Rais
wa klabu ya Rotary Dar es Salaam Oyster Bay kwa mwaka huu wa 2015-2016,
Mohamed Versi akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani)
katika mji wa Kerege jana Novemba 15. wakati wa zoezi hilo la kambi ya
bure ya upimaji wa afya. (Picha zote na Andrew Chale ).
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[BAGAMOYO]
Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oyster Bay, kwa mara nyingine tena
imeendesha matibabu katika kambi maalum ya matibabu ya bure katika mji
wa Kerege uliopo Bagamoyo, Mkoani Pwani.
Kambi
hiyo iliyofanyika siku ya Jumapil Novemba 15.2015 ambapo zaidi ya
wahudumu 50 wa Afya walipima na kutibu magonjwa kwa wakazi hao wa
Kerege waliojitokeza kwa wingi wanaokadiriwa kufikia zaidi ya 700.
Kambi
hiyo ya matibabu bure imedhaminiwa na benki ya Diamond Trust Bank
(DTB) imeweza kuwa faraja kubwa kwa wananchi na wakazi wa Kerege kupata
Huduma hiyo kwani imeweza kuwafikia muda muafaka kwao kupata fursa za
matibabu na vipimo bure.
Akizungumza
na wanahabari Rais wa klabu hiyo ya Rotary Dar es Salaam Oyster Bay kwa
mwaka huu wa 2015-2016, Mohamed Versi amebainisha kuwa wito mkubwa kwa
wananchi wa Kerege kujitokeza kunawapa faraja kuendelea kutembelea na
kuweka kambi kwa mwaka mara moja katika mji huo.
“Mwaka
huu ni wa tano tokea kuanza kutoa matibabu bure kwa kuweka kambi hizi
za matibabu. Kwa hapa Kerege huu ni mwaka wa nne tunafika hapa na
kuhudumia wananchi huku zaidi ya wananchi, 600 hadi 700 wanahudumiwa
ikiwemo vipimo na matibabu” alisema Versi.
Aidha,
Rais huyo alibainisha kuwa, mbali na kutoa matibabu bure pia wameweza
kutoa dawa pamoja na neti za kuzuia mbu kwa kila mwananchi aalijitokeza
kwenye kambi hiyo.
Naye
Mkuu wa Kitengo cha Masoko kutoka benki hiyo ya DTB, Bw. Sylvester
Bahati amebainisha kuwa kujitokeza kudhamini kambi hiyo ni miongoni mwa
taratibu za benki hiyo kuweza kusaidia jamii.
“Tunawapongeza
Rotary Klabu kwa kuona umuhimu wa kusaidia kambi hii ya Kerege matibabu
bure na ufadhili wetu hapa unaendana na sawa na taratibu tulizojiwekea
za kutoa gawio kwa jamii kama zilivyotaratibu nyingine tulizonazo”
alibainisha Bw. Bahati.
Aidha,
ameeleza kuwa Benki hiyo ya DTB ina matawi zaidi ya 20 nchini huku
ikitarajia kufungua matawi zaidi kwa nchi nzima ikiwemo Zanzibar.
Kwa
upande wake daktari na mratibu wa magonjwa ya Kisukari, Dk. Bashiru
Rajab ameeleza kuwa, wengi wa wa wagonjwa walipatikana katika kambi hiyo
ni wale wa matatizo ya mapigo ya moyo (Blood pressure ).
“Katika
kambi hii wengi wa wananchi wanaofika hapa wanakabiriwa na matatizo ya
Presha na ugonjwa wa Maralia huku wa kisukari wakiwa wachache. Inatia
faraja sana kwani wamepata kujua hali ya afya zao za mwili na
tunawashahuri wawe na taratibu ya kupima afya mara kwa mara” alibainisha
Dk. Bashiru.
Kwa
upande wao baadhi ya wananchi walipongeza waandaaji wa kambi hiyo
ambapo imewasaidia kujua afya zao hivyo kuchukua hatua ikiwemo suala la
kuzingatia kanuni za kufuata pamoja na ushahuri wa kitabibu.
Matibabu,
sehemu mojawapo ya Miradi ya Afya ya Jamii, ambayo hufanyika kila mwaka
toka ilipozinduliwa mwaka 2011 katika kitongoji cha Chanika jijini Dar
es Salaam ambapo takribani wananchi 600 walijitokeza kupima malaria,
VVU, Kisukari, magonjwa ya mfumo wa upumuaji, macho na viashiria vya
magonjwa sugu na baadae kuamia katika mji huo wa Kerege kwa mwaka wa
nne sasa huku wakitoa dawa na miwani bure.
