Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi
ya Jamii (SSRA),Ansgar Mushi (kushoto), akisisitiza jambo katika
mkutano huo.
Wanahabari
waliokuwepo kwenye mkutano huo wakichukua taarifa hiyo. Kushoto mwenye
tai ni Ofisa Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sterwat Bisanda.
Mkurugenzi
wa Sheria wa SSRA, Ngabo Ibrahim (kulia), akitoa ufafanuzi kwa
waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria.
MAMLAKA
ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) imesema haitasita
kumchukulia hatua mtu yeyote anayekiuka sheria za kujiunga na mfuko wowote
ulioanzishwa kwa sheria ya Bunge.
Hayo yalibainishwa na Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka hiyo Ansgar Mushi wakati akitoa taarifa kwa umma kupitia kwa
waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu uandikishwaji wa wanachama wapya
wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini.
Alisema SSRA jukumu lake kubwa ni
kusimamia na kudhibiti shughuli zote za sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini ikiwa
ni pamoja na Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii iliyoanzishwa kwa sheria za Bunge
ambayo ni NSSF, PSPF, PPF, GEPFE, LAPF na NHIF.
“Kwa mamlaka tuliyonayo hatutasita
kumchulia hatua mtu yeyote atakayekiuka sheria zilizopo za uandikishaji wa
wanachama wapya katika mifuko hiyo baada ya kuwepo kwa ukiukaji huo” alisema
Mushi.
Alisema sheria inayoruhusu mifuko hiyo
kuandikisha wanachama wapya wanaoingia kwa mara ya kwanza kwenye ajira kutoka
sekta rasmi au sekta binafsi isikiukwe.
Alisema sheria hiyo namba 5 ya mwaka
2012 pia inaruhusu wafanyakazi ambao wako kwenye ajira lakini hawajawahi
kuandikishwa na mfuko wowote kujiunga na mfuko watakaouchagua.
Mushi alisema kuwa siku za hivi
karibuni kumeibuka malalamiko ya uandikishaji wa wanachama wapya na kuwa baadhi
ya vitendo vinavyolalamikiwa ni mfuko kutengeneza, kutoa nyaraka za uwongo kwa
madhumuni ya kupotosha umma na hali halisi ya kupata ridhaa ya
wafanyakazi,waajiri na wadau wengine.
Alitaja mambo mengine kuwa ni kuandikisha
wafanyakazi kwenye mfuko kwa lazima wakati yupo kwenye mfuko mwingine na
mwajiri kumlazimisha mfanyakazi kujiunga na mfuko fulani.
Mushi alitaja malalamiko mengine kuwa
ni mwajiri kuwa na sera au miongozo ya ajira inayoelekeza wafanyakazi wake kujiunga
na mfuko fulani na matumizi ya njia za usajili zisizifaa kuandikisha wanachama.
Alisema vitendo hivyo vyote
vimeharamishwa chini ya Sheria namba 8 ya mwaka 2008 na miongozo ya
uandikishaji wanachama (socia Security Schemes (Memberrship Registration)
Guidelines, 2013 iliyotolewa chini ya sheria hiyo na kuwa yeyote atayejihusisha
na vitendo hivyo anavunja sheria.
Mushi alisema SSRA inapenda
kuwakumbusha ,Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wadau wote wakiwemo
waajiri na wafanyakazi kuzingatia matakwa ya Sheria namba 8 ya mwaka 2008
pamoja na miongozo ya uandikishaji wanachama ili kulinda uhuru wa wanachama wa
kujiunga na Mfuko wanaoupenda.




No comments :
Post a Comment