RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli hatimaye ametungua
kitendawili cha nani atakayekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, baada ya kumteua Mbunge wa Ruangwa mkoani Lindi, Mh. Kassim Majaliwa.
Spika
wa Bunge Job Ndugai, alipokea bahasha yenye jina la mteule huyo wa Rais, kutoka
kwa Mpambe wa Rais, ambaye akiwa ndani ya sare zake za Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania, JWTZ, aliongozwa na wapambe wa Bunge hadi kwenye meza ya
Spika Ndugai na kumkabidhi bahasha hiyo mapema leo Novemba 19, 2015.
Baada
ya Mh. Ndugai kupokea bahasha hiyo aliwaonyesha wabunge na kusema bahasha hii
imewekewa seal, hivyo akamwita Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashilila na
kumtaka aifungue ili kujua jina la Waziri Mkuu ni nani.
Dkt.
Kashilila aliifungua bahasha hiyo na kukumbana na bahasha ya pili, hata
alipoifungua bahasha hiyo ya pili akakumbana na bahasha ya tatu na
ilipofungunliwa akakutana na kadi maalum yenye ujumbe ulioandikwa kwa mkono na
Mh. Rais mwenyewe kuonyesha kuwa haikupitia kwenye mkono wa mtu mwingine na
hivyo kusoma jina la mteule huyo ambaye sasa anasubiri kuthibitishwa na wabunge
baadaye Alhamisi Novemba 19, 2015 kwenye kipindi cha bunge majira ya jioni
Mh.
Kassim Majaliwa alikuwa Naibu Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), kwenye
serikali ya awamu ya nne akishughulika sana na masuala ya elimu.
Mh.
Kassim Majaliwa alizaliwa Desemba 22 1960 huko mkoani Lindi, na amekuwa mbunge wa
jimbo ;la Ruangwa moani Lindi tangu mwaka 2010.
Chini
ni matukio mbalimbali ya kiutendaji ambayo Mh. Kassim Majaliwa alikuwa
akiyatekeleza kwenye nafasi yake ya Ubunge na Unaibu Waziri wa TAMISEMI






No comments :
Post a Comment