Sunday, February 20, 2022

Majaliwa aongeza siku saba uchunguzi mauaji Mtwara, Kilindi

majaliwa pic

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

By Mwandishi Wetu

Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongeza siku saba kwa kamati maalum iliyopewa jukumu la

kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, Tanga.

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili Februari 20, 2022 na imesema kuwa Kamati hiyo iliyoanza kazi Februari 4, 2022 ilipaswa kukamilisha ripoti yake ndani ya siku 14, zilizoishia Februari 17, 2022.

SOMA:Majaliwa aunda kamati kuwachunguza Polisi mauaji Mtwara

Taarifa hiyo imesema kuwa kutokana na ukubwa wa kazi na mahitaji ya kujiridhisha na baadhi ya masuala, kamati imeomba kuongezewa siku saba kuanzia Februari 17 hadi Februari 23, 2022.

Kamati hiyo iliundwa na Waziri Mkuu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la  Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa Februari 4, 2022 mjini Magu, Mwanza akiwa njiani kuelekea Musoma, Mara kwenye maadhimisho ya miaka 45 ya CCM.

Waziri Mkuu huyo ametoa wito kwa mamlaka husika kuendelea kutoa ushirikiano kwa kamati ili iweze kuikamilisha kazi hiyo kwa wakati na ufanisi.

No comments :

Post a Comment