Wednesday, December 21, 2022

RAMAPHOSA ACHAGULIWA TENA KUONGOZA CHAMA CHA ANC

Na Mwandishi Wetu


Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa tena kuwa Kiongozi wa Chama Tawala cha ANC kwa shangwe baada ya kupata kura nyingi zaidi ya mpinzani wake, Zweli Mkhize katika Uchaguzi wa Chama hicho uliofanyika mapema wiki hii, mjini Johannesburg nchini humo.

Rais Cyril Ramaphosa ambaye anakabiliwa na kashfa ya ubadhirifu wa fedha alipata Kura 2,476 dhidi ya Kura 1,897 za mpinzani wake, Mkhize. Ramaphosa anakabiliwa na tuhuma hizo za ufujaji wa fedha wakati Mkhize anakabiliwa na tuhuma za ufisadi, wote wamekana tuhuma hizo zinazowakabili.

Ushindi huo umemuweka Ramaphosa katika nafasi nzuri ya kuongoza Chama hicho cha ANC katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika mwaka 2024 na huenda akatetea nafasi hiyo ya Urais. Ramaphosa anaendelea kuchunguzwa na Mamlaka za Uchunguzi nchini Afrika kwa tuhuma hizo za madai ya ufujaji wa fedha $580,000 (£475,000) kwenye Makochi katika Shamba lake na kisha kuficha wizi wake.

Hata hivyo, Jopo la Wataalamu wa Sheria walioteuliwa na Spika wa Bunge la Afrika Kusini limesema kuwa Ramaphosa ana kesi ya kujibu kwani huenda wote wawili wamekiuka Katiba na kuvunja Sheria ya kupambana na Rushwa.

Wafuasi wake walishangilia ushindi huo wa Ramaphosa, baada ya kutangazwa mshindi katika matokeo yaliyomfanya ashinde kwa tofauti kubwa ya Kura dhidi ya Mpinzani wake, ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipowania Uongozi wa Chama hicho cha (African National Congress) mnamo mwaka 2017.

ANC ilitumia wingi wa Wabunge wake kupiga Kura za maoni, na hali hiyo ilimfanya Ramaphosa kushinda tena katika Uchaguzi huo, huku akikana kufanya makosa na ameanzisha hatua za Kisheria kubatilisha ripoti ya Jopo hilo.

Amesema kiasi cha Dola hizo za Marekani 580,000 zilitokana na mauzo ya Nyati, lakini jopo hilo lilisema kulikuwa na "Mashtaka Makubwa" kama shughuli hiyo ilifanyika. Mkhize alikuwa Waziri wa Afya katika Serikali ya Ramaphosa hadi alipolazimika kujiuzulu mwaka jana kwa madai ya matumizi mabaya ya fedha zilizotengwa kukabiliana na janga la COVID-19.

Mkhize pia amekana kufanya makosa yoyote, na Wafuasi wake waliona madai hayo kama jaribio la kumchafua ili asishinde Uchaguzi huo. Hata hivyo, Ramaphosa ndiye aliyepewa nafasi kubwa ya kushinda, huku baadhi ya Wafuasi wa Mkhize walionekana kushangazwa na matokeo hayo ya ushindi wa Ramaphosa.

Walikuwa na uhakika wa ushindi baada ya kutoa nyadhifa muhimu kwa viongozi wengine wenye nguvu katika mikataba iliyofikiwa kabla ya wajumbe kupiga kura zao kwenye mkutano huo.

Pande zote mbili zilikanusha tuhuma za ununuzi wa kura.

No comments :

Post a Comment