Sunday, November 14, 2021

BOT YAHUSISHWA UPORAJI WA HEKALU

- Kiapo cha wakili wa Benki inayodaiwa kupora hekalu chaitaja Benki Kuu kubariki uporaji huo


-Chakushangaza hakuna upande uliopewa nakala ya kinachoitwa uchunguzi na hukumu ya BOT kama ilivyodaiwa katika kiapo cha wakili 


- Makubwa zaidi yaibuka, Rais Samia aombwa kuingilia kati haki ipatikane


Na.Mwandishi wetu 


Sehemu ya kiapo kilichowasilishwa mahakamani na wakili wa utetezi wa benki ya Equit kilichosainiwa tarehe 21 Septemba 2020 mbele ya wakili Shamimu Kikoti, imezua sintofahamu ya uvurugaji wa ukweli wa mambo baada ya kueleza kuwa Benki kuu ya Tanzania kupitia barua ya mlalamikaji ya tarehe 05 mwezi wa nne 2019 imefanya uchunguzi wa malalamiko ya kughushiwa saini na kubaini kuwa hakuna ukweli wowote na hivyo kuipa mkono wa heri upande wa walalamikiwa ambao ni benki ya Equity 


Sehemu ya kiapo hicho kilichoandikwa kwa lugha ya kiingereza inasomeka "......I state further that the applicants' purpoted allegations in this application where reported to the regulator , Bank of Tanzania (BOT) via 3rd applicant and applicants' lawyer's letters dated 05th April2019. The BOT investigated the complaint and found there was no irregularity hence cleared the first respondent." Inasomeka sehemu ya kiapo hicho ambacho gazeti hili baada ya ufuatiliaji wa sakata hili limefanikiwa kupata  nakala yake


Aidha haijafahamika mara moja ni kwa namna gani wakili huyo alipata nakala ya uamuzi wa benki hiyo na kwanini hajaiambatanisha nakala hiyo ya maamuzi katika kiapo chake wakati upande uliolalamika hadi sasa haujapokea majibu yoyote kutoka BOT na mara zote wamekuwa wakifuatilia bila mafanikio


Utata huo unaongeza sintofahamu ya namna gani suala hilo limekuwa likienda na ni kwa namna gani haki halali itapatikana ikiwa nyaraka nyingi zinazotajwa hazijazifikia pande husika


Uchunguzi wa gazeti hili unaendelea kuonyesha kuwepo kwa mapengo mengi ya ufahamu katika sakata hilo lililopelekea nyumba ya kifahari ya mfanyabiashara Mohamed Iqbal kuuza kwa bei ya kutupwa licha ya jitihada za mfanyabiashara huyo kutumia njia halali za kisheria kupigania mali yake hiyo


"Kwa hali inavyokwenda hapo, hakuna namna ni kumuomba tu mama (Rais Samia) aingilie kati kunusuru udharimu huu wa wazi unaotaka kufanywa na unaoendelea kufanywa dhidi ya watu wenye haki zao". Alisema msiri mmoja


Taarifa zaidi zinasema kuwa baada ya kuvuja taarifa za kuuzwa kinyemela kwa hekalu linalomilikiwa na Mkurugenzi wa kampuni ya ZEDEM INVESTMENT LIMITED anayemiliki makampuni mengine kadhaa Mohamed Ikbal, na Benki ya Equity kununuliwa pia kinyemela na mfanyabiashara mwingine maarufu nchini, mambo makubwa kadhaa yamebainika ,gazeti hili linaweza kukujuza


Miongoni mwa mambo yaliyobainika ni ukimya wa benki kuu ya Tanzania juu ya sakata hilo ambapo taarifa za uhakika zinasema kuwa mfanyabiashara Ikbal ameiandikia taasisi hiyo inayosimamia masuala yote ya fedha na mabenki nchini kuwa mali yake imeuzwa kinyume na utaratibu na kwamba kuna maeneo saini zake zimefojiwa na maofisa wa benki ili kufanikisha uuzwaji huo


Gazeti hili limeona nakala ya barua kutoka kwa mfanyabiashara huyo kwenda Benki kuu akilalamikia jambo hilo na tulipofuatilia katika vyanzo vyetu hatujapata kujua kama benki kuu wamejibu chochote hadi sasa.


