Friday, July 8, 2016

MWENYEKITI WA BODI YA NSSF, MSAJILI WA HAZINA NA KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI, MAWASILINO NA UCHUKUZI WATEMBELEA BANDA LA NSSF

 

Meneja kiongozi wa Masoko na Uhusiano Eunice Chiume akimpatia Maelezo juu ya Mradi wa Nyumba wa Kijichi Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF Prof. Samwel Wangwe alipotembelea Banda la NSSF kwenye Maonesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Joseph Nyamhanga akifurahia baada ya kupewa maelezo juu ya Miradi ya Nyumba ya Mtoni Kijichi, Toangoma na Dungu Farm, Miradi hiyo iliyopo kigamboni imevutia watu wengi kutokana na urahisi wake wa kufikika kupitiaDaraja la Nyerere
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Joseph Nyamhanga akifurahi baada ya kupewa Maelezo ya Mradiwa Viwanja Vya Kiluvya na Meneja kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF Eunice Chiume alipotembelea banda la NSSF.
Msajili wa Hazina Lawrence Mafuru akifurahia maelekezo aliyokuwa akipewa na Meneja Kiongozi wa Masoko na Uhusiano Eunice Chiume alipotembelea banda la NSSF kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara.

WAZIRI MKUU ASITISHA VIBALI VYA UVUNAJI MBAO

MKUU WA JESHI LA POLISI MALAWI AFANYA ZIARA NCHINI, WAJADILIANA NA WAZIRI MWIGULU MASUALA YA USALAMA

HUAWEI YALETA SIMU ZA KISASA ZENYE UWEZO WA 4G KWA GHARAMA NAFUU

Balozi wa Huawei Jennipher Lazaro, akimuonyesha mteja Catherine Mosha ubora wa simu ya Huawei Y 3lite alipotembelea banda la tigo katika maonyesho ya Sabasaba.
 
Dar es Salaam, Julai 2016;. Kampuni ya Huawei wakishirikiana na makampuni ya mtandao wa simu Vodacom, Airtel na Tigo wamezindua promosheni kwa ajili ya wananchi wote watakaohudhuria maonyesho ya Saba Saba katika matoleo yake ya simu za kisasa za Y3II, Y3 C, na toleo mahususi la Y3 Lite. Katika maonyesho hayo, wananchi wataweza kujipatia simu mpya halisi kwa bei rahisi zaidi

Tukizingatia kwamba kila Mtanzania anayo haki ya kuendelea kuunganishwa na ndugu, jamaa na marafiki kwa njia ya mawasiliano ya simu bila kujali tofauti zao za kipato, Huawei kwa mara nyingine inafanikisha hilo kwa kuleta simu zake za Yseries ili kuwezesha upatikanaji wa simu za kisasa za gharama nafuu kwa watumiaji wa simu wa kipato cha chini Tanzania.

Huawei Tanzania kwa kupitia mkakati wake huu wa kushirikiana na makampuni ya mawasiliano; Tigo, Vodacom na Airtel inampa mtumiaji fursa ya kugusa, kuhisi na kufurahia namna za kipekee za utendaji wa matoleo haya ya Y series ikiwamo Y3II, Y3Lite, Y3 C na Y6 Pro.

Akizungumzia kuhusu ofa na punguzo hili la simu, Meneja Masoko wa Huawei Tanzania Bi. Jane Wang amewahimiza wananchi wote watakaofika katika maonyesho ya Saba Saba kutembelea mabanda ya Vodacom, Tigo na Airtel katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kuanzia tar 28 June mpaka tar 8 Julai ili kujipatia moja ya hayo matolea ya simu za Huawei.


”Ofa ya Huawei na Vodacom ni katika simu ya Huawei Kishkwambi kwa gharama y ash. 100,000 ambapo mteja atajipatia kifurushi cha bure cha dakika 1000 na interent GB6 kwa muda wa miezi 12.” Alisema.

Promosheni ya Huawei na Tigo huwawezesha wateja kununua simu ya Huawei Y3 Lite kw ash. 125,000 tu, ikiwa na kifurushi cha GB 2 za data pamoja na muda wa maongezi wa thamani ya sh. 10,000 kwa muda wa miezi 6. 


Kwa Y3II Tigo inatoa ofa ya GB 10 na dakika 3000 kwa kupiga Tigo – Tigo na dakika 500 kupiga mitandao mingine kwa muda wa miezi 3. Y3 C inakuja na dakika 100 za kupiga mitandao yote, kifurushi cha internet cha GB1 na sms 10,000 kwa miezi 4 kutoka Airtel”

Akizungumzia kuhusu simu za gharama ya chini na uhitaji wake kwa watu wa kipato cha chini, Mkurugenzi wa Mauzo wa Huawei Tanzania, Bw. Sylvester Manyara alisema, ukiziangalia simu hizi ni vigumu kuamini kuwa ni simu za gharama ya chini kwa sababu simu zote zimeundwa kwa muundo na teknolojia ya hali ya juu na ya kimataifa. 


