Wednesday, July 6, 2016

MWANARIADHA MLEMAVU WA MIGUU PISTORIUS AHUKUMIWA JELA MIAKA SITA

SWALA YA ED-EL-FITR ILIVYOFANYIKA VIWANJA VYA MWEMBE YANGA JIJINI DAR ES SALAAM LEO ASUBUHI

Sheikh Abdulkadir Mohamed akiongoza swala ya Ed- El- Fitr iliyofanyika Viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi.
                                            Waumini wa dini ya kiislam wakiwa kwenye swala hiyo.
Mratibu wa swala hiyo ya Ed El-Fitr, Sheikh Othman Abdallah Dishi (kulia), akizungumza katika swala hiyo.
                                                                                         Watoto wakishiriki swala hiyo
  Sheikh Zaki akiwasalimia waumini wenzake waliokuwepo kwenye swala hiyo.
                                                                                                                Ibada ikiendelea.

RWEYUNGA BLOG INAWATAKIA EID MUBARAK WATANZANIA WOTE

WAKUU WA WILAYA ZA MKOA WA IRINGA WALA KIAPO, WAAHIDI UTENDAJI ULIOTUKUKA

MIMOSA BLACK CARD YADHAMINI MASHINDANO YA GOLF LUGALO

MOTO WATEKETEZA MABWENI MATATU YA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA MGONGO, IRINGA

Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ( mwenye kanzu ) akiwa eneo la tukio
Mkuu wa wilaya Iringa, Richard Kasesela ( mwenye kanzu ) akishirikiana na Kikosi cha Zimamoto kuzima moto na kuwapanga wananchi
Mkuu wa wilaya Iringa, Richard Kasesela akizungumza na watoto ambao vitu vyao vimeungua .

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela alishiriki katika kuzima moto uliounguza bweni wanalokaa watoto yatima katika kituo cha Mgongo. 

Moto huo ilioanza kwa hitilafu ya umeme umeteketeza mabweni 3 na kuunguza mali za watoto hao ikiwemo nguo, madaftari magodoro. 

Kikosi cha zimamoto chini ya Mrakibu Komba kilifanya kazi ya ziada kuzuia moto huo usieneee majengo mengine. Wananchi wa eneo la Mgongo wamefanya kazi kubwa wakisaidiana na jeshi la zima moto.
Akizungumza na wananch,i Mh Kasesela ameahidi kuomba wahisani pia kuangalia uwezekano wa kuwasaidia waathirika wa janga hili la moto. Inakadiriwa watoto zaidi ya 45 wameathirika na moto huu ingawaje hamna majeruhi hata mmoja.

 " nilipata taarifa nikiwa kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB ikabidi niache nije mara moja nafurahi kuona tumefanikiwa kuzima moto ingawaje umeleta madhara makubwa Pongezi ziwandee jeshi la Zimamoto pamoja na changamoto walifanikiwa kuzima moto huo" aliesema Mkuu wa Wilaya. 

Mkuu wa wilaya alikutana na watoto na kuwapa matumaini serikali ipo pamoja nao. Serikali ya Wilaya ya irnga inawaomba wadau wajitokeze kusaidia watoto hawa mahitaji makubwa ni magodoro, blanketi na nguo hasa kipindi hiki cha baridi.

No comments :

Post a Comment