Aidha taarifa za uhakika ambazo gazeti hili linazo kuhusiana na jambo hilo ni ukakasi wa majibu ya polisi kuhusiana na malalamiko ya kughushiwa saini za mfanyabiashara huyo na wake zake ambapo badala ya polisi kufanya uchunguzi na kukamilisha, japo malalamiko yalipelekwa na Ikbal, hadi sasa Ikbal bado hajapewa majibu yoyote kuhusiana na uchunguzi aliouomba ufanyike.


Tulipomtafuta mfanyabiashara huyo kujua ukweli kuhusu hili ameilalamikia benki ya Equity kuuza nyumba yake iliyopo kigamboni eneo la maweni kinyume na utaratibu


Akizungumza na gazeti hili mfanyabiashara huyo alisema anaishangaa benki hiyo kuuza mali yake hiyo kinyume cha utaratibu wakati wakijua wazi dhamira ya yeye kuiweka dhamana nyumba hiyo ya kifahari ni kuomba mkopo wa dola laki nne na elfu thamanini ili amalizie jengo lake la biashara lililopo kariakoo jijini Dar es salaam

‘’unajua kampuni yetu ya ZEDEM ilikuwa na mradi wa kujenga maduka uwanja wa mpira temeke (TEFA) na tukaomba mkopo benki hiyo wa zaidi ya dola milioni moja, na tukakubaliana kuulipa, na kweli tuliendelea kuulipa’’. Alisema Ikbal


‘’tukiwa tunaendelea na mradi ulizuka mgogoro baina yetu na TEFA na wapangaji wa maduka tuliyojenga, hivyo tukayumba kurudisha mkopo, tukawajuza benki kila kitu kila hatua hata ikafikia hatua ya kupanga upya mfumo wa ulipaji (Restructuring)’’. Aliongeza Ikbal


Ikbal anasema anashangaa kugeukwa na benki hiyo kwani katika mpango wao wa kurejesha mkopo huo ambao ulikuwa umeshalipwa na kupungua kutoka 1.2 milioni dola za kimarekani hati kufika dola laki 8, alikubaliana na benki hiyo wamkopeshe mkopo mwengine wa dola laki nne na elfu themanini ili amalizie jengo lake la biashara lililopo kariakoo na kwamba katika jengo hilo baada ya kukamilika atapokea kodi kwa kushirikiana pamoja yeye, na benki hadi deni hilo litakapokwisha na kuendelea kulipa deni la mwanzo


‘’tulipofika hapo tulikubaliana kwamba niandae Board Resolution kuomba mkopo mpya wa dola 480,000 na resolution nyingine niombe kubadilisha mfumo wa malipo wa mkopo wa awali, jambo ambalo sisi kwa upande wetu tulilifanya na kukabidhi hati ya nyumba ya kigamboni kama dhamana ya mkopo mpya’’.


Inashangaza kabisa ikawaje mara tu baada ya kukabidhi hati, niliposafiri huku nyuma wenzetu badala ya kutupatia mkopo wao wakatengeneza mkataba bandia na wakashuhudia tumeusaini mbele ya wakili wao na kwamba eti dhamana ile tumeweka kuudhamini mkopo wa awali, kitu ambacho si sahihi kabisa. Dhurma’’. Alisikitika Ikbal


‘’hata kama wangetaka kuongeza mkopo ule wa awali, tayari dhamana tuliyoiweka ya zaidi ya dola milioni moja na nusu ingetosha kujidhamini, lakini haijulikani ni kwanini waliamua kunidhulumu na kughushi saini yangu na ya wake zangu na kuuza mali yangu’. Aliongeza Ikbal


Anasema kuwa alisafiri kwenda india tarehe 28/11/2017 na kurudi nchini tarehe 25/01/2018 iweje aonekane amesaini tarehe 21/12/2017  mbele ya wakili hapa hapa nchini wakati hakuwepo nchini huku wakili wa benki akisema amenishuhudia mbele yake

