Saturday, April 9, 2022

Wakulima wapewa somo kuzalisha kwa tija

wakulimapiic

By Mwandishi Wetu

Wakulima nchini wametakiwa kufuata maelekezo ya wataalamu kwa usahihi wakati wa matumizi ya viuatilifu ili kuongeza tija kwenye uzalishaji.

Hatua hiyo imetokana na kile kilichoelezwa kwamba, baadhi ya wakulima wamekuwa wakienda kinyume na maelekezo ya wataalamu wakati wa matumizi ya pembejeo hizo hivyo, kusababisha kutoonekana kwa tija huku wenyewe wakiishia kulalamika.

Hayo yameelezwa jana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mo Green International, Matolo Felician wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa viatilifu vipya ikiwemo cha Mo Strong kwa ajili ya kukabiliana na wadudu waharibifu hasa kwenye zao la pamba.

Amesema licha ya wakulima kupewa maelekezo sahihi na wataalamu, lakini wengi hawafuati kama ushauri huo kikamilifu hivyo, vita ya kuwaangamiza wadudu kuwa ngumu.

Felician amesema matumizi ya viatilifu katika kukabiliana na wadudu waharibifu yamekuwa na msaada mkubwa katika jitihada za kuongeza tija kwenye kilimo nchini.

“Matumizi ya viuatilifu ikiwemo Mo Strong yameleta mapinduzi makubwa kwenye kilimo nchini. Udhibiti wa wadudu waharibufu umekuwa mkubwa tofauti na miaka ya nyuma.

ADVERTISEMENT

Lakini, bado kuna changamoto kidogo kwa baadhi ya wakulima kutofuata maelekezo sahihi ya wataalamu wa kilimo kwenye matumizi licha ya elimu kutolewa.

“Niwahakikishe kuwa hii Mo Strong imekuwa mkombozi mkubwa kwa wakulima wa pamba na mazao mengine kwa kuwa hata gharama yake ni rafiki kwa wakulima wengi,” alisema Felician.

Akizungumzia kuhusu mikakati ya kilimo nchini, Felician amesema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita kufanya mapinduzi makubwa ya kilimo, imeonyesha kuwa na tija na inaungwa mkono na wadau wengi.


Amesema wadau wa kilimo nchini wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha changamoto za mkulima zinapatiwa ufumbuzi ikiwemo upatikanaji wa viuatilifu ambavyo vimesaidia kuongeza tija.

No comments :

Post a Comment