Kwa
mwaka huu imedhaminiwa na benki ya Diamond Trust Bank, Rotary Club of
Seattle4 huku ikiandaliwa kwa kushirikiana na Shree Hindu Mandal
Hospital, Vital Supplies, Kids Care Tanzania, Elite Dantal Clinic,
Whitedent, Sayona, Ultimate Security na wengine wengi.
Mkuu wa kitengo cha Masoko kutoka benki
ya Diamond Trust Bank [DTB] akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)
wakati wa zoezi hilo la kambi ya matibabu bure. DTB ndio wadhamini
wakuu katika kambi hiyo.
Daktari
na mratibu wa magonjwa ya Kisukari, Dk. Bashiru Rajab akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo la kambi ya bure ya Matibabu
katika mji wa Kerege,Bagamoyo Pwani.
Mkazi
wa Kerege akiwa katika mstari wa kwenda kumuona Daktari kwa ajili ya
kupima afya zake sambamba na mtoto wake wakati wa kambi hiyo Novemba
15.2015.
Zoezi la Kambi hiyo ya matibabu bure likiendelea katika mji huo wa Kerege..
Mmoja wa wananchi wa Kerege (kulia) akimwelezea Daktari wa kambi hiyo..
Upande wa huduma za macho...katika kambi hiyo
Kitengo cha dawa wakiwa tayari kwa kutoa huduma hiyo wakati wa kambi hiyo..
Wananchi wakipatiwa dawa bure wakati wa kambi hiyo..
Huduma ya kinywa ikiendelea..
Baadhi ya vifaa maalum kwa ajili ya matibabu ya kinywa ikiwemo meno kutoka Elite Dental Clinic wakati wa kambi hiyo..
Baadhi ya madaktari wa
magonjwa ya kinywa wakiwa tayari kwa ajili ya kutoa huduma kwa mmoja wa
wakazi wa Kerege aliyefika katika kambi hiyo. Huduma ya Kinywa ilitolewa
na Elite Dental Clinic.
Huduma hizo za kinywa zikiendelea..
Picha za juu na chini ni eneo la upimaji wa magonjwa wa kinywa na meno iliyokuwa ikitolewa na Elite Dental Clinic
Mtaalamu wa tiba ya macho akiendelea na uchunguzi kwenye kambi hiyo
Zoezi hilo la upimaji likiendelea katika vitengo mbalimbali wakati wa kambi ya upimaji na matibabu bure katika mhi wa Kerege.
zoezi likiendelea kwa wananchi kupitia hatua moja hadi nyingine...
Baadhi ya wanachama wa Rotary Klabu ya Dar es Salaam Oyster Bay wakiwa katika kambi hiyo kutoa huduma..
Baadhi ya wananchi wa
Kerege waliojitokeza wakiwa kwenye foleni katika Kambi hiyo huku
wakipatiwa maelezo mbalimbali juu ya afya..
Baadhi ya wananchi upande wa wanawake waliojotokeza kwenye kambi hiyo..
Wananchi wakipata kusajiliwa kwa lengo la kuelekea kumuona Daktari na vipimo..
Baadhi ya waanachi hao wakiwa kwenye moja ya foleni kuingia kwa madaktari na vipimo mbalimbali wakati wa zoezi hilo.
Wananchi hao wakiwa katika kambi hiyo..
Huduma na somo likiendelea wakati wa kambi hiyo..
Soma zaidi hapa:
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Diamond
Trust (DTB), Viju Cherian (kushoto), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika Hoteli ya Serena Dar es Salaam leo
asubuhi kuhusu benki hiyo kuuza hisa zenye thamani ya sh. bilioni 30 na
kusherehekea miaka 70 ya uwepo wake tangu ianzishwe hapa nchini. Kulia
ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa benki hiyo, Joseph Mabusi.
Mkurugenzi wa Fedha
na Utawala wa benki hiyo, Joseph Mabusi (kulia), akizungumzia mafanikio
mbalimbali na shughuli zinazofanywa na benki hiyo.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya
Uzalishaji na Masoko wa benki hiyo, Sylvester Bahati (kushoto),
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu
masuala mbalimbali ya benki hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
........................................................................................................................................
Benki ya Diamond Trust (DTB Tanzania) hivi karibuni
imefanikiwa kuuza hisa stahili (Rights Issue) zenye thamani ya shilingi 30
billion kwa wanahisa wake kwa bei ya shilingi 5,200 kwa kila hisa. Hii ni mara
ya tatu kwa DTB Tanzania kuuza hisa stahili ambapo mwaka 2007 iliuza hisa kama
hizo zenye thamani ya shilingi bilioni 5.3 na mwaka 2012, shilingi bilioni 12.4
Uuzaji wa hisa unaimarisha mtaji wa benki na kuendelea
kuwekeza kwenye matawi mapya, teknolojia na uanzishwaji wa huduma mpya. DTB Tanzania imeendelea kukua ikianza na
matawi manne (4) mnamo mwaka 2007 wakati wa hisa stahili za kwanza hadi matawi
24 hivi sasa.
