Sunday, February 20, 2022

Rais Mwinyi aipa CRDB jukumu la kusimamia ajenda ya uchumi wa buluu

buluu pic1

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi (katikati) pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali Zanzibar na Benki ya CRDB wakifurahia uzinduzi wa ushirikiano baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Benki ya CRDB kupitia Mikopo ya Wajasiriamali ya Inuka na Uchumi wa Buluu.

By Maliki Muunguja

Zanzibar. Rais wa Zanzibar, Dk Hus­sein Ali Mwinyi ameika­bidhi Benki ya CRDB Plc jukumu la kutoa elimu ya fedha na kutoa mikopo isiyo na riba kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wado­go walioko visiwani ikiwa ni sehemu ya kutambua maendeleo ya ajenda ya uchumi wa buluu.

Akizungumza visiwani humo Jumamosi iliyopita wakati akizindua programu ya “Inuka na Uchumi wa Buluu” inayotekelezwa kwa ushirikiano na benki hiyo, Rais Mwinyi alisema seri­kali yake iliweka kiasi cha Sh81.5 bilioni kwa lengo la kuvinufaisha vikundi vya wajasiriamali na wafanya­biashara wadogo.

“Tumeipa Benki ya CRDB jukumu la kutoa elimu ya fedha na mikopo bila riba kwa vikundi vya wajasiria­mali na wafanyabiashara wadogo kwa sababu ya rekodi nzuri ufuatiliaji ya benki,” Dk Mwinyi alisema.

buluu pic2

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi akitoa hutuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi wa ushirikiano baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Benki ya CRDB kupitia Mikopo ya Wajasiriamali ya Inuka na Uchumi wa Buluu.

Aliongeza kuwa benki hiyo iliyoko jijini Dar es Salaam inatarajiwa kutenga kiasi sawa cha fedha kwa ajili ya kuwapa wafanyabiasha­ra kuwekeza katika sekta mbalimbali zikiwemo za kuuza chakula, bodaboda, saluni za kike, wavuvi, wakulima wa mwani na wafanyabiashara.

Alisema Serikali yake tayari imeanza kuwapatia wafanyabiashara wadogo vitambulisho ili wasin­yanyaswe wanapofanya biashara zao akisema serikali hiyo pia inajenga masoko ya kimataifa ili kumpa eneo la biashara kila mtu ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara wadogo wadogo.

“Ushauri wangu kwenu ni kwamba naomba muon­doke katika eneo ambalo ujenzi wa masoko hayo unafanyika na niwahakiki­shie kwamba mara baada ya miradi hiyo kukamilika, mtapewa kipaum­bele wakati wa kutenga maduka,” alisisitiza huku akiwaonya wasaidizi wake kuwa yeyote atakayejaribu kukwamisha juhudi za ajen­da ya uchumi wa buluu yu mbioni kufutwa kazi.bulue 3 pic

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi akipokea maelezo kwa mmoja wa wajasiriamali waliohidhuria hafla ya uzinduzi wa ushirikiano baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Benki ya CRDB kupitia Mikopo ya Wajasiriamali ya Inuka na Uchumi wa Buluu. Kushoto kwake ni Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Omari Said Shaaban, na kulia kwake ni, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.

Mpango huu utakapo­kamilika, utazalisha ajira rasmi zaidi ya 300,00 huku takribani wamiliki wa biashara 700,000 wakinu­faika moja kwa moja na mikopo lakini pia mafunzo ya ujuzi wa masuala ya fedha.

Akitoa maelezo kwa Dk Mwinyi kuhusu shughuli za benki hiyo visiwani humo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema makubaliano hayo na Serikali ya Zanzibar ni fursa mpya kwa wafanya­biashara kujinufaisha na kukua zaidi kufikia kuwa kampuni kubwa baadaye.

“Tangu mwaka jana tayari tumeshatoa mikopo ya zaidi ya Sh150 bilioni kwa wafanyabiashara wa sekta mbalimbali ikiwemo utalii, uvuvi, kilimo na biashara,” Nsekela alisema huku aki­fafanua chini ya mpango wa ‘Inuka na Uchumi wa Buluu’, wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo wadogo tayari wameshaan­za kupata mafunzo ya ujuzi wa masuala ya fedha.

Alisema biashara zisizo rasmi ambazo huchan­gia angalau asilimia moja ya pato la taifa la visiwa hivyo, ni sehemu muhimu ya wateja wanaohudumiwa na benki kubwa nchini kwa upande wa amana na tha­mani halisi ya mali.

“Kupitia Mpango wa Inu­ka, benki imetenga Sh60 bilioni kukopesha wafanya­biashara na ikihitajika zaidi itatolewa bila riba kama ilivyokubaliwa na serikali,” aliongeza. Kabla ya kuzin­dua mpango wa uchumi wa buluu, benki ilikuwa imetoa mikopo yenye thamani ya Sh94 milioni kwa vikundi vitano.bulue pic4

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akitoa hutuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi wa ushirikiano baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Benki ya CRDB kupitia Mikopo ya Wajasiriamali ya Inuka na Uchumi wa Buluu.

“Pia tumeidhinisha mko­po wa Sh2 bilioni kwa kikundi cha wavuvi kununua boti za

kisasa za uvuvi na nguo maalumu za uvuvi,” Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB alibainisha. Katika mwaka uliopita, CRDB pia iliwekeza mabilioni ya shi­lingi katika miradi ya jamii kama sehemu ya uwajibi­kaji wake wa kijamii na shughuli nyingine nyingi za kusaidia kufanyika kwa tamasha la utamaduni la ‘Kizimkazi’ ambalo mwaka jana lilipambwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika haf­la hiyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dk Juma Malik Akil alisema Sh81.5 bilioni pamoja na mambo mengine, zitatoa mikopo kwa wavuvi ili kupata boti 577 za uvuvi, meli nyingine ndogo 500 ili kuwezeshawakulima wa mwani ambao wengi wao ni wanawake kutembea kwa urahisi kwenye masham­ba yao yaliyoko baharini na ujenzi wa kiwanda cha kusindika mwani katika visiwa vya Pemba.

“Mradi huu unatarajiwa kuwanufaisha wajasiria­mali zaidi ya 700,000 moja kwa moja wakati wa hat­ua ya awali kwa sababu ufadhili huo unaendelea na utadumu miaka kadhaa ijayo,” Dk Akil alisema huku akiwataka walengwa hasa wanaume kuacha matumizi mabaya ya fedha kwa kuoa wake wa pili.

Akitoa ushuhuda wa programu hiyo, mmoja wa wanufaika, Hamis Hamad Hamis kutoka Visiwani Pemba alisema kikundi chake cha wanachama 20 kinachojishughulisha na ufugaji kimeweza kupata mkopo wa Sh25 milioni kuanzisha kiwanda cha kusindika maziwa.

“Kutokana na uongezaji wa thamani, maziwa yetu ambayo yalikosa soko la uhakika hapo awali na hivyo kuharibi­ka, yameongezeka bei ambapo lita sasa inauzwa zaidi ya Sh3,000 kutoka Sh1,500,” Hamis alisema huku akibainisha kuwa kikundi kilichokuwa kinazalisha lita 100 kwa siku pia kimeonge­za uzalishaji hadi lita 500.

No comments :

Post a Comment