho na Kampuni ya New Rambo Circus
inachofanya maonesho katika miji mbalimbali nchini India na nchi jirani.
Alisema wakiwa huko walifanya maonesho katika miji ya Pune, Bangalore, Gujirat, Mumbay na miji ya mipakani na nchi ya Nepal.
PBZ YAADHIMISHA MIAKA 50
Mkurugenzi
Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir na Mgeni Rasmin Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Fedha Zanzibar Ndg Ali Khamis, wakijumuika na Wananchi na
Wafanyakazi wa PBZ katika futari ilioandaliwa kuadhimisha Miaka 50 ya
Kuanzishwa kwa PBZ mwaka 1966 2016.iliofanyika katika viwanja vya hoteli
ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar,
Baadhi
ya Wafanyakazi wastaaf wa PBZ wakijumuika katika futari Maalum ya
kusherehekea Miaka 50 ya PBZ wakipata futari katika viwanja vya hoteli
ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Wafanyakazi wa PBZ wakipata futari katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Baadhi
ya Wafanyakazi wastaaf wa PBZ wakijumuika katika futari Maalum ya
kusherehekea Miaka 50 ya PBZ wakipata futari katika viwanja vya hoteli
ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Wafanyakazi wa PBZ wakipata futari katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Wafanyakazi wa PBZ wakipata futari katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Iftar
Maalim ilioandaliwa na PBZ kwa Wateja wao na Wafanyakazi wa PBZ
kusherehekea miaka 50 tangu kuunda kwa Benki hiyo mwaka 1966 -2016
Imetayarishwa na Othman Mapara.Blog. Zanzinews.com
E-mail othmanmaulid@gmail.com.
Waziri UMMY MWALIMU AKUTANA NA UJUMBE WA WANAHARAKATI WA MAENDELEO YA JINSIA NA WATOTO
Ujumbe
wa wanaharakati wa maendeleo ya jinsia na watoto waliokutana na waziri
wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,wa kwanza kushoto ni
mkurugenzi wa TGNP Liliani Liundi,katikati ni Naemy Sillayo toka LHRC na
Janeth Mawinza kutoka WAJIKI
Picha
ya pamoja kati ya Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto,Mhe.Ummy Mwalimu pamoja na Wajumbe hao na viongozi wa
Wizara(Picha na Wizara ya Afya)
———————————————————-
———————————————————-
Na. Catherine Sungura. WAMJW
Serikali
imejipanga kuhakikisha kuwa dhamira ya kufikiwa kwa uwakilishi wa 50
kwa 50 katika ngazi mbalimbali za maamuzi inchini inafikiwa.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na ujumbe wa wanaharakati wa
maendeleo ya jinsia na watoto waliofika ofisini kwake na kufanya nao
mazungumzo
Mhe.Ummy
Mwalimu alisema jitihada zinafanyika kuhakikisha kuwa teuzi mbalimbali
zinahusisha jinsia zote, ikiwa ni pamoja na wajumbe wa bodi mbalimbali
za uongozi wa Idara na Taasisi za Serikali.
“Nitoe
wito wangu kwa Mashirika mbalimbali ya Serikali na Yasiyo ya Serikali
kuzingatia usawa wa jinsia wakati wa teuzi mbalimbali za uongozi wa juu
pamoja na wajumbe wa Bodi”.
Aidha,
amewathibitishia wajumbe hao kuwa serikali ina dhamira ya dhati ya
kuifanyia marekebisho ya Sheria ya Ndoa, “jitihada za maksudi
zinafanyika kuhakikisha marekebisho ya kifungu cha 13 na 17 cha sheria
ya ndoa, kinachoruhusu mtoto chini ya miaka 18 kuolewa vinafanyiwa
marekebisho kwa kuwasilisha muswada Bungeni kabla ya mwaka kuisha.
Hata
hivyo alisema jitihada hizo za kufanya mabadiliko ya sheria zitahusisha
pia sheria ya Mirathi inayomnyima mtoto wa kike na wanawake kurithi
mali.
