Mojawapo ya majengo ya vitega uchumi ya Mfuko wa pensheni wa PSPF lililopo mjini Dar es salaam
Na Christian Gaya majira April 01, 2014
Mifuko ya pensheni ya
hifadhi ya jamii nchini inatakiwa kujiwekea malengo na mikakati mbalimbali ili
kuleta ufanisi na tija katika shughuli za ulipaji wa mafao. Nafikiri mmeona
baadhi ya taasisi za kifedha hasa mabenki na mengineyo wana na utaratibu wa
kuwa na mapatano ya utoaji wa hudhuma baina taasisi hizo na wateja wao kwa
kuanzisha mikataba ya huduma kwa wateja.
Ambapo mikataba hiyo
inakuwa ni hatua muhimu sana katika utoaji wa huduma bora katika misingi ya
uwazi na uwajibikaji. Kwa kufanya hivyo kwa mifuko ya pensheni ya hifadhi ya
jamii wateja wao ambao ni wanachama, wastaafu na familia zao, waliojiajiri
wenyewe, na wageni wanaofanya kazi kwa
mikataba watapata uhuru na uelewa wa kufahamu matarajio yao katika huduma
zinazotolewa na mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii na hata viwango vya muda
ambavyo vitawawezesha kupanga mambo yao wateja vyema kabisa bila kusumbuka,
badala ya kusubiri huduma bila ya kufahamu upatikaji wake wa huduma hizo na kwa
viwango fulani vilivyoanishwa wazi kwa wateja wa ndani na wa nje.
Mifuko ya pensheni ya
hifadhi ya jamii kwa kufanya hivyo itawezesha kuwa na mapatano
yatakayowawezesha wateja wao kufahamu huduma zinatolewa na mifuko ya pensheni
ya hifadhi ya jamii, vikiwemo na hata viwango vya huduma na hatua ambazo mteja
anaweza kuzichukua iwapo viwango vya huduma vitakuwa kinyume na matarajio ya
mkataba.
Jambo la kuangalia
kuhusu mifuko ya pensheni ni kujua bidhaa au huduma zake. Je huduma hiyo
inahitajika na watu wote, chukua mfano wa chumvi. Hivyo jaribu kujiunga na
mfuko wa pensheni ambayo huduma zake zinahitajika na wengi au wafanyakazi wengi
na familia zao, pamoja na wazee, vijana, watoto, walemavu, wajane, pamoja na
watoto yatima kwa kukidhi mahitaji yao wanapopatwa na majangwa ya aina
mbalimbali. Lazima ujiulize kama je huduma zinazotolewa na mfuko wa pensheni
zina mbadala au hazina mbadala. Na hiyo huduma ina uhakika mkubwa wa soko. Ina
nguvu kubwa ya ukiritimba nikiwa na maana ya kuwa na uwezo wa huduma kuwa na
soko kubwa lenye uwezo wa kudai bei kubwa bila kupunguza uhitaji na matumizi.
Hivyo tafuta andika na jiunge na mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii wenye
huduma zenye sifa nzuri.
Unahitaji kufanya
uchunguzi wa kutosha au kina kuhusu utendaji wa mifuko hii hasa kwa kufanya
utafiti wa kutambua thamani, soko, kutatua udhaifu, kutoa majibu ya maswali
tata, kupata taarifa zaidi na za uhakika. Kujiunga na mfuko wa pensheni wowote
wa hifadhi ya jamii ni kutafuta sehemu yenye usalama ya kuweza kuwekeza
michango yako ya kila mwezi kwa ajili ya
aina mbalimbali ya majanga yanayoweza kusababishwa na ugonjwa, kuumia ukiwa
kazini, kifo, kupata ulemavu, na kadhalika. Hivyo unahitaji kufanya utafiti wa
makini sana kwa kuchunguza taarifa mbalimbali juu ya mfuko huo wa hifadhi ya
jamii unaotaka kujiunga nao ili taarifa hizo ziweze kukusaidia kutoa maamuzi wa
busara wa kukuwezesha kuzingatia kanuni misingi na vigezo maalumu ambazo
vitakusaidia kujibu maswali mengi.
Baadhi ya maswali
muhimu yanaweza kuwa kama vile utawezekeza wapi? Na mfuko upi wa pensheni ya
hifadhi ya jamii, na watakata kiasi cha asilimia ngapi kutoka katika mshahara
wangu, na mwajiri wangu yeye atatoa kiasi cha asilimia ngapi kama umeajiriwa.
Hivyo ni juu ya mfanyakazi mwenyewe kama mwekezaji kufanya utatafiti wa kina
ili kujua ubora wa mfuko huo unaotegemea kujiunga nao kabla ya kujisajiri.
Unatakiwa usiwe mwepesi wa kufanya maamuzi bila kwanza kuwekeza kwenye utafiti
hasa kama vile kuwaona wataaalamu wanao weza kukusaidia kukupa ushauri mahiri.
Ni muhimu kuangalia
mifuko hii ya pensheni kwa kuangalia uongozi, yaani menejimenti, hali ya
kifedha, thamani ya mfuko wa pensheni kwa sasa, taarifa mbalimbali, matarajio
ya mfuko wa pensheni kwa kipindi kijacho
kama pamoja na thamani ya mfuko wa pensheni kwa miaka ijayo. Uchambuzi unahitajika uwe unaolenga zaidi
katika kuchambua thamani ya mfuko wa pensheni kutokana na taarifa halisi
zilizopo na siyo taarifa za matarajio ya baadaye. Mchangiaji wa michango au
Mwekezaji makini anatakiwa aweke mkazo katika kufanya makosa makubwa kwa sababu
uchunguzi au utafiti au upembuzi wa mifuko hii ya pensheni ya hifadhi ya jamii
inatakiwa ufanyike kisanyansi kwa kuzingatia uchambuzi wa takwimu na uchambuzi
nyinginezo ingawa vigezo hivi vya takwimu vinaweza kuwa muhimu lakini mara
nyingi huwa havijitesholezi hata kidogo. Hivyo shughuli kubwa katika mambo ya
kujiunga au kujisali na mifuko hii ya pensheni ya hifadhi ya jamii inatakiwa
kufanya utafiti, ingawa unagharimu muda mwingi kabla ya maamuzi sahihi.
Uamuzi wa kuwa
mwanachama wa mfuko wa pensheni ya hifadhi ya jamii unatakiwa utokana na
takwimu na taarifa nyinginezo makini zinazotakiwa zifanywe na mfanyakazi
mwenyewe na siyo kufuata mkumbo wa watu wengi wanasemaje. Kwa kufanya hivyo
tumeona mara nyingi wafanyakazi wengi hukosea kwa sababu alifuata mazungumzo ya
watu wengi juu ya mfuko fulani wa pensheni hivyo anatakiwa kufanya utafiti na
uamuzi wake ufuate utafiti na takwimu siyo uzushi au habari motomoto ambazo
hazijafanyiwa uchunguzi wowote. unahitaji wewe kama mfanyakazi kuhakikisha ya
kuwa unafanya utafiti au uchunguzi wa kina
na kuchambua ripoti za kila mwaka za mifuko ya hifadhi ya jamii huku
ukuzingatia yale yanayotendeka katika sekta tofauti nchini na kwingineko katika
nyanja za mifuko ya hifadhi ya jamii.
Unahitaji kujua usalama
wa michango yako unayochangia kila mwezi. Lazima ujue hiyo michango yako
huwekezwa mahali ambapo uwezekano wa kupata hasara ni mdogo sana, na kuchunguza
kama huwekezwa sehemu ambapo kuna uwezekano mkubwa wa kupata faida. Hii
ijulikane na itambulike ya kuwa kiupambele katika ufuatiliaji wake kwenye
michango yako au fedha yako unayochangia kwanza inatakiwa kuwa na usalama wake
na siyo faida. Kipa umbele hapa kwanza ni inatakiwa kuwa michango yako na siyo
faida unayotakiwa kutarajia. Faida inatakiwa kushika nafasi ya tatu na siyo
nafasi ya kwanza au ya pili.
