Wednesday, February 23, 2022

JK ARIDHISHWA NA DHAMIRA YA SERIKALI KWENYE SEKTA YA MADINI

RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Dkt.Jakaya Kikwete amesema kuwa, kauli mbiu ya mwaka huu katika Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Uwekezaji Katika Sekta ya Madini inadhirisha nia ya Serikali ya kuifanya Sekta ya Madini iweze kutoa mchango unaostahili kwa Taifa.

Kauli mbiu hiyo ya "Mazingira Wezeshi kwa Maendeleo ya Sekta ya Madini" ilikuwa inaongoza mkutano huo wa siku mbili ambao ulifanyika kati ya Februari 22 hadi 23, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere kilichopo jijini Dar es Salaam.


Dkt. Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla maalum ya Usiku wa Madini uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam amesema kuwa, kauli mbiu hiyo inaonesha dhamira ya kuiwezesha Sekta ya Madini itoe mchango stahiki kwa maendeleo ya Taifa letu tofauti na miaka ya nyuma.

"Pia inahakisi azma ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama yetu mpendwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kusimamia mabadiliko ya kisera, mabadiliko ya kiutawala ili kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha kuvutia uwekezaji katika Sekta ya Madini barani Afrika.
"Ninafarijika kuona dhamira hiyo ipo pia katika shughuli nyinginezo za kiuchumi na kijamii hapa nchini, lakini ili azma hii itimie, nchi yetu haina budi kuwa na sera zinazotabirika. Hakuna mwekezaji anayewekeza mahali ambapo alipoingia mmepa mashariti haya, anapoendelea katikati mnamwambia mmegairi.
"Sasa huyu mwekezaji anapofanya plans (mipango) yake ya investment (uwekezaji) anaijenga kwenye misingi ya masharti mnayompa sasa.Hata anapokwenda kuchukua mkopo benki anachukua kwa misingi ya masharti anayopewa. Endelea kumsikiliza Mheshimiwa Dkt.Kikwete hapa nchini.
  Source:Dira Makini Blog.
*********
Matukio katika picha wakati wa hafla hiyo




















No comments :

Post a Comment