Na Humphrey Shao, Michuzi Tv
Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameamua kutinga katika ofisi za Dawasa eneo la Gerezani na kuzungumza na uongozi usiku huu juu ya kupambana na changamoto ya uhaba wa maji katika mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha kuwa mfumo wa ugawaji maji unarejea katika hali yake ya kawaida.
akizungumza na Manejimenti ya DAWAWASA Waziri Aweso amesema watumishi wa Mamlaka sasa wana kila sababu ya kufanya kazi usiku na mchana na kuhakikisha migao ya maji inatolewa kwa uwiano na bila upendeleo hili kupunguza minong'ono iliyopo kwa wana jamii.
kutokana na tatizo hili la upungufu wa maji lililotakana kuungua kwa maji katika mto Ruvu Waziri Aweso Ameitaka DAWASA kutoa bei elekezi kwa watoa huduma binafsi wa maji kupitia magari( bowsers). hili kuondoa sitofahamu iliyojitokeza mjini kwa baadhi ya watu kuanza kuuza maji kwa bei zao wenyewe kwa kukiuka utaratibu uliyowekwa na Dawasa.
Aidha Waziri Aweso amehahidi ushirikiano baina ya Wizara na Dawasa katika kukabiliana na changamoto zilizopo kwa sasa kwa kuhakikisha kuwa watu wote wanapata maji kwa wakati namgao kuwa nauwino sawa kila sehemu.
Waziri wa maji Jumaa Aweso akisisitiza jambo katika kikao chake na Manejimentoi ya Dawasa ju ya mpango sahii wa ugawaji wa maji katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
No comments :
Post a Comment