Unatakiwa kulikumbuka
hili jambo sana ukitaki ufanikiwe kutokana na mifuko hii ya pensheni ya hifadhi
ya jamii hakikisha unafanya utafiti au uchunguzi kuhakikisha ya kuwa mfuko
unafuata utaratibu wa kisayansi wa uwekezaji wa michango yako kwa kufuata
kanuni za kulinda usalama wa fedha zako unazotegemea kuchangia na uwekezajji
uwe ule wa kuleta faida na kuwa na uwezo wa kitega uchumi kubadili kuwa fedha
taslim na siyo vinginevyo, na mfuko ambao unajitoa kuchangia masuala ya kijamii
inayoizunguka na kuwa na uwezo mkubwa wa kutawanya uwekezezaji wa michango yako
bila kufuata misukumo ya wanasiasa badala ya kufuata kanuni za kulinda usalama
wa michango yako ya pensheni.
Hata hivyo, ili mifuko
ya pensheni ya hifadhi ya jamii iweze kutoa huduma bora kwa wakati kama
ulivyokusudiwa katika mapatano hayo, lazima wategemee kupata muuitikio na
ushirikiano kutoka kwa wateja ili kutimiza makubaliano yaliyowekwa katika
mkataba. Na mifuko ya pensheni ya hifadhi ikumbuke ya kuwa wateja ndiyo viungo
muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa malengo ya kila siku ya mifuko, kwa
kuwa taarifa zinazotoka ndizo zinazowezesha mifuko ya pensheni ya hifadhi ya
jamii kutoa huduma stahiki.
Utahitaji kujifunza zaidi
utendaji wa mifuko ya pensheni kutoka kwa wataalamu na mamlaka inayohusika kama
vile mdhibiti na msimamizi wa mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii yaani SSRA
na hata kwenye makala za kijamii kama vile makala za hakipensheni
Sawa umepewa uhuru huo wa
kuchagua kujiunga na mifuko hii ya pensheni, hivyo ningependa kukuuliza wewe
mfanyakazi uliyeajiriwa leo je unajua mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii
unaotoa mafao bora zaidi ya kulingana na kiwango cha shirika la kazi duniani
ILO? yaani kwa idadi ya mafao, ubora wa mafao, na kulipwa pensheni kulingana na
ukali wa maisha ya kila siku.
Mfanyakazi unahitaji kujua
kiundani zaidi juu ya ubora wa mifuko hii ya pensheni ya hifadhi ya jamii,
lazima ujue hata viwango vya ubora huduma zao, mazingira ya sehemu unapopatiwa
huduma kuanzia getini kwa askari mpaka unapofungulia madai ambapo yanahitaji
kuwa sehemu za kuvutia zaidi. Je huchukua siku ngapi kupata hundi yako ya
pensheni au ya mafao ya kujitoa, je ahadi zako zinatekelezwa kama
walivyokuahidi, na anayekuhudumia anakuchagamukia na kukuhudumia kama ndiye
mfalme wa mfuko huo wa pensheni. Je hao wafanyakazi wa mifuko ya pensheni
wanajua ya kuwa wewe ndiye mwajiri wao.
Wanaandaa pensheni yako ya
kustaafu baada ya mwezi mmoja kama walivyokuahidi. Kuna mambo mengi ya
kuchunguza kwanza kabla ya kujiunga hasa kama mwanachama mchangiaji utahitaji
kujua kwanza utaratibu wa kujisajiri kiwango cha kuchangia ni asilimia ngapi ya
kipato chako cha mwezi, mchango huo unakatwa kwenye mshahara kabla ya
marupurupu mengine au baada ya kuchanganya na marupurupu mengine yaani kwenye
basic salary au kwenye gross salary. Je mafao yako ya pensheni yanakatwa kodi
au hayakatwi.
