Thursday, February 17, 2022

RAIS MWINYI ATENGUA UTEUZI WA KAMISHNA MKUU WA BODI YA MAPATO ZANZIBAR (ZRB)

 

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametengua uteuzi wa Kamishna Mkuu wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Salum Yussuf Ali ili kupisha uchunguzi wa kina wa upotevu wa  fedha za makusanyo ya mapato zilizopotea.


Rais Dk. Mwinyi amefikia maamuzi hayo leo wakati akiwa katika Ofisi za Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Mazizini Zanzibar ambapo alipata fursa ya kuzungumza na uongozi wa Bodi ya Mapato, Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mapato  pamoja na uongozi wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA), mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mamlaka hiyo.

Pia, Rais Dk. Mwinyi ameiagiza Bodi ya Mamlaka hiyo kumsimamisha kazi na kupisha ukaguzi wa kina wa maelekezo ya  Mkurugenzi wa Usajili, Ukaguzi na Upelelezi wa Walipa Kodi, Hashim Kombo Haji kupisha ukaguzi wa kina wa maelekezo yake ya kuondoa taarifa za ukaguzi ambazo hatimae hazikupelekwa kwenye Bodi.

Sambamba na hayo, aliiagiza Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na watendaji waliofanya uchunguzi pamoja na kushirikiana na vikosi vyote vya ulinzi na usalama watakavyovihitaji ili kujua fedha hizo zimeendea wapi.

No comments :

Post a Comment