KAMPUNI ya mafuta ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited ambayo awali ilijulikana kama Total Tanzania Limited imehitimisha wiki ya huduma kwa wateja ya TotalEnergies kwa mwaka 2021, kuwaahidi Watanzania kampuni hiyo itashirikiana kikamilifu na Watanzania, kuijenga Tanzania bora zaidi na kuahidi kufanya makubwa Tanzania.
Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Jean-Francois Schoepp aliyasema hayo katika hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa wateja, iliyohitimishwa katika Ofisi za TotalEnergies, Masaki jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Huku akinukuu kauli ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Jean-Francois Schoepp amesema Nyerere alisema "Maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu, na sio maendeleo ya vitu, ili kupata maendeleo ya kweli ni lazima wananchi washirikishwe."
Hivyo ameahidi kwamba TotalEnergies Marketing Tanzania Limited itafanya makubwa Tanzania, kwa kuwashirikisha Watanzania, wakiwemo wateja wa TotalEnergies, katika mipango mkakati wa kampuni, na kuwataka wafanyakazi kuendelea kujituma kwa bidii hata ikibidi kufanya kazi ya ziada ili kukidhi mahitaji ya jamii kikamilifu.
Katika wiki hii, wafanyakazi wa TotalEnergies Marketing Tanzania Limited wakiongozwa na mkurugenzi mkuu, Bw. Jean-Francois Schoepp walitoa huduma kwa wateja waliotembelea vituo mbalimbali vya TotalEnergies zaidi ya 100, vilivyotapakaa nchini kote Tanzania na kupata fursa ya kusikiliza maoni ya wateja, kuboresha mahusiano na wateja wao kwa nia ya kuziba mapengo yoyote yaliwepo na kuweza kujenga TotalEnergies Marketing Tanzania Limited kwa pamoja na wateja wao.
Zaidi ya hayo, wateja walipata nafasi kutoa maoni yao kuhusu huduma za Total Energies na kucheza gurudumu la bahati katika vituo hivyo na walijishindia zawadi kadhaa zikiwemo fulana, chupa za maji, kofia, bidhaa za kutunza magari kama vile baridi na air freshener, na vocha ya zawadi zilizowawezesha kununua bidhaa zozote katika maduka la Cafe Bonjour yaliyopo kwenye kila kituo.
Akiyataja miongoni mwa makubwa ambayo TotalEnergies inapanga kuyafanya Tanzania, Mkurugenzi Jean-Francois Schoepp, amesema kufuatia changamoto za upatikanaji umeme wa uhakika, TotalEnergies imejipanga kusaidia Tanzania kufua umeme, na imejipanga kufikia mwaka 2050, itakuwa inatumia nishati jadilifu (renewable energy) ambazo ni rafiki wa mazingira zikiwemo umemejua, umeme upepo na umeme jotoardhi.
Mpaka kwa nchini Tanzania, kampuni ya TotalEnergies ndio inayoongoza kwa mtandao mkubwa wa vituo vya usambazaji mafuta ambapo inavyo vituo zaidi ya 100 nchini Tanzania, ambapo baadhi ya vituo vinamilikuwa na kampuni na kuendeshwa na kampuni kwa mtindo wa COCO, (Company Owned, Company Operated) vingine vinamilikiwa na kampuni lakini vinaendeshwa na Watanzania kwa mtindo wa CODO, (Company Owned, Dealer Operated) lakini vituo vingine ni TotalEnergies, imewajengea uwezo Watanzania, hivyo vinamilikiwa na kuendeshwa na Watanzania kwa mtindo wa DODO, (Dealer Owned, Dealer Operated).
TotalEnergies ndio kampuni inayoongoza kwa uwekezaji wenye thamani kubwa Tanzania, kuliko uwekezaji mwingine wowote wowote Tangu Tanzania imepata uhuru, Mradi wake wa Bomba la mafuta ghafi, kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga, nchini Tanzania, ndio mradi mkubwa wa uwekezaji nchi Tanzania kuliko mradi mwingine wowote.
Na hiki kiwanda cha vilanishi cha TotalEnergies, Lubricant and Oil Blending Plant (LOBP) ndicho kiwanda kikubwa kuliko vyote cha vilainisha kwa nchi za Afrika Mashariki, kati na Kusini, kikitumia tekinojia ya kisasa na kutoa sio tuu ajira kwa Watanzania, bali Watanzania wamejengewa uwezo wa kitaalamu na ndio wanaoendesha kiwanda.
No comments :
Post a Comment