Na lazima ujue ni kwa
sababu gani ukate kwenye basic au gross salary. Na ni nani anayetakiwa
kukuandikisha wewe kwenye mfuko huo wa pensheni. Na kiwango gani mwajiri naye
inatakiwa akuchangie ili ichanganye pamoja na kupelekwa kwenye mfuko wa
pensheni. Na hiyo michango inatakiwa ipelekwa kwenye huo mfuko kwa wakati gani
wa muafaka. Je ni wajibu wa nani kuhakikisha kuwa michango hiyo inapelekwa
kwenye mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii. Na chama cha wafanyakazi kina
wajibu gani juu ya michango hii ya pensheni kazini.
Je mfumo gani wa hifadhi
ya jamii ni wa pensheni au wa akiba ya wafanyakazi. Ni aina gani ya mafao
yanayotolewa na mfuko huo wa hifadhi ya jamii. Je kuna mafao ambayo unaweza
kunufaika wakati unapoendelea kufanya kazi yaani ya muda mfupi na ya yale
ambayo utanufaika baada ya kustaafu yaani ya muda mrefu. Je familia yako
unawezaje naye kunufaika na mafao hayo ya muda mrefu na ya muda mfupi. Je
ukusanyaji wa michango ya pensheni una urasimu mwingi na usio na uwazi na
ukweli kwa mchangiaji.
Je mipango ya malipo ya
mafao kwa mwanachama inalipwa kwa wakati muafaka na kwa usahihi wa uhakika
kabisa bila ya mapunjo au kuzidishiwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Je
wanachama anaweza kutegemea kupata habari zote na ushauri na zilizokamilika
karibu na mahali karibu anapoishi. Mwanachama anaweza kupata habari na ushauri
wowote hata bila ya kuanza yeye kudai huduma hiyo. Je muda unaotumika kukokotoa
mafao yake ya pensheni ni mfupi au ni wa muda mrefu.
Je maamuzi yeyote juu ya
huduma za mwanachama zinahudumiwa kirafiki. Ni muhimu vile vile kama mwanachama
kujua wewe kama mchangiaji pamoja na mwajiri wako kila mmoja ana wajibu gani kwenye
mfuko huo wa hifadhi ya jamii. Mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii lazima
uweke wazi juu ya haki za wanachama hasa zile za kumruhusu mwanachama kuapili
kwenye bodi ya sheria au mahakamani atakapoona kwamba pale hajatendelewa haki
inavyotakiwa na mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii. Kama wanachama
mchangiaji wa mfuko wa pensheni je utashirikishwaje kwenye maamuzi na
uendeshaji wa mfuko huo na kwa faida ya nani. Sasa ni juu ya mfanyakazi
mwenyewe kuchagua kwa kutumia vigezo vya kitaalamu
Hivyo kuna haja kubwa
kila mfuko wa pensheni ya hifadhi ya jamii kuwa na mkataba wa huduma kwa wateja
wao ili kukuza uelewa kuhusu upatikanaji wa huduma na ubora wa huduma
zinazotolewa na mifuko hii pensheni ya
hifadhi ya jamii. Hii itawezekana kabisa hasa kwa kuwa na dhamira ya kuwasaidia
wanachama, wastaafu na familia zao na wadau wengine wa hifadhi ya ja namna ya
kuboresha na kutoa huduma bora zaidi mii nchini kuzielewa shughuli za mifuko
kwa ujumla, na namna ya kuwasiliana na mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii
pamoja na viwango vya huduma vinavyotarajiwa na jinsi hata kutatua matatizo kwa
muda muafaka pale yanapojitokeza. Mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii
itambue ya kwamba kuwa na mkataba wa huduma kwa wateja utawezesha wateja wao
kujua mafao yatolewayo, haki na wajibu wao ndani ya mifuko hiyo na kwa upande
mwingine mifuko hii ya hifadhi ya jamii itatoa fursa za wazi kwa wateja
kuwasiliana na mifuko ili kutoa mapendekezo ya namna ya kutoa huduma bora zaidi.
No comments :
Post a Comment