Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla (kulia) akizungumza na viongozi wa mfuko wa Abbott (Abbott
Fund) kutoka Marekani na Tanzania waliomtembelea Ofisini kwake jijini
Dar es salaam leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya uboreshaji wa huduma
za Afya na Elimu kupitia program mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo
nchini. Kutoka Kulia ni Makamu Mtendaji wa Rais wa Mfuko wa Abbott,
Stephen Fussell na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott
Fund Bi.Elaine Leavenworth (katikati).
Makamu
wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund) Bi.Elaine
Leavenworth (kulia) akimweleza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) juu ya namna
Mfuko wa Abbott ulivyojipanga kuendelea kutekeleza Program mbalimbali
nchini Tanzania zikiwemo za Matumizi ya Teknolojia ya kisasa katika
utoaji wa Tiba, maabara za kisasa, dawa na vifaa vya mafunzo kwa
wanafunzi wa masomo ya Sayansi.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla (kulia) akifurahia jambo na Makamu wa Rais Mwandamizi wa
Mfuko wa Abbott (Abbott Fund) Bi.Elaine Leavenworth (kulia) leo jijini
Dar es salaam mara baada ya kutembelewa na ujumbe wa viongozi wa mfuko
huo kutoka nchini Marekani.
Ujumbe
wa viongozi wa mfuko wa Abbott (Abbott Fund) kutoka Marekani
ukimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake
leo.
Makamu
wa Rais wa Mfuko wa Abbott (Abbot Fund) nchini Tanzania Andy Wilson
akielezea utayari wa Mfuko huo katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto
zinazoikabili sekta ya Afya na Elimu nchini kupitia ufadhili wa Programu
mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo kwa niaba ya Watu wa Marekani.
PICHA/ Aron Msigwa –MAELEZO.
NAIBU WAZIRI HAMAD MASAUNI AONGOZA KIKAO CHA KUJADILI MKAKATI WA KUPUNGUZA AJALI NCHINI
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni
akizungumza katika kikao cha Baraza hilo cha kujadili Mkakati wa
Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni
Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama
Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha zote na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto
meza kuu) akimsikiliza Mjumbe wa Kikao hicho, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo
cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dk. Zakaria Mganilwa (kulia)
alipokuwa anachangia mawazo katika Kikao cha kujadili Mkakati wa
Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni
Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama
Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni
akizungumza katika kikao cha Baraza hilo cha kujadili Mkakati wa
Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuriwa na
wajumbe mbalimbali wa Baraza hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto
meza kuu) akimsikiliza Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkuu wa
Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga
(kulia meza kuu) alipokuwa akizungumza katika Kikao cha kujadili Mkakati
wa Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MRADI WA HARAMBEE NI MKOMBOZI WA WANANCHI WA KIJIJI CHA CHOLE, MAFIA – PWANI
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole,
Shehari Ahmadi akielezea waandishi wa habari maendeleo ya kijiji cha
Chole ikiwa ni pamoja na kutolea ufafanuzi suala la kauli iliyoleta
mkanganyiko hivi karibuni ya kuwa mwekezaji amemilikishwa mapango ya
kale kinyume cha sheria jambo ambalo si halina ukweli wowote kwa vile
linachafua sura ya kijiji chao. Picha zote na Cathbert Kajuna wa
Kajunason Blog.
—
Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog – CHOLE, MAFIA.
—
Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog – CHOLE, MAFIA.
Wananchi wa kijiji cha Chole, wilayani Mafia – Pwani wameusifia mradi wa Harambee unaowapatia elimu watoto wao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
na Kajunason Blog iliyoweka kambi kijijini hapo kujionea hali halisi ya
kisiwa hicho, wananchi hao walisema ujio wa mwekezaji umekuwa mkombozi
wa wanachi kwa vile ni mambo mengi waliyofaidika kwa muda wote ambao
amekuwepo mwekezaji kijijini hapo.
Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati
ya Harambee, Hamis Musa Athuman alisema mpaka sasa zaidi ya Sh. milioni
500 zimetumika kugharimia ada na mahitaji muhimu ya wanafunzi shuleni wa
kijiji cha Chole, kupitia mradi huo.
Aliongeza kuwa pesa hiyo imeweza kuwafikia jumla ya wanafunzi wapatao 300.