Mwaka huu, DTB Tanzania imezindua akaunti maalum za akiba
kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye kipato tofauti kutimiza malengo yao. Akaunti
hizi ni pamoja na Akaunti ya watoto (Smart Saver), akaunti ya akina mama
(Amani), akaunti ya wazee (Faraja) na akaunti ya wanafunzi wa sekondari na vyuo
(Kisomi Zaidi).
Pia uongezaji wa mtaji wa benki unakusudia kuendana na matakwa
ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), juu ya kanuni za mitaji ya mabenki. DTB
Tanzania ni benki ambayo siku zote imukuwa mstari wa mbele kutimiza matakwa ya sheria
juu ya mitaji ya mabenki ikiwa ni pamoja na ongezeko la viwango vya mitaji
(core /total capital ratios). Benki ya DTB Tanzania imekuza mtaji utakaoendena
na mipango ya kibiashara kwa miaka ijayo.
DTB Tanzania ambayo inasherehekea miaka 70 ya uwepo wake
Tanzania, imepata mafanikio ya kuridhisha kwa kipindi cha miezi tisa iliyoishia
tarehe 30 Septemba 2015. Faida bila kodi imefikia shilingi 20.0 bilioni; ikiwa
ni ukuaji wa asilimia 30.1 ikilinganishwa na shilingi 15.4 bilioni iliyopatikana
katika kipindi kama hicho mwaka jana. DTB Tanzania ni miongoni mwa benki chache
nchini Tanzania, zilizofanikiwa na ongezeko kabla ya faida ya zaidi ya asilimia
31 kwa miaka mitano sasa.
Amana za wateja imekua kwa asilimia 30 kutoka shilingi 504
bilioni Septemba 2014, hadi shilingi 720 bilioni mwishoni mwa Septemba 2015.
Mali za Benki (Total Assets) zimefikia shilingi 858 bilioni ikilinganishwa na
shilingi 632 bilioni mwezi Septemba 2014, ikiwa ni ukuaji wa asilimia 26. Mali
za Benki (Total Assets) ziliongezeka kwa asilimia 24 mwaka 2012, asilimia 26
mwaka 2013 na asilimia 36 mwaka 2014.
Amana zisizo na riba (Casa deposits) zilikuwa shilingi 372
bilioni, ongezeko la asilima 40.5 toka shilingi 265 bilioni mwezi Septemba
2014. Mikopo kwa wateja ilikuwa shilingi 512 bilioni ikilinganishwa na shilingi
391 bilioni kwa kipindi kama hicho mwaka 2014, ikiwa ni ongezeko la asilimia
23.
Kwa sasa DTB Tanzania ina mtandao wa matawi 24 nchi nzima. Matawi
10 yakiwa Dar es Salaam (Tawi Kuu la Dar, Kariakoo, Magomeni, Masaki, Mbagala,
Mbezi, Morocco, Nelson Mandela na Upanga iliyopo barabara ya Umoja wa Mataifa. DTB
Tanzania pia ina matawi 14 kwenye miji mikubwa nchini, ikiwa ni matawi 2 jijini
Arusha, matawi 2 Jijini Mwanza na tawi
moja moja katika miji ya Dodoma, Iringa, Kahama, Mbeya, Morogoro, Moshi,
Mtwara, Tabora, Tanga na Zanzibar.
DTBT ni kampuni tanzu ya Diamond Trust Bank Group yenye
matawi zaidi ya 115 katika nchi za Tanzania,
Kenya, Uganda na Burundi. DTB ni mshirika wa Mfuko wa Maendeleo ya Uchumi wa Aga
Khan (Aga Khan Fund for Economic Development -AKFED), ambayo ni sehemu ya Mtandao
wa Maendeleo wa Aga Khan (Aga Khan Development Network).
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki akizungumza mbele ya
wanahabari, madaktari na baadhi ya akina mama waliokuwa na watoto
waliozaliwa kabla ya wakati maarufu kama Njiti (Hawapo pichani). Kushoto
ni DoriS Mollel ambaye ni Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya
Doris Mollel Foundation (DMF) na wengine ni maafisa kutoka Hospitali ya
Taifa Muhimbili. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[DAR
ES SALAAM] Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongeza
juhudi binafsi zinazofanywa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation (DMF)
katika harakati zake za kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati
(njiti) na mambo ya elimu hapa nchini huku ikiahidi kuendelea
kushirikiana nayo kufikia malengp yake.
Kauli
hiyo imetolewa mapema leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi
Meck Sadiki wakati wa kupokea vifaa maalum vya kusaidia watoto njiti
vilivyotolewa na taasisi hiyo ya Doris Mollel Foundation tukio
lililofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jengo la Watoto.