Akiongeza kuhusu jambo hili Ikbal anasema kuwa alishapeleka malalamiko yake polisi kuhusiana na kughushiwa saini zake na za wake zake na kwamba maelezo yote aliyotoa ni kuhusiana na uchunguzi huo uliopo jeshi la polisi


BENKI WANENA

Gazeti hili lilipomtafuta mmoja wa maafisa wa benki ya Equity kuzungumzia suala hilo alisema yeye hana ufahamu kuhusiana na madai ya mfanyabiashara huo na kusisitiza kuwa haiingii akilini benki iuze nyumba ambayo haijakopewa


‘’hebu tu reason pamoja, hivi wewe hujakopa, benki inawezaje kuuza nyumba yako?, anatakiwa aeleze ukweli namna ilivyokuwa, ilikuwaje kuwaje hadi benki imefikia kuuza na sio kupotosha’’. Alisema bwana Godwin Semunyu


Alipoombwa kutoa ufafanuzi zaidi alisema kama mfanyabiashara huyo ametoa malalamiko hayo kwenye vyombo vya habari, basi milango ipo wazi kwa wanahabari kumwandikia mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo ili atoe taarifa rasmi ya benki kuhusiana na ufafanuzi wote kwenye jambo hilo, huku akisisitiza kuwa haiingii akilini kwa benki kuuza mali ya mtu bila utaratibu


Aidha muda mchache kabla hatujakwenda mtamboni, bwana Godwin Semunyu wa Equity Bank alipiga simu tena chumba cha habari na kusema kuwa kesi iko mahakamani hivyo hawawezi kutoa taarifa zaidi

‘’nimetoka kuongea na mwanasheria hapa, ameniambia kuwa hiyo kesi tayari iko mahakamani hivyo hawezi kutoa comment yoyote zaidi’’


Gazeti hili linaendelea na uchunguzi kuhusiana na sakata hilo kama lilivyoanza kuliripoti


Zaidi soma hapa malalamiko ya Ikbal kuhusiana na

Muhtasari mfupi kuhusu tatizo langu na benki ya Equity. - IKBAL


Niliomba mkopo wa takriban USD 1,000,000/= katika mwaka wa 2013 kwa benki ya hisa kwa ajili ya mradi wangu mmoja (TEFA PROJECT) na benki ya equity ilinipa mkopo.


Baada ya muda kulitokea matatizo katika mradi huo na mradi kukwama kwani wapangaji walinifungulia kesi na kupata zuio kutoka mahakamani, kutokana na kukwama kwa mradi huo nilikuwa na matatizo ya kurejesha mkopo hivyo niliomba. kwa upangaji upya mwaka 2016, ombi langu la kupangiwa upya ratiba ya ulipaji lilikubaliwa hata baada ya kupangiwa sikuweza kuwalipa kulingana na sheria na masharti ingawa nilipunguza mkopo wangu hadi USD 898,663/=. Nilikuwa nikipata mawasiliano  kadhaa kutoka benki kulipa mkopo huo lakini mradi ulikuwa bado umekwama sikuweza kulipa awamu ya mkopo ya kila mwezi hivyo niliiomba benki kunipa mkopo mpya wa mradi mwingine ambao ulikuwa umekamilika kwa asilimia 80 na  20 % tu imesalia na kwamba mkandarasi anahitaji karibu USD 480,000/= kukamilisha jengo na benki ikitoa mkopo huo baada ya kukamilika kwa jengo ningekodisha maduka na ningepokea kiasi kisichopungua USD 30,000/= na ningekuwa kulipa huo katika mkopo wa zamani wa 2013 kila mwezi na mara nitakapomaliza kulipa mkopo wa zamani ningeendelea kwa kumaliza kulipa mkopo mpya.

Niliwafahamisha pia kwamba wanaweza kuthibitisha na kuangalia kwa watu wa karibu na kuhakikishiwa kwamba ninaweza kupokea angalau USD 30,000 kwa mwezi na walithibitisha nami kwamba ni kweli ninaweza kupokea kima cha chini cha USD 30,000 au zaidi. Maafisa wa benki ya Equity na maafisa wangu pia walitembelea tovuti hiyo kimwili.