Y3 Lite inafaa Zaidi kwa ajili ya watu wazima, wanafunzi na watu wa kipato cha kati na cha chini ambao kwao gharama na utendaji wa simu huwa na umuhimu sawia. 

Simu hii inawafaa wale ambao wanahitaji kuitumia simu kwa muda mrefu sana bila kuichaji. Ni moja ya simu pekee katika zenye thamani hii zinazoweza kuvumilia matumizi makubwa. Betri yenye uwezo mkubwa ya Huawei Y3 Lite inayohifadhi nguvu kwa kiwango cha juu inaiwezesha simu hii kudumu na chaji kwa zaidi ya siku nzima.

POLISI WANNE WAUWAWA KATIKA MAANDAMANO JIJINI DALLAS

Mdunguaji amewapiga risasi na kuwauwa polisi wanne na kujeruhi wengine saba huko Dallas, Marekani katika maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi yanayofanywa na polisi.

Milio ya risasi ilisikika wakati waandamanaji walipokuwa wakiandamana katika mji huo. Mtu mmoja anashikiliwa na polisi na mwingine mmoja aliyeonekana na bunduki amejisalimisha.
                                                           Polisi wakiwa kazini wakimsaka mdunguaji 
Hali ilikuwa inatisha kiasi ya watu kujificha kwenye magari wakati polisi wakihaha kumsaka mdunguaji
Huyu aliamua kundamana na bunduki yake, na sasa amejisalimisha polisi kwa mahojiano zaidi.

WENYEJI UFARANSA WATINGA FAINALI EURO 2016 SASA KUIVAA URENO

WASHINDI WANNE WANYAKUA ZAWADI KATIKA KAMPENI YA FAIDIKA NA AMANA BANK

Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akimkabidhi zawadi ya Television mshindi wa kwanza wa kampeni ya Faidika na Amana Bank Bi PIKIRA NLONGANE wakati wa Hitimisho la kampeni hiyo iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo watanzania wa kuwekeza zaidi,Hitimisho la Kampeni hiyo limefanyika wakati wa siku ya maonyesho ya kimataifa ya biashara saba saba Jijini Dar es salaam ambayo Bank ya amana ni moja kati ya wafanyabiashara waliokuwa na Banda katika Maonyesho hayo
Zawadi ya JOKOFU kwenda kwa mshindi wa pili ambaye ni SHAKIRA IBRAHIMU imekabidhiwa na kupokelewa na mwakilishi wake ambaye ni AHMED SANDE (Pichani) akikabidhiwa zawadi hiyo na Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD wakati wa utoaji wa zawadi hizo.
Mshindi wa nne amepata zawadi ya Table Feni  ya kisasa yenye AC pia.Pichani ni Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD  akimkabidhi zawadi Bwana HEMED SULEIMAN ambaye ameibuka mshindi wa nne katika kampeni ya Faidika na Amana Bank iliyochezeshwa ndani ya banda la Bank hiyo katika maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya saba saba Jijini Dar es salaam ambapo washindi wanne wamejinyakulia zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi za kitanzania Million Tano
Katika kuadhimisha kilele cha kampeni ya FAIDIKA NA AMANA BANK,Bank imezawadiwa wateja wake waliobahatiika kushinda zawadi mbalimbali kutokana na kujiwekea akiba zao na Benk hiyo leo siku ya kilele cha maonyesho ya saba saba Tarehe 7/7/2016.
 

Wateja hao walichaguliwa kitaalam katika droo iliyochezeshwa ndani ya viwanja vya saba saba katika banda la amana bank na kupewa taarifa ya kufika kupokea zawadi zao kutoka uongozi mkuu wa bank hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji DR MUHSIN SALIM MASOUD.
 

Kampeni hiyo iliyojumuisha wateja wa akaunti za akiba binafsi kujiwekea akiba katika akaunti zao kuanzia kiasi cha shilingi 500,000 na kuendelea kwa muda wa miezi mitatu na kuweza kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali za vifaa vya matumizi ya nyumbani kama Luninga,Jokofu,Microwevu,Pamoja na Table Feni yenye AC Pia.
Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akizungumza na wanahabari wakati wa Utoaji wa zawadi hizo kwa washindi wanne wa Kampeni ya Faidika na Amana Bank ambapo amewataka watanzania kuwa na utamaduni wa kuwekeza kwani ni utamaduni mzuri na unaofaa kuendelezwa

FRANCE PLEDGES SUPPORT FOR REFORMS AT EAC SECRETARIA

KAIMU NAIBU MKURUGENZI WA TANESCO ATEMBELEA BANDA LA SHIRIKA HILO SABA SABA

Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Sophia Mgonja (wa tatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam 2016 kwenye viwanja vya Biashara vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Dar es Salaam leo.
 Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya kuendeleza jotoardhi Tanzania(TGDC) wa pili kushoto akitoa maelezo kwa Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Sophia Mgonja.
Kaimu Meneja Uhusiano Tanesco, Leila Muhaji (kushoto), akiwa na Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Sophia Mgonja walipotembelea banda la TGDC.
 Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Sophia Mgonja (kushoto), akimsikiliza mteja aliyetembelea banda hilo.

No comments :

Post a Comment