Ujenzi wa daraja la Kigamboni sasa kuanza mwakani
9th November 2011
B-pepe
Chapa
Maoni
Hatimaye
ujenzi wa daraja la Kigamboni lililokuwa likisubiriwa na wakazi wengi
wa jiji la Dar es Salaam, unatarajia kuanza mapema mwakani.
Daraja hilo linatarajia kujengwa eneo la
Kurasini ambapo litaunganisha mji wa Kigamboni na sehemu zingine za jiji
la Dar es Salaam.
Akizungumza katika maonyesho ya wiki
Mashirika ya Hifadhi za Jamii, yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi
Mmoja, Ofisa Mkuu wa miradi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), John
Ndazi, alisema tenda zilizotangazwa kwa ajili ya kupata kampuni
itakayojenga daraja hilo zitafunguliwa mwezi ujao.
Ndazi alisema baada ya kupata kampuni
moja, kazi ya ujenzi itaanza mapema mwaka ujao ambao utagharimu dola za
Marekani milioni 130. Alisema serikali itatoa asilimia 40 ya fedha hizo
na NSSF itatoa asilimia 60 na kwamba baada ya ujenzi wake kukamilika,
magari yatakayokuwa yanapita katika daraja hilo yatakuwa yanalipia.
“Magari yote yatakuwa yanalipia wakati
yanapita katika daraja hilo kwa kipindi cha miaka 25 na baada ya hapo
daraja litakuwa mali ya serikali,” alisema. Daraja hilo ni miongoni mwa
miradi mikubwa ya NSSF ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na wananchi
wengi lakini kwa bahati mbaya uanzishwaji wake umekuwa kitendawili.
Aidha, NSSF imesema inatarajia kujenga nyumba 18,000 za bei nafuu ambazo itaziuza kwa wanachama wake.
Maonyesho hayo ya wiki ya mifuko ya
hifadhi yalifunguliwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Kazi na
Ajira, Gaudentia Kabaka na kuhudhuriwa na wananchi mbalimbali.
CHANZO:
NIPASHE
No comments :
Post a Comment