Mwenyekiti mstaafu wa kijiji cha
Chole (kulia) ambaye alianza kazi yake 1999 – 2014, Bw. Maburuki Sadiki
aliishukuru kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development kwa
kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kuwajengea shule ya msingi,
Zahanati, shule ya ChekeChea, Darasa la watu wazima kujifunza kingereza,
watoto kwenda sekondari na mengine mengi. Pembeni ni mwenyekiti wa sasa
Shehari Ahmadi.
Mkazi wa kijiji cha Chole, Bi. Riziki Hassan Selenge ambaye anasomeshewa watoto wake wawili na Mfuko wa maendeleo wa Harambee.
Mkazi wa Chole, Bw. Johari Rajabu Fadhil ambaye ndiye mmoja ya waasisi waliompokea mwekezaji, na aliweza kupata ufadhili wa kwenda kusoma masomo ya kufundisha watoto ya miaka 2.
Mkazi wa kijiji cha Chole, Bi. Riziki Hassan Selenge ambaye anasomeshewa watoto wake wawili na Mfuko wa maendeleo wa Harambee.
Mkazi wa Chole, Bw. Johari Rajabu Fadhil ambaye ndiye mmoja ya waasisi waliompokea mwekezaji, na aliweza kupata ufadhili wa kwenda kusoma masomo ya kufundisha watoto ya miaka 2.
Mkazi wa kwanza wa kijiji cha
Chole wilayani Mafia kijiji cha Chole Mjini kupata digrii ya chuo kikuu,
Zubeda Bhai akiwaelezea waandishi wa habari abato Kasika na Florence
Mugarula waliotembelea eneo hilo la kihistoria jinsi ambavyo taasisi ya
Chole Mjini Conservation and Development ilivyomsaidia gharama zote za
kupata elimu ya juu.
—
Alisema kuwa miaka ya nyuma wakazi wa Chole hawakuwa na mwamko wa elimu, lakini baadaye wakapata mwekezaji ambaye amechangia shughuli mbalimbali za maendeleo na kuwafanya wakazi wa kisiwa hicho kuwa nma mwamko wa elimu.
—
Alisema kuwa miaka ya nyuma wakazi wa Chole hawakuwa na mwamko wa elimu, lakini baadaye wakapata mwekezaji ambaye amechangia shughuli mbalimbali za maendeleo na kuwafanya wakazi wa kisiwa hicho kuwa nma mwamko wa elimu.
“Tuna mwekezaji ambaye ni kampuni
ya Chole Conservation & Development inayosimamia na kutunza magofu
ya Kijerumani, ametusaidia sana kutuamsha na sasa hapa Chole kuna mwamko
mkubwa wa elimu,” alisema Kingi.
Alisema kuwa mwekezaji huyo
aliwahamasisha kuanzia kamati hiyo ndipo ufaulu wa wanafunzi wa darasa
la saba ukaanza kuongezeka kuanzia mwaka 2007 na umekuwa ukizidi kupanda
kadri miaka inavyokwenda.
Wanafunzi wa Chekechea wakifundishwa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya
sekondari wanaonufaika na mfuko wa maendeleo wa Harambee. wakiwa pamoja
na mkurugenzi wa Kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development Bi.
Anne K. de Villiers.
Moja ya usafiri wa boti unaotumika kuwavusha wakazi wa Chole kwenda Mafia Mjini.
Wageni waliofika kutembelea kisiwa cha Chole kujionea majumba ya kizamani yenye histori za mababu zetu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee,
Hamis Musa Athuman akielezea maendeleo ya kijiji cha Chole katika
upande wa elimu akiwa na katibu wa kamati hiyo Mohamed Kingi (kulia).
Shule ya msingi ya Chole iliyojengwa na Mwekezaji wa Kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development.
Majengo ya kale yanayosimamiwa na kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development yakionekana katika sura nzuri ya utunzaji wa hali ya juu.
Mkazi wa Kijiji Cha Chole Mjini kilichopo Mafia mkoani Pwani, Faharani Shomari, akiwaonyesha picha ya magofu ya kihistoria yalivyokuwa yameharibika na yalivyo sasa baada ya kufanyiwa ukarabati na kampuni ya Chole Mjini Conservation & Development wakati waandishi hao walipoenda kutembelea eneo hilo.
Majengo ya kale yanayosimamiwa na kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development yakionekana katika sura nzuri ya utunzaji wa hali ya juu.