“Tunatambua
mashine hizi ni bei kubwa na Serikali pekee yake haina pesa hivyo kwa
kusaidiana na wadau kama hivi n faraja sana na tunapongeza juhudi hizi
za taasisi ya DMF kwa kujitokeza kusaidia mashine kwa watoto njiti”
ameeleza Mkuu wa Mkoa huyo.
Mkuu
wa Mkoa huyo aliongeza kuwa, Mashirika mengine yaendelee kujitokeza
kusaidia huduma za kijamii ikiwemo vifaa kama taasisi ya Doris Mollel
kwani asilimia 100 ya wagonjwa na watu wengine wenye mahitaji katika
tiba wanakimbilia Dar es Salaam hasa Hospitali ya Muhimbili.
“Tunaomba
tena mukipata nyingine musisite kutiletea hapa maana Mkoa huu unapokea
wagonjwa wengi kutoka maeneo mengi ya Tanzania na vifaa vya tiba mara
nyingi vinakuwa ni vichache, Huko mikoani wanapewa rufaa waanakuja hapa
pia hivyo DMF musisite kuja tena” alimalizia Mkuu wa Mkoa huyo.
Hata
hivyo kwa upande wake Mwanzilishi na mtendaji Mkuu wa DMF, Doros
Mollel amemweleza Mkuu wa Mkoa Meck Sadik kuwa wataendelea kushirikiana
na Serikali bega kwa bega katika juhudi za kusaidia watoto njiti nchini
ikiwemo kutoa elimu, vifaa na usaidizi kwa jamii dhidi ya kukabiliana
na watoto njiti nchini.
Katika
tukio hilo, Mkuu wa Mkoa alishudia vifaa hivyo na kupokea kutoka DMF
sambamba na kutembelea wote ya watoto njiti pamoja na ile ya Kangaroo
ambayo wamama wenye watoto njiti wanakuwa wanapatiwa uangalizi maalum
dhidi ya watoto wao ikiwemo kupata joto la Mama na baadae alipanda mti
maalum mbele ya jengo hilo la Watoto kama kumbukumbu na juhudi za wadau
katika kusaidia jamii dhidi ya watoto njiti.
DMF
imeweza kusaidia vifaa katika wodi hiyo ya watoto Muhimbili vikiwemo
(Suction machines, Oxygen Concentrators na Feeding tubes). Aidha Doris
Mollel amebainisha kuwa baada ya hapo wanatarajia kuelekea mikoa ya
Kanda ya Ziwa kutoa vifaa kama hivyo huku lengo ikiwa ni kufika mikoa
yote ya Tanzania.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili wakishuhudia tukio hilo maalum
la taasisi ya DMF ilipotoa vifaa hivyo katika kitengo cha Jengo la
Watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadik akipata maelezo juu ya vifaa hivyo vilivyotolewa na Taasisi ya DMF.
Msimamizi wa
wodi ya akina mama wanaopatiwa huduma ya Kangaroo dhidi ya watoto wao
ambao walizaliwa njiti, akimpatia maelezo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
alipotembelea wodi hiyo leo.
Picha ya juu
na chini Mkuu wa Mkoa wa Dar e Salaam akiwafariji baadi ya wakinamama
waliojifungua watoto kabla ya wakati maarufu njiti wakati alipotembelea
wodi hiyo ya watoto mapema leo.
Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam akimpatia zawadi ambayo ni jozi ya soksi kwa ajili ya
kusaidia watoto njiti kwa mmoja wa wamama waliokuwa katika wodi hiyo ya
watoto njiti.
Keki maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya siku maalum ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati maarufu njiti
Mtoto Amne Salim (3) ambaye ni njiti akikata keki maalum kwa niaba ya watoto wenzake katika tukio hilo mapema leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akimlisha keki mtoto Amne Salim katika tukio hilo.
Mtoto Amne Salim akimlisha keki Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadik katika tukio hilo.
Baadhi ya
akina mama waliokwenye mpango maalum wa kutunza watoto wao waliozaliwa
njiti ujulikanao kama Kangaroo wakiwa wodini mapema leo wakati wa ugeni
wa DMF na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam walipotembelea wodi hiyo.
Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaamm Meck Sadik akipokea na kukabidhi vifaa maalum kwa
ajili ya kusaidia watoto njiti katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
vilivyotolewa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation mapema leo.
Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Meck Sadik akipanda mti maalum baada ya zoezi hilo la
Taasisi ya Doris Mollel Foundation kutoa misaada ya vifaa vya watoto
njiti.
Shughuli hiyo ya upandaji mti wa kumbukumbu ikiendelea..
Mama mzazi wa Doris Mollel akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

No comments :
Post a Comment