Saturday, April 9, 2022

Siku tatu zilivyotumika kumhoji Mkapa kitabu cha Nyerere

kitabu pic

Rais Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua Vitabu 3 vya Hayati Mwalimu Nyerere katika Mdahalo wa Kumbukizi ya miaka 100 iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Uongozi Kibaha mkoani Pwani leo Jumapili Aprili 09, 2022. Picha na Ikulu

By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Mwanazuoni maarufu, Profesa Issa Shivji, ameeleza namna

walivyochukua siku tatu kumuhoji Rais wa awamu ya tatu Hayati Benjamin Mkapa, kwa ajili ya kuandika kitabu kuhusu wasifu wa Mwalimu Nyerere.
Profesa Shivji ameyasema hayo leo Jumamosi Aprili 9, 2022 alipokuwa anaeleza kuhusu kitabu hicho kwenye mdahalo wa kitaifa kuadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwake,unaofanyika katika shule ya  Uongozi Kibaha Mkoani Pwani.

SOMA: Rais Samia aonya udini, ukabila
Profesa Shivji amesema katika uandaaji wa kitabu hicho waliwahoji viongozi mbalimbali wakiwemo waliowahi kufanya kazi na Mwalimu Nyerere, akiwemo Hayati Benjamin Mkapa ambaye walimuhoji kwa siku tatu.
“Nichukue nafasi hii kuwashukuru viongozi waliotenga muda wa wa kutukubalia kuwahoji akiwemo Hayati Benjamin Mkapa ambaye tulimuhoji kwa siku tatu na kila siku tulitumia zaidi ya saa mbili kumuhoji,” amesema Profesa Shivji.
Viongozi wengine wa ngazi ya juu waliowahoji, aliwataja kuwa ni Rais Mstaafu awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, waliowahi kushika cha Waziri Mkuu kwa nyakati tofauti akiwemo Cleopa David Msuya, Salim Ahmed Salim Joseph, Warioba na Samuel Malecela.
Wengine ni pamoja na aliyewahi kuwa Spika wa Bunge, Pius Msekwa, Hashim Mbita, Job Lusinde, Hayati Seif Sharif  Hamad na Joseph Butiku.
Pia Profesa Shivji alitumia nafasi hiyo kumshukuru Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abraham Kinana kwa kutoa kibali cha kuwawezesha kufanya utafiti wao katika ofisi za Dodoma wakati huo akiwa Katibu Mkuu wa chama na pia kumuhoji.
Hata hivyo, mwanazuoni huo alimwambia Kinana kuwa kwa kuwa amerudi katika uongozi ndani ya CCM ni vema akajenga makazi TANU na CCM katika ofisi hiyo kwa kuwa ni muhimu ambapo yataweza kutumika na watafiti mbalimbali katika taifiti zao.
“Kwani katika utafiti wetu tuliposoma yale mafaili kwa mara ya kwanza tulijua chama cha TANU na   baadaye CCM, tuligundua vilikuwa vikiendeshwa kwa demokrasia kubwa sana na tuliweza kusoma hata hoja zilizotolewa na nyingine zikimpinga hata mwalimu.
“Tulikuta utamaduni mmojawapo wa chama alioujenga Mwalimu wa kuwa na vikao katika ngazi zote za chama,” alisema.

No comments :

Post a Comment