Mkazi wa Kijiji Cha Chole Mjini kilichopo Mafia mkoani Pwani, Faharani Shomari, akiwaonyesha picha ya magofu ya kihistoria yalivyokuwa yameharibika na yalivyo sasa baada ya kufanyiwa ukarabati na kampuni ya Chole Mjini Conservation & Development wakati waandishi hao walipoenda kutembelea eneo hilo.
Picha zikionyesha jinsi majengo ya kale yalivyoonekana kabla hayajakarabatiwa na kufanyiwa usafi.
Katibu wa Harambee wa Kijiji Cha
Chole Mjini kilichopo Mafia Mkoa wa Pwani, Mohammed Kingi akiwafundisha
wanafunzi wa Shule ya Msingi Chole. Shule hiyo pamoja na masomo hayo
yanafadhiliwa na kampuni ya Chole Conservation and Development
Kituo cha elimu ya watu wazima, hapa ndipo hujifunza kingereza.
—
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Chole Mjini Conservation & Development, Anne K. de Villiers, alisema kuwa wafadhili wa Kamati ya Harambee wako nchini Uingereza.
—
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Chole Mjini Conservation & Development, Anne K. de Villiers, alisema kuwa wafadhili wa Kamati ya Harambee wako nchini Uingereza.
Alisema kuwa aliwatafuta baada ya
kubaini kwamba wakazi wa kijiji hicho hawana mwamko wa elimu na
wamekuwa wakifadhili hata ujenzi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa
nyumba za walimu na mambo mengine ya muhimu kwa ajili ya elimu.
“Mbali na hilo kwa sasa tuna
shule ya chekechea, kituo cha wanawake cha kujufunza kusoma, kituo cha
kujifunza kompyuta na kituo cha wanafunzi na watu wengine kujifunza
lugha ya Kiingereza na maktaba,” alisema mkurugenzi huyo na kuendelea:
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole,
Shehari Ahmad alisema kuwa serikali imekuwa ikifaidika kwa kupata dola
10 kwa kila mgeni anayeingia na kulala katika hoteli ya Chole mjini
inayosimamiwa na kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development
sambamba na dola 5 kwa kila mgeni anayetembelea majengo ya kale ya
mapango ya Chole ambayo yakikuwa yakitumika katika biashara ya watumwa.
Nae Bi. Riziki Hassan Selenge
alisema kuwa hapo mwanzo mambo yalikuwa magumu tokea kuingia kwa
mwekezaji huyo ndiye amekuwa mwasisi wa maendeleo kijijini kwao kwa vile
asilimia 99 wakazi wa Chole hali zao ni masikini na hawakuweza kupeleka
shule watoto wao.
Upande wake Mwenyekiti mstaafu,
1999 – 2014, Bw. Maburuki Sadiki aliishukuru kampuni ya Chole Mjini
Conservation and Development kwa kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwa
kuwajengea shule ya msingi, Zahanati, shule ya ChekeChea, Darasa la
watu wazima kujifunza kingereza, watoto kwenda sekondari na mengine
mengi.
Akitoa historia fupi Bw. Sadiki
alisema mchakato wa kumpokea mwekezaji huyo ulifanyika Desemba 4, 1993
kwa kueleza dhamila yake na tulimkubalia kwa kufuata sheria zote na
makubaliano tuliwekeana nae tokea kipindi hicho ambapo tokea ameingia
mwekezaji huyo amekuwa akitekeleza mkataba aliyopewa na kijiji.
TAMWA kupambana na ajali za barabarani kuokoa vifo vya akinamama na watoto
………………………………………………………………………………………………………………
CHAMA cha Wanahabari Wanawake
Tanzania (TAMWA) kimezindua mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za
vyombo vya moto barabarani ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali za
vyombo hivyo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto
pamoja na jamii nzima. Akizindua mradi huo Makao Makuu ya Ofisi za
TAMWA, Sinza jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha
Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga amepongeza jitihada hizo kwani
zitasaidia kuongeza elimu juu ya masuala ya usalama barabarani na namna
ya kukabiliana na ajali.
Akizungumza awali Mkurugenzi
Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga alisema chama hicho kimeguswa
kushiriki katika mapambano ya ajali za barabarani kutokana na kuona ipo
idadi ya wanawake wengi na watoto wamekuwa wakiathiriwa na ajali hizo
kila uchao. Alisema ujio wa usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda
watumiaji wengi wa usafiri huo ni wanawake wanapokuwa katika shughuli
zao za kila siku na ndio wanaoguswa na ajali hizo.
Alisema wapo wakina mama ambao
wamekuwa wakifanya biashara zao pembezoni wa barabara kundi ambalo nalo
limekuwa likiathiriwa kwa kiasi kikubwa na ajali za barabarani
zinapotokea. Akifafanua zaidi alisema chama hicho kitajikita katika
kutoa elimu ya usalama barabarani; ikiwa ni pamoja kupinga ulevi wakati
wa uendeshaji vyombo vya moto, kuhamasisha uvaaji wa kofia ngumu
(helment) kwa waendesha pikipiki pamoja na abiria wao, kuhamasisha
ufungaji mikanda kwenye magari pamoja na kuelimisha jamii kuwa mwendo wa
kasi barabarani ni hatari.
Kwa upande wake mgeni rasmi
katika tukio hilo, Kamanda Mohammed Mpinga alisema kuna kila sababu ya
wadau kama TAMWA kujitokeza kupambana na ajali za barabarani kwani
zinamguza kila mmoja. Alisema licha ya idadi ya ajali kuendelea kupungua
mwaka hadi mwaka ukilinganisha, lakini bado kuna roho na mali za raia
zinapotea kila wakati hivyo kuna kila sababu ya elimu ya usalama
barabarani na mapambano yakafanywa kwa ushirikiano wa wadau wote.
Alitolea mfano kwa kipindi cha
miezi sita kuanzia Januari 2016, jumla ya ajali za barabarani
zilizotokea ni 5,152, ambapo vifo vilikuwa 1,580 na majeruhi ni 4,659
huku vifo hivyo vikigharimu maisha ya wanawake 301. Uzinduzi huo ambao
uliambatana na kutoa mada mbalimbali juu ya mikakati na mapambani katika
mradi huo, wakiwemo viongozi wa Serikali, madereva na mashirika anuai
yasiyo ya kiserikali pamoja na waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Bodi ya JKCI , Profesa William Mahalu apongeza utendaji wa JKCI.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete-JKCI- Profesa William
Mahalu( katikati) akiwasili ndani taasisi hiyo kwa mara ya kwanza tangu
ateuliwe na Rais John Magufuli , kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
JKCI , Profesa Mohamed Janabi na kulia ni Afisa Uhusiano wa Taasisi
hiyo Maulid Kikondo.
Profesa
William Mahalu akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika
ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Profesa Mohamed Janabi akielezea utendaji kazi wa taasisi hiyo .
Baadhi ya viongozi wa Taasisi ya JKCI wakimsikiliza Profesa Mahalu wakati akizungumza nao mara baada ya kujitambulisha .
……………………………………………………………………………………………….
Dar es salaam,
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya
Moyo ya Jakay Kikwete JKCI- Profesa William Mahalu kwa mara ya kwanza
tangu ateuliwe na Rais John Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi
hiyo ametembelea JKCI kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na
viongozi.
Katika mazungumzo hayo amewataka
viongozi wa taasisi hiyo kuwa mfano na kufanya kazi kwa bidii ili
kuendana na kasi ya Rais John Magufuli ya hapa kazi tu.
Pia amewapongeza kwa kazi kubwa
wanayoifanya katika kuhakikisha watanzania wenye magonjwa ya Moyo
wanapatiwa matibabu hapa hapa nchini hatua ambayo imepunguza gharama
kubwa ya kugharamia matibabu nje ya nchi.
SAYONA FRUITS LTD YAMPIGA TAFU RIDHIWANI KIKWETE
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa na mwakilishi wa kampuni
ya sayona fruits ltd Abubakary Mlawa kwenye moja ya meza na kiti ambavyo
alikabidhiwa kutoka kwa kampuni hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa shule za
sekondari tano jimboni humo.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akikabidhiwa viti na meza kwa
ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari tano za jimbo hilo ,kutoka kwa
mwakilishi wa kampuni ya Sayona fruits ltd ,Abubakary Mlawa huko
katika shule ya sekondari ya Lugoba .Kampuni hiyo imetoa viti 724 na
meza 724 vyote vikiwa na gharama ya mil.80.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………………………………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
MBUNGE
wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ,amepokea msaada wa viti 724 na
meza 724 kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari tano jimboni
humo.
