Thursday, December 2, 2021

'Afrika Court' Yatoa Hukumu Dhidi Ya Mashauri 14 Yaliyowalishwa

Meza kuu ya majaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu wakitoa hukumu katika kesi zilizowasilishwa katika mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu le Desemba 2, 2021 jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kituo cha msaada wa Sheria kwa wanawake (WLAC), Thedosia Muhulo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuhudhuria hukumu zilizotolewa na mahakama ya Afrika ya haki za bianadamu na watu katika kituo cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuhudhuria hukumu zilizotolewa na mahakama ya Afrika ya haki za bianadamu na watu katika kituo cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Desemba 2,2021.
Kutoka kulia ni Rais wa Mahakama ya Haki za binadamu na watu, Jaji Imani Aboud akizungumza wakati wa kutoa hukumu za mashauri yaliyopelekwa katika mahakama ya Afrika ya haki za bianadamu na watu katika kituo cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Desemba 2,2021.
Jaji Modibo Sacko akizungumza wakati wa kutoa hukumu za mashauri yaliyopelekwa katika mahakama ya Afrika ya haki za bianadamu na watu katika kituo cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Desemba 2,2021.
Jaji Chafika Bensaoula akizungumza wakati wa kutoa hukumu za mashauri yaliyopelekwa katika mahakama ya Afrika ya haki za bianadamu na watu katika kituo cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Desemba 2,2021.






Baadhi ya wadau wa mahakama wakisikiliza mwenendo wa hukumu zilizokuwa zikitolewa leo katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu jijini Dar es Salaam leo Desemba 2,2021. 

Na Mwandishi wetu, Globu ya Jamii
MAHAKAMA ya Afrika na Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR), imetoa hukumu ya mashauri 14 kutoka nchi tano wanachama wa Umoja wa Afrika ambapo katika mashauri hayo nane yanatoka Tanzania.

Hukumu hizo zimesomwa na Rais wa Mahakama hiyo Jaji Imani Aboud kwa kushirikiana na Jopo la majaji 11 kutoka nchi hizo wanachama.

Akisoma hukumu hizo Jaji Amani amesema wamepitia mashauri yote yaliyowasilishwa na nchi zote wanachama huku mashauri mashauri yote yaliyofunguliwa kutoka Tanzania yakiwa yanamuhusu mtu mmoja

Nchi zingine zilizowasilisha mashauri hayo na kutolewa hukumu ni Rwanda, Mali, Benini, Malawi na Ivory Coast  ambapo yalisikilizwa kwa muda wa mwezi mmoja kutoka katika kikao cha 63 cha mahakama hiyo.

Kwa mara ya kwanza hukumu hizo zimesomwa jijini Dar es Salaam, ikiwa pia ni mara ya kwanza kwa mahakama hiyo kufanya shughuli zake katika jiji hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusomwa kwa mashauri hayo, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa, amesema kesi zilizotolewa hukumu kutoka Tanzania zilizofunguliwa katika mahakama hiyo ni zinahusu mtu mmoja mmoja.

"Mashauri hayo nane yaliyotolewa maamuzi leo Desemba 2,2021 yanahusu haki za binadamu, mojawapo ikiwa ni kesi ya kunyimwa uraia wa Tanzania kwa mtu aliyedaiwa ni mzaliwa wa nchini Kenya.

"Kesi nyingi zimefunguliwa na Watanzania kwa sababu mahakama ipo Tanzania, ukaribu wa mahakama hii unafungua mianya ya watu wengi zaidi kudai haki zao mahakamani hapo. Pia kuwapo kwa mahakama hapa nchini kumepunguza gharama za ufunguzi wa kesi kwa sababu mahakama hiyo ingekuwa ipo nchi za mbali ingesababisha gharama kuwa kubwa, " amesema Ole Ngurumwa.

Akielezea taratibu za kufungua kesi, Ole Ngurumwa amssema kuwa taratibu za ufunguzi wa kesi katika mahakama hiyo kuwa ni lazima mwenye kesi awasilishe shauri hilo katika Tume ya Haki za Binadamu Afrika ambayo itapeleka shauri hiyo katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu.

Naye, Mkurugenzi wa Kituo cha msaada wa Sheria kwa wanawake (WLAC), Thedosia Muhulo, amesema mfumo huo wa utoaji maamuzi kwa mashauri inaonekana kuzitendea haki kesi ambazo zimewasilishwa, kwani mara nyingi kesi hizo zilikuwa hazisikilizwi vizuri.

No comments :

Post a Comment