Baada ya kuomba benki, benki ilikubali ombi langu hili na kunitaka niandike maazimio ya bodi mawili (2) na barua 2 za azimio la bodi moja na barua ilikuwa ya kupanga upya muda wa mkopo wa zamani na azimio lingine la barua na bodi lilikuwa la kuomba mkopo mpya wa USD 480,000/ = ambayo ningeweka mali mpya ambayo iko Magogoni.


Nilikuwa nimetayarisha nyaraka zifuatazo na kuwasilisha kila barua na azimio la bodi benki na walizipokea.


Hapa ndipo hasa mchezo ulipoanzia.


Mwanzoni mwa Januari benki waliniomba hati miliki kwa ajili ya kushughulikia mkopo mpya wa USD 480,000. Niliwapa hati miliki.


Mnamo Aprili, 2018 afisa kutoka benki ya equity alikuja na hati fulani za kutiwa saini na kuniomba nitie sahihi.


Nilimwambia afisa huyo siwezi kusaini kwa sababu nahitaji wakili wangu apitie nyaraka anieleze na nikisharidhika nitasaini huku akinishuhudia na atasaini na kugonga muhuri upande wangu.


Afisa huyo aliniomba nizisaini kwa kuwa afisa wao mmoja ambaye anatakiwa kusaini hati hizo hizo pia alikuwa anasafiri na mara afisa huyo akishazisaini atanirudishia hati hizo ili wakili wangu azipitia na baadaye kuzisaini mara nitakapokuwa nimeridhika lakini cha kushangaza baadaye nilipopitia zile nyaraka nikagundua kuwa mwanasheria wa benki alisaini ambapo wakili wangu alitakiwa kusaini.


Baada ya siku 10 za uandikishaji wa rehani nilipata notisi ya kutolipa mikopo benki na pia ilitangazwa kwenye gazeti nilishangaa sana, baada ya siku chache niliona kwenye gazeti likitangazwa kupigwa mnada wa mali zangu zote mbili zilizohifadhiwa kwa mkopo wa zamani na ambao nilikuwa nimeuhifadhi hivi majuzi kwa mkopo wa pili na mkopo ambao sikuwahi kuupokea kutoka benki.


Walichukua mali ya pili (mali ya Magogoni) kwa kututapeli.


Inawezekanaje kwamba mkopo wa kwanza ambao ulikuwa wa usd 1,250,000/= ungeweza kufidiwa na mali yangu ambayo ilikuwa na thamani ya USD 1,368,810/= na baadaye baada ya kupunguzwa hadi USD 898,663/= mali hiyo hiyo isingetosha wakati iliimarika zaidi lakini badala yake Equity ilichukua mali yangu mpya iliyokuwa na thamani ya USD 1,050,429/= niliyoomba kwa mkopo mpya wa USD 480,000/= na kuiongeza kwenye rehani ya zamani ya mkopo. Na kupiga mnada mali ya Magogoni.


Hapo ndipo nilipofungua kesi nikapata stop orders kwamba benki isipige mnada mali hata baada ya stop order na wakati kesi ikiendelea mahakamani bilo bado aliendelea kutangaza kwenye magazeti ya mali zote mbili.


Wakati kesi tofauti na benki ya equity zikiendelea, mnamo 2020 mmoja wa wakili wangu alipitia hati za kesi vizuri na akaona barua hii ya ofa. Aliniuliza ikiwa nilitia saini barua hii ya ofa kwani alikumbuka katika tarehe hizi sikuwa nchini.


Niliona barua ya ofa na pia nikajaribu kukumbuka kama nilikuwa nimesafiri na pia kuangalia katika hati yangu ya kusafiria na kugundua kuwa sikuwepo nchini kuanzia tarehe 28/11/2017 hadi 25/01/2018 ndipo nilipojua kuwa benki imetuchezea mchezo mchafu na pia kughushi sahihi yangu na wake zangu.


Nimeeleza kwa kina kuhusu ghushi zote zilizofanywa na benki pamoja na wakili wao Oliver Mark. 

No comments :

Post a Comment