Tuesday, October 19, 2021

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA MABALOZI WA NCHI ZA KIARABU By Emmanuel Mbatilo - October 19, 2021



Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba akimwelezea jambo Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) nchini Tanzania, Mh. Khalifa Abdulrahman M.A Almarzooqi baada ya kukutana kwa mazungumzo, leo Oktoba 18, 2021 katika ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam. Aliye pamoja nao (kushoto) ni Afisa Uhusiano wa Ubalozi, Bw. Saddam Ahmed Ali. 


wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) nchini Tanzania, Mh. Khalifa Abdulrahman M.A Almarzooqi akimwelezea jambo Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba baada ya kukutana kwa mazungumzo, leo Oktoba 18, 2021 katika ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam. 


ya viongozi walioshiriki kwenye mazungumzo baina ya Waziri wa Nishati, January Makamba na mabalozi wa nchi za Saudi Arabia, Qatar za Falme za Kiarabu (UAE) wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Hemedi Iddi Mgaza, Kamishna wa Petroli na Gesi Bw. Michael Mjinja, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Dkt. James Mataragio na Msaidizi wa Waziri, Wakili Dunford Mpelumbe.

Waziri wa Nishati, Mh. January Makamba akizungumza na Balozi wa Qatar nchini Tanzania Mh. Hussain Ahmad Al Homaid, leo Oktoba 18, 2021 katika ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam. Pamoja nao ni Mkalimani Bw. Fawaz Ibrahim Argof aliyeambatana na Balozi.


Waziri wa Nishati, Mh. January Makamba akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Mh.  Abdulaziz Hamad Alasim, leo Oktoba 18, 2021 katika ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam. Pamoja nao ni Kamishna wa Petroli na Gesi Bw. Michael Mjinja (kulia) na Bi. Sabra Omar (kushoto) aliyeambatana na Balozi.

*******************************

Waziri wa Nishati, Mh. January Yusuf Makamba, leo Oktoba 18, 2021 kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi wa mataifa ya Saudi Arabia, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Algeria nchini Tanzania, kwenye ofisi ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Waziri Makamba, mazungumzo hayo yanalenga kuimarisha uhusiano wa kisekta baina ya Tanzania na nchi hizo, ili kuiongezea tija sekta ya nishati kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.

“Rais wetu Mh. Samia Suluhu Hassan yuko mstari wa mbele katika kuhakikisha sekta ya nishati inaimarika na kulinufaisha taifa kiuchumi, hususani katika kuvutia wawekezaji na kutumia vyema rasilimali za mafuta na gesi asilia,” ameeleza Waziri Makamba.

Mabalozi waliofanