Msajili wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Bw. Marcel
Katemba akitoa
ufafanuzi wa kazi ya uhakiki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuhimiza wadau kuitikia
zoezi hilo katika muda uliowekwa na Serikali alipokutana na waandishi wa
habari leo Septemba 1, 2017 katika ukumbi wa Mikutano ya Wizara UDOM, Dodoma.
NA KITENGO
CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WAMJW
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto ambayo inajukumu la kusajili, kuratibu na kufuatilia uendeshaji wa shughuli za Mashirika Yasiyo
ya Kiserikali nchini imeamua kuongeza muda wa siku 16 kwa
Mashirika ambayo bado hayajahakiki taarifa zake kwa Msajili wa Mashirikka
yasiyo ya Kiserikali kukamilisha uhakiki huo.
Akizingumza na waandishi wa Habari Mjini Dodoma leo
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia
Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga amesema kuwa kumekuwa na mwitikio mkubwa
wa Mashirika yasiyo ya kiserikali kuja kuandikisha taarifa za asasi zao katika
vituo mbalimbali vya usajili vya kanda.
Bibi Sihaba ameongeza kuwa Serikali ina nia njema ya
na siyo mbaya kama watu wanavyohisi katika utekelezaji wa zoezi hili la uhakiki
linaloendelea nchi nzima katika vituo vya Kanda tano (5), na lengo ni la zoezi
ni kutambua takwimu halisi ya Mashirika yanayofanya kazi ili kuweka utaratibu
mzuri wa kutambua mchango wa kila asasi katika kuhudumia jamii katika nyanja
mbalimbali.
“Niwaombee wadau wetu watumie muda huu tuliouongeza
vizuri kwa kujitokeza kwa wingi kufanya uhakiki wa Mashirika yao na wale wenye
changamoto tutawaelekeza namna bora ya kuzitatua”alisema Bibi Sihaba.
Aidha Msajili wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Bw.
Marcel Katemba amewahikikishia wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini
kuwa hakuna tatizo katika zoezi la uhakiki wao na ni muhimu sana kujihakiki ili
kujiwekea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao kwa uhuru na uwazi.
“ Niwahakikishie wadau wetu kuwa zoezi hili ni muhimu
sana kwenu na kwetu pia katika namna ya kuboresha utendaji kazi wetu”alisema
Bw. Katemba.
Naye Katibu wa Baraza la Mashirika yasiyo ya
Kiserikali nchini Bw. Ismail Suleiman ameishukuru Serikali kuwa kuandaa na
kuratibu zoezi la uhakiki wa mashirika hayo na kuwaomba wamiliki wa mashirka
yasiyo ya kiserikali nchini kujitokeza kuhakiki mashirika yao.
“Niwaombe wamiliki wa Mashirika yasiyo ya kiserikali
nchini tuendelee kujitokeza kwa wingi tuje tuhakiki mashirika yetu ili
tuondokane na usumbufu mara baada ya kumalizika kwa kuda wa uhakiki
ulioongezwa”alisema Bw. Ismail.
Zoezi la uhakiki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
nchini lilizinduliwa na katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Agosti 21,2017 na uhakiki huo ulitekelezwa kwa muda wa wili
mbili mpaka Septemba 04,2017.
Hata hivyo kutokana na sababu za kijiografia na
mwitikio mkubwa wa mashirika kutaka kuhakikiwa ikaamuliwa kuongeza kwa muda wa
siku 16 mpaka Septemba 20 mwaka huu, ambao ndio utakuwa mwisho wa uhakiki.
Katibu wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali
(NACoNGO’s) Bw. Ismail Suleiman akieleza kuridhishwa kwake na nafasi ya
ushiriki wa NGOs katika uendeshaji wa zoezi la kuhakiki mashirika hayo
linaloendelea kote nchini.
Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii
Bibi Sihaba Nkinga wakati akitoa tamko la kuongeza muda wa uhakiki wa asasi
hizo.
Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii
Bibi Sihaba Nkinga wakati akitoa tamko la kuongeza muda wa uhakiki wa asasi
hizo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga
akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali muda
mfupi baada ya kutoa tamko la kuongeza muda wa uhakiki wa NGOs kutoka tarehe
4/9- 20/9/2017.(PICHA NA KITENGO CHA
MAWASILIANO SERIKALINI, WAMJW)
No comments :
Post a Comment