NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Kwa kiasi kikubwa Wajasirimali wadogowadogo nchini wamekuwa hawajajiunga na Mifuko ya Uhifadhi wa Jamii kutokana na uelewa mdogo wa mifuko hiyo na kupelekea kutopata unafuu pale anaposhindwa kufanya kazi yake.
Ameyasema hayo Dkt.Godbertha Kinyondo kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe wakati akieleza matokeo ya Utafiti wa sekta zisizo rasmi na hifadhi ya jamii ambapo amesema kuna umuhimu mkubwa wajasiriamali wadogo kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii yenye manufaa kwao hapo baadae.
Amesema Utafiti unaohusu wajasiriamali wadogowadogo na Uhifadhi wa Jamii waliianza mwaka 2017 na kilichowasukuma kufanya utafiti huo ilikuwa kuona jinsi wajasiriamali wadogowadogo wanaweza kujikimu katika uhifadhi wa jamii.
Aidha amesema katika utafiti huo wameenda katika mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma na sasa wamepata majibu ya tafiti ambayo wameyapata mwaka 2021 na wameandika kitabu ambacho kipo kwenye tovuti pamoja na machapisho.
"Mpaka sasa bodaboda wameshaanza kuwa na uelewa kuhusu hifadhi ya jamii kwani wameshaanza kutafuta mikopo na wamekuwa wakikopesheka na hata wengine kuingia kwenye vikundi ambavyo vinawasaidia katika kujikimu kimaisha kupitia shughuli zao". Amesema
Kwa upande wake Afisa Biashara wa Jijini la Dar es Salaam Bw.Nikasi Msemwa amesema utafiti huo ni muhimu sana kwani unaenda kutoa majibu mengi na makubwa katika jamii yetu, utafiti huo umejikita katika kuangalia kesho ya wajasiriamali pamoja na wale wenye kipatacho cha chini.
Amesema Pensheni itakuwa ni msaada wao wanapokuwa wamezeeka lakini Bima ya Afya itaenda kutoka majibu kwa wao wenyewe wajasiriamali lakini pia kwa familia zao.
"kwa kuwa tafiti hii ndo imetangazwa itakuwa imesambaa kwa watu wote kwahiyo zile taasisi ambazo ni wadau wataangalia fursa kwenye hii tafiti kwasababu kuna baadhi ya vitu, mfano hizi taasisi za kifedha zipo tayari kufanya jambo lolote lile lakini kama kuna tafiti kama huu uko tayari kuna uhakika taasisi mbalimbali kuingia". Amesema
Afisa Habari Msaidizi wa Shirikisho la Vyama vya Waendesha Pikipiki (bodaboda na bajaji) Mkoa wa Dar es salaam, Bw.Saidi Msisiri amesema bodaboda wengi hawafahamuu nini maana ya hifadhi ya jamii, lakini kupitia Chuo cha Mzumbe, kwa kiasi kikubwa bodaboda wameanza kuwa na uelewa mpana juu ya kujiweka hifadhi ya maisha yao.
"Bodaboda wote wameitikia wito na wako tayari kuanza sasa kuhifadhi, kutunza fedha zao lakini pia kujiwekea bima ya maisha yao, na kazi yote hii imefanywa na Chuo Kikuu cha Mzumbe". Amesema
Amesema kuwa baada ya mkutano huo wanatarajia vijana hao wa bodaboda watajiunga katika mifuko ya hifadhi ya jamii, watakata bima za afya pamoja na bima za vyombo vyao vya moto.
No comments :
Post a Comment