Sabasaba
Moshingi akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye picha) juu ya
Utendaji kazi wa Benki ya Posta kwa Nusu mwaka. Katikati ni Mkurugenzi
wa Fedha Regina Semakafu na Mkurugenzi wa Sheria, Mystica Mapunda
Ngongi. Benki ya Posta imepata faida ya shilingi bilioni 8.84 kabla ya
kodi kwa nusu mwaka wa 2016.
NUSU
ya kwanza ya Mwaka 2016 iliyoisha mwezi Juni, imekuwa yenye mafanikio
makubwa sana kwa Benki ya Posta Tanzania (TPB). Pamoja na changamoto
mbalimbali ambazo bado zinaikabili benki yetu, kwa kipindi kirefu sasa,
lakini Benki imefanikiwa kupata faida kabla ya kodi ya shilling bilioni
8.84 ukilinganisha shillingi bilioni 5.48 zilizopatikana kipindi kama
hicho mwaka 2015,ambayo ni sawasawa na ukuaji wa asilimia 61.47%.
Ukuaji
huu wa faida katika kipindi hiki cha nusu mwaka wa 2016 umewezesha
kukua kwa mtaji wa wawekezaji hadi kufikia shillingi billioni 48 kutoka
shillingi bilioni 37 mwezi Juni mwaka 2015.
Mapato
ya Benki kwa nusu mwaka 2016 yaliongezeka hadi kufikia shilling bilioni
42.5 kutoka bilion 34 iliyofikiwa nusu ya mwaka 2015, huu ni ukuaji wa
asilimia 38%. Vilevile katika kipindi hichohicho amana za wateja
ziliongezeka na kufikia shilingi bilioni 294.64 kutoka shilingi bilioni
263.68 June mwaka 2015, ukuaji wa asilimia 11.74%.
Mikopo
imeongezeka hadi kufikia shillingi billioni 278 kutoka shilingi
billioni 241.51 Juni mwaka 2015, ongezeko la asilimia 15.22%. Sehemu
kubwa ya mikopo hii imetolewa kwa wafanyabiashara wadogowadogo pamoja na
wafanyakazi wa sekta ya umma na serikali kuu.
Rasilimali
za benki zilikuwa hadi kufikia shilling 390.8 bilioni mwezi Juni mwaka
huu 2016 kutoka shillingi billioni 333.96 Juni mwaka 2015 ongezeko la
asilimia 17.16%.Benki ya Posta kwa mwaka 2016, iliendelea na jitihada zake za kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi, mwanzoni mwa mwaka huu benki ilifungua tawi lake jipya la Songea, Mkoani Ruvuma, ambapo Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, pamoja na tawi la Babati Mkoani Manyara, ambapo mgeni rasmi alikuwa Msajili wa Hazina Bw.Lawrence Mafuru.
Matawi
hayo mawili yamejengwa kwenye viwanja vinavyomilikiwa na TPB. Benki
ilihamishia Makao yake Makuu kutoka jengo la Extelecoms lililopo mtaa wa
Samora na kuhamia kwenye Jengo la Millenium Towers, Kijitonyama.
Pia,
benki imehamisha tawi lake la Moshi kwenda kwenye jengo jipya la NSSF,
na hivi karibuni itahamisha matawi yake yaliyoko Kahama na Tanga kwenda
kwenye majengo mapya na ya kisasa. Hizi zote ni jitihada za benki za
kuongeza ufanisi na pia kutoa huduma zake kwenye mandhari bora naya
kisasa zaidi.
Hadi
hivi sasa TPB inayo matawi 30 na madogo (min branches) 30, Mashine za
kutolea pesa (ATM) zinazo milikiwa na benki ya posta ni 38 na 200 za
umoja wamabenki (Umoja switch), hivyo kuwawezesha wateja wetu kupata
huduma ya pesa nchi nzima.
Pia benki inao mawakala wa benki 133 kupitia TPC,na vituo vya huduma 200 kupitia mawakala binafsi.
Benki ya posta inaendelea na jitihada zake za kuongeza wigo wa biashara kwa njia mbalimbali, zikiwemo:
kutoa
mikopo kwa vikundi vidogo vidogo (group lending), ambapo hadi sasa
tumetoa mikopo ya kiasi cha shilingi 6.5 bilioni na huduma ya
kuwakopesha wazee (wastaafu loan) kupitia mifuko ya jamii kama vile
PSPF,NSSF na ZFF, ambapo hadi sasa tumetoa mikopo ya kiasi cha shilingi
56 bilioni.
Kwa
kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),
enki imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi Milioni 541 ili kuviinua
kiuchumi vikundi vilivyo chini ya Baraza hilo.
Kufungua account za vikundi visivyo rasmi(VICOBA informal groups) ambapo hadi sasa akaunti 30 elfu zimefunguliwa.
Huduma
za kibenki kupitia simu za kiganjani,ambapo kwa kipindi cha nusu ya
mwaka huu akaunti 271,427 zilifunguliwa, kulinganisha na akaunti 236,981
zilizofunguliwa hadi mwishoni mwa mwaka jana. Hili ni ongezeko la
akaunti 34,446, sawasawa na asilimia 15.
Benki
ya Posta imejidhatiti kuendelea kutoa huduma bora, nafuu na za kisasa
kwa maana ya kutumia teknolojia zaidi katika kipindi hiki. Tunaamini
kwamba bado kwa kutumia teknolojia ya TPB POPOTE tutaweza kuwafikia
Watanzania walio wengi hasa vijijini ambao bado hawajaingia kwenye mfumo
wa kifedha.
Pia
benki itaendeleza na kuboresha mahusiano yake na makampuni za simu ili
kuweza kupeleka huduma zake karibu zaidi na wananchi, na pia ushirikano
wake na Saccos pamoja na Vicoba.
Benki
ya Posta inapenda kuwashukuru wateja wake na Watanzania wote kwa ujumla
kwa kutuamini na kuendelea kutumia huduma zetu. Tunaahidi
hatutawaangusha, na tutaendelea kuboresha huduma zetu zenye gharama
nafuu.
Pia
shukrani za pekee ziende kwa Bodi ya Wakurugenzi kwa uongozi wao
thabiti na usimamizi imara, unaoendelea kuhakikisha kuwa benki inakuwa
miongoni mwa taasisi bora za kifedha hapa nchini.
SHIRIKA LA NYUMBA LAIKABIDHI BENKI KUU MAJENGO KWA AJILI YA WAFANYAKAZI WAKE MTWARA
Jengo la ghorofa tano ambalo NHC imeikabidhi Benki kuu ya Tanzania eneo la Shangani Manispaa ya Mtwara.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akimkaribisha Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania Profesa Benno Ndulu alipowasili eneo la Shangani kukabidhiwa
Nyumba walizonunua.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akimkabidhi ufunguo Gavana wa Benki kuu ya Tanzania- BOT Prof. Beno Ndulu.
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania- BOT Prof. Beno Ndulu akimsikiliza Mkurugenzi wa Masoko kitengo cha Makampuni makubwa wa BancABC, Khalifa Zidadu wakati wa uzinduzi wa nyumba za BOT Mtwara na kushoto kwa gavana ni Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu.
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania- BOT Prof. Beno Ndulu akifafanua jambo kuhusina na ununuzi wa nyumba kwa ajili ya wafanyakazi wa benki hiyo mkoani mtwara, kulia kwa gavana ni Mkurugenzi wa Masoko Kitengo cha Makampuni makubwa wa BancABC Khalifa Zidadu na kushoto kwa gavana ni Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu.
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania- BOT Prof. Beno Ndulu akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Masoko Kitengo cha makampuni makubwa wa BancABC Khalifa Zidadu wa pili kushoto na Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu aliyevaa fulana.
Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akitoa maelezo ya kukamilika kwa mradi wa nyumba kwa ajili ya wafanyakazi wa benki kuu ya Tanzania mkoani Mtwara kwa Gavana wa benki hiyo Profesa Beno Ndulu na Mkurugenzi wa Masoko Kitengo cha makampuni makubwa wa BancABC Khalifa Zidadu.
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania- BOT Prof. Beno Ndulu akimshukuru Mkurugenzi wa Masoko Kitengo cha makampuni makubwa wa BancABC Khalifa Zidadu kwa kuwezesha BOT kununua nyumba hizo mkoani Mtwara, kushoto kwa Gavana ni Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu.
WASANII KUNUFAIKA NA MFUMO MPYA WA UONYESHWAJI FILAMU
Msemaji kutoka kituo cha Sibuka Televisheni wa kwanza kulia Bw.
George Nangale akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati
wa uzinduzi wa kipindi cha INABAMBA “Ni bongo movie bandika bandua”
kitachokuwa kinaonyeshwa katika kituo hiko cha matangazo uliofanyika leo
jijini Dar es salaam, kushoto ni Afisa habari wa kampuni ya Step
Entertainment Bw. Moses Mwanyilu.
Mkurugenzi wa matamasha kutoka kampuni ya usambazaji filamu nchini Steps Entertainment katikati
Bw. Jonas Sabuni akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati
wa uzinduzi wa kipindi cha INABAMBA “Ni bongo movie bandika bandua”
ambao uliofanyika leo jijini Dar es salaam, kushoto ni Afisa habari wa
kampuni hiyo Bw. Moses Mwanyilu na kulia ni mwigizaji wa bongo movie
Jimmy Mafufu.
Afisa
habari wa kampuni ya Step Entertainment Bw. Moses Mwanyilu wa kwanza
kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa
uzinduzi wa kipindi cha INABAMBA “Ni bongo movie bandika bandua”
kitachokuwa kinaonyeshwa katika kituo cha matangazo Sibuka Televisheni
uliofanyika leo jijini Dar es salaam,katikati ni , Msemaji kutoka kituo
cha Sibuka Televisheni Bw. George Nangale na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Masoko kutoka Startimes Bw. Awino Felia.
Meneja
Masoko kutoka Startimes Bw. Awino Felia wa kwanza kushoto akiongea na
waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa kipindi cha
INABAMBA “Ni bongo movie bandika bandua” kitachokuwa kinaonyeshwa katika
kituo cha matangazo Sibuka Televisheni kupitia king’amuzi cha
Startimes uliofanyika leo jijini Dar es salaam
PICHA ZOTE NA ALLY DAUD-MAELEZO.
Serikali yatenga bilioni 1.6 kwa ajili ya uanzishwaji wa mfumo wa kielekroniki wa kusajili wakazi.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI Injinia Mussa Iyombe akiongea na
wanahabari wakati wa kupokea maendeleo ya mfumo wa kuboresha upatikanaji
wa taarifa sahihi katika serikali za mitaa, hafla hiyo ilifanyika
jijini Dar es Salaam.
Diwani
wa Kata ya Mapinga Wilaya ya Bagamoyo Ibrahimu Mbonde akiongea jambo
wakati wa kupokea maendeleo ya mfumo wa kuboresha upatikanaji wa taarifa
sahihi katika serikali za mitaa, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam.
Kamishna
wa Sensa ya Watu na Mkazi Hajjat Amina Mrisho Said akiongea jambo
wakati wa kupokea maendeleo ya mfumo wa kuboresha upatikanaji wa taarifa
sahihi katika serikali za mitaa, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam.
(Picha zote na Benjamin Sawe- Maelezo)
PROF. MBARAWA AFUNGUA MKUTANO WA NNE WA WADAU WA SIMU
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akifungua
mkutano wa nne wa Chama cha Kampuni za Simu Duniani, GSMA Mobile 360,
jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akikata
utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mkutano wa nne wa Chama cha Kampuni za
Simu Duniani, GSMA Mobile 360 jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akishuka
kwenye gari maalum la mawasiliano baada ya kukagua mitambo mbalimbali ya
Mawasiliano ya simu jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wajumbe wa mkutano wa nne wa Chama cha Kampuni za Simu Duniani,
GSMA Mobile 360, wakifatilia mada jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………………….
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezungumzia
umuhimu wa wananchi wa mjini na vijijini kutumia simu ili waweze
kunufaika na huduma mbalimbali za kimtandao zinazotumika hapa nchini.
Akizungumza
mara baada ya kufungua mkutano wa nne wa kimataifa wa chama cha kampuni
za simu duniani GSMA mobile 360, Prof . Mbarawa amesema Serikali
imejipanga kuhakikisha miundombinu ya mawasiliano ya simu inawafikia
wananchi wote ili kuwezesha kunufaika na huduma za simu za kisasa.
‘Ili
wananchi waweze kupata maendeleo kwa haraka na kunufaika na fursa za
kimtandao katika masuala ya elimu, biashara, kilimo, afya na ustawi wa
jamii kwa ujumla kunahitajika uwepo wa simu za kisasa zinazoweza
kuruhusu mifumo ya kimawasiliano’, Amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Ameitaja
mifumo hiyo kuwa ni Elimu Mtandao, Afya Mtandao, Biashara Mtandao,
Kilimo Mtandao, Serikali Mtandao, Hali ya Hewa Mtandao ambavyo kwa
pamoja vitamhudumia mwananchi kwa ubora na wakati.
Amesisitiza
kuwa serikali inashirikiana kwa karibu na kampuni za mawasiliano ya
simu ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha huduma za simu zinakuwa za
uhakika na salama.
Serikali
inaendelea kuhakikisha kwamba mfuko wa Mawasiliano Vijijini unaendelea
kunufaisha watanzania na mkakati wa kuhakikisha umeme unafika vijijini
unaimarika sambamba na uwepo wa simu za kisasa za bei nafuu.
Takribani laini za simu milioni 39.9 nchini zinatumika katika huduma mbalimbali na hivyo huchangia uchumi wa nchi.
Waziri
Prof. Mbarawa amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira
mazuri ya uwekezaji ili kukuza sekta ya mawasiliano hapa nchini ambapo
hadi sasa tayari kilomita 18,000/- za mkongo wa taifa wa taifa wa
mawasiliano zimejengwa hapa nchini.
“Serikali
itaendelea kudhibiti vifaa vya mawasiliano visivyo na ubora ili
visiingie nchini na hivyo kuhakikisha watumiaji wa mitandao ya simu
wanakuwa salama na wanaitumia mitandao hiyo kwa wakati wote’.
Amesisitiza Prof. Mbarawa.
Mkutano
huo wa siku mbili ambao pia umehudhuriwa na Naibu Waziri Mkuu wa Nchi
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Bw. Thomas Luhaka ambapo
pamoja na mambo mengine utajadili Changamoto mbalimbali na kuja na
suluhisho na namna bora ya kuendeleza Sekta ya Mawasiliano duniani.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI AWATAKA WATUMISHI KUJIANDAA NA MABADILIKO KATIKA UTUMUSHI WA UMMA.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu
Kayandabila akiongea na watumishi wa Wizara ya Ardhi walioajiriwa hivi
karibuni wakati wa mafunzo ya awali kwa watumishi wa umma.
Baadhi
ya watumishi wa Wizara ya Ardhi walioajiriwa hivi karibuni
wakimsikiliza kwa makini Dkt. Yamungu Kayandabila wakati wa mafunzo ya
awali kwa watumishi wa umma.
Baadhi
ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
walipokutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi wakati wa mafunzo ya
awali kwa watumishi wa umma katika ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma
cha Magogoni jijini Dar es salaam.
………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila awataka watumishi
wa Sekta ya Ardhi kujiepusha na rushwa, kuzingatia kanuni na maadili ya
utumishi wa umma pamoja na kujiandaa kuhamia Dodoma.
Kayandabila aliyasema hayo wakati
akifungua mafunzo ya awali kwa watumishi wa umma walioajiriwa hivi
karibuni yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma cha
Magogoni jijini Dar es salaam.
WATEJA WAFURAHIA MICHUANO YA ICC INAYOONEKANA KUPITIA STARTIMES
Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka akizungumza na
timu ya StarTimes na maveterani wa uwanja wa Mwembe Yanga – Temeke kabla
ya mchezo wa kirafiki uwanjani hapo. StarTimes iliweka kambi uwanjani
hapo ikiwa ni uzinduzi wa michuano ya ICC mwaka 2016 iliyokwishaanza
kutimua vumbi Julai 22 wiki iliyopita ambapo ilidhamiria kuonyesha
mchuano mkali wa ‘Manchester Derby’ uliopaswa kuchezwa jijini Beijing,
China lakini kwa bahati mbaya ukaahirisha kutokana na hali ya hewa kuwa
mbaya na hivyo wateja wakapewa kutazama marudiano ya mchezo baina ya
Manchester United na Borrusia Dortmund ambapo Dortmund waliibamiza
United kwa magoli 4.
Baadhiya wateja na mashabiki wa soka waliojitokeza kutazama mchezo wa
‘Manchester Derby’ uliopaswa kuchezwa jijini Beijing, China lakini kwa
bahati mbaya ukaahirisha kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya na hivyo
wateja wakapewa kutazama marudiano ya mchezo baina ya Manchester United
na Borrusia Dortmund ambapo Dortmund waliibamiza United kwa magoli 4 –
1.
Mmoja
wa wateja waliofika katika viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, akipata
maelekezo juu ya huduma za StarTimes kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa
kampuni hiyo.
………………………………………………………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
Wateja
wa StarTimes na watanzania kwa ujumla wameipongeza kampuni inayouza na
kusambaza visimbuzi vya matangazo ya dijitali, Starimes, kwa kuwaletea
michuano ya kombe la mabingwa kimataifa au ICC mwaka 2016 moja kwa moja
kupitia chaneli yake ya ST WORLD FOOTBALL.
Hayo
yalisemwa na wateja mbalimbali waliohudhuria tamasha la uzinduzi wa
michuano hiyo iliyoanza katika viwanja vya Temeke, Mwembe Yanga.
Katika
tamasha hilo StarTimes walitinga viwanjani hapo na timu kamili ya
wafanyakazi wake wa vitengo mbalimbali ambapo pia walifunga luninga
uwanjani ili kuonyesha moja kwa moja mtanange wa watani wa jadi kutoka
jiji la Manchester unaojulikana kama ‘Manchester Derby’ uliopangwa
kufanyika jijini Beijing China lakini kutokana na hali ya hewa mbaya
ikabidi uahirishwe.
Akizungumza
katika viwanja hivyo Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David
Kisaka alibainisha kuwa, “Siku ya leo tumefika viwanjani hapa kwa lengo
kubwa la kutaka kuwapa fursa wateja wetu kujionea uhondo wa michuano ya
ICC inayonekana moja kwa moja kwenye visimbuzi vyetu. Michuano hii
inayofanyika katika nchi ya Marekani, Ulaya, Australia na China
inazishirikisha timu kubwa duniani kama vile Real Madrid, Barcelona,
Manchester United na City, Juventus, Chelsea, Liverpool na nyiginezo.”
“Michuano
hiyo imekwishaanza tangu Ijumaa ya wiki iliyoishia ambapo
tumekwishashuhudia tayari timu kama Manchester United, Borussia
Dortmund, Celtic, Leicester City, Inter Milan na PSG zimekwishatinga
uwanjani. Siku ya leo tumekuja hapa kwa lengo la kuonyesha Manchester
Derby lakini tunasikikita kuwa mchezo huo umeahirishwa kutokana na hali
ya hewa mbaya kulikumba jiji la Beijing ambamo mchezo huo ulipangwa
kuchezwa. Lakini badala yake tunaonyesha mchezo wa marudio baina ya
Manchester United na Borussia Dortmund.” Aliongezea Bw. Kisaka
Meneja
huyo wa Mauzo alimalizia kwa kusema, “Ningependa kuchukua fursa hii kwa
kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kufurahiamichuano hii mikubwa
zaidi ambayo ni ya awali au maandalizi kabla ya ligi kuu mbalimbali
kuanza mwishoni mwa mwezi wa Agosti.
StarTimes
pia tunaonyesha ligi hizo ambapo wateja watafurahia mechi zote za ligi
za Bundesliga na Serie A kupitia chaneli zetu za michezo za SPORT ARENA,
SPORTS FOCUS, WORLD FOOTBALL, SPORT LIFE NA SPORT PREMIUM na bila
kusahau ligi za Ufaransa na Ubelgiji kupita chaneli ya FOX SPORTS.
Ili
kufaidi michuano hii ya ICC mwaka 2016 wateja itawabidi kulipia malipo
kiduchu ya kifurushi cha Mambo kwa shilingi 12,000/- tu na kuweza
kutazama mechi zote moja kwa moja ambazo zitarajiwa kuisha Agosti 13.”
Michuano
ya ICC mwaka 2016 imekwishaanza Julai 22 ambapo mechi ya kwanza
iliyofungua pazia ilikuwa ni kati ya Machester United na Borrusia
Dortmund ambapo Dortmund iliibamiza United kwa
mabao 4 – 1. Michezo mingine iliyokwishachezwa ni pamoja na PSG kuitandika 3 -1 Inter Milan na Leicester City kuwashinda Celtic kwa mikwaju 6 – 5 ya penati baada ya kutoshana nguvu kwa kufungana magoli 1 – 1 ndani ya dakika 90.
mabao 4 – 1. Michezo mingine iliyokwishachezwa ni pamoja na PSG kuitandika 3 -1 Inter Milan na Leicester City kuwashinda Celtic kwa mikwaju 6 – 5 ya penati baada ya kutoshana nguvu kwa kufungana magoli 1 – 1 ndani ya dakika 90.
Siku
ya leo Jumanne kutakuwa na mechi nyingine ambapo mabingwa wa Italia,
Juventus watashuka dimbani kuwakabili timu ya Tottenham Hotspurs ya
Uingereza katika mishale ya saa 7 mchana kwa muda wa hapa nyumbani
Tanzania kupitia chaneli ya WORLD FOOTBALL ndani ya ya
StarTimes pekee.
StarTimes pekee.
No comments :
Post a Comment