Monday, February 28, 2022

Bolt Na Mpango Wa Kuwawezesha Madereva Kiuchumi

 Mkiwa ni dereva wa Bolt nchini Tanzania ambaye kwa miaka miwili sasa, amekuwa akitumia gesi iliyochakatwa kwa mfumo asilia ‘Compressed Natural Gases’ (CNG) badala ya kutumia petrol katika gari lake.


Anasema kuwa tangu ameanza kutumia gesi hiyo asili ameona tofauti kubwa ikiwamo kuongezeka kwa kipato chake tofauti na hapo awali..

“Tangu nianze kutumia gesi ya CNG kipato changu kama dereva kimeongezeka kwa kupitia Bolt App yameongezeka kwa asilimia 85 kwani gharama kubwa za awali zimepungua sana.

“Kwa sasa, natumia Tshs. 15,000 kujaza gesi, lakini hapo awali ningetumia Tshs. 30,000 hadi 35,000 ili kujaza petrol ambayo haikai muda mrefu kama .

Ningependa kuishauri jamii kubadilika na kutumia gesi ya CNG,”alisema Mkiwa

Bolt mtandao unaoongoza kwa usafirishaji wa abiria barani Afrika , huko mbioni kuhakikisha kuwa huduma zake zinapatikana kila kona kwa huduma rafiki ili kuwasaidia walio wengi.

Katika kufikia azma hiyo, kampuni ya Bolt imeanza kampeni maalumu ya kuwahimiza madereva nchini Tanzania kutumia gesi Asilia iliyochakatwa kwa mfumo wa CNG, ambayo inatajwa kupunguza gharama pia kulinda mazingira.

Pamoja na mipango hiyo ya Bolt ya kutaka kukabiliana na soko la ushindani na kujikuza zaidi kibiashara kwa kutumia vyombo vya kisasa,,kampuni hiyo pia inahamasisha madereva wenye mapenzi mema na mazingira kutumia bidhaa ambazo ni rafiki wa mazingira, na ambazo zitawapunguzia gharama, lakini pia kupunguza kaboni ambayo ni adui mkubwa wa mazingira kwa kiasi kikubwa.

Meneja wa Bolt nchini Remmy Eseka alisema lengo kuu la matumizi ya gesi asilia ya CMG, ni kutoa mwongozo katika kulinda mazingira ili kuwa na miji bora huku wakiwawezesha madereva kuongeza kipato kwa kutumia gesi yenye bei nafuu.

Alisema Bolt inaendelea kuwekeza kwa dhati katika katika sekta ya usafiri kote barani Afrika na inataka kupanua njia mbadala endelevu za kuwapa huduma bora wateja wake, huduma hizo zitajumuisha kitengo cha wapanda farasi wa Bolt na baiskeli za kielektroniki.

Katika hatua nyingine dereva mwingine wa Bolt, Elias Mruma anasema kuwa, Gesi ya CNG ni rafiki wa mazingira ndani yake ikiwa na kiwango cha mchanganyiko wa asilimia moja ya methanol katika ujazo wake.

Anasema CNG ni salama kuliko petroli na dizeli, na inapunguza utoaji wa kaboni kwa 90 hadi 97%. CNG hutumiwa katika magari ya jadi ya petroli/injini ambazo zimerekebishwa au zimetengenezwa mahususi kwa matumizi ya CNG.

“Kupitia matumizi ya CNG, nimeweza kupunguza gharama na kuwapeleka watoto wangu wawili katika shule za kimataifa.

“Kiwango cha Juu kabisa, ninaweza kutumia hadi Tshs 17,500 kujaza gari na gesi, na kuniwezesha kupata angalau Tshs 70,000 kwa siku nikitumia jukwaa la Bolt. Kwa hiyo, matumizi ya gesi asilia yanasaidia kupunguza gharama za mtu hadi asilimia 75.’ Alisema Mruma, dereva huyo wa wa Bolt.


No comments :

Post a Comment