MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetwaa Tuzo ya Umahiri katika Uwasilishaji wa Taarifa za mahesabu kwa mwaka 2020.
Akizungumza baada ya kupokea Tuzo hiyo katika hafla ya kufunga mafunzo pamoja na utoaji wa Tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2020 (Best Presented Financial Statements for the Year 2020 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa
na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam Desemba 4, 2021, Mkurugenzi wa Fedha, PSSSF, Bi. Beatrice Musa-Lupi alisema Ushindi huo ni ishara ya kwamba PSSSF inaandaa mahesabu kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kimataifa lakini pia inaashiria uwepo wa weledi wa tasnia husika kwa upande wa watumishi.“Sambamba na hayo niliyoyasema pia inaashiria uwepo wa usimamizi makini wa fedha za wanchama na hii inatupatia heshima kama taasisi.” Alisema Mkurugenzi huyo wa Fedha PSSSF.
Aliwahakikishia Wanachama dhamira ya PSSSF kuhakikisha usalama wa michango yao unazingatiwa kwa kiwango cha juu wakati wote, ikiwa ni pamoja na kuwepo uwazi kwenye usimamizi na utunzaji wa rasilimali za Mfuko.
No comments :
Post a Comment