Friday, September 1, 2017

DKT. SHEIN AHUTUBIA BARAZA LA EID ADH'HA HUKO FUMBA MJINI UNGUJA


DSC_4141
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (kushoto)alipokuwa akipungia mkono Viongozi mbali mbali kama ishara ya kuwaaga baada ya kumalizika kwa  sherehe za Baraza la Eid El Hajj lililofanyika leo  katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi,[Picha na Ikulu.] 01/09/2017.

DSC_3747
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala  Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman alipowasili katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi katika sherehe za Baraza la  Eid el Hajj lililofanyika leo,[Picha na Ikulu.] 01/09/2017.
DSC_3806
Wananchi na Viongozi wakiwa katika ukumbi wa mkutano  wa Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi katika sherehe za Baraza la  Eid el Hajj lililofanyika leo,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)[Picha na Ikulu.] 01/09/2017.
DSC_3872
DSC_3889
Baadhi ya Akinamama waliohudhuria katika sherehe za Baraza la  Eid el Hajj lililofanyika leo,katika ukumbi wa mkutano  wa Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 01/09/2017.
DSC_3898
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (kushoto) akiwa na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa katika sherehe za Baraza la  Eid el Hajj lililofanyika leo katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)[Picha na Ikulu.] 01/09/2017.
DSC_3903
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Viongozi wengine wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake leo katika sherehe za Baraza la Eid EL Hajj lililofanyika katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi,[Picha na Ikulu.] 01/09/2017.
DSC_3904
Baadhi ya Wake wa  Viongozi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake leo katika sherehe za Baraza la Eid EL Hajj lililofanyika katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi,[Picha na Ikulu.] 01/09/2017.
DSC_3940
Baadhi ya Akinamama waliohudhuria katika sherehe za Baraza la Eid el Hajj  wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake leo katika sherehe hizo zilizofanyika  katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi,[Picha na Ikulu.] 01/09/2017.
DSC_3973
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akipokea salamu ya heshma kwa kikosi cha pilisi cha FFU mara alipowasili katika sherehe za Baraza la  Eid el Hajj lililofanyika leo katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi,[Picha na Ikulu.]01/09/2017.
DSC_4019
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (kushoto)alipokuwa akisalimiana na Wananchi na Viongozi mbali mbali baada ya kutoa hutuba yake  katika sherehe za Baraza la Eid El Hajj lililofanyika leo  katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi,[Picha na Ikulu.] 01/09/2017.
DSC_4057
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (kushoto)alipokuwa akisalimiana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Viongozi mbali mbali baada ya kutoa hutuba yake  katika sherehe za Baraza la Eid El Hajj lililofanyika leo  katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi,[Picha na Ikulu.] 01/09/2017.

JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA LAADHIMISHA MIAKA 53 TOKA KUANZISHWA KWAKE


8
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya  Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha na Jenerali wa kwanza Mzalendo kuliongoza Jeshi hilo Jenerali Mstaafu Mirisho Sarakikya wa kwanza kushoto  pamoja na Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange mara baada ya kuzungumza kuhusu kuhusu miaka 53 tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo la Wananchi katika Makao makuu ya Jeshi hilo Ngome jijini Dar es Salaam.

3
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya  Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akizungumzia  maadhimisho ya miaka 53 tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo la Wananchi katika Makao makuu ya Jeshi hilo Ngome jijini Dar es Salaam.
9
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya  Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha na Jenerali wa kwanza Mzalendo kuliongoza Jeshi hilo Jenerali Mstaafu Mirisho Sarakikya wanne kutoka kushoto Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wanne kutoka kulia Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Mwakibolwa watatu kutoka kushoto mstari wa mbele pamoja na Wakuu wa Kamandi na machifu wa Makao makuu ya Jeshi hilo.(PICHA NA MPIGA PICHA WETU)

SERIKALI YAONGEZA MUDA WA UHAKIKI WA NGO’s



Msajili wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Bw. Marcel Katemba akitoa ufafanuzi wa kazi ya uhakiki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuhimiza wadau kuitikia zoezi hilo katika muda uliowekwa na Serikali alipokutana na waandishi wa habari leo Septemba 1, 2017 katika ukumbi wa Mikutano ya Wizara UDOM, Dodoma.


NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WAMJW
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambayo inajukumu la kusajili, kuratibu na kufuatilia uendeshaji wa shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini imeamua kuongeza muda wa siku 16 kwa Mashirika ambayo bado hayajahakiki  taarifa zake kwa Msajili wa Mashirikka yasiyo ya Kiserikali kukamilisha uhakiki huo.
Akizingumza na waandishi wa Habari Mjini Dodoma leo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga amesema kuwa kumekuwa na mwitikio mkubwa wa Mashirika yasiyo ya kiserikali kuja kuandikisha taarifa za asasi zao katika vituo mbalimbali vya usajili vya kanda.
Bibi Sihaba ameongeza kuwa Serikali ina nia njema ya na siyo mbaya kama watu wanavyohisi katika utekelezaji wa zoezi hili la uhakiki linaloendelea nchi nzima katika vituo vya Kanda tano (5), na lengo ni la zoezi ni kutambua takwimu halisi ya Mashirika yanayofanya kazi ili kuweka utaratibu mzuri wa kutambua mchango wa kila asasi katika kuhudumia jamii katika nyanja mbalimbali.
“Niwaombee wadau wetu watumie muda huu tuliouongeza vizuri kwa kujitokeza kwa wingi kufanya uhakiki wa Mashirika yao na wale wenye changamoto tutawaelekeza namna bora ya kuzitatua”alisema Bibi Sihaba.
Aidha Msajili wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Bw. Marcel Katemba amewahikikishia wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini kuwa hakuna tatizo katika zoezi la uhakiki wao na ni muhimu sana kujihakiki ili kujiwekea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao kwa uhuru na uwazi.
“ Niwahakikishie wadau wetu kuwa zoezi hili ni muhimu sana kwenu na kwetu pia katika namna ya kuboresha utendaji kazi wetu”alisema Bw. Katemba.
Naye Katibu wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini Bw. Ismail Suleiman ameishukuru Serikali kuwa kuandaa na kuratibu zoezi la uhakiki wa mashirika hayo na kuwaomba wamiliki wa mashirka yasiyo ya kiserikali nchini kujitokeza kuhakiki mashirika yao.
“Niwaombe wamiliki wa Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini tuendelee kujitokeza kwa wingi tuje tuhakiki mashirika yetu ili tuondokane na usumbufu mara baada ya kumalizika kwa kuda wa uhakiki ulioongezwa”alisema Bw. Ismail.
Zoezi la uhakiki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini lilizinduliwa na katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Agosti 21,2017 na uhakiki huo ulitekelezwa kwa muda wa wili mbili mpaka Septemba 04,2017.
Hata hivyo kutokana na sababu za kijiografia na mwitikio mkubwa wa mashirika kutaka kuhakikiwa ikaamuliwa kuongeza kwa muda wa siku 16 mpaka Septemba 20 mwaka huu, ambao ndio utakuwa mwisho wa uhakiki.

Katibu wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NACoNGO’s) Bw. Ismail Suleiman akieleza kuridhishwa kwake na nafasi ya ushiriki wa NGOs katika uendeshaji wa zoezi la kuhakiki mashirika hayo linaloendelea kote nchini.



Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga wakati akitoa tamko la kuongeza muda wa uhakiki wa asasi hizo.


Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga wakati akitoa tamko la kuongeza muda wa uhakiki wa asasi hizo.



Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali muda mfupi baada ya kutoa tamko la kuongeza muda wa uhakiki wa NGOs kutoka tarehe 4/9- 20/9/2017.(PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WAMJW)

BREAKING NEWS:ODINGA AMBWAGA KENYATTA KORTINI; MAHAKAMA KUU HYA KENYA YAAMURU UCHAGUZI MKUU WA KENYA URUDIWE BAADA YA SIKU 60



NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari
MAHAKAMA Kuu nchini Kenya, imetengua ushindi wa Rais wa sasa Uhuru Kenyatta, dhidi ya hasimu wake mkuu Raila Odinga, urudiwe ndani ya siku 60 kuanzia leo Septemba 1, 2017.
Mahakama Kuu ya Kenya, imefikia uamuzi huo leo Septemba 1, 2017, kufiuatia maombi ya Mgombea wa Muungano wa upinzani NASA, chini ya mgombea wake, Bw. Raila Odinga, ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais uliofanyika Agosti 8, 2017 na kumpa ushindi Rais Kenyatta.
Katika maombi yake, Bw. Odinga alisema, kura zake zilipunguzwa kwenye baadhi ya vituo na kuongezewa kwa mpinzani wake, lakini kubwa zaidi ni kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi ambapo baadhi ya fomu muhimu za matokeo ya uchaguzi kama vile fomu namba 34A,B na C, hazikupatikana siku ya kutangazwa kwa matoko.
Katika uamuzi wa mahakama hiyo, majaji wanne kati ya sita (6), wamekubaliana kuwa tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya, (IEBC), imeshindwa kusimamia vema uchaguzi huo na hivyo kusababisha kasoro kadhaa ambazo zinakwenda kinyume na katiba ya Kenya. Hata hivyo, Mahakama hiyo imesema, hakuna ushahidi wowote, ulioonyesha kuwa Rais Uhuru Kenyatta, alitenda makosa katika mchakato huo wa uchaguzi.

