Saturday, November 13, 2021

KARIBU ASILIMIA 75 YA WANAOTEMBELEA BANDA LA BoT WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KITAIFA DAR ES SALAAM WANAHITAJI KUWEKEZA KWENYE DHAMANA ZA SERIKALI (HATI FUNGANI)

Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki BoT, Bi. Vicky Msina (wakwanza kulia) na Deogratius Mnyamani (Wapili kulia) na Afisa Mkuu Mwandamizi, Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha BoT, Bw. Deogratius Mnyamani wakimsikiliza Bi. Anna Ndimbo ambaye ni mjasiriamali aliyetembelea banda la BoT kwenye Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa Novemba 13, 2021.
Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki BoT, Bi. Vicky Msina akifafanua jambo
Mchambuzi wa Masuala ya Fedha BoT, Bi. Glory Chelunga (kushoto) akitoa elimu kwa mwananchi
Afisa Uhusiano BoT, Bi.Beatrice Ollotu (kushoto), akimsikilzia mwananchi.
Mkaguzi wa Mabenki BoT, Bw.Michael Tumaini (kushoto) akitumia kipeperushi kutoa elimu.
Afisa Mwandamizi wa Benki, Bi. Joyce Njau (kulia), akifafanua jambo kwa mwananchi aliyefika katika banda la BoT.
Afisa Mkuu Mwandamizi, Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha BoT, Bw. Deogratius Mnyamani akimuelimisha mwananchi aliyefika kwenye banda la BoT.

Bi. Zalia Mbeo (kushoto) Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BOT) akitoa elimu kwa wananchi aliotembelea band ala BoT kwenye Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Novemba 13, 2021.

Mchambuzi wa Masuala ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ephraim Madembwe (kushoto), akitoa elimu kwa wananchi hawa waliofika kupata uelewa wa fursa zilizopo kwenye Sekta ya Fedha.

NA MWANDISHI WETU, MNAZI MMOJA, DAR ES SALAAM

ASILIMIA 75 ya Wananchi wanaotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, wanataka kujua utaratibu wa kujiunga na mpango wa kuwekeza

kwenye dhamana za Serikali kwa jina lingine Hati Fungani, Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki BoT, Bi. Vicky Msina amesema.

Dhamana za Serikali (Hati Fungani)ambazo ziko katika makundi mawili za Muda Mfupi (Treasury Bills) na za Muda Mrefu (Treasury Bonds) ni nyenzo zinazotumiwa na serikali kukopa fedha kutoka kwa umma.

Bi. Msina ameyasema hayo leo Novemba 13, 2021 wakati akitoa tathmini yake kuhusu utoaji Elimu ya Huduma za Fedha na maswali gani yamekuwa yakiulizwa na wananchi wanaofika kwenye banda hilo.

“Pamoja na kutoa elimu ya Huduma za Fedha ikiwemo kanuni mpya za Huduma ndogo ya Fedha, Utunzaji mzuri wa noti lakini wananchi wengi takriban asilimia 75 wengi wao wakiwa ni watumishi wanaokaribia kustaafu  wamekuwa wakiuliza namna ya kuwekeza kwenye dhamana za serikali (Hati Fungani) tena zile za muda mrefu (Treasury Bonds).” Alisema Bi. Msina na kuongeza…..Pia wananchi wengi hususan wale walio katika kundi la Huduma ndogo za Fedha kama vile, Vikoba, Saccos na mawakala wamekuwa wakiulizia kuhusu Kanuni Mpya za Huduma ndogo za Fedha ambazo zinalenga kumlinda mtumiaji wa Huduma ndogo za Fedha ili kuleta Usawa na Haki ambazo zinazingatiwa na watoa huduma za fedha wote nchini zikiwemo benki na makampuni ya simu, makampuni ya karadha, watoa huduma ndogo za fedha, na watoa huduma za malipo..

Mmmoja wa wananchi waliofika kwenye banda hilo, Bi.Anna Ndimbo fundi cherehani mkazi wa Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, alisema kilichomleta kwenye banda la BoT, ni kutaka kujua kama BoT wanawatambua watu wanaopita mitaani hususan mtaani anakoishi na kutoa mikopo midogo kwa akina mama ambayo masharti yake ni kurejesha ndani ya siku 30 (mwezi mmoja).

Akifafanua zaidi Bi. Ndimbo alitoa mfano ukikopeshwa shilingi Laki Moja (100,000/=) unatakiwa kurejesha shilingi 4,500 hadi 5,000 kila siku kwa siku 30 ambapo jumla yake ni kati ya shilingi 135,000/= na 150,000/=

“Kule kwetu tunaita mikopo hii KAUSHA DAMU, hapa wameniambia wanaita MIKOPO UMIZA, kwakweli inaumiza sana akina mama,”alisema Bi. Ndipo.

Alisema baada ya kupewa elimu kuhusu huduma za fedha ameambiwa kuwa BoT haiwatambui watu hao na kuwataka wananchi kuwa makini na wasichukue uamuzi wa kukopa hadio watakapojiridhisha uhalali wa hao wanaotoa mikopo.

Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ambayo ilianza Novemba 8, 2021 inatarajiwa kumalizika Jumapili Novemba 14, lengo kuu ni kuwapa fursa wananchi kutoka kada mbalimbali kukutana na taasisi za fedha ili kujua fursa za huduma za fedha zilizopo na hivyo wapate kufaidika nazo.

Kauli mbiu ya Wiki hiyo inayoratibiwa na Wizara ya Fedha ni “Boresha Maisha kupitia Elimu ya Fedha.”

No comments :

Post a Comment