Akizungumza
kwa niaba ya ujumbe huo wa wanaharakati, mkurugenzi wa Mtandao wa
jinsia Tanzania (TGNP) bi. Liliani Liundi alisema ipo haja ya Serikali
kuongeza nguvu zaidi katika kuhakikisha sheria ya Ndoa kifungu cha 13 na
17 inafanyiwa marekebisho, kwakuwa inarudisha nyuma jitihada za kuleta
usawa wa jinsia nchini.
Aidha,
alieleza kuwa mabadiliko ya Sheria ya Elimu katika kifungu
kinachokataza kuoa / kuoza mtoto wa shule ya Msingi na Sekondari ni
jitihada inayohitaji kuungwa mkono.
“Ipo
haja ya kuongeza nguvu zaidi katika kuwalinda watoto walio nje ya shule,
kwakuwa mabadiliko haya ya sheria ya Elimu yaliyopitishwa na Bunge la
11 yawewaacha nje pasipo ulinzi wa sheria watoto wengi walio nje ya
shule”Alisema.
Ujumbe
wa wanaharakati uliwasilisha maoni yao na changamoto mbalimbali zinazo
ikabili nchi katika kuleta maendeleo ya mtoto na usawa wa jinsia nchini,
ikiwa ni pamoja na suala la Marekebisho ya Sheria ya Ndoa na Nafasi ya
uwakilishi wa mwanamke katika vyombo mbalimbali vya maamuzi. Ujumbe huo
uliongozwa na Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Bibi Lilian Liundi na
Wanaharakati wa Shirika la LHRC, WAJIKI, TANZANIA Widows Association na
shirika la Wanawake katika Jitihada za Kimaendeleo (WAGIC)
Kampuni ya Resolution insurance ltd yafturisha wadau mbali mbali
Mkurugenzi
Mkaazi wa Kampuni ya Resolution Insurance Ltd Oscar Osir akiongea na
wadau mbalimbali(hawapo pichani) kwa ajili ya kuwashukura kwa kuja
katika iftar iliyoandaliwa na kampuni ya Resolution Insurance LTD jijini
Dar es Salaam.
Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam Sheikh Alhadi Musa Bin Salum |
Wafanyakizi wa Resolution Insurance |
Wateja wa kampuni ya Resolution Insurance wakipata iftar |
Wadau mbali mbali wakipata iftar |
Wadau mbali mbali wakipata iftar |
Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam Sheikh Alhadi Musa Bin Salum akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkaazi wa Kampuni ya Resolution Insurance Ltd na Mwenyeketi wa Bodi ya Wakurugenzi Bi.Zuhura Muro |
UCHUNGUZI UNAENDELEA KUBAINI BAWA LA NDEGE LILILOOKOTWA NA WAVUVI KATIKA KISIWA CHA KOJANI PEMBA
Na Masanja Mabula –Pemba
————————–
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga
Tanzania imesema uchunguzi wa kitaalamu bado unaendelea ili kubaini
iwapo bawa la ndege lililookotwa na wavuvi katika Kisiwa cha Kojani
Pemba ni mabaki ya ndege ya Malyasia .
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo
Vallery Luanda Chamlungu ameyabainisha hayo wakati wa makabidhiano ya
bawa hilo yaliyofanyika katika bandari ya Kojani na kushuhudiwa na
Viongozi wa mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya
Wete .
Alisema , pamoja na uchunguzi wa
kitaalamu unaofanywa na mamlaka hiyo , lakini pia Uongozi unaendelea
kuwasiliana na mashirika ya ndege ya kimataifa ya ili kusaidia
kukamilisha machakato wa kutambua asili ya ndege hiyo .
“Uchunguzi bado unaendelea ili
kubaini kwamba bawa hilo ni mabaki ya ndege ya Malyasia iliyopotea miaka
kadhaa iliyopita , tunafanya mawasiliano na mashirika ya ndege ya
kimataifa na hili bawa tunatarajia wenzetu kutoka Malyasia watakuja
”alifahamisha Chamlungu .
