Kuna njia nyingi za
kujifunza kama vile kusoma vitabu, kujifunza kutoka kwa watu waliokutangulia,
wenye uzoefu, mahiri na wenye mafanikio katika katika mfuko unaotaka kujiunga
nao. Utahitaji kujifunza zaidi utendaji wa mifuko ya pensheni kutoka kwa
wataalamu na mamlaka inayohusika kama vile mdhibiti na msimamizi wa mifuko ya
pensheni ya hifadhi ya jamii (SSRA)
Sawa umepewa uhuru huo wa kuchagua
kujiunga na mifuko hii ya pensheni, hivyo ningependa kukuuliza wewe mfanyakazi
uliyeajiriwa leo je unajua mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii unaotoa mafao
bora zaidi ya kulingana na kiwango cha shirika la kazi duniani ILO? yaani kwa
idadi ya mafao, ubora wa mafao, na kulipwa pensheni kulingana na ukali wa
maisha ya kila siku.
Je mfuko wa pensheni una mpango wa
kutoa angalau theluthi mbili ya mafao ya pensheni ya mwanachama kama amana ya
kupatiwa mkopo wa nyumba?
Mfanyakazi unahitaji kujua
kiundani zaidi juu ya ubora wa mifuko hii ya pensheni ya hifadhi ya jamii,
lazima ujue hata viwango vya ubora huduma zao, mazingira ya sehemu unapopatiwa
huduma kuanzia getini kwa askari mpaka
unapofungulia madai ambapo yanahitaji kuwa sehemu za kuvutia zaidi. Je huchukua
siku ngapi kupata hundi yako ya pensheni au ya mafao ya kujitoa, je ahadi zako
zinatekelezwa kama walivyokuahidi, na anayekuhudumia anakuchagamukia na
kukuhudumia kama ndiye mfalme wa mfuko huo wa pensheni. Je hao wafanyakazi wa
mifuko ya pensheni wanajua ya kuwa wewe ndiye mwajiri wao.
Wanaandaa pensheni yako ya
kustaafu baada ya mwezi mmoja kama walivyokuahidi. Kuna mambo mengi ya
kuchunguza kwanza kabla ya kujiunga hasa kama mwanachama mchangiaji utahitaji
kujua kwanza utaratibu wa kujisajiri kiwango cha kuchangia ni asilimia ngapi ya
kipato chako cha mwezi, mchango huo unakatwa kwenye mshahara kabla ya marupurupu
mengine au baada ya kuchanganya na marupurupu mengine yaani kwenye basic salary
au kwenye gross salary. Je mafao yako ya pensheni yanakatwa kodi au hayakatwi.
Na lazima ujue ni kwa
sababu gani ukate kwenye basic au gross
salary. Na ni nani anayetakiwa kukuandikisha wewe kwenye mfuko huo wa pensheni.
Na kiwango gani mwajiri naye inatakiwa akuchangie ili ichanganye pamoja na
kupelekwa kwenye mfuko wa pensheni. Na hiyo michango inatakiwa ipelekwa kwenye
huo mfuko kwa wakati gani wa muafaka. Je ni wajibu wa nani kuhakikisha kuwa
michango hiyo inapelekwa kwenye mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii. Na chama
cha wafanyakazi kina wajibu gani juu ya michango hii ya pensheni kazini.
Je mfumo gani wa hifadhi
ya jamii ni wa pensheni au wa akiba ya wafanyakazi. Ni aina gani ya mafao
yanayotolewa na mfuko huo wa hifadhi ya jamii. Je kuna mafao ambayo unaweza
kunufaika wakati unapoendelea kufanya kazi yaani ya muda mfupi na ya yale
ambayo utanufaika baada ya kustaafu yaani ya muda mrefu. Je familia yako
unawezaje naye kunufaika na mafao hayo ya muda mrefu na ya muda mfupi. Je
ukusanyaji wa michango ya pensheni una urasimu mwingi na usio na uwazi na
ukweli kwa mchangiaji.
Je mipango ya malipo ya
mafao kwa mwanachama inalipwa kwa wakati muafaka na kwa usahihi wa uhakika
kabisa bila ya mapunjo au kuzidishiwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Je
wanachama anaweza kutegemea kupata habari zote na ushauri na zilizokamilika
karibu na mahali karibu anapoishi. Mwanachama anaweza kupata habari na ushauri
wowote hata bila ya kuanza yeye kudai huduma hiyo. Je muda unaotumika kukokotoa
mafao yake ya pensheni ni mfupi au ni wa muda mrefu.
Je maamuzi yeyote juu ya
huduma za mwanachama zinahudumiwa kirafiki. Ni muhimu vile vile kama mwanachama
kujua wewe kama mchangiaji pamoja na mwajiri wako kila mmoja ana wajibu
gani kwenye mfuko huo wa hifadhi ya
jamii. Mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii lazima uweke wazi juu ya haki za
wanachama hasa zile za kumruhusu mwanachama kukata rufaa kwenye bodi ya sheria
au mahakamani atakapoona kwamba pale hajatendelewa haki inavyotakiwa na mfuko
wa pensheni wa hifadhi ya jamii. Kama wanachama mchangiaji wa mfuko wa pensheni
je utashirikishwaje kwenye maamuzi na uendeshaji wa mfuko huo na kwa faida ya
nani. Sasa ni juu ya mfanyakazi mwenyewe kuchagua kwa kutumia vigezo vya
kitaalamu
No comments :
Post a Comment