Katika kumuenzi marehemu, Benno Ndulu, baadhi ya viongozi wa benki kuu za Afrika
walikusanyika katika kikao kilichoendeshwa mtandaoni siku ya Jumanne tarehe 22 Februari
pamoja na familia ya Prof. Ndulu na jamaa kutoka nchi mbalimbali duniani kuadhimisha dira
yake ya kipekee ya kiuchumi wa Afrika.
“Leo ni mwaka mmoja tangu tumpoteze shujaa wetu. Msomi mashuhuri, mchumi mahiri wa
maendeleo, mwanabenki mwenye maono, mchambuzi wa masuala ya kifedha, mtu mashuhuri,
na mtu wa vitendo. Huyu ndiye Profesa Benno Joseph Ndulu.”
Ndivyo alivyosema Prof Florens Luoga aliyemrithi Prof. Ndulu kuwa Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania.
Hafla hii iliandaliwa na FINSYS, wataalamu wa ushauri wa maendeleo ya sekta ya kifedha, na
kuongozwa na Prof. Njuguna Ndung’u, Mkurugenzi Mtendaji wa African Economic Research
Consortium. Profesa Ndulu alikumbukwa sana na wazungumzaji mashuhuri wa Kiafrika akiwemo
Prof. Luoga, mwanauchumi wa Uganda Dk Louis Kasekende na Gavana wa Benki ya Hifadhi ya
Afrika Kusini Lesetja Kganyago. Prof. Ndung’u alitoa maoni yake:
"Inapendeza kuona jumuiya mashuhuri ikiungana pamoja kumkumbuka rafiki yetu mkubwa, na
kuchunguza jinsi ya kuendeleza maono yake."
Aidha, tukio hilo halikuwa ukumbusho tu. Wazungumzaji waliangazia jinsi ya kutimiza maono ya
Prof. Ndulu, ikiwa ni pamoja na African Continental Free Trade Agreement (AfCFTA), sana sana
katika kuendeleza miundombinu ya malipo ya kikanda ya gharama nafuu na ya haraka – Shauku
ya Profesa Ndulu.
Dk Kasekende alieleza umuhimu wa kuimarisha malipo ya Afrika:
"Moja ya michango ya kipekee ya Profesa Ndulu ilikuwa kutambua umuhimu wa kuchochea
ukuaji kupitia biashara ya kikanda na ndani ya bara. Biashara ya ndani ya Afrika inawakilisha
16.6% tu ya biashara zote za kuvuka mpaka za Afrika; kuongeza hii itakuwa na faida kubwa za
kiuchumi kwa Afrika. Aliona maendeleo ya malipo ya mipakani kama sababu moja muhimu
katika kuunga mkono dira hii, na akaanzisha maendeleo ya muda mrefu ya miundombinu ya
malipo ya Tanzania na kikanda.”
1
Kama Gavana Kganyago alivyoona,
“Bara letu ni miongoni mwa mabara yenye malipo ghali zaidi duniani. ...Mifumo mipya ya
malipo ya kuvuka mipaka itahitaji uratibu wa kimataifa na usaidizi wa kisiasa na [hii] itategemea
sana sekta ya umma na ya kibinafsi kushirikiana. Hatuthubutu kushindwa katika jitihada hii.”
Katika mtazamo wa kimataifa, maono haya ya Kiafrika yaliungwa mkono kwa nguvu,
ikithibitishwa na michango kutoka kwa Prof. Klaas Knot, Mwenyekiti wa Bodi ya Financial
Stability Board (FSB), ambaye alielezea Mwongozo wa FSB wa kuimarisha malipo ya mipakani na
kazi inayoendelea ya kutambua fursa maalum za uboreshaji.
Kulingana na Prof. Knot:
"Mafanikio ya yatategemea ushirikiano wa umma na sekta binafsi, uratibu wa mifumo ya
udhibiti na usimamizi, uelewa wa miundombinu ya mifumo ya malipo iliyopo na upunguzaji wa
gharama na kuboresha usindikaji wa data."
Huku FSB imeweka dhamira yake katika kuleta mabadiliko ya kweli kwa watu binafsi, biashara na
sekta za kifedha duniani kote. Bara la Afrika linanafasi ya kufanikiwa zaidi kutokana na utimizaji
wa malengo haya ya kimataifa kwani bado kuna changamoto za gharama, urahisi na uharaka wa
upatikanaji wa huduma za kifedha.
Gerard Hartsink, Mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Malipo la Ulaya, alichangia uzoefu wa
Ulaya katika kuunda Single Euro Payments Area (SEPA) (mfumo wa malipo katika nchi za Ulaya),
akisisitiza uongozi thabiti kutoka benki kuu na ushiriki wa sekta kibinafsi. Wazungumzaji wote
wawili walisisitiza uwiano wa maendeleo ya kimataifa na mtazamo wa Kiafrika wa Prof. Ndulu.
Prof. Luoga alieleza mantiki ya msingi ya malipo ya gharama nafuu, haraka, jumuishi na ya
uwazi:
"Profesa Ndulu aliamini katika kuwawezesha watu maskini, hasa kwa kupata huduma za kifedha
kama njia ya kupambana na umaskini. Katika kufanikisha hili, ushirikishwaji wa kifedha ulitawala
Ugavana wake ambao uliiwezesha Tanzania kutoka katika hali duni na kufikia mojawapo ya nchi
zinazoongoza barani Afrika.”
Katika kutimiza ndoto ya Profesa Ndulu, Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
iliitisha kongamano katika utekelezaji wa majukumu yake chini ya Kifungu cha 26 cha Mkataba
wa Eneo Huria la Biashara linalozitaka wanachama wa EAC, COMESA, na SADC kushirikiana na
kuimarisha uratibu katika masuala yanayohusu mifumo ya malipo. Kongamano lilijadili chaguzi
za kuimarisha mipango ya malipo ya rejareja ili kuboresha biashara ya mipakani. Uongozi wa
Benki Kuu za nchi mbalimbali katika EAC, SADC, COMESA unapaswa ushughulikie haraka
mapendekezo yanayotokana na kongamano hilo.
No comments :
Post a Comment