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo
alisema wataendelea kushirikiana na wananchi kufanya utafiti hasa
sehemu za baharini sambamba na kuwashukuru wavuvi wa Kojani kwa kuweza
kulihifadhi bawa hilo .
Aidha , Mkuu wa Wilaya ya Wete
Rashid Hadid Rashid akikabidhi bawa hilo aliwataka wananchi
kuwasiliana na vyombo vya ulinzi wanapookota vitu baharini , na kuacha
kuvihifadhi majumbani kwani baadhi vinaweza kuwa ni hatari kwa maisha
yao .
Alisema , Serikali ya Wilaya
ilisimamia ili kuona kwamba bawa hilo linahifadhiwa , na linabaki
katika mazingira yaliyo salama ili kupisha uchunguzi wa kitaalam
ufanyike .
“Pamoja na juhudi zenu , lakini
pia naomba nitoe wito kwa wavuvi kutoa taarifa Serikalini ili kuepisha
utokea kwa madhara yasiyotarajiwa , baada ya kuhifadhi majumbani mwenu ”
alisisitiza Mkuu wa Wilaya.
Mmoja wa mashuhuda waliookota
bawa hilo Chungua Hamad Chungua aliishauri mamlaka ya Usafiri wa Anga
kuwaandalia mazingira mazuri ya kuwapatia mashine ya uvuvi ambayo
itawasaidia katika kazi zao za uvuvi .
Alisema , ni vyema Mamlaka hiyo
kuwazawadia mashine ya supa kumi au kumi na tano kutokana na usumbufu
walioupata wakati wa kulikokota kwani ni zito na bahari ilikuw
aimechafuka .
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Usafiri wa Anga iimekabidhi shilingi milioni mbili wavuvi
waliofanikisha kuliokota na kulihifadhi kama ni zawadi .
Kwa mujibu wa taratibu na sheria
, Mamlaka ya Usafiri wa Anga haina ulazima wa kuwalipa wananchi
wanaokota vitu aidha baharini au nchi kavu , isipokuwa hulazimika kutoka
zawadi ili kuwajenga imani wananchi ya kuvihifadhi vitu wanavyo viokota
Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa yaendelea na uhakiki wa Vyama Nchini.
Mhasibu
kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw.Willium Brown Nyamtiga
akisisitiza jambo kwa viongozi wa Chama cha Alliance for Democratic
Change (ADC) Jana wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za
chama hicho zilizopo Jijini Buguruni Dar es salaam .
Zoezi la uhakiki wa utekelezaji
wa masharti ya usajili wa Vyama va Siasa kwa upande wa Tanzania Bara
linaendelea .Tayari vyama 18 vimekwishakuhakikiwa. Vyama vinne
vinatarajiwa kuhakikiwa Julai 4. Zoezi hili ni zoezi la kawaida na
endelevu ambalo hufanyika kila mwaka ili kupima endapo vyama vya
siasa vinakidhi matakwa ya Sheria ya usajili wa vyama vya Siasa.
Uhakiki wa Vyama vya siasa ni
zoezi muhimu sana kwa sababu ni zoezi ambalo hugusa uhai wa kila chama
cha siasa. Kwa upande wa Tanzania Visiwani , uhakiki unatarajiwa
kuanza mara baada ya kumalizika Bara kwa tarehe ambazo zitatangazwa
baadaye.
Bw.Eugene
Kabendera, Katibu Mwenezi Taifa wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA)
akitoa taarifa wa watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya
Siasa wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za chama hicho
zilizopo Jijini Makumbusho Dar es salaam Jana
Kaimu
Katibu Mkuu wa Chama cha Jahazi Asilia, Bw. Mbwana S. Kibanda
akifafanua jambo wakati wa zoezi la uhakiki liliofanyika Leo katika
ofisi za chama hicho zilizopo ilala Jijini Dar es salaam . Kulia ni
Mwenyekiti wa chama hicho na kushoto ni watumishi kutoka Ofisi ya
Msajili wa Vyama vya Siasa
Bi.
