Kama manejimenti
inayohusika na kuendesha na kusimamia mfuko
wa hifadhi ya jamii wafahamu ya kama kweli wanazingatia utaratibu na
kanuni za utawala bora kuwa utawala bora basi hawana budi kuhakikisha kuwa
mfuko unaendeshwa na kuongozwa na utawala bora na kwa ufanisi wa hali ya juu
zaidi. Na ikumbukwe ya kuwa wanachama ndio waliotoa fedha zao kila mwezi kama
mtaji wa kuendesha mfuko na wanatarajia ya kuwa watapata huduma kama
walivyoahidiwa pale wanapokumbana na majanga ya aina mbalimbali kama vile ya kuumia
na kupatwa na magonjwa yanayotokana na kazi, ujauzito na kujifungua mtoto,
kuugua kufiwa na aliyekuwa mwanachama na alikuwa anategemewa na familia,
kufikia umri wa kustaafu na mengineyo.
Hivyo kama mwanachama
na kama unahitaji kuwa mwanachama unahitaji kujiuliza maswali mengi juu ya
mfuko wa hifadhi ya jamii unaotaka kujiunga nao kama linazingatia kanuni na
vigezo vya utawala bora. Kama mfuko huo unazingatia kanuni za uongozi bora
huenda kukawa na uwezokano mkubwa kwa mfuko kuwa na utendaji mzuri unaofikia
malengo na kukidhi matarajio ya wanachama wake na familia zao. Nafikiri
mmeshuhudia hata baadhi ya taasisi na makampuni makubwa ya kimataifa ufilisika
na kuanguka na mara nyingi makampuni haya yamekuwa yakitoa taarifa za uongo za
matumizi ya fedha na za kiutendaji, na wizi uliokithiri, malipo na marupurupu
yasiyoya kawaida kwa viongozi, mifumo ya ndani dhaifu ya udhibiti wa fedha,
kushidwa kudhibiti hatari na majanga, mawasiliano duni kati viongozi na
wanachama na uendeshaji mbaya unaosababisha wanahisa kupoteza mitaji yao na kupata
hasara. Mara nyingi wanachama wamekuwa wakijiuliza kuwa imekuwaje viongozi
hawakujua kuwa kuna hatari ya kufilisika?
Mfano mzuri ni huu wa
mfuko pensheni wa watumishi wa serikali (PSPF) kaimu mkurugenzi mkuu ndugu Adam
Mayingu anasema kuwa mfuko katika hali mbaya kifedha na mambo yakiendelea hivyo
hivyo kwa muda wa miaka mitatu mfululizo huenda mfuko ukafilisika na mpaka sasa
mfuko umepungua uwezo wa asilimia 10 kutoka katika kiwango kiwango
kinachotakiwa cha asilimia 40. Na kwamba hali ikiendelea hivi itabidi serikali
kama mdhamini wa mfuko na mdaiwa mkubwa wa mfuko huo itabidi iwajibike kulipa
michango na mafao yote ya wanachama
Taarifa inaonyesha kuwa
kutokana na utafiti uliofanya na wataalam wa pensheni unaonyesha kuwa PSPF
hauna fedha tena za kulipia mafao ya wanachama wake, ingawa kabla ya kuanzishwa
mfuko huu wa PSPF mwaka 1999 serikali ilifanya utafifi na kuonyesha ya kuwa
serikali ilikuwa na malimbikizo ya jumla ya bilioni 250 za kitanzania kama
michango ya wafanyakazi. Kabla yamwaka 1999 mfuko ulikuwa ukichangiwa na
serikali tu na watumishi wote wa serikali walikuwa hawakatwi katika mishahara
yao, lakini baada ya kubadilishwa mwaka 1999 na kiuitwa PSPF wanachama wake
wote walianza rasmi kuchangia nao. Na
mpaka kufikia mwaka 2006 malimbikizo hayo yalifikia kiasi cha shilingi bilioni
658.23 na kama serikali haijalipa mpaka leo njia nyingine ni kwamba PSPF
inatakiwa kuongeza kiwango cha kuchangia kutoka katika mishahara ya wanachama
wake ili kuendeleza mfuko ama ndio uwe mwisho wake.
PSPF ni taasisi ya
hifadhi ya hifadhi ya jamii iliyoanzishwa kwa sheria namba 2 ya mafao ya
hitimisho la kazi kwa watumishi wa umma ya mwaka 1999. Mpaka sasa watumishi wa
serikali pamoja na wakala za serikali huchangia asilimia 5 ya mshahara wa
mtumishi na waajiri wao huchangia asilimia 15. Inaonyesha mfuko ulianzishwa
bila kuwa na mtaji wa kuanzia kutokana na malimbikizo ya michango ya watumishi
(wafanyakazi) wa serikali kutolipwa na serikali
Kiwango au kiasi cha
mfuko wakati huo kilichotakiwa na serikali ilitakiwa kuchangia asilimia 93.3
ingawa tangia hapo serkali haikuweza kutoa kiasi chochote, ingawa naibu wa
fedha mheshimiwa Janeth Mbene aliiambia kamati ya mahesabu ya umma ya bunge ya
kwamba kwa mwaka huu wa fedha serikali itapunguza deni hilo kwa kiasi cha
shilingi bilioni 50 kwa kuilipa PSPF.
Katika kipindi cha pili
cha utafiti uliofanywa baaada ya PSPF kuanza kulipa mafao kwa wanachama wake
mwaka 2007, taarifa za kifedha ilionyesha kuwa mfuko ulizidi kuzorota zaidi kwa
kuwa na upungufu wa fedha za mafao kufikia trilioni 3.3 za kitanzania
ukilinganisha na malimbikizo ya kabla ya mwaka 1999 ya billion 250 za
kitanzania zilizokuwa zinadiiwa na PSPF kutoka serikalini.
No comments :
Post a Comment