SALA YA EID AL ADH'HA: MUFTI WA TANZANIA AWAASA WASILAMU KUITUNZA AMANI KWANI NI KAMA YAI


SHEIKH Mkuu wa Tanzania, Mjufti Abubakary Bin Zubeiry, amewaasa Waislamu nchini kuitunza amani kwani ni kama yai.
"Unajua yai lilivyo, ukilichezea likakuponyoka na kudondoka chini, huwezi tena kulikusanya na kulitumia, hivyo niwajibu wetu sisi Waislamu na wananchi kwa ujumla kuitunza amani tuliyo nayo na huu ndio ujumbe wangu muhimu kwa leo hii." Alifafanua Mufti Zubeiry baada ya ibada ya sala ya Eid Al Edh'ha na Baraza la Eid lililofanyika Masjid (Msikiti) wa Taqwa, ulioko Ilala Bungoni jijini Dar es Salaam leo asubuhi Septemba 1, 2017.
Mufti Zubeiry amesema, Mwenyezimungu aliwaambia waliofarakana kuwa hawawezi kuingia peponi mpaka wakapatane kwanza, na kwa hakika tunawaomba watu wote waliohitilafiana, wenye chuki, wenye vinyongo, wenye vifundo, waondoshe na leo ndio siku ya kukaa pamoja na kula pamoja, katika sikukuu hii ya Eid al hadh'ha, alisema Mufti.

SERIKALI YAWAONGEZEA MUDA WAAJIRI KUJISAJILI KATIKA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, WCF

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw. Masha Mshomba

BANDARI KAVU YA KWALA –VIGWAZA KUANZA KUTUMIKA JANUARI MWAKANI.


Waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasilino, Profesa Makame Mbarawa mwenye kofia ya njano akiwa katika majukumu ya ukaguzi wa ujenzi wa bandari kavu ya Kwala-Vigwaza inayojengwa mkoani Pwani.


Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya bandari Tanzania (TPA) Eng. Deusdedit Kakoko akifafanua jambo kwa waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasilino, Profesa Makame Mbarawa alipokagua maendeleo ya ujenzi wa bandari kavu ya Kwala –Vigwaza mkoani Pwani.


NA WUUM, PWANI
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa bandari kavu katika eneo la Kwala Vigwaza Mkoani Pwani na kumtaka mkandarasi Suma JKT kuongeza kasi na kuzingatia ubora.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo ameiagiza Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRL) na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuhakikisha wanaunganisha kwa haraka ili reli na barabara zinazoingia katika bandari kavu hiyo zinakamilika na hivyo kuiwezesha bandari kavu hiyo kuanza kutumika ifikapo Januari mwakani.
“TPA, TRL na TANROADS uzuri wote mko kwenye wizara moja shirikianeni na hakikisheni kilomita 15 za barabara inayoingia kwenye bandari kavu hii na kilomita moja ya reli zinajengwa haraka,” Amesema Profesa Mbarawa.
Profesa Mbarawa amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Deusdedit Kakoko kuhakikisha ujenzi wa bandari kavu ya Kwala-Vigwaza unazingatia ubora na viwango vilivyopo katika mkataba ili kuiwezesha kuhudumia zaidi ya makontena milioni moja kwa mwaka na hivyo kupunguza msongamano katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
“Hakikisheni eneo la bandari kavu linakuwa na maegesho ya kutosha, taa, maji ya uhakika, gari la zimamoto, uzio na mashine ya ukaguzi wa mizigo scanner itakayowezesha kupima kila mzigo unaopandishwa na kushushwa katika eneo hili,” amesisitiza Profesa Mbarawa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Kakoko amesema TPA imejipanga kuhakikisha ujenzi huo unatumia gharama nafuu na mifumo yote ya teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA inakuwepo katika bandari hiyo ili kuiwezesaha kufanya kazi kisasa na kwa ufanisi zaidi.
“Tukifanikiwa kuhamia hapa mzigo uliokuwa unasafirishwa kwa siku saba sasa utatumia siku tatu kufika Mwanza hali itakayovutia wasafirishaji wengi kutumia bandari ya Dar es Salaam na hivyo kukuza uchumi wa nchi na kuibua fursa za ajira,” amesema Eng. Kakoko.
Bandari Kavu ya Kwala –Vigwaza inayojengwa na Mkandarasi SUMA JKT ambapo takribani kiasi cha shilingi bilioni 9 kinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo ili kuboresha huduma za usafirishaji katika bandari ya Dar es Saalaam ambapo zaidi ya hekta 500 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi huo ambapo kwa kuanza hekta 120 sawa asilimia 24 zinajengwa katika awamu ya kwanza.




Waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasilino, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akitoa maelekezo kwa Eng. Charles Salu Ogare anayesimamia ujenzi wa bandari kavu ya Kwala-Vigwaza  mkoani Pwani.