Esther B.Mwanri, Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
akikagua katiba ya Chama cha Wananchi (CUF) wakati wa Zoezi la uhakiki
uliofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni Malapa Jijini
Dar es salaam. Kushoto ni Bw. Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa uchumi na
Mipango.
Msajili
Msaidizi wa Vyama Siasa “Gharama za uchaguzi na Elimu kwa Umma “Bi.
Piencia Kiurea akimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha United
Democratic Party (UDP) Bw. Godluck Ole-Medeye wakati akitoa taarifa
muhimu za chama chake katika zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Kisiasa
unaoendelea Jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party (DP) Bi. Georgia Mtikila
(kushoto) akitoa taarifa za chama chake kwa Afisa Sheria kutoka Ofisi ya
Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini (kulia), Bi. Jacqueline Kilama wakati
wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya
Sheria ya Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam Juni 28 mwaka huu.
Msajili
Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Usajili wa vyama vya Siasa , Bw.
Sisty Nyahoza (kushoto) akihakiki daftari lenye orodha ya wanachama wa
Chama cha NRA ( National Reconstruction Alliance) wakati wa zoezi
la kuhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria
ya Vyama vya Siasa Jana Jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party (DP) Bi. Georgia Mtikila
(kushoto) akitoa taarifa za chama chake kwa Afisa Sheria kutoka Ofisi ya
Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini (kulia), Bi. Jacqueline Kilama wakati
wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya
Sheria ya Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam Juni 28 mwaka huu.
(Picha zote na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa)
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufungua ofisi Kigali,Rwanda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais wa Rwanda
Paul Kagame.
PICHA NA IKULU
—————————————-
Na Daudi Manongi,MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dk Joseph Pombe Magufuli amesema kuwa Mamlaka ya Mapato
Tanzania(TRA) watafungua ofisi nchini Rwanda ili kuraisisha uhakiki wa
bidhaa kwa wafanyabiashara wa Rwanda wanaoingia nchini.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo
Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa Rwanda Mhe.Paul Kagame
anafanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania ikiwemo ufunguzi
wa Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.
Aidha amesema kuwa Serikali imetoa
eneo la bandari kavu (ICD) kwa ajili ya kuhifadhia Bidhaa kutoka nchi
ya Rwanda ili kupunguza urasimu ambao umekuwa kikwazo kwa maendeleo ya
biashara hapa nchini na kwa namna hiyo biashara itakua kwani tunategemea
uchumi utapanda kutoka asilimia 7 ya sasa mpaka asilimia 7.2.
Pia amesema kuwa Serikali
imepunguza vituo vya ukaguzi barabarani kutoka Tanzania kwenda Rwanda
kufikia vitatu na kwa kufanya hivyo itarahisisha safari za magari ya
biashara njiani na hivyo kufikisha bidhaa kwa haraka.
Aidha amesema kuwa serikali iko
mbioni kuanzisha kituo kimoja cha kukusanya mapato badala ya kila sehemu
kuwa na mfumo wake ambao unapoteza mapato mengi kwa kuwa mifumo hiyo
haina uthibiti mmoja na hivyo serikali ya Rwanda itasaidia kwa kuleta
wataalamu wa Tehama ambao watasaidia kutoa mafunzo ili kusaidia mapato
yetu kuwa katika udhibiti mmoja.
Kwa upande Rais wa Rwanda Paul
Kagame amesema kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika
kuendeleza Uchumi wa nchi izi mbili kwani zina historia ndefu na kwa
kuendelea kufanya biashara pamoja nchi izi mbili zimejenga taswira mpya
katika mahusiano.
Awali Mawaziri wa mambo ya Nje wa
nchi za Tanzania na Rwanda walitia saini Muhtasari wa Tume ya
Ushirikiano wa pamoja baina ya nchi izi mbili.
No comments :
Post a Comment