Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Waziri Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 20,2022 katika Ofisi za RITA Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV)
Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
WAZIRI wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi kutoka baadhi ya taasisi ambazo ziko chini ya Wizara hiyo kwa ajili ya kujadili namna ya kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Tathmini ya wanafunzi wa Law School kundi la 33.
Mazungumzo hayi yamefanyika leo Desemba 20, 2022 jijini Dares Salaam kimehudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatibu Kazungu, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Profesa Elisante Ole Gabriel.
Mambo kadhaa yamejadiliwa kwenye mazungumzo hayo yakiwemo yaliyotajwa katika ripoti ya Kamati hiyo Maalum iliyoundwa kufanya tathmini ya wanafunzi wa Law School kundi la 33.
Miongoni mwa yaliyojadiliwa a kuazimiwa kutekelezwa ni pamoja na kuwa na Mahakama ya kufundishia, kujenga mgahawa na mabweni kwa ajili ya wanafunzi, kurekebisha baadhi ya kanuni hasa zinazohusu ukataji wa rufaa kwenye matokeo, kuimarisha mifumo ya TEHAMA yaLaw School na kuangaliwa upya kwa Baraza la Elimu a Sheria kulinganisha na matakwa ya Law School.
Taarifa kuhusu kikao hicho inaeleza kwamba baada ya kufanyika kwa majadiliano viongozi wakiongozwa na Dk.Ndumbaro wamekubaliana kutekeleza mapendekezo hayo kila mmoja kwenye eneo lake ili kuondoa malalamiko ya kufeli kwa wanafunzi hao.
Mkutano ukiendelea.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV)
No comments :
Post a Comment