na christian gaya -majira
kwa mujibu wa kifungu
cha 30 cha Sheria ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii na
sheria za mifuko kama zilivyorekebishwa, mfanyakazi ambaye hajawahi kujiunga na
mfuko wowote wa pensheni au anayeajiriwa kwa mara ya kwanza anao uhuru wa
kuchagua mfuko wowote kati ya mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii. Hii ina
maana mfanyakazi anapaswa kuwa mwanachama wa mfuko mmoja tu wa pensheni.
Kifungu hicho kinaendelea kusisitiza ya kuwa ni makosa makubwa kwa mfanyakazi
mpya kujiunga au kujiandikisha kwenye mifuko zaidi ya mmoja wa pensheni.
Hiki ni kitu kizuri ili
kuleta ushindani zaidi kwa mifuko ya
pensheni ya hifadhi ya jamii nchini na kuleta uwiano wa wanachama. Na huenda
hii inaweza kusaidia changamoto ya kuongezea idadi kubwa ya wanachama kwenye
mifuko hii ya hifadhi ya jamii hasa kutoka katika sekta isiyokuwa rasmi ambayo kwa muda mrefu imesahaulika na badala
ya kuegamia sheria zilizoanzisha mifuko hii ya pensheni. Kwa sababu mpaka
inakisiwa kuwa idadi ya watanzania wote inakisiwa kuwa
ni milioni 45.
Je mfuko wa pensheni una mpango wa
kutoa angalau theluthi mbili ya mafao ya pensheni ya mwanachama kama amana ya
kupatiwa mkopo wa nyumba?
Kati ya hawa asilimia 70 wako maeneo ya vijijini. Na idadi ya nguvu kazi
ya watanzania inakisiwa kuwa ni milioni 16 ambapo asilimia 5.4 ya nguvu kazi au
asilimia 2.7 ya idadi yote ya watanzania ndiyo iliyojiunga na mfumo kamili wa
lazima wa hifadhi ya jamii. Na asilimia 93 ya nguvu kazi yaani ya watu
wanaojiweza kufanya kazi imejikita kufanya kazi kwenye sekta isiyo kuwa rasmi
kwa sehemu zote za mijini na vijijini. Na asilimia 80 ya hao ambao wamo kwenye
sekta isiyo rasmi wanashughulika na kilimo
Inayokisiwa kuwa ni milioni 1.0 hii ni asilimia 5.4%
ya nguvu kazi yote ambayo ni kama milioni 16 ya Watanzania wote. Hii ina maana
yakuwa karibu milioni 15 ya nguvu kazi inashughulika na sekta isiyo rasmi na
wote wako katika hali hatarishi kwa vile hawana kinga yeyote ya hifadhi ya
jamii
Hifadhi ya jamii ina maana ni aina ya hatua
madhubuti au shughuli zilizobuniwa za kuhakikisha kuwa wananchi wa jamii hiyo wanapata
mahitaji yao ya lazima na ya msingi na
wanapewa kinga ya hifadhi ya kutokana na majanga ili kuwawezesha kuwa na
kiwango cha maisha ya kuishi kulingana na mila na desturi za jamii
Na lengo kubwa la
hifadhi ya jamii ni kuzuia umasikini, kupunguza au kuondoa umasikini, kuifidia
jamii, kugawanya mapato sawasawa kwa wanajamii. Masuala mengi yanayogusa
hifadhi ya jamii ni ya nyeti sana, yanagusa ni kiini muhimu sana cha
wafanyakazi kwenye sekta rasmi na sekta zisizo rasmi hasa za watu masikini
pamoja na sekta ya bima za jumuiya za waajiri
Mfumo wa hifadhi ya jamii ambayo ni ya lazima
kisheria ambayo wafanyakazi pamoja na mwajiri wanachangia pamoja na kupeleka
michango kwenye chombo cha mfuko wa pensheni (pension fund) au mfuko wa akiba
ya wafanyakazi (provident fund).
Taasisi za hifadhi ya
jamii ya jamii nchini Tanzania zimekuwa zikiwekeza orodha ya fedha kwa faida
kwenye mikopo, nyumba za kupangisha, hatifunganishi, kuweka akiba benki zote
hizi zimechangia maendeleo.
Kumekuweko na ongezeko dogo sana la kuelewa juu ya
mfumo wa hifadhi ya jamii hasa juu ya mafao yanayotolewa, jinsi ya kujiunga
kuwa wanachama, vitega uchumi na shughuli mbalimbali za sekta. Mapungufu yaliyomo kwenye mfumo huu wa
hifadhi ya jamii ambayo yanahitajika kutatuliwa na sera hii ya hifadhi ya
jamii. Watu waliomo katika mifuko hii ya hifadhi ya jamii ni wale tu
ambao wameajiriwa kwenye sekta iliyo rasmi
Hivyo kama mfanyakazi utahitaji kujifunza ili kujua na kuzingatia mambo muhimu kabla ya kufanya maamuzi ya kujisajili na mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii wowote ule. Najua kila mmoja wetu anaweza kuwa na lengo lake la kutaka kujiunga na mifuko hii ya pensheni. Na wawekezaji wengi mara nyingi hutumia vigezo vya takwimu au vigezo vya kifedha, na vigezo vingine au taarifa nyinginezo mbali na fedha. Hivyo kuna vigezo muhimu hata kama utasikia habari au ripoti kwenye runinga, magazeti, rafiki, redio n.k. kutoka sehemu tofauti kuhusu uzuri wa mfuko fulani wa pensheni ya hifadhi ya jamii hakikisha kwanza unaupima kwanza kwa vigezo vyako.
No comments :
Post a Comment