Dkt. Ramadhani Dau mkurugenzi mkuu wa NSSF
Na Christian Gaya Majira Machi 18, 2014
Asilimia
kati ya 70 na 75 ya wananchi wa Tanzania wanaishi katika makazi holela. Hadi
sasa Tanzania ina mahitaji ya zaidi ya nyumba milioni tatu kwa ajili ya makazi
ya watu katika maeneo mbalimbali ya nchi
Kwa ajili ya kusaidia serikali
katika kutatua changamoto zinazolikumba
taifa NSSF limekuja na sera yake ya uwekezaji wa kuhakikisha ya kuwa angalau asilimia
ya 75 ya fedha za uwekezaji kila mwaka wa fedha zinatengwa kwa ajili ya
uwekezaji na asilimia 25 inayobakia inatumika kwa ajili ya kulipa mafao,
shughuli za utawala na uendeshaji wa mfuko na shughuli zingine za maendeleo za
shirika
“Tumeamua
kuweka mikakati zaidi kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu kwa ajili ya kuhakikisha
ya kuwa wateja wetu wanamiliki nyumba zao za kisasa zinazouzwa kwa bei nafuu
ili kumwezesha kila mwanachama mchangiaji wa
mfuko huu wa NSSF anamiliki
nyumba na kuboresha maisha yake” Daktari Dau ambaye ndiye mkurugenzi mkuu
anasema.
Shirika
la taifa la hifadhi ya jamii linasema linategemea kupanga muda wa kumaliza wa
kujenga mradi wa nyumba za gharama na nafuu zipatazo kama 7600 kama jitihada za
mfuko huo katika kujenga nyumba zenye staha kwa watanzania
Mkurugenzi mkuu anasema ila
isipokuwa nyumba hizi za gharama nafuu zimelengwa hasa kuuziwa wanachama wa
NSSF kwa mkopo wa muda mrefu na zinategemewa kujenga maeneo na sehemu za kijiji
cha Dege na kigamboni wilayani Temeke. Daktari Dau anaeleza ya kuwa mradi huu
utagharimu kiasi cha tabribani fedha za kimarekani zipatazo dola 5048 na
zinategemewa kumalizika kujenga ufikapo mwaka 2018
Kulingana na maelezo yake Dau
anasema mradi huu utamepakiwa kutekelezwa kwa awamu kuu tatu, wakati awamu ya
kwanza itakayokuwa imejenga nyumba zipatazo 2,500 imepangwa kumalizika mwisho
mwa mwaka 2016
Na awamu ya pili inategemewa
kumalizika mnamo mwaka unafuata wa mwaka 2017 ambapo nyumba zitapato 2,500
zitakuwa zimesha ezekwa tayari kwa mauzo kwa wanachama wa mfuko wa NSSF. Wakati kwa awamu ya tatu
mpaka kufikia mwaka 2018 nyumba zipatazo 2,460 zinategemewa kumalizika
“Nyumba hizo zinategemewa kuuzwa
katika ya fedha za kimarekani dola 80,000 mpaka dola 130,000 na mfuko uko
tayari kupokea fedha hizo kuanzia sasa kwa wanachama yeyote anayetaka
kutanguliza malipo” anasema.
Daktari Dau anawahakikishia kwa
yeyote atayekuwa mkazi wa huko Dege, ya kwamba kijiji cha Dege kitakuwa na
huduma zote za muhimu za kijamii zikiwemo shule, hospitali, nyumba za
ibada, sehemu za kupaki magari, sehemu za burudani na starehe na vifaa vyote
vya usalama na ulinzi
Pamoja na hayo mwenyekeiti wa bodi
ya wakurugenzi Bwana Abubakar Rajabu
anasema ya kuwa bodi yake imeridhika na maendeleo ya mradi huo na ana uhakika
ya kuwa wa muda uliopangwa kumaliza kazi utatekelezwa vile vile bila wasiwasi.
Kijiji cha Dege kinajengwa na NSSF
baada ya NSSF kuingia ubia na Kampuni ya Azimio ambayo inamiliki ekari karibu
3000 zilizoko Dar es Salaam
Mpaka kumalizika kwake daraja la
Kigamboni litagharimu fedha za kimarekani zipatazo dola milioni 33 ambazo ni
sawa sawa na shilingi za kitanzania bilioni 214.6 ikitekelezwa na NSSF kwa
asilimia 60 ya fedha ikishirikiana na serikali kwa asilimia 40 ya gharama hizo
za ujenzi. Ambayo inahusisha kwa upande mmoja kujenga barabara ya lami ya
kilomita moja( km 1) zikiwa na barabara nyembamba zipatazo sita kutoka kurasini
zikiwa juu ya daraja lenye meta 680 na barabara nyingine ya lami yenye kilometa
moja na nusu (km1.5) ambayo vile vile kwa upande mwingine itakuwa na barabara
nyembamba zipatazo sita
kulingana
na mpango yakinifu daraja la kigamboni lilitegemewa kumalizika mwezi Januari mwaka 2015 lakini kutokana na
mwingiliana wa changamoto mbalimbali ,
zikiwemo na baadhi ya wakazi kukataa
kuondoka huenda mradi huo ukaishia kumalizika mnamo mwezi wa sita au wa saba
mwakani
kwa upande wa meneja wa mradi Bwana Karim Mattaka anasema
kutokana na wakazi kukataa kuhama wamesababisha ujenzi wa daraja kupungua kasi
ya ujenzi wake. Tulikuwa tulipanga
kumaliza mradi huu mwezi wa juni
mwaka ujao, lakini kutokana na changamoto hii, huenda ikachukua miezi
sita au zaidi alisisitiza
Mattaka
ambaye ndiye meneja wa mradi huo anawakumbusha serikali kuchangia asilimia 40
ya fedha inayotakiwa kwa ajili ya kutoa msukumo wa mwendelezo wa ujenzi wa
mradi, anasema mpaka sasa NSSF imekuwa ikitumia fedha yake na kama serikali
watachelewesha sana hizo fedha huenda
wakawa ndiyo kizuizi cha maendeleo ya mradi na mradi kutomalizika kwa muda wake
uliopangwa
Mkurugenzi mkuu
anasema katika mwaka wa fedha 2012/2013 Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
yaani NSSF liliweza kupata mapato ya kiasi cha shilingi milioni 678,708.5 ambalo
ilikuwa sawa na asilimia 88.7 ya lengo. Makusanyo
haya ya mapato yaliweza kutumika katika kulipa mafao ya Wanachama, kuwekeza
katika vitega uchumi, kulipa gharama za uendeshaji na miradi ya maendeleo.
Daktari anabainisha
ya kuwa wakati huo huo wa mwaka fedha semina 542 zilifanyika kwa waajiri na wanachama
nchi nzima ili kuweza kuelewa vizuri mfumo mpya wa Hifadhi ya Jamii kwa ujumla
ukiwemo na Mkutano Mkuu wa Tatu wa wadau uliofanyika mwezi Februari 2013 ambao
ulihudhuriwa na wanachama na wadau wa sekta ya jamii wapatao 745. Vile vile katika
mwaka wa fedha 2012/2013 Shirika liliweza kupima afya za wanachama wake wapatao
6,283 kama wajibu wa sehemu yake wa fao bima ya afya na Wanachama wapatao 78,670 ambao ni sawa na asilimia
68.11 ya lengo la wanachama 115,500 waliweza kuandikishwa kwa kipindi hicho cha
katika mwaka wa fedha 2012/2013.
Aidha, katika mwaka wa
fedha 2012/2013 Shirika lilipa mafao mbalimbali kama vile mafao ya muda mrefu ambayo ni kama vile
pensheni ya uzee, pensheni ya ulemavu na pensheni ya urithi na kundi la pili ni mafao ya muda mfupi
ambayo ni kama vile mafao ya
uzazi, mafao ya kuumia kazini na magonjwa yatokanayo na kazi, msaada wa mazishi
na mafao ya bima ya afya yaani “mafao ya matibabu” (SHIB). Shirika pia hulipa mafao ya kujitoa uanachama
kwa mfumo wa akiba kwa wanachama aliyeondoka katika ajira kwa sababu mbalimbali
ya jumla ya shilingi bilioni 185.32 ambazo ni asilimia 183.03 ya lengo la shilingi
bilioni 101.24 kwa wanachama 54,840.
Pamoja na hayo mkurugenzi
mkuu anasema mchakato umeanza wa utekelezaji wa mradi wa uzalishaji umeme wa
megawati 150 katika eneo la Mkuranga. Hivi sasa mradi upo katika hatua ya
kupata washauri elekezi kwa ajili ya usanifu wa njia ya kusafirishia umeme
kutoka Mkuranga hadi kwenye Gridi ya Taifa Kinyerezi-Dar es Salaam na mradi
huu, utatekelezwa kwa ushirikiano na TANESCO. “Wakati taratibu za kupata
mshauri elekezi kwa ajili ya kituo cha kufua umeme wa megawati 300 zimeshaaanza
mwaka wa fedha 2013/14, baada ya kufahamu mazingira ya mradi na njia ya
usafirishaji umeme. Lengo ni kufanya miradi hii itekelezwe na kumalizika kwa
wakati mmoja” anasema
“Ujenzi wa daraja la
Kigamboni unaendelea vizuri. Aidha, daraja la muda la kusaidia ujenzi wa daraja
la kudumu limekamilika na kazi ya ujenzi wa daraja la kudumu imeanza. Mbali na
mafanikio hayo, kuna changamoto ya kulipa fidia kwa wamiliki wa maeneo ya
upande wa Kurasini na Kigamboni ambayo yamo ndani ya eneo la barabara unganishi
ambapo tathmini imefanyika ingawa huu mradi wa ujenzi wa daraja la kigamboni unategemewa
kukamilika Januari, 2015” mkurugenzi mkuu wa NSSF anaeleza.
Daktari Dau
anaendelea kusema ya kwamba ujenzi wa ofisi na vitega uchumi umekamilika katika
mikoa ya Arusha, Kigoma pamoja na wilaya ya Kahama. Aidha, ujenzi unaendelea
katika mikoa ya Morogoro, Shinyanga, Moshi, Mwanza, wilaya za Ilala na Temeke
pamoja na ujenzi wa kambi ya Jeshi eneo la Kihangaiko, Wami za Jeshi la
wananchi (TPDF) kwa kutumia mitambo ya UBM
pamoja na ujenzi wa ofisi za kumbukumbu za wanachama katika mikoa ya
Kilimanjaro na Mara tayari umeshakamilika.
Dau anasema shirika
limeshamekamilisha utayarishaji wa eneo la zahanati ya Apollo kwenye jengo la
Mwalimu Julius Nyerere lililopo barabara ya Bibi Titi/Morogoro, Dar es Salaam
ikiwemo na Ujenzi wa ofisi za Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) unaendelea na
ujenzi wa jengo la Mzizima jijini Dar es Salaam ambao nao umeshaanza. Aidha
ujenzi wa hoteli ya kisasa Mwanza, ujenzi wa kijiji cha kisasa Kigamboni
(Tuangoma na Dungu “Farm”) upo katika hatua za kupata makampuni ya ujenzi na katika
kutekeleza mpango wa kufanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa barabara ya Dar es
Salaam mpaka Chalinze, NSSF imeingia makubaliano na kampuni ya Malaysia kwa
kuwasilisha maombi ya kazi ya ujenzi wa barabara hiyo.
“Aidha katika mwaka
wa fedha 2013/14 Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii linategemea kukusanya jumla ya shilingi trilioni 1.2 na
kutumia kiasi hicho cha fedha kulipia mafao ya wanachama, kuwekeza kwenye
vitega uchumi mbalimbali, gharama za uendeshaji na miradi ya maendeleo;na kuendelea
kutoa elimu kwa wanachama, waajiri na umma kwa ujumla ili waweze kuelewa vizuri
mfumo wa hifadhi ya jamii, Shirika litaendelea na mpango wa kupima Afya za
wanachama wake, Kufanya Mkutano Mkuu wa Nne wa wadau wa NSSF, Kufanya tathimini
ya uwezo wa mfuko kifedha ili kulipa mafao kwa wanachama wake kwa muda mrefu
ujao na kuanza utekelezaji wa mradi wa uzalishaji umeme wa megawati 300 katika
eneo la Mkuranga; na mradi wa uzalishaji umeme megawati 49 katika eneo la
Malagarasi mkoa wa Kigoma” Daktari Dau anasema”
Anasema mwaka wa
fedha 2013/14 Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii litaendelea na ujenzi wa
Daraja la Kigamboni na ujenzi wa ofisi na vitega uchumi katika mikoa ya Morogoro,
Shinyanga, Mbeya, Kilimanjaro, Mara, Mwanza, wilaya za Ilala, Temeke na
Kinondoni, kushiriki katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Apollo jijini Dar
es Salaam, na kuendelea na ujenzi wa ofisi za RITA na ujenzi wa jengo la
Mzizima jijini Dar es Salaam, hoteli ya kisasa Mwanza, ujenzi wa kijiji cha
Kisasa Kigamboni (Tuangoma na Dungu “Farm”), ujenzi wa kijiji cha kisasa
Kigamboni (Azimio) na Ujenzi wa Jengo la Maadili Dar es Salaam pamoja na kuanza
ujenzi wa kituo cha mabasi Mwandiga Kigoma, Kijiji cha Bunge Dodoma (MP’s
Village); ofisi za Bunge Dar-es-Salaam na nyumba za watumishi wa Serikali nchi
nzima.
