Mwenyekiti wa Shrikisho la
Wafanyabiashara wa ya Viwanda na Kilimo wa Ujerumani na Tanzania, Dirk
Smelty, (kushoto), akiwa na Naibu Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, John
Reyels, akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Ujerumani
lililoko kwenye jengo la ukumbi wa Karume kwenye viwanja vya Mwalimu
Nyerere kunakofanyika maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Dar es
Salaam Juni 30, 2016
Mwenyekiti wa Shrikisho la Wafanyabiashara wa ya Viwanda na Kilimo wa Ujerumani na Tanzania, Dirk Smelty, (kushoto)
NA
K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
UJERUMANI imerejea kwa kishindo kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016 baada ya kukaa kando
na maonyesho hayo kwa takriban miaka 20.
Makampuni manane ya Kijerumani yameweka kambi kuonyesha bidhaa
zake pale viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye banda la Ujerumani lililoko kwenye jingo la
Karume mita chache baada ya kuingia lango kuu la viwanja hivyo mapema leo Juni
30, 2016, Naibu Balozi wa Ujerumani nchini, John Reyels amesema, Tanzania ni
nchi inayokua kwa kasi kiouchumi ni inategemewa kuwa kitovu cha uchumi wa
Afrika Mashariki, hivyo Ujerumani inayofuraha kuwakaribisha Watanzania kujionea
bidhaa zake mbalimbali na zilizo bora kutoka jumla ya makampuni manane ya
Kijerumani ambayo ni pamoja na Kampuni ya Acheli (Tanganyika) Limited ambayo
inajishughulisha na utengenezaji na usambazaji wa vifaa vya ujenzi, vifaa vya
maabara na tiba, mafuta na gesi pamoja na uchapishaji.
Ametaja
kampouni nyingine kuwa ni pamoja na Acto GmbH, Renner GmbH Kompressoren, Mabisol
GmbH, Riel Karl-Heinz Knoop e.K , SUNSET Energietechnik GmbH. Tupopamoja
Holding AG na Twiga Cement Co Limited.
Maonyesho
hayo ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayotayarishwa na Mamlaka ya Uendelezaji
Biashara Tanzania, TANTRADE, yanatarajiwa kufunguliwa rasmi Ijumaa Julai 1,
2016 na Rais wa Rwanda Paul Kagame majira ya alasiri.
Naibu Balozi wa Ujerumani nchini, John Reyels |
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya
Kijerumani ya SUNSET Solar, Dkt.Olaf W. Fleck (kushoto), akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa mkutano huo, Kulia ni msaidizi mtendaji wa
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mobisol, Leslie Otto.
Msaidizi mtendaji wa Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya
Kijerumani ya Mobisol, Leslie Otto, (kulia) akizungumza. Kulia ni Afisa
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Kijerumani ya SUNSET Solar, Dkt.Olaf W. Fleck
Mkurugenzi mkazi wa Mobisol, Livinus Manyanga, akitoa ufafanuzi juu ya bidhaa za kampuni hiyo yenye makazi yake jijini Arusha
Nfally Jarju, kutoka kampuni ya Renner Kompressoren ya Ujerumani akizungumzia bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo
Waandhi wa habari
Afisa habari wa Ubalozi wa Ujerumanio nchini, John Merikion, (kulia), akizungumza jambo na mwandishi wa East
Africa TV (C5), wkaati wa maswali ya waandishi wa habari
No comments :
Post a Comment