Wednesday, July 27, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA APOKEA SALAAM MAALUM KUTOKA SUDAN YA KUSINI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Sudan ya Kusini Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik aliyeleta ujumbe maalum wa Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na kupokelewa na Makamu wa Rais ,Ikulu jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Sudan ya Kusini Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik pamoja na  ujumbe wake walioleta ujumbe maalum wa Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na kupokelewa na Makamu wa Rais ,Ikulu jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri
wa Biashara na Viwanda wa Sudan ya Kusini Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik pamoja na ujumbe wake ambao walileta ujumbe maalum wa Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na kupokelewa na Makamu wa Rais ,Ikulu jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………………………………………………..
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemtumia ujumbe maalum Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru kwa jitihada za serikali ya
Tanzania za kusaidia kupatikana kwa amani katika nchi hiyo. Ujumbe huo wa Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir umewasilishwa nchini  na Waziri wa Biashara na Viwanda wa nchi hiyo Stephen Dhieu Dau Ayik kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ikulu jijini Dar es Salaam Tarehe 27-Jul-16.
Waziri huyo wa Serikali ya Sudan Kusini Stephen Ayik amesema hali ya usalama kwa sasa imeendelea kuimarika kufuatia kusitishwa kwa mapigano kati ya wanajeshi watiifu wa Rais Salva Kiir na wanajeshi wa watiifu wa Aliyekuwa Makamu wa Rais Riek Machar
Akipokea ujumbe maalum wa Serikali ya Sudan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali ya Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha amani
inapatikana katika Taifa hilo changa barani Afrika ambayo itawezesha wananchi wa taifa hilo kufanya kazi za maendeleo kwa amani na utulivu.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pia amezitaka pande hizo MBILI zinazohasimiana kuzingatia na kuheshimu mkataba wa amani waliosaini jijini Arusha mwaka 2015 uliolenga kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe na kurejesha amani katika Taifa hilo.
Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa kufanyika kwa mazungumzo ya amani ya kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huo ili kukomesha  vita ambavyo vimekuwa vikigharimu mali na maisha ya mamia ya wananchi wa Sudan Kusini 

Wagonjwa 45,000 wa saratani hugundulika tanzania kila mwaka

UG1 
Mhe Ummy Mwalimu  akiwa na waziri wa afya (Uganda) Mhe .Sara Opendi na Mhe Omar Sey Waziri wa Afya wa  Gambia.
UG2 
Waziri wa afya Ummy Mwalimu akifuatilia mkutano huo
UG3.
Picha ya pamoja ya wake wa marais na mawaziri wa afya wa afrika,waliohudhuria mkutano wa 10 wa kupambana na saratani ya shingo ya Kizazi,matiti na tezi dume (picha/habari na wizara ya afya)
……………………………………………………………………………………………………….
Na.Mwandishi wetu,Addis Ababa
Ugonjwa wa saratani nchini Tanzania  ni chanzo cha magonjwa na vifo,hivyo inakadiriwa Takribani wagonjwa wapya wa saratani 45,000 hugundulika kila mwaka.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika Mkutano wa 10 wa kupambana na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume barani Afrika unaofanyika nchini hapa.
Waziri Ummy amesema kati ya wagonjwa hao asilimia 38  ni wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake, asilimia 14  saratani ya ngozi, asilimia 10  saratani ya matiti na saratani ya tezi ni asilimia 4
Hatahivyo,takribani watu 35,000 hufariki kila mwaka kutokana na magonjwa ya Saratani.
Licha ya changamoto mbalimbali zinazokwamisha jitihada za kukabiliana na magonjwa hayo ikiwemo  uhaba wa Miundombinu ya kutolea huduma za afya, vifaa tiba, Uhaba wa Watumishi wa Afya, rasilimali fedha na gharama kubwa za dawa za matibabu ya saratani,Waziri Ummy amesema Serikali ya Tanzania  imepitisha Sera za Kitaifa na Miongozo mbalimbali ya Kupambana na Saratani, kutoe Elimu kwa jamii na watoa huduma za afya nchini kuhusu Saratani.
Aidha, kuanzishwa kwa huduma za upimaji wa saratani katika Hospitali na vituo vya afya zaidi ya 300 nchini na huduma za Tiba kupitia Hospitali ya Saratani ya Ocean Road.
“Serikali itapanua wigo wa matibabu ya saratani katika Hospitali ya Bugando Mwanza na KCMC, Kilimanjaro. Mipango ya baadae ni huduma hizo pia kutolewa ktk Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.”hii itapunguza wagonjwa kufuata huduma kwenye hospitali ya saratani ya Ocean Road
Mkutano wa 10 wa Saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume barani Afrika unafanyika kwa kuasisiwa kwa juhudi za wake za Marais wa bara la Afrika.
Mkutano huu unahudhuriwa na Wake wa Marais wa Afrika, Mawaziri wa Afya wa Afrika, Wanataaluma na Wadau wa Maendeleo. Lengo kuu ni kufanya mapitio ya hatua zilizochukuliwa na nchi za Afrika, changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya pamoja na ya nchi katika kukabiliana na saratani.
Wakati wa kukabidhiwa uenyekiti wa Umoja wa Wake wa Marais wa Afrika wa Kupambana na saratani ya Shingo ya Kizazi, Matiti na Tezi Dume kutoka kwa Mwenyekiti anaemaliza muda wake, mke wa Rais wa Kenya mama Magreth Kenyatta, Mke wa Waziri Mkuu wa Ethiopia mama Roman Tesfaye Abneh ameleeza masikitiko yake kwa jinsi ambavyo ugonjwa wa saratani unavyoua kuliko hata ugonjwa wa UKIMWI na kifua kikuu. Hivyo ameziomba nchi za Afrika kuongeza uwekezaji katika eneo hili hasa kwa kuhakikisha dawa zinakuwepo za kutosha, kuboresha utoaji wa huduma za afya ikiwemo upimàji na tiba, kuhakikisha nchi zinatoa mafunzo ya Kutosha kwa watumishi  wa afya katika fani hii

SERIKALI ZA TANZANIA NA KOREA, ZIMETILIANA SAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA MIRADI YA MAENDELEO

KOA1Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Wizara ya Fedha ya Korea Weon-Kyoung Jo (kushoto) akizungumza wakati wa mjadala wa Ushirikiano katika misaada ya maendeleo ya kiuchumi kabla ya kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Korea, yenye thamani ya dola Milioni 300, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dar es salaam.
KOA13 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Hamis Shaban  na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo wakibadilishana Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo baada ya kusainiwa. Hati hiyo ina thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 650.
KOA14 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Hamis Shaban  na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo wakisaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo, yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 650.
KOA15 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi.  Amina Hamis Shaban  na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo wakipeana mikono baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo, yenye thmani ya zaidi ya dola za Marekani milioni 300, katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
KOA16 
Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi.  Mamelta Mutagwaba, akipeana mkono na mmoja wa wajumbe kutoka Korea baada ya kusaini  Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo, yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 650.
KOA8 
Wajumbe kutoka Serikali ya Korea wakisoma Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo nchini na Serikali ya Korea kabla ya kusainiwa.
KOA9 
Wajumbe kutoka Serikali ya Tanzania wakifuatilia mjadala wa Ushirikiano katika Misaada ya Maendeleo ya Kiuchumi uliofuatiwa na kutiliana saini kwa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo nchini.  
KOA10 
Mjumbe kutoka Tanzania akichangia hoja katika mjadala wa Ushirikiano katika Misaada ya Maendeleo ya Kiuchumi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara jijini Dar es salaam kati ya Tanzania na Korea, kabla ya kusainiwa kwa Hati ya Ushirikiano ambapo Korea imeahidi kutoa zaidi ya shilingi Bilioni 650.
KOA11 
Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mamelta Mutagwaba (kulia) na wajumbe wengine wakifuatilia mjadala kuhusu Ushirikiano katika Misaada ya Maendeleo ya Kiuchumi kabla ya kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo.
KOA17 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Amina Hamis Shaban (kushoto)  na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo (katikati) wakibadilishana mawazo baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo, kulia ni Afisa kutoka Korea.
KOA19 
Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Hamis Shaban (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tanzania na Korea baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo .
……………………………………………………………………………………………..
Na Benny Mwaipaja,MoFP
SERIKALI za Tanzania na Korea Kusini, zimetiliana saini Hati ya Makubaliano (Aide Memoire) kwa ajili ya Ushirikiano wa utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo wa Maji, Nishati, Kilimo, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano-TEHAMA na Viwanda  itakayogharimu Dola za Marekani Milioni 300, sawa na TSh.Bilioni 650, katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2016 hadi 2020.
Fedha hizo ni sawa na ongezeko la Dola Milioni 100 ikilinganishwa na kiasi cha Dola Milioni 200 ambazo nchi hiyo ya Korea iliipatia Tanzania kama mkopo wenye masharti nafuu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita (2014 hadi 2016).
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban, ametia saini makubaliano hayo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, huku upande wa Korea Kusini ukiwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Fedha ya Korea Bw. Weon-Kyoung Jo.
Kusainiwa kwa makubaliano hayo ni mwanzo wa matayarisho ya kuandaa Mpango kazi wa namna ya kutekeleza miradi hiyo ili iende sambamba na Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa miaka 5 uliozinduliwa hivi karibuni mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Mkakati Mbadala wa Kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA Successor Strategy).
Akizungumza mara baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban, amesema kuwa miradi hiyo ya maendeleo iliyochaguliwa kutekelezwa katika sekta zilizotajwa zitachochea ukuaji wa uchumi wa Taifa na kupunguza umasikini kwa wananchi.
Bi. Amina Shaaban alisema kwamba Hati hiyo ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Korea Kusini, yamejikita zaidi katika uboreshaji wa mifumo ya Tehama, kuimarisha sekta ya kilimo pamoja na kuboresha miundombinu inayosaidia ukuaji wa viwanda hususan ya nishati ya umeme katika kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2016/17 hadi 2020/21.
“Ushirikiano wa Tanzania na Korea Kusini umeanza tangu mwaka 2000, kwa kuhusisha taasisi zake mbili ambazo ni Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA) ambalo limeipatia Tanzania kiasi cha zaidi ya dola za Marekani 30.9 na Benki ya Exim-Korea ambayo imetoa Dola za Marekani zaidi ya Milioni 455 sawa na zaidi ya Tsh 900 bilioni kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii katika kipindi cha miaka 10 iliyopita” alisema Bi. Amina Shaaban
Ametoa wito kwa nchi hiyo kuwekeza hapa nchini kutokana na fursa mbalimbali zilizopo za kiuchumi zikiwemo mazingira mazuri ya uwekezaji, rasilimali za kutosha ikiwemo gesi asilia, madini, sekta ya utalii, hali nzuri ya hewa pamoja na amani na utulivu.
Akizungumza katika tukio hilo Weon-Kyoung Jo, amesema kuwa Tanzania inaongoza katika bara la Afrika kupata misaada na mikopo nafuu kutoka Korea Kusini baada ya nchi hiyo kuridhishwa na mipango mizuri ya maendeleo iliyowekwa na Serikali ya Tanzania.
Amesema kwamba vipaumbele vilivyowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano zikiwemo Sekta za Viwanda, Kilimo na TEHAMA vinaungwa mkono na nchi yake na kwamba wako tayari kusaidia kwa njia ya kutoa ruzuku na mikopo yenye masharti nafuu.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda, Afrika Mashariki na Kimataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi, amesema kuwa serikali ya Tanzania inatarajia kufungua ubalozi wake nchini Korea Kusini ili kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo mbili.

SERENGETI BOYS YATUA SALAMA MADAGASCAR

SE 
Msafara wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, uliondoka jana alfajiri Dar es Salaam, Tanzania imetua salama jijini Antananarivo, Madagascar kwa ajili kambi ya siku 10 kujiandaa na mchezo dhidi ya Afrika Kusini kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Agosti 6, 2016.
Mchezo wa marudiano utafanyika Agosti 21, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam, ulioko Chamazi-Mbagala, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kwamba mshindi atakuwa amejiwekea mazingira mazuri ya kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana, zitakazofanyika mwakani huko Madagascar.
Mkuu wa msafara akiwa ni Ayoub Shaibu Nyenzi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Vijana, maofisa wengine waliosafiri na timu hiyo ni Kocha Mkuu, Bakari Nyundo Shime maarufu zaidi kwa jina la Mchawi Mweusi, Daktari wa timu hiyo, Shecky Francis Mngazija na Mtunza Vifaa, Andrew Vanance Andrew.
Pia yumo Juma Kaseja Juma ambaye kwa muda amechukua nafasi ya makocha wasaidizi, Sebastian Nkoma na Muharam Mohammed ‘Shilton’ wanaohudhuria kozi ya makocha ngazi ya juu inayoratibiwa na CAF.
Nyota waliosafiri ni pamoja na makipa, Ramadhani Awm Kabwili, Kelvin Deogratius Kayego na Samwel Edward Brazio wakati mabeki wako Kibwana Ally Shomari, Nickson Clement Kibabage, Israel Patrick Mwenda, Dickson Nickson Job, Ally Hussein Msengi, Issa Abdi Makamba na Enrick Vitalis Nkosi.
Viungo ni Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali, Syprian Benedictor Mtesigwa, Ibrahim Abdallah Ali, Shaban Zuberi Ada huku washambuliaji wakiwa ni Mohammed Abdallah Rashid, Yohana Oscar Mkomola na Muhsin Malima Makame.
Serengeti Boys inakwenda kucheza na Afrika Kusini baada ya kuwatoa Shelisheli kwa jumla ya mabao 9-0 katika mechi zake mbili za kimataifa. Mshindi wa jumla kati ya Serengeti Boys na Afrika Kusini, atacheza na timu mshindi kati ya Namibia na Congo-Brazaville.
Hivi karibuni Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki. Ilishika nafasi ya tutu nyuma ya Korea Kusini na Marekani.

MAAGIZO KWA KLABU ZA LIGI KUU, LIGI DARAJA LA KWANZA

index 
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine ameziasa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutimiza masharti ya kupata vibali vya kuishi na kufanya kazi Tanzania kwa Wataalamu wa kigeni wakiwamo makocha, madaktari na wachezaji kabla ya kuingia kandarasi.
Masharti hayo ni vibali vya kufanya kazi nchini, visa ya kuishi nchini, vibali vya kucheza mpira wa miguu nchini, vibali vya kufundisha mpira na vibali vya watalaamu wengine kama madaktari na hayo ni kwa mujibu wa Idara ya Uhamiaji na Serikali, lakini wakati huohuo kwa wachezaji nao kukatiwa leseni ya kucheza kutoka TFF.
“Mchezaji au mtaalamu ye yote anapokuja nchini na kuanza mazoezi na timu yo yote anachukuliwa yuko kazini. Tusingependa watu wapate usumbufu. Kama Katibu Mkuu nimepata taarifa kutoka mamlaka zinazohusika kuwa nifuatiulie kuwa kuwa sisi ndio waratibu soka nchini, natakiwa kufuatilia,” amesema Selestine.
“Vilabu vihakikishe vyeti vya taaluma vinawasilishwa TFF kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kutiliana kandarasi na wachezaji au walimu. Inawezekana hawahitajiki. Ni vema wakafanya uratatibu wa kuhakiki,” amesema.
Wakati huohuo, huo huo TFF imeagiza klabu kuendelea na usajili kabla ya Agosti 6, 2016 ambayo itakuwa siku ya mwisho na kwamba hakutakuwa na muda wa kuongezwa kwa klabu ambayo itashindwa kukamilisha usajili kwa wakati.

SERIKALI YATANGAZA MAOMBI RUZUKU AWAMU III

index 
Na Asteria Muhozya, DSM
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini ambayo inatekeleza Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) imetoa taarifa ya kukaribisha maombi ya Ruzuku Awamu ya Tatu kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini.
Akizungumza katika Kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Televisheni ya Taifa, TBC1, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe alisema kuwa, kiasi cha ruzuku kilichotengwa kwa shughuli hiyo ni Dola za Marekani Milioni Tatu.
Profesa Mdoe alisema kuwa, taratibu zote za kupata washindi wa ruzuku hiyo zitafanyika kwa uwazi huku zikishirikisha Vyama vya Wachimbaji vya Mikoa (REMA), lengo likiwa ni kupata walengwa stahiki kutokana na kuwa, vyama hivyo vinawatambua wanachama wao.
“Mbali na vyama vya wachimbaji, pia Serikali itashiriki kupitia ofisi zetu za Kanda zilizoko katika Mikoa yote kabla ya kufikishwa katika ngazi ya Wizara ambapo pia kutakuwa na Kamati Maalum ya kushughulikia suala hilo,”alisisitiza Prof. Mdoe.
Akizungumzia lengo la utoaji ruzuku hiyo alisema kuwa, ni kukuza mitaji ya wachimbaji wadogo na kuongeza kuwa, tayari Serikali imekwisha toa ruzuku hiyo katika Awamu Mbili, ambapo katika Awamu ya Kwanza kwa mwaka wa fedha 2013/14, Serikali ilitenga kiasi cha Dola Laki Tano (US $ 500,000), ambapo jumla ya vikundi 11 vya wachimbaji vilinufaika na kila kikundi au mchimbaji walipata kilipata wastani wa Dola Elfu Hamsini (US $ 50,000).
Akizungumzia ruzuku Awamu ya Pili alieleza kuwa, kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Serikali ilitenga takriban shilingi Bilioni 7.2, ambapo wanufaika 111 walishinda kati ya waombaji 720.
“Waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao ndani ya siku 21 kuanzia tarehe 20 Julai, 2016. Mwombaji anatakiwa kujaza nakala Tatu (3) za fomu za maombi na kuziwasilisha katika Ofisi ya madini ambapo wahusika wanafanya shughuli zao,” alisema Prof. Mdoe.
Pia alizitaja nyaraka ambazo mwombaji anatakiwa kuambatisha na maombi yake kuwa ni pamoja na;  Nakala ya leseni ya uchimbaji au biashara ya madini au leseni ya biashara iliyothibitishwa na Kamishna wa viapo;  Nakala ya Cheti na Katiba ya kuandikishwa kwa kampuni au ushirika.
Aidha, alisema nyaraka nyingine ni pamoja na Nakala za stakabadhi za malipo ya Serikali ya ada za mwaka, mrabaha na kodi; Nakala ya Cheti cha Mlipa Kodi (TIN); Mpango wa Utunzaji Mazingira (EPP) ulioidhinishwa na Afisa Madini Kanda ikiwemo taarifa ya uzalishaji kwa kipindi kisichopungua miezi sita.
Yapo mafanikio ambayo yamepatikana kufuatia Serikali kutoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo. Baadhi ya  mafanikio ya wanufaika wa ruzuku Awamu ya kwanza ni pamoja na Kikundi cha Itandura Miners Cooperation Society cha Nyamongo  kilichoongeza uzalishaji wa dhahabu, kampuni ya Precious Decor ya Tanga inayomilikiwa na Mwanamama  inayochimba madini ya stone  ambayo sasa ni maarufu jijini Dar Es Salaam kwa kurembesha kuta .
Aidha, mbali na utoaji ruzuku, Serikali imefanya jitihada kadhaa za kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa madini na kuhakikisha kuwa, uchimbaji mdogo unakuwa endelevu na unakua kutoka uchimbaji mdogo kwenda uchimbaji  wa Kati hatimaye mkubwa.
Kufuatia malengo hayo, tayari Serikali imetenga maeneo 35 kwa wachimbaji wadogo yenye jumla ya hekta 242,400.81 sehemu mbalimbali Tanzania Bara.
Pia, Serikali imepanga kujenga vituo saba vya mfano katika maeneo ambayo kuna uchimbaji mwingi wa madini, ambapo vituo hivyo vinatarajiwa kujengwa kati ya mwaka 2016 hadi 2018. Aidha, vituo hivyo, vitaitwa centres of excellence ambapo migodi ya mfano itajengwa na mitambo ya uchenjuaji itasimikwa ili wachimbaji wapate huduma ya kuchenjuliwa madini yao kwa gharama nafuu.
Aidha, ili kuhakikisha madini ya vito yanayochimbwa nchini yanaongezwa thamani, Serikali imefungua Kituo cha mafunzo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kilichopo Mkoani Arusha kwa ajili ya kufundisha uchongaji na ukataji wa madini hayo ili kuyaongezea thamani.
Pia, Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), linatoa huduma ya mafunzo ya kitaalamu ya nadharia na vitendo kwa wachimbaji wadogo wa madini na kuwapatia miongozo ili kuboresha shughuli zao.
Miradi inayoweza kupewa ruzuku katika awamu ya III ni kama ifuatavyo:
 NA AINA YA MIRADI KIWANGO CHA JUU CHA RUZUKU (USD)
1 Miradi ya kuendeleza, kuboresha na kupanua uchimbaji madini au kurekebisha mazingira yaliyotokana na shughuli hizo. 100,000
2 Miradi ya kupanua na kuboresha uchenjuaji madini au kurekebisha mazingira yaliyotokana na shughuli hizo. 100,000
3 Miradi ya kuboresha teknolojia ya uchimbaji madini, uongezaji thamani au uchenjuaji usiotumia zebaki. 100,000
4 Miradi ya uongezaji thamani hususani ukataji na uchongaji madini / mawe. 100,000
5 Miradi ya wakina mama katika maeneo ya uchimbaji mdogo yenye lengo la kutoa huduma kwa wachimbaji wadogo. 15,000

MKATABA KATI YA TTCL NA BHART AIRTEL WAISHA RASMI

TT1 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu Tanzania (TTCL), jinsi ya mfumo wa kutoa taarifa kwa wafanyakazi unavyofanya kazi wakati alipotembelea ofisini hiyo jijini Dar es salaam.
TT2 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni  ya Simu Tanzania (TTCL) Dkt . Kamugisha Kazaura akisoma taarifa ya utendaji kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Hayupo pichani) wakati alipoongea na uongozi wa kampuni hiyo, jijini Dar es salaam.
TT3Mwenyekiti wa bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Profesa Tolly Mbwete akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati Waziri alipotembelea ofisi hiyo, jijini Dar es salaam.
TT4 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na Uongozi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakati alipotembelea kampuni hiyo, Jijini Dar es salaam.
TT5 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni  ya Simu Tanzania (TTCL) Dkt . Kamugisha Kazaura akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipofanya mazungumzo na wafanyakazi wa kampuni hiyo,jijini Dar es salaam.
TT6 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),Jijini Dar es salaam.
PICHA ZOTE NA BENJAMINI SAWE -MAELEZO
…………………………………………………………………………………………………..
Serikali imehitimisha ubia kati ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), na Kampuni ya Bhart Airtel ya India kwa kuilipa kampuni hiyo Shilingi Bilioni 14.9 na hivyo kuirudisha TTCL mikononi mwa Serikali kwa asilimia miamoja.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hatua hiyo ni mkakati wa Serikali wa kuiwezesha TTCL kujitegemea ili kuzalisha faida, Kuimarisha Miundombinu yake, na kutoa gawio Serikalini.
“Tunawataka TTCL mjipange vizuri mjitangaze ili muwe kampuni kubwa na bora ya mawasiliano hapa nchini”, amesema Prof. Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa amesema katika kuiongezea nguvu TTCL Serikali itawapa kituo cha  Kutunza Taarifa cha Kijitonyama (Internet Data Center) ili ikisimamie na hivyo kujipatia mapato kupitia gharama za uendeshaji na usimamizi wa kituo hicho.
Amewataka wafanyakazi wa TTCL kufanya kazi kwa bidii, kasi, uaminifu, ubunifu na kuulinda Mkongo wa Taifa ili uwawezeshe kuwa na huduma bora na za uhakika wakati wote.
“Tumetumia fedha za mkongo wa taifa kumlipa mbia mwenzenu bhart airtel ili kuiwezesha TTCL kumilikiwa na Serikali kwa asilimia miamoja hivyo changamoto inayowakabili sasa ni kufanya mabadiliko makubwa katika upande wa kutafuta masoko ili kuweza kuongeza idadi ya wateja na kufanya kazi kwa faida”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Aidha Prof Mbarawa amesema katika kuijali TTCL, Serikali imeipa masafa ya 1800 na masafa ya 2100 na itawaongezea masafa ya 800 yatakayowawezesha kuwa na huduma ya 4G LTE yenye  mtandao wenye kasi na hivyo kuiongezea wateja hususani katika huduma za data.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL,  Profesa Tolly Mbwete amesema TTCL imejipanga kutoa huduma zake katika maduka makubwa, hospitali, stesheni za treni, mabasi ya mwendokasi na viwanja vya ndege katika jiji la Dar es salaam na Miji mikubwa ili kuwawezesha wananchi kunufaika na huduma za mtandao na data wakati wote.
Naye,  Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura, ameishukuru Serikali kwa fursa mbalimbali inazoipa kampuni hiyo na kumhakikishia Waziri Prof Mbarawa kuwa katika kipindi cha miezi mitatu ijayo matokeo ya mkakati wa mabadiliko ya kibiashara yataanza kuonekana.
Dkt. Kazaura amesema kuwa tayari watumishi wenye mtazamo wa mabadiliko ya kiteknolojia wameajiriwa na wengine watapewa mafunzo ili kuhimili soko la kibiashara na kuiwezesha TTCL kunufaika na miundombinu yake iliyopo nchi nzima.
Waziri Prof. Mbarawa alikuwa akizungumza na Menejimenti na wafanyakazi wa TTCL ikiwa ni utaratibu aliojiwekea kuzungumza na wafanyakazi na taasisi zilizopo chini ya Wizara yake.

NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA JUMAMOSI 30 JULAI 2016 STUTTGART,UJERUMANI

index 
Baada ya kuwadatisha washabiki katika maonyesho mawili makubwa kule bayreuth na tubingen sasa kamanda Ras Makunja anakipeleka kikosi kazi cha Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni katika onyesho kubwa la XXL Afro Summer Jam mjini Stuttgart nchini ujerumani,onyesho hilo litafanyika siku ya jumamosi 30 Julai 2016 katika ukumbi mkubwa Kulturhaus
Arena,uliopo Ulmer Str. 241, 70327 Stuttgart,ujerumani,akiongea na vyombo vya habari kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja alisema Ngoma Africa band ni mali ya washabiki na ina kazi moja tu nayo kudatisha washabiki katika kila onyesho bila kuremba remba , bendi hiyo iliyojizolea umaarufu na maelfu ya washabiki kila kona duniani
imejiwekea rekodi ya aina yake kuwa ni bendi ya mwanzo ya kiafrika kuimiri vishindo,na kudumu kwa miaka 23 ughaibuni na kufanikiwa kuwanasa washabiki wa kimataifa.
ungana nao at www.ngoma-africa.com

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, DK ANGELINA MABULA AAGIZA HALMASHAURI YA UYUI KUKAMILISHA UNUNUZI WA NYUMBA ZA NHC UYUI

 
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akitembelea nyumba za gharama nafuu Uyui zilizopo Isikizya wilayani Uyui, Tabora ambapo ameiagiza Halmashauri ya Uyui kulipia nyumba zilizojengwa na NHC ili watumishi wake waweze kuhamia. Kushoto kwake ni Meneja wa NHC mkoani Tabora, Dickson Ngonde.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tabora muda mfupi baada ya kutembelea nyumba za gharama nafuu Uyui ambapo ameiagiza Halmashauri ya Uyui kulipia nyumba zilizojengwa na NHC ili watumishi wake waweze kuhamia. PICHA ZOTE ZA KITENGO CHA MAWASILIANO KWA UMMA NA HUDUMA KWA JAMII CHA NHC.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akisikiliza taarifa kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Ardhi Tabora, Bw. Biseko Musiba wakati Waziri huyo alipofanya ziara katika mkoa wa Tabora na kujione hali ya maendeleo ya sekta ya ardhi mkoani humo pamoja na kutembelea miradi ya maendeleo ya taasisi zake.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akimsikiliza Kamishna Msaidzi wa Kanda ya Magharibi, Dorothy Wanzala wakati akikagua masjala ya ardhi ya Tabora. 
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akisoma mojawapo ya mafaili yaliyopo katika masjala ya Ardhi huku Kamishna Msaidizi wa Kanda ya Magharibi, Dorothy Wanzala akishuhudia. 
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Tabora muda mfupi baada ya kufika katika ofisi hizo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akizungumza na watumishi mbalimbali wa sekta ya ardhi mkoani Tabora.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Tabora muda mfupi baada ya kufika katika ofisi hizo.

BENDI 10 MAARUFU ZA MUZIKI WA DANSI KUWASHA MOTO JUMAMOSI VIWANJA VYA LEADERS

 Mwanamuzi wa mziki wa dansi, Ali Choki akiwaongoza wenzake kutoa burudani mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda walipofika ofisini kwake leo, kuzungumzia Tamasha la muziki huo litakalofanyika Jumamosi  Viwanja vya Leaders ambalo litashirikisha bendi 10 maarufu za hapa nchini.
 Baadhi wa wadau wa muziki wa dansi na wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
 wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 Mdau wa muziki wa dansi, Asha Baraka akizungumza katika mkutano huo kuhusu tamasha hilo la kukata na shoka ambalo alijawahi kufanyika hapa nchini.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda akizungumza na wanamuziki hao kuhusu tamasha hilo la muziki wa dansi nchini.
 Mkutano ukiendelea.
RC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wanamuziki wa dansi baada ya kuzungumza nao ofisi kwake.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-)

Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali awataka wananchi kutumia vielelezo sahihi vya Taifa

chp1 
Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo (kulia) akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)  rangi sahihi zinazotakiwa kutumika katika bendera ya Taifa wakati akielezea umuhimu wa wananchi kutumia vielelezo sahihi vya Taifa na kuachana na vile vya kughushi, kulia ni Afisa Habari toka Idara ya Habari (Maelezo) Bw. Frank Shija.
chp2 
Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa wananchi kutumia vielelezo sahihi vya Taifa na kuachana na vile vya kughushi, kushoto ni Afisa Habari toka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Nyamagori Omari
chp3 
Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo (katikati) akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)  baadhi ya vielelezo sahihi vya Taifa vinavyotakiwa kutumiwa na wananchi wakati alipokuwa akielezea umuhimu wa wananchi kutumia vielelezo sahihi vya Taifa na kuachana na vile vya kughushi mapema hii leo Jijini Dare s Salaam kulia ni Afisa Habari toka Idara ya Habari (Maelezo) Bw. Frank Shija na kushoto ni Afisa Habari toka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Nyamagori Omari.
Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo

TANZANIA YAENDELEA KUPATA MAFANIKIO KATIKA KUKABILIANA NA UGONJWA WA VIKOPE (TRACHOMA).

VIKO1Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Neema Rusibamayila akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano uliowahusiaha  Wadau wa Wizara hiyo na washirika wa maendeleo Maendeleo kutoka Mfuko wa Malkia Elizabeth unaojihusisha na utokomezaji wa Ugonjwa wa Vikope na wale wa Idara ya Kimataifa ya Maendeleo (DFID).
VIKO3Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Malkia wa Uingereza unaojihusisha na utokomezaji wa ugonjwa wa Vikope katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania Dk. Aristid Bonifield akieleza namna Mfuko huo utavyoendelea  kuisaidia Tanzania kwa kuwa inafanya vizuri katika kuhakikisha ugonjwa huo unatokomezwa nchini leo jijini Dar es salaam.
VIKO4 
Mkuu wa Idara ya Kimataifa ya Maendeleo nchini Tanzania (DFID) Vel Gnanendra akifafanua namna wadau wa maendeleo walivyojipanga kuiunga mkono Tanzania kwa kuhakikisha ugonjwa wa vikope (Trachoma) unatokomezwa nchini.
VIKO5 
Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele,   Upendo John Mwingira akizungumza wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
VIKO6Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Sightsavers kutoka Uingereza Dk. Caroline Harper akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa kutokomeza ugonjwa wa Vikope leo jijini Dar es salaam.
VIKO7 
Washiriki wa Mkutano wa Kutokomeza Ugonjwa wa Vikope kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto  na Wale wa Mashirika ya Kimataifa wakiwa katika picha ya Pamoja leo jijini Dar es salaam.
Picha/Aron Msigwa – MAELEZO.
………………………………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
 Dar es salaam.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeeleza kuwa licha ya Tanzania kuendelea kupata mafanikio katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Vikope (Trachoma) jamii bado inalojukumu la kuendelea kuzingatia na kufuata kanuni za afya kwa kufanya usafi wa mwili na mazingira ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Wadau wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele,  Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Neema Rusibamayila amesema kuwa Tanzania imepiga hatua katika kupunguza ugonjwa huo ikishirikiana na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Amesema kupitia idadi ya wagonjwa wanaougua vikope imeendelea kupungua mwaka hadi mwaka kupitia afua mbalimbali chini mpango ujulikanao kama “SAFEambao unahusisha huduma za Upasuaji,utoaji wa dawa za Antibayotiki, kuosha  pamoja na usafi wa mazingira
Ameongeza wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeweza kufanikisha upunguzaji wa ugonjwa huo kwa kutoa dawa/tiba kinga kwa wananchi katika maeneo yaliyoathirika ambapo amesema kufuatia utafiti uliofanyika mpaka sasa wilaya 22 ugonjwa huo umepungua sana kiasi cha wananchi wa maeneo hayo kutohitaji dawa za tiba kinga.

Kampuni ya TBL kuendelea kufanikisha utoaji elimu ya usalama katika jamii

JIS1 
Afisa Mwandamizi kutoka Kitengo cha Elimu katika Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani , ASP. Mossi Ndozero akitoa Elimu ya usalama barabarani kwa baadhi ya walimu wa shule za Mkoa wa Mwanza yaliyofanyika katika Chuo cha Polisi Wanamaji jijini Mwanza yaliyoendeshwa na jeshi hilo chini ya udhamini wa kampuni ya TBL Group.
JIS2 
SGT Bahati Nzunda akitoa somo kwa walimu wakati wa mafunzo hayo.
JIS3 JIS4 
Baadhi ya walimu wakifanya mazoezi katika makundi
JIS5 
Walimu wakifuatilia mafunzo ya usalama barabarani
…………………………………………………………………………………………………….
Kampuni ya TBL Group imetangaza  kuwa itaendelea kutoa elimu ya Usalama katika maeneo yake ya kazi na kwa jamii ili kuhakikisha matukio ya ajali zisizo za lazima zinapungua hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na  Meneja wa Usalama kazini wa kiwanda cha  TBL cha mjini Mwanza,Bw.Method Marco  wakati akielezea mafunzo ya usalama ambayo yamefadhiliwa na kampuni kwa ajili ya walimu wa shule za msingi na sekondari na wakaguzi wa magari kutoka Jeshi la polisi nchini mkoani humo.
Bw.Method alisema linapokuja suala la usalama na afya haliwahusu wafanyakazi wa kampuni na familia zao tu bali kwa jamii nzima kwa kuwa wafanyakazi wa TBL Group ni sehemu ya jamii  na wanaishi kwenye jamii.
“Sera za kampuni yetu zinahimiza kulipa kipaumbele mkubwa suala la Usalama na afya sio kwa wafanyakazi tu bali usalama wa jamii nzima na ndio maana kampuni imekuwa mstari wa mbele kufadhili na kushiriki katika kampeni mbalimbali za usalama na miradi ya Afya na Mazingira”.Alisema Marco.
Kuhusiana na ufadhili wa  semina ya wakaguzi wa magari kutoka Jeshi la polisi  na walimu wa shule  za msingi na ekondari alisema kuwa kampuni imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na taasisi hizo kuhusiana na masuala ya usalama hususani kampeni za usalama barabarani lengo kubwa likiwa ni kupunguza matukio ya ajali nchini.
Moja ya lengo lengo letu tunalotekeleza ni kuhamasisha unywaji wa kistaarabu kwa jamii hivyo kama kampuni inayotengeneza vinywaji tunalo jukumu la kuelimisha masuala ya usalama kwa ujumla na tunaamini Jeshi la polisi kama msimamizi wa masuala ya usalama barabarani nchini linapaswa kuungwa mkono na kupewa ushirikiano mkubwa kuhakikisha linafanikisha kufikisha elimu ya usalama na usalama barabarani kwa wananchi wengi.
Kwa upande wa walimu na wanafunzi alisema kuwa kampuni itaendelea kushirikiana nao  ikiwemo wadau wengine kuhakikisha  wanapata elimu ya usalama barabarani “Ukifundisha walimu ni rahisi elimu hii kuwafikia wengi na wanafunzi wakipata elimu ya awali ya masuala ya usalama na usalama barabarani wanakua wakiwa na uelewa mpana wa kujikinga na kuchukua tahadhari.
Alisema suala la kuelimisha jamii kuhusiana na usalama barabarani ni  jambo ambalo kampuni ya TBL Group itaendelea kulivalia njuga kwa nguvu zote kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na wadau wengine

Kampuni ya Tigo yakabidhi vifaa vya michezo kwa chama cha mpira wa miguu wilaya iringa vijijini

Katibu wa chama cha mpira mkoani iringa (IRFA) Ramadhani Mahano akiwa na Meneja wa kampuni ya Tigo kanda  ya Kusini DAVIS KISAMO na kulia ni katibu wa chama cha mpira iringa vijijini JUMA LALIKA wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa chama cha mpira wa miguu wilaya iringa vijiji kwa ajili ya mashindano ya ligi  daraja la pili, Tigo  ndio wadhamini wa mashindano hayo.

 Meneja wa kampuni ya Tigo kanda  ya Kusini DAVIS KISAMO na katibu wa chama cha mpira iringa vijijini JUMA LALIKA wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa timu shiriki

 Katibu wa chama cha mpira iringa vijijini JUMA LALIKA akimshuru meneja wa kampuni ya Tigo kanda  ya Kusini, DAVIS KISAMO mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo kutoka kampuni ya tigo wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa chama cha mpira wa miguu wilaya iringa vijiji kwa ajili ya mashindano ya ligi  daraja la pili, Tigo  ndio wadhamini wa mashindano hayo.

Meneja wa kampuni ya Tigo kanda  ya Kusini, DAVIS KISAMO akizungumza na baadhi ya viongozi wa timu shiriki zinazoshiri ligi ya wilaya ya iringa vijijini.
Meneja wa kampuni ya Tigo kanda  ya Kusini DAVIS KISAMO akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwakabidhi vifaa vya michezo kwa viongozi wa chama cha mpira wa miguu iringa vijijini

Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge na Watu wenye Ulemavu kuhamia Dodoma wiki ijayo

JES1 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Kushoto) akiongea leo jijini Dar es Salaam na Watendaji Wakuu na Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu utekelezaji wa kuhamia Dodoma, Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Dr. Abdallah Possi.
JES2 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Kushoto) akiongea leo jijini Dar es Salaam na Watendaji Wakuu na Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu utekelezaji wa kuhamia Dodoma, Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Dr. Abdallah Possi.
JES3 
Baadhi ya Watendaji Wakuu na Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Jenista Mhagama wakati wa kikao kuhusu utekelezaji wa kuhamia Dodoma.
……………………………………………………………………………………………………….
Na Jonas Kamaleki, MAELEZO
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu,Bunge, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu itahamia Dodoma juma lijalo kufuatia agizo la Mhe. Rais John Pombe Magufuli la Serikali kuhamia Dodoma.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi ,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati akiongea na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizoko chini ya ofisi hiyo.
“Mchakato wa kuhamia Dodoma umekwisha kilichobaki kwa sasa ni utekelezaji, mimi na manaibu mawaziri wangu tunahamia juma lijalo ili tukamkaribishe Mhe. Waziri Mkuu anayehamia Septemba mwaka huu,” alisema Mhagama.
Mhagama amesema kuwa kila kiongozi anayehamia Dodoma inabidi awakute walio chini yake tayari wamekwishahamia ili kumpokea, hivyo akawataka na watendaji ambao wako chini yake watangulie kwa ajili ya kumpokea yeye na viongozi wenzake.
Aidha, Waziri huyo amesema kwa sasa hakuna mjadala wa kuhamia Dodoma lilobaki ni utekelezaji  tu wa kuhamia Makao Makuu.
Mhagama amesema kama kuna Taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu imetenga fedha kwenye bajeti kwa ajili ya ujenzi, shughuli hiyo ikafanyike Dodoma ambako Serikali inahamia. Kwa kusema hivyo kadhalika na ofisi au Wizara nyingine za serikali ambazo zimetenga fedha ya ujenzi wakajenge Dodoma.
Suala la kuhamia Dodoma sio geni bali limekewepo kwa kipindi kirefu ila utekelzaji wake ndio ulikuwa bado; pia katika Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 suala hili lipo, alisema Mhagama na kuongeza kuwa kipindi cha nyuma Wizara saba (7) ziliwahi kuhamia Dodoma na kwa sasa Wizara inayoshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) iko Dodoma.
Waziri Mhagama ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuanza ujenzi wa jengo lake mjini Dodoma na kusisitiza kuwa Wizara na Taasisi nyingine za Serikali kuiga mfano huo kwa kujenga ofisi zao Dodoma.
“Kwa kuwa sisi ni waratibu wa wizara zote inabidi tuunde kikosi kazi kitakachofanya kazi ya uratibu wa kuhama kikiwa Dodoma ili kuwawezesha na watumishi wenzetu kutekeleza agizo la Mhe. Rais la serikali nzima kuhamia huko,”alisema Mhagama.
Mhagama amesema kuwa Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma (CDA) wameshafanya kazi nzuri ya upimaji eneo la serikali ambalo litatumika kwa ajili ya ofisi.
“Tumefika mwisho wa mchakato sasa ni utekelezaji na tunataka watumishi walielewe vizuri suala hili na wawe tayari kulipokea,”alisisitiza Mhagama.
Kuhamia Dodoma katika kipindi hiki kunatokana na agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alillolitoa tarehe 25 Julai, 2016 mjini Dodoma kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ambo ulimchagua kuwa Mwenyekiti wa tano wa chama hicho tawala.

DC BAGAMOYO AJITUA MZIGO WA MADAWATI ,AOKOA MAMILIONI YA FEDHA

index 
Mmoja wa wadau waliochangia madawati wilayani Bagamoyo, afisa uhusiano wa kampuni ya MMI ,Abubakar Mlawa ,akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo, madawati 1,200 yaliyochangiwa na kampuni hiyo.(Picha na Mwamvua Mwinyi)index 
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,alhaj Majid Mwanga ,wa kwanza kushoto ,wa pili afisa mahusiano wa kampuni ya MMI Abubakar Mlawa na wa tatu ni mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo na wengine wakiangalia madawati 6,946 yaliyokabidhiwa na mkuu wa wilaya huyo juzi wilayani Bagamoyo. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
……………………………………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
MKUU wa wilaya ya Bagamoyo,alhaj Majid Mwanga amekabidhi madawati 6,943 yenye thamani ya sh.Mil 557.6 kwa mkuu wa mkoa wa Pwani ,ambayo yatagawanywa katika shule za msingi na sekondari wilayani humo.
Alhaj Mwanga amesema madawati hayo yametolewa na wahisani mbalimbali hivyo kuokoa kiasi hicho ambacho kingetumika kutolewa na serikali ya wilaya hiyo.
Akikabidhi madawati kwa mkuu wa mkoa wa Pwani ,Mhandis Evarist Ndikilo,alisema amefanikiwa kuokoa fedha hizo baada ya wilaya yake kuzungumza na wahisani na wadau ambao walikubali kuchangia fedha zote.
Alhaj Mwanga aliwataja waliochangia kuwa ni pamoja na kampuni ya MMI, kampuni ya IPP,  madiwani,  wakuu wa Idara,  TANAPA, TASAF na wadau wengine wa ndani na nje ya wilaya hiyo .
Alieleza kuwa kati ya madawati 6,943 ,madawati 2,036  ni kwa ajili ya shule za sekondari ambayo yamegharimu kiasi cha sh.115.9.
Aidha alisema,  kwa upande  shule wa shule za msingi ni madawati  4,907 yametengenezwa kwa gharama ya sh.mil.441,630,000 .
Alhaj Mwanga alisema, baada ya kukamilisha zoezi hilo sasa wanajipanga kutatua  tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa ulipo katika baadhi ya shule  wilayani hapo.
“Nawashukuru wahisani wote ,na natumia nafasi hii jamii ijenge tabia ya kushirikina katika kuchangia masuala ya kijamii na elimu ili kuinua maendeleo ya wilaya yetu pasipo kujali itikadi zetu” alisema alhaj Mwanga.
Akipokea madawati hayo ,mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Ndikilo alimpongeza mkuu huyo wa wilaya na watendaji wake kwa kukamilisha zoezi hilo.
Mhandisi Ndikilo alieleza kuwa katika mkoa huo  zoezi la madawati kwa upande wa shule za sekondari limekamilika na lipo kwenye hatua za mwisho.
Alisema  madawati ya shule za msingi zoezi bado linaendelea ambalo linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu.
Mhandisi Ndikilo aliwataka walimu wakuu wa shule kuzingatia utunzaji wa madawati hayo na kuwaasa maafisa tarafa ,watendaji wa kijiji na kata kusimamia vizuri madawati hayo.

ASKARI ALIYEMUUA MWANAHABARI DAUDI MWANGOSI AFUNGWA JELA MIAKA 15

Ndugu  wa Marehemu  Daudi  Mwangosi  mama Mfugale  kushoto  akitoka mahakama  kuu kanda  ya  Iringa akiwa na furaha baada ya  hukumu ya  kesi  hiyo  kutolewa leo kwa askari  aliyeuwa  kufungwa  jela miaka 15 Picha zote na MatukiodaimaBlog
Mjane  wa marehemu Daudi  Mwangosi Itika Mwangosi mwenye  kilemba cheusi  akiwa katika  foleni ya ukaguzi  wa polisi ili   kuingia mahakama kuu kanda  ya  Iringa leo
Mjane  wa marehemu Daudi  Mwangosi Itika Mwangosi mwenye  kilemba cheusi  akiwa katika  foleni ya ukaguzi  wa polisi
Mjane  wa marehemu Daudi  Mwangosi Itika Mwangosi mwenye  kilemba cheusi  akifurahi jambo na ndugu  yake  mzee Marko Mfugale mahakamani  hapo  leo
Rais  wa umoja  wa klabu  za waandishi wa habari Tanzania Bw  Deo Nsokolo  akizungumza na wanahabari  baada ya hukumu ya kesi ya mauwaji  ya  Mwangosi
Wanahabari  mkoa wa Iringa  wakimsikiliza Bw Nsokolo leo
Wanahabari  wakiwa nje ya viwanja  vya mahakama baada ya  kesi  kumalizika

Mjane  wa Mwangosi Itika  Mwangosi  mwenye  kilemba  akitoka mahakamani hapo huku akiwa na uso wa furaha  baada ya  hukumu  kutolewa kwa  muuaji kufungwa miaka 15  jela
Mjane  wa Mwangosi  akiwa katika  viwanja  vya mahakama  kuu kanda  ya Iringa
Mjane  wa marehemu Daudi Mwangosi  akizungumza na  wanahabari ikiwa ni  pamoja na  kuwashukuru kwa  umoja  wao
Rais  wa UTPC Deo  Nsokolo akiwa na mtaalam wa IT Lukelo Mwaipopo leo nje ya mahakama kuu kanda  ya Iringa 

JAJI MKUU ATEMBELEA JENGO LA MAHAKAMA YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI LEO

CHAN1 
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (Katikati) akimsikiliza Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania, Khamadi Kitunzi akimuelezea jambo alipotembelea jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililoko kwenye Shule ya Sheria (Law School) Sinza jijini Dar es salaam. Kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Ferdinand Wambali. 
CHAN2 
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (Katikati) akimuelezea jambo Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga alipotembelea  jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililoko kwenye Shule ya Sheria (Law School) Sinza jijini Dar es salaam. Kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Ferdinand Wambali. 
CHAN3 
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (Katikati) akimuelezea jambo Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga alipotembelea  jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililoko kwenye Shule ya Sheria (Law School) Sinza jijini Dar es salaam. Kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Ferdinand Wambali. 
CHAN4 
Hili ni jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililopo kwenye Shule ya Sheria (Law School) Sinza jijini Dar es salaam.

NAY WA MITEGO AFUNGIWA KUJIHUSISHA NA KAZI ZA SANAA KWA MUDA USIOJULIKANA, ATOZWA FAINI YA TSH. MILIONI 1

nay 
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia kwa kipindi kisichojulikana Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kwa jina la Nay wa Mitego hadi hapo litakapojiridhisha kwamba ametekeleza maagizo yote aliyopewa na Baraza sambamba na yeye kubadilika katika kubuni kazi zenye maadili na zisizo dhalilisha watu wa kada mbalimbali.
Maagizo aliyopewa Msanii Nay ni pamoja na kulipa faini (adhabu) ya kiasi cha Shilingi milioni 1, kufanya marekebisho ya mashairi ya wimbo wake wa ‘Pale Kati’, kufuata sheria, kanuni na taratibu za urasmishaji sekta ya Sanaa kwa maana ya kusajiliwa na BASATA na kuhakikisha wimbo wake umefuata taratibu zote.
Aidha, Msanii Nay ameagizwa kuwaomba radhi watanzania kwa kutoa kazi ya muziki yenye kuvunja maadili na kudhalilisha watu wa kada mbalimbali hususan wanawake.
Maamuzi haya yamefanyika kwa mujibu wa kifungu cha 4(2) cha sheria nambari 23 ya mwaka 1984, ikisomwa pamoja na kifungu cha 30(1)(2) na waraka wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo wa tarehe 16/7/2009 ambayo kwa sasa inafahamika kama Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Adhabu hizi zimetolewa kufuatia BASATA kufanya kikao cha pamoja na Msanii huyu jana siku ya Jumanne tarehe 26/07/2016 kwenye Ukumbi wa Baraza na yeye kukiri makosa na kuahidi kubadilika.
Makosa aliyosomewa na yeye kuyakiri kwa maandishi ni pamoja na;
  1. Kujihusisha na shughuli za Sanaa pasipo kusajiliwa na BASATA.
  2. Kutoa wimbo wa “Pale Kati” na kuupakia katika mitandao ya kijamii bila kuuleta kufanyiwa uhakiki wa maudhui yake.
  3. Maudhui ya wimbo wa ‘Pale Kati’ kwa sehemu kubwa hayafai kwa matumizi ya wazi na ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya mtanzania.
Ikumbukwe kwamba mnamo tarehe 16/07/2016 BASATA lilitoa taarifa kwa umma ya kuufungia wimbo wa Pale Kati kufuatia kubeba maudhui yenye uvunjifu mkubwa wa maadili na kupambwa na picha dhalilishi kwa wanawake.
Aidha, tarehe 12/02/2016 BASATA liliufungia wimbo wa Shika Adabu Yako wa Msanii huyuhuyu kwa makosa yanayofanana na haya. Hivyo adhabu hii imetolewa ili kumpa muda wa kujifunza, kujitathimi na kujirekebisha kama kweli ana nia ya kuendelea kufanya kazi ya muziki
SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI
Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA

MKOA WA PWANI WAZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUPAMBANA NA VVU NA UKIMWI

index 
Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo akionyesha kitabu cha taarifa cha mpango mkakati wa kudhibiti virusi vya ukimwi na ugonjwa wa ukimwi ,mpango ambao ni wa miaka mitano ijayo ,baada ya kuzindua mpango huo jana katika mkutano  maalum wa kazi.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
……………………………………………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo amezindua mpango mkakati wa kudhibiti ukimwi wa miaka mitano ijayo lengo likiwa kupambana na maambukizi mapya ya gonjwa hilo.
Amesema mkoa huo ni miongoni wa mikoa  kumi nchini iliyo na kiwango cha maambukizi ya virusi  vya ukimwi juu ambapo una kiwango cha asilimia 5.9 wakati kitaifa ni 5.1.
Mhandisi Ndikilo aliyasema hayo ,katika mkutano  maalum wa kazi ambao agenda juu ilikuwa  ni kuzindua mpango huo ,uliofanyika  ukumbi wa mikutano uliopo ofisi  ya mkuu wa mkoa wa Pwani,Kibaha.
Alielezea kuwa taarifa ya matokeo ya tathmini ya maambukizi ya VVU kitaifa iliyofanyika mwaka 2011/2012 mkoa huo ulikadiriwa kuwa na kiwango cha maambukizi ya VVU kwa kiasi hicho ambacho ni kikubwa.
Mhandisi Ndikilo alisema kwa kuanza na mpango mkakati huo utasaidia kupunguza kiwango cha maambukizi ya virusi hivyo mkoani hapo.
“Huu ni mwitiko wa agizo alilolitoa rais  mstaafu wa awamu ya nne  Jakaya Kikwete alipozindua taarifa ya matokeo ya utafiti wa viashiria vya VVU na ukimwi na malaria THMIS mwaka 2011/2012”
Mhandisi Ndikilo alisema Kikwete aliagiza kila mkoa uandae mpango mkakati wa kudhibiti ugonjwa huo hatari ambao utalenga kudhibiti vichocheo vya maambukizi kulingana na eneo husika.
Alitaka mkakati ufanyiwe kazi na utekelezaji kwa vitendo pasipo kuuweka kwenye makabati na kuishia kwenye makabrasha.
Aidha mhandisi Ndikilo aliwaomba viongozi wa dini mkoani humo  kushirikiana na serikali kuhubiri kwa waumini kuwa na maadili mema na kuachana na ngono zembe.
“Mapadre na mashehe nyie pia ni msaada mkubwa  kusaidia hili  ,nawaomba tushirikiane kwa hili  licha ya vitabu vya dini kutokubaliana na masuala haya hasa  ya kuhubiri matumizi ya kondom  ” alisema mhandisi Ndikilo.
Mkuu huyo wa mkoa alitoa ushauri wa kutumiwa kwa vikundi vya sanaa  na maigizo ili kufikisha ujumbe wa jamii kupitia sanaa.
Alikemea  vigodoro na mikesha isiyo na tija  ambayo baadhi ya watu huitumia vibaya na kusababisha kuugua magonjwa ya zinaa na ukimwi.
Mratibu wa ukimwi mkoani Pwani Grace Tete alieleza kuwa watahakikisha wanatekeleza mpango huo pasipo kuishia kwenye makabati.
Grace alisema mpango huo utekelezaji wake ni hadi ifikapo 2020 na unalengo la  kufikia sifuri 3 ambazo ni maambukizi mapya,ya unyanyapaa na sifuri ya vifo  vitokanavyo na ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Alisema mpango mkakati utatumiwa na halmashauri zote za mkoa kuanzia sasa ili kukabiliana na janga la  gonjwa hilo.
Nae msaidizi wa shehe  mkuu na kadhi wa mkoani hapa ,Hamis Mtupa aliwaasa wanandoa waache michepuko na badala yake wawe waaminifu kwenye ndoa zao ili kujiepusha na magonjwa ya zinaa.
Mtupa alisema kuhusu agizo la  mkuu wa mkoa wamelipokea hivyo ametoa wito kwa viongozi wengine wa dini kutenga sehemu ya kutoka elimu juu ya ukimwi.

NMC ARUSHA NI MALI YA SERIKALI

images 
Na Mahmoud Ahmad Arusha
SERIKALI,imesema kuwa kinu cha kusaga mazao cha shirika la taifa la usagishaji,NMC ,cha Arusha hakijauzwa kama ilivyoenezwa na kitaendelea kuwa mali ya serikali na kwamba anaendesha kinu hicho ni mpangishaji na si vingine.
Hayo yameelezwa na msajili wa Hazina, Lawrance Mafuru, alipokuwa akikabidhi umiliki wa kinu hicho  cha  kusaga nafaka cha NMC ,cha Arusha kutoka kwa shirika hodhi la mali za serikali, CHC,kwenda kwa bodi ya Nafaka na mazao mchanganyiko. .
Mafuru, amesema uamuzi huo wa kukabidhi umiliki wa kinu hicho kwa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko ni maelekezo ya serikali kwa ajili ya kukiendeleza kinu hicho na vingine vilivyopo, Mwanza, Iringa na Dodoma.
Amesema kuwa bodi hiyo ambayo ni mmiliki mpya itakuwa na jukumu la kukiendesha kinu hicho  itapitia mkataba wa upangaji na kampuni ya uwekezaji ya Monaban Trading Company limited kwa kuwa hiyo ni sehemu ya biashara.
 Amesema kabla ya kukikabidhi kinu hicho kwa mmiliki mpya  walijiridhishwa kwa kufanya  uhakiki wa vitu vilivyopo.
Mafuru,amevitaja vinu vingine ambavyo havitabinafisishwa na vitabakia kuwa ni mali ya serikali ni pamoja na shirika la usagishaji la taifa NMC, Mwanza, NMC,Dodoma na NMC,Iringa ,ambavyo navyo vimekabidhiwa kwa mimiliki mpya ambayo ni bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko.
Ameongeza kuwa kinu hicho cha NMC ,Arusha, kilipangishwa mwaka  2008 kwa kampuni ya Monaban Trading limited,kutokana na uamuzi wa serikali uliofanywa kwa wakati huo lakini sasa  mali zote za shirika la usagishaji la taifa hazitauzwa zitabakia kuwa mali ya serikali.
Nae Kaimu mkurugenzi mkuu wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko, John Damasi  Maige, amesema bodi hiyo itasimamia shughuli zote za kinu hicho pia watazingatia mkataba unaomwezesha mpangaji kampuni ya Monaban  kuendesha kinu hicho.
Amesema kuwa  mara baada ya kupitia mkataba na mpangaji ambae ni kampuni ya Monaban Trading Compan Limited,kuna mambo watakubaliana kwa masilahi ya pande zote mbili.
Maige, amesema kuwa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko  inaendesha maghala yaliyopo Dodoma, na kufufua mashine za kusagisha zilizopo NHC Mwanza,ambacho kilikuwa ni kwa ajili ya kusagisha  na kusindika mpunga, kinu cha Dodoma kilikuwa cha kusagisha na kusindika mtama .
Lengo la kuvifufua  ni kuviwezesha kufanya kazi na hivyo kutoa ajira hasa kwa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Monabani Trading Limited, Gerad Mandala, amesema watashirikiana na mmiliki mpya kwa kuwa kinu hicho ni mali ya serikali na kiwanda kitaendelea  kama kawaida.
Akawaondoa hofu wananchi kwa kueleza kuwa kampuni ya Monaban ni mpangaji na ina mkataba wa muda mrefu  na itaendelea kuwa msagishaji wa nafaka na mazao mengine hivyo wananchi wataendelea kupata huduma ya unga na mahitaji mengine kama kawaida..

NHC ARUSHA YAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUWEKEZA MRADI WA SAFARI CITY

index 
Na Mahmoud -Ahmad Arusha
Shirika la nyumba la Taifa limeanza ujenzi wa nyumba za mfano kwa ajili ya uwekezaji wa
pamoja na wananchi katika kata ya Olmort jijini hapa mradi utakaojulikana kama
Safari city huku likikaribisha wananchi kuja kuwekeza kwenye mradi huo.
Akizungumza na vyombo vya habari Meneja wa shirika hilo mkoani hapa James Kisarika alisema
kuwa mji huo unajengwa kwa awamu na utakuwa na vitu vyote jamii inavyohitaji
ikiwemo maji, umeme na mtambo wa kuchakata maji taka.
Alisema kuwa kila kiwanja kitakuwa na huduma za bomba la maji,utengenezaji wa
barabara,uandaji wa hati miliki pamoja na michoro huku katika awamu ya kwanza
shirika likitoa haki za uendelezaji wa viwanja vyenye ukubwa wa mita za mraba
200-600 na yatapatikana kwa shilingi 35,000 tu kwa mita moja ya mraba.
“Mji huu ni miongoni mwa miji ya kisasa hapa nchini na utaweza kusaidia watu wa kada mbali
mbali kupata kumiliki nyumba na kujenga sisi tutakuwa wasimamizi wa mradi huu”alisema
kisarika
Alisema kuwa ili kuwa mmoja wa wawekezaji katika mradi huo unapaswa kufuata utaratibu kwa
kuchukuwa fomu ambayo ni bure na inatolewa na shirika hilo popote hapa nchini au
tembelea tovuti yao www.thesafaricity.comna utalipia asilimia 25% ya thamani ya kiwanja unachotarajia kununua.
 Aidha shirika la nyumba la taifa kupitia mradi huo linatoa fursa kwa makundi mbali
mbali ya wawekezaji wenye mahitaji ya uendelezaji wa nyumba za makazi kwa
vipato tofauti(chini,kati,na juu) majengo ya ofisi na biashara,maduka makubwa(Shoping
mall)pamoja na madogo,maeneo ya biashara,maendeleo ya viwanda vidogo
vidogo,burudani na utalii,Hospital.uwanda wa elimu,sanjari na huduma zote za
kijamii.
Baada ya  hayo wanahabari walipata fursa ya kutembelea eneo hilo na kujionea ujenzi
wa nyumba za mfano za mradi huo ikiwemo nyumba za makazi nafuu ambazo zitakuwa
za mfano kwa nyumba za makazi ambazo wawekezaji hao watatakiwa kujenga kwa
mfano huo.
Kutakuwepo na eneo la msitu pamoja na mashine maalumu ya kuchakata maji taka ambayo baada
ya kuyachakata maji hayo yatatumika tena kwa ajili ya umwagiliaji kwenye mradi
huo.

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA SEKRETARIETI NA WAFANYAKAZI WA CHAMA DODOMA MJINI DODOMA

Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa mara baada ya kuwasili makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa mara baada ya kuwasili makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na wafanyakazi wa makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana akisikiliza maoni na changamoto toka kwa wafanyakazi wa makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo

SERENGETI BOYS YATUA SALAMA MADAGASCAR

Msafara wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, uliondoka jana alfajiri Dar es Salaam, Tanzania imetua salama jijini Antananarivo, Madagascar kwa ajili kambi ya siku 10 kujiandaa na mchezo dhidi ya Afrika Kusini kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Agosti 6, 2016.

Mchezo wa marudiano utafanyika Agosti 21, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam, ulioko Chamazi-Mbagala, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kwamba mshindi atakuwa amejiwekea mazingira mazuri ya kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana, zitakazofanyika mwakani huko Madagascar.

Mkuu wa msafara akiwa ni Ayoub Shaibu Nyenzi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Vijana, maofisa wengine waliosafiri na timu hiyo ni Kocha Mkuu, Bakari Nyundo Shime maarufu zaidi kwa jina la Mchawi Mweusi, Daktari wa timu hiyo, Shecky Francis Mngazija na Mtunza Vifaa, Andrew Vanance Andrew.

Pia yumo Juma Kaseja Juma ambaye kwa muda amechukua nafasi ya makocha wasaidizi, Sebastian Nkoma na Muharam Mohammed ‘Shilton’ wanaohudhuria kozi ya makocha ngazi ya juu inayoratibiwa na CAF.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MWENYEKITI PAMOJA NA KATIBU WA TUME YA UTUMISHI WA WALIMU (TSC) IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA

chm1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Oliva Joseph Mhaiki kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
chm3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Winfrida Gaspa Rutaindurwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
chm5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Oliva Joseph Mhaiki (kushoto) pamoja na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Winfrida Gaspa Rutaindurwa (kulia) mara baada ya kuwaapisha ) katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.

MAAGIZO KWA KLABU ZA LIGI KUU, LIGI DARAJA LA KWANZA

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine ameziasa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutimiza masharti ya kupata vibali vya kuishi na kufanya kazi Tanzania kwa wachezaji na wataalamu wa kigeni wakiwamo makocha na madaktari kabla ya kuingia nao kandarasi za ajira.

Masharti hayo ni vibali vya kufanya kazi nchini, visa za kuishi nchini, vibali vya kucheza mpira wa miguu nchini, vibali vya kufundisha mpira na vibali vya watalaamu wengine kama madaktari na hayo ni kwa mujibu wa Idara ya Uhamiaji na mamlaka nyingine za serikali na kanuni za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini ,TFF.

“Mchezaji au mtaalamu ye yote anapokuja nchini na kuanza mazoezi na timu yo yote anachukuliwa yuko kazini. Tusingependa watu wapate usumbufu. Kama Katibu Mkuu na mtendaji mkuu, nimepata maelekezo kutoka mamlaka zinazohusika kuwa nifuatiulie kuwa TFF kamamratibu mkuu wa mchezo wa mpira wa miguu ina jukumu la kuhakikisha wanachama wake wanafuata taratibu.natakiwa kufuatilia,” amesema Selestine.

“Vilabu vihakikishe vyeti vya taaluma vinawasilishwa TFF kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kutiliana kandarasi na wachezaji au walimu. . Ni vema wakafanya uratatibu wa kuhakiki Hii itaviepusha vilabu na gharama za fidia au kesi za madai endapo mamlaka za serikali au za mpira zitasita kumruhusu mhusika kufanya kazi nchini,” amesema.

Vilevile Katibu Mkuu wa TFF amezitaka klabu kumalizana na wachezaji na wataalamu zinaoachana nao kabla ya kufikiria kuingiza wapya.TFF tayari ina barua kadhaa za madai ya wachezaji na watumishi wa vilabu waliomaliza au kukatishwa mikataba yao bila kulipwa mafao yao.TFF inawataka kumaliza masuala haya ili kuweza kujikita vema katika kupanga safu zao kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi.

Wakati huohuo, huo huo TFF imeagiza klabu kuendelea na usajili kabla ya Agosti 6, 2016 ambayo itakuwa siku ya mwisho na kwamba hakutakuwa na muda wa kuongezwa kwa klabu ambayo itashindwa kukamilisha usajili kwa wakati.

No comments :

Post a Comment