Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa siku tatu ,kujadili njia mbadala ya kupata vyanzo vya Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri,kulia kwake ni John Cheyo Mkurugenzi wa Sera mipango Ofisi ya Rais Tamisemi
John Cheyo Mkurugenzi wa sera mipango Ofisi ya Rais Tamisemi,anasema fursa hii ya hatifungani kwa manispaa itainaweza kuwa chachu ya maendeleo Peter Malika mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mfuko wa mitaji wa maendeleo ,akitilia mkazo jambo
Wajumbe wa Mkutano wakiwa tayari kujadili njia mbadala ya kupata fedha kwaajili ya Mpango wa miradi ya mendeeleo katika halmashauri.
Mkutano wa siku tatuuliandaliwa na Umoja wa Mataifa Shirika la Umoja wa Mataifa la mfuko wa Mitaji wa Maendeleo (USDF) Serikali pamoja na wadau wengine ikiendelea katika Hotel ya 4Point iliyopo Jijini Arusha
Na.Vero Ignatus Arusha
Shirika la Umoja wa Mataifa la mfuko wa Mitaji wa Maendeleo (UNCDF) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania , wanashirikiana katika kutoa mafunzo ya hati fungani,ikiwa ni njia mbadala kwaajili ya halmashauri na taasisi nyingine za Umma, ili kupata fedha za miradi ya maendeleo
John Cheyo ni Mkurugenzi wa Sera Mipango Ofisi ya Rais Tamisemi ,amesema fursa hiyo inaweza kuwa chachu ya maendeleo, katika kuendeleza halmashauri, kwani ndiyo njia mbadala katika suala zima la maendeleo ,kwa kutoa huduma kwa wananchi
“Ukiangalia bajeti ya serikali kwa mwaka huu tunaoendelea nao kwenye mpango wa maendeleo ni zaidi ya trillion 12,ambapo kila halmashauri ikiwa na mradi wa kuombea fedha, haitowezekana kila mmoja kupata fedha ,hivyo badala yake jambo la hatifungani ndio njia mbadala ya kuzisaidia halmashauri katika suala zima la maendeleo’’
Cheyo alisema kuwa wameona kwamba Jambo hilo litasaidia sana kwenye halmashauri ambazo miradi yake inaweza kuendeleza mapato na kuendesha gharama ya ukopaji,kwa maana nyingine halmashauri hazitakimbilia Serikali kuu kuchukua fedha zilizopo,badala yake watapata fedha kutoka kwenye vyanzo vingine.
Aidha alisisitiza kuwa Halmashauri huwa zinaomba fedha, kwaajili ya miradi ya maendeleo ya kutoa huduma kwa wananchi,hivyo sheria inawataka kuwa na mapato yanajitosheleza, na siyo kukimbilia serikali kuu,ndivyo namna hatifungani inaweza kuwa chachu ya maendeleo
Akifungua mkutano huo wa siku tatu Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela alisema kuwa Suala hilo ni geni ,hivyo inahitajika jitihada ya ziada,kufafanuliwa kwa kina ,Ili kila mmoja apate uelewa wa kutosha, ili watakapoingia kwenye utekelezaji,usijeleta ukakasi
Mongela alisema Jambo Hilo jema, na linaonekana kuleta ufanisi wa tija, hivyo aliwataka wawezeshaji kuhakikisha kuwa wanatoa Elimu kwa kina, ili kila mmoja aelewe,na liweze kuleta mafanikio katika halmashauri, na kuitumikia Jamii katika Mpango wa Maendeleo
Kamishna Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Charles Mwamwaja ,alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na UNCDF pamoja na wadau wengine ,wamekuja pamoja ,kuhakikisha Suala la hatifungani linaeleweka kwa upana zaidi ,na kwenda kutende kazi kwani lipo katika mwongozo wa serikali
Dkt.Mwamwaja alisema kuwa tayari kama Taifa upo katika Mpango mkuu wa Maendeleo ,kwenye sekta ya fedha, ambapo ni wa miaka 10,na moja ya malengo tajwa itawasaidia katika kuhakikisha upatikanaji wa fedha zitakazo wasaidia kugharamiwa Mpango wa Maendeleo.
Alisema kuwa Mpango wa Sasa wa Maendeleo wa miaka 5,katika utekelezaji ipo namna ambayo Mpango huo utagharamiwa,na moja ya Meneo ambayo yanatakiwa kuchangia Mpango huo ,ni kutumia vyanzo mbadala wa miradi hiyo ya Maendeleo
Ipo miradi ambayo nisema ukweli haistahili kugharamiwa kwa kupitia Kodi ya Serikali, kwasababu mapato hayo hayatoshelezi na hayo kidogo bado yana mambo mengi yanayohitaji kutekeleza kwayo.alisema Dkt.Mwamwaja
Peter Malika ni mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mfuko wa Mitaji wa Maendeleo,amesema kuwa,wamekutana jijini Arusha kwaajili ya kuandaa njia ya haraka ,kuwezesha miradi ya maendeleo iweze kupata fedha kwa kwa njia mbadala
Alisema wamekuja na njia nyingine ambazo serikali ilikuwa haizitumii,hivyo sasa hivi kuna sera ambayo imepitisha pamoja na sheria ya kuruhusu kutumia njia mbadala,ya kupata pesa kwaajili ya miradi ya maendeleo kwa wananchi ,kwa kukopa kwenye masoko ya mitaji ya ndani
“Kusema ukweli ni suala jipya ndiyo maana tupo hapa kwa siku tatu na watu tofauti ambao tunajadili wote tuelewe kwa pamoja,tupo serikali ,Taasisi za Umma na sisi Shirika la Umoja wa Mataifa pamoja na watu wengine pia ili wote tuelewekwa pamoja ,kitu kinachotakiwa kufanyika namna ya kupata hizo fedha vilevile zitumike kama zilivyokusudiwa,Alisema Malika
Nicodemus Mkama ni Afisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Msoko ya Mitaji na dhamana (CMSA),anasema jambo la kwanza la msingi lazima kuwe na bankable project,ilete ushawishi kwa wawekezaji ili waweze kuwekeza,kwani maandiko yatapitiwa kwa makini kwasababu wataweka fedha zao, na watahitaji kujua Kama kile watakachokiwekeza kitawalipa ama la Katika Suala hilo Mkama a,ambao baadhi yao ni Benki.
No comments :
Post a Comment