Msaada huo umetolewa na kampuni ya Sayona fruits ltd ambapo viti na meza hizo zimegharimu kiasi cha sh.mil 80.
Aidha mdau huyo wa maendeleo ametoa madawati 1,200 yaliyogharimu sh.mil
90 ,katika shule za msingi wilayani Bagamoyo ambapo kati ya madawati
hayo 600 ni ya jimbo la Chalinze na 600 ni jimbo la Bagamoyo.
Akipokea
msaada huo,kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya sayona fruits na kampuni
mama ya MMI ,Abubakary Mlawa,mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani alisema
walimfuata mkurugenzi mtendaji wa kampuni hizo Shubash Patel ambae
amewatatulia tatizo lao.
Alieleza
kuwa ufadhili huo ni mkubwa kwani awali halmashauri hiyo ilikuwa
ikikabiliwa na mapungufu ya meza na viti 1,500 katika shule za sekondari
lakini kwasa itabaki upungufu wa meza na viti 120.
Ridhiwani alisema wanaelekeza nguvu zao kuhakikisha wanamaliza tatizo hilo ifikapo mwezi octoba mwaka huu.
Alisema
jitihada hizo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais John Magufuli na ya
mikakati yake ya kukabiliana na changamoto katika sekta ya elimu hivyo
halmashauri ya Chalinze inafanya kwa vitendo kuunga mkono mikakati hiyo.
Hata
hivyo Ridhiwani alisema kuwa amejipanga na halmashauri ya Mji wa
Chalinze kuendelea kutatua tatizo la meza,viti na madawati ili hali
kumaliza hali hiyo na kubaki historia.
Alieleza
kwasasa wanajielekeza katika kutatua tatizo la upungufu wa madarasa
ambalo limejitokeza kutokana na mpango wa elimu bure.
“Tumejipanga
kujielekeza katika tatizo lililoibuka la mahitaji mapya la madarasa
,maeneo mengine madawati sio tatizo lakini sasa yamejaa hadi walimu
hawana nafasi ya kuandika kutokana na wingi wa wanafunzi “
“Tumetenga
fedha kuanza ujenzi katika baadhi ya shule lakini pia tunaomba wahisani
wajitokeza kuungana nasi kuboresha sekta ya elimu ili wanafunzi waweze
kusoma kwenye manzingira mazuri”alisema Ridhiwani.
Ridhiwani alisema kuwa program hiyo inatarajia kumalizika ndani ya miaka mitatu kutokana na halmashauri yao kuwa bado changa .
Awali
akikabidhi viti na meza kwa mbunge huyo, mwakilishi wa kampuni ya
Sayona fruits ambae pia ni afisa mahusinao wa kampuni ya MMI ,Abubakary
Mlawa alisema wataendelea kushirikiana na jamii ili kutatua changamoto
mbalimbali.
Alisema
lengo la kusaidia vitu hivyo ni kuhakikisha wanafunzi wanakaa kwenye
viti ,meza na madawati na kuondokana na kero ya kukaa chini.
Mlawa
alisema wanatarajia kujenga kiwanda eneo la Mboga jimbo la Chalinze
kutokana na hilo ni sehemu yao kushirikiana na jamii inayowazunguka ili
kuinua maendeleo .
Nae
mkuu wa shule ya sekondari ya Lugoba Abdallah Sakasa aliishukuru
kampuni hiyo na kuueleza bado wana changamoto nyingi hivyo wasichoke
kuwasaidia.
Sakasa
alimuomba mwakilishi huyo amfikishie salamu za shukrani mkurugenzi
mtendaji wa kampuni hiyo Shubash Patel ambapo walikabidhiwa choroko
kilo 50 kama zawadi yao.
MWENYEKITI WA CCM DK MAGUFULI AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA CCM MJINI DODOMA
Mwenyekitib wa CCM Dk JohnMagufuli akizunguza na wafanyakazi wa CCM Makao Makiiu yaCCM mjini
Dodoma leo.
Dodoma leo.
……………………………………………………………………………..
Bashir Nkoromo
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa mara ya kwanza
amekutana na kuzungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya chama hicho na
baadaye wafanyakazi wa CCM Makao Makuu katika Ofisi za Chama hicho Mjini
Dodoma ikiwa ni siku tano tangu achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Tano wa
Chama hicho.
Mhe.
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amekutana na watendaji hao wa CCM kwa
lengo la kuwasalimia, kupokea maoni na ushauri wao juu ya utendaji kazi
ndani ya Chama.
Katika
mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania amewapongeza watendaji wote wa Chama Cha Mapinduzi kwa kazi
kubwa wanayoifanya na kwa namna ya pekee kwa jinsi walivyotoa mchango
mkubwa kuhakikisha CCM inapata ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka
jana.
Pia
amewataka kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa lengo la
kuendelea kukiimarisha Chama hicho ambacho kimebeba dhamana ya kuongoza
Serikali kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Dkt.
Magufuli amewahakikishia kuwa chini ya uongozi wake atafanyia kazi
changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi wa CCM ikiwemo maslahi
duni, vitendea kazi na kuondoa utegemezi.
Aidha,
Dkt. Magufuli amewataka watumishi wa chama kutoa ushirikiano katika
zoezi la uhakiki wa mali za Chama litakalosimamiwa na sekretarieti ya
chama na ameahidi kuwa atahakikisha mapato yatokanayo na vyanzo vya
mapato vya chama yanatumika ipasavyo.
Kwa
upande wao watumishi wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho
Ndugu Abdulrahaman Kinana wamempongeza Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
kwa kuchaguliwa kwa asilimia mia moja na wajumbe wa Mkutano Mkuu
uliofanyika tarehe 23 Julai, 2016 Mjini Dodoma kuwa Mwenyekiti wa Chama
hicho Taifa.
Watumishi hao wamemuahidi kuendeleza utumishi uliotukuka na wameelezea matumaini yao ya kuboreshewa maslahi.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
SIHABA NKINGA: JITOKEZENI KUSAIDIA MAKAZI YA WAZEE NA WATU WENYE ULEMAVU NCHINI.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.
Sihaba Nkinga akisalimiana na wazee alipotembelea Makazi ya kulea wazee
ya Kolandoto leo Mkoani Shinyanga.
Afisa
Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe
akimkabidhi taarifa ya kituo hicho Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga wazee alipotembelea
Mkazi hayo leo Mkoani Shinyanga.
Afisa
Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe
akimuleza Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Bi. Sihaba Nkinga (kulia) changamoto za Makazi hayo na
kumuomba kusaidia kusimamia utatuliwaji wa matatizo hayo ikiwemo ujenzi
wa majengo kwa ajili ya malazi ya wazee hao, Katikati ni Afisa Maendeleo
ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Bi. Amina.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.
Sihaba Nkinga akiongea na Wazee wanaoishi katika Makazi ya Kulea Wazee
ya Kolandoto leo Mkoani Shinyanga na kuwahakikishia serikali kuendelea
kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili ili kuwawezesha kuishi
katika mazingira rafiki. Katikati ni Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka
Wizara hiyo Bi. Amina… na kushoto ni Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea
Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe
Afisa
Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe
akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga sehemu ya nyumba zinazohitaji ujenzi
kwa ajili ya Makazi ya Wazee hao. Wakati wa Ziara ya Kutembelea Makazi
ya Wazee na kuona hali halisi ya makazi hao.
MPIGA CHAPA MKUU WA SERIKALI ATOA TAMKO JUU YA MATUMIZI YA ALAMA ZA TAIFA.
Mpigachapa Mkuu
wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo akizungumza jambo kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano na waandishi hao katika
kueleza jamii umuhimu wa kuzingatia matumizi sahihi ya vielelezo vya
Taifa walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Julai 27,
2016 kulia kwake ni Afisa Habari Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Nyamagory
Omary.
Mpigachapa Mkuu
wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo akiwaonesha wanahabari (hawapo
pichani) muonekano sahihi wa Nembo ya Taifa wakati wa mkutano wake na
wanahabari Juali 27, 2016, wa kwanza kulia ni Afisa Habari Idara ya
Habari Maelezo Bw.Frank Shijja.
Mpigachapa Mkuu
wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo akionesha baadhi ya Vielelezo muhimu
vya Taifa wakati wa Mkutano wake na waandishi wa habari katika Ukumbi wa
Mikutano wa ofisi yake Julai 27, 2016.
Mtangazaji
wa Televisheni ya Taifa Bw.Elisha Elia akiuliza swali kwa
Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo (hayupo pichani) wakati
wa Mkutano wake na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………………………………………
Na.MWANDISHI WETU
Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Ofisi
ya Waziri Mkuu Bw.Cassian Chibogoyo amewataka wananchi kuzingatia
matumizi sahihi ya vielelezo vya Taifa kama njia ya kuheshimu Taifa na
kuonesha uzalendo.
Chibogoyo ameyasema hayo hii leo
katika kipindi cha pili cha ‘TUJITAMBUE’ ambacho kimewakutanisha
waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari Jijini Dar es salaam kwa lengo
la kutoa muendelezo wa elimu sahihi ya vielelezo vya taifa kwa jamii.
Akitaja alama tatu muhimu za Taifa
ambazo ni Bendera ya Taifa, Wimbo wa Taifa na Ngao ya Taifa, Chibogoyo
amesema kila kimoja kinasimamiwa na sheria ili kuhakikisha matumizi yake
yanaliletea heshima Taifa la Tanzania hivyo, wananchi ni vyema wakawa
sehemu ya kutunza tunu hizo na kujiepusha na matumizi yasiyo sahihi.
Katika ufafanuzi wake ameeleza
kuwa, Wimbo wa taifa una Tone Maalum na maneno maalum yaliyowekwa hivyo
uimbaji unaoongeza vibwagizo kinyume cha uhalisia wake ni kosa kisheria.
Akielezea matumizi ya Bendera ya
Taifa amesema ni kinyume cha sheria kubadili rangi zilizoainishwa
kisheria kwani kila rangi ina maana yake na kuwa matumizi ya bendera
serikalini yana utaratibu maalum kuanzia Ofisi ya Rais hadi kwa viongozi
wa ngazi za chini.
“Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania pekee ndiye anayeweza kufanya mabadiliko ya Bendera ya Taifa na
Ngao ya Taifa kama kinavyoagiza kifungu cha 5 cha sheria ya vielelezo
vya Taifa Na. 15 ya mwaka 1971.” Alisema Chibogoyo.
Kuhusu Nembo ya Taifa amesema ziko
nembo nyingi feki mtaani ambazo pia zinatumiwa na wananchi katika
matangazo au shughuli za kibiashara kinyume na matakwa ya sheria huku
akitumia kipindi hicho kuonesha tofauti zilizopo katika alama sahihi na
zile ambazo si, sahihi.
Bwana Chibogoyo alihitimisha kikao
hicho kwa kuwashukuru wadau wote na kusema kuwa tarehe ya kikao kingine
itatolewa kupitia Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Waziri
Mkuu.
MARAIS WASTAAFU NCHI ZA AFRIKA WAWASILI JIJINI DAR KUHUDHURIA MKUTANO MKUU WA UONGOZI WA MWAKA 2016
Rais mstaafu wa Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki (pichani kulia) akiwasili leo jijini Dar Es Salaam akiwa na Mwenyeji wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja,kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 utakoanza kesho hapa jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.Mkutano huo utakaodumu kwa siku mbili utawajumuisha wadau mbalimbali.
PICHA NA MICHUZI JR.MMG.
Raisi mstaafu wa Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki akisalimiana na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Mh. Thamsanga Dennis Msekelu baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 utakoanza kesho hapa jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro wa siku mbili.Pichani kati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa
Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja .
Raisi mstaafu wa Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki akizungumza na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Thamsanga Dennis Msekelu baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 utakoanza kesho hapa jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya
Hyatt Kilimanjaro.
Rais mstaafu wa Msumbiji, Armando Emilio Guebuza akikaribishwa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya UONGOZI mara baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam kuhudhuria mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 unaotarajiwa kuanza hapo kesho jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro kwa siku mbili.
Rais mstaafu wa Msumbiji, Armando Emilio Guebuza akikaribishwa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya UONGOZI mara baada ya kuwasili jioni ya leo jijini Dar Es Salaam kuhudhuria mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 unaotarajiwa kuanza hapo kesho jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya
Hyatt Kilimanjaro kwa siku mbili.
Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano akikaribishwa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya UONGOZI mara baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam jioni ya leo kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 wa siku mbili,utakoanza hapo kesho jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.Pichani shoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya
UONGOZI Profesa Joseph Semboja .
No comments :
Post a Comment