Shirika la taifa la
hifadhi ya jamii linakupa nafasi ya kumiliki nyumba ya kisasa zilizojengwa
mtoni kijichi, kigamboni katika eneo la kuvutia lenye eneo maalumu la maduka,
kituo cha afya. Nyumba hizi zinauzwa moja kwa moja na NSSF bila kupitia benki.
Anasema nyumba hizo zipo 300 ndani ya eneo la mtoni kijicchi, kigamboni, umbali
wa kilometa 15 kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam , Nyumba ni za vyumba 2
hadi 4 vyenye ukubwa wa mita za mraba 75 hadi 125. Unaweza kununua kwa fedha
taslim au kwa mkopo wa miaka 15 kwa kutozwa riba ya asilimia 11.4 kwa mwaka na fomu
zinapatikana ofisi za NSSF nchi nzima kwa tozo la shilingi 5000/ tu.
“Kwa ujumla nyumba ina
sakafu ya vigae vyoo na bafu ndani , chumba kikuu chenye choo, jiko kubwa
pamoja na maji ya moto, umeme na maji, na ili kuhakikishia usalama ni kwamba
nyumba imejengwa kwa nondo za usalama kwenye milango na madirisha, madirisha ya
kisasa, eneo la kuegesha gari na ukuta wa uzio kwa kila nyumba 50”. anasema
mkurugenzi mkuu.
“Sifa
kubwa ya kuuziwa nyumba hizi na kumilikishwa ni kwa watanzania ambao ni
wanachama wa NSSF au wanachama wapya watakaojiandikisha wakati wa manunuzi au
watakao jiandikisha kama wanachama wa hiari kama tayari wapo kwenye mfuko
mwingine wa hifadhi ya jamii na watanzania waishio nje ya nchi wenye mafao ya
WESTADI” Daktari Dau anabainisha.
Anasema utaratibu wa
ununuzi wa nyumba hizi kwa kutoa fedha taslimu yaani papo kwa papo na kwa kwa mkopo na kwamba fomu zote zinawasilishwa
NSSF makao makuu ghorofa ya 11, kwa ajili ya kufanyiwa uchambuzi na baadaye mnunuzi
mwenye sifa ataarifiwa kwa barua aina ya nyumba aliyopata na kupewa mkataba wa
manunuzi na mnunuzi mwenye sifa atalipa kwa mkupuo au malipo ya miezi mitatu ya
awali na bei inategemea ukubwa wa nyumba, idadi ya vyumba. “Bei inaanzia shilingi milioni 65 hadi
milioni 113 bila kodi na malipo yote yanatakiwa kufanyika NSSF na vigezo na
masharti kuzingatiwa” mkurugenzi mkuu anasisitiza.
Mkurugenzi mkuu anasema shughuli za uwekezaji za shirika zinafanywa
chini ya ibara ya 62 ya sheria Na 28 ya mwaka 1997 na sera ya uwekezaji ya
shirika ambayo inafanyiwa marekebisho ya mara kwa mara ili iendane na
mabadiliko ya uchumi ndani na nje ya nchi.
“Shirika linafanya uwekezaji katika miradi
mbalimbali kwa malengo ya kulinda thamani ya michango ya wanachama, kupata fedha
za uendeshaji wa shughuli za shirika, kuboresha mafao kwa wanachama na
kuchangia juhudi za serikali katika kuinuia uchumi wa nchi, shirika kwa kufuata kanuni za usalama wa mtaji,
uwezo wa kuleta faida, uwezo wa kitega uchumi kubadilika kuwa fedha taslimu,
kuchangia masuala ya kijamii, na kutawanya uwekezaji” anasisitiza
kwa kuzingatia kanuni zilizopo hapo juu shirika huwekekeza katika
maeneo tofauti kwa viwango tofauti kulingana na sera ya uwekezaji kama vile
kwenye dhamana za kiserikali, akiba ya muda maalumu, miradi ya ujenzi, hisa
kwenye makampuni, mikopo kwa makampuni, dhamana za makampuni na hisa kwenye
soko la mtaji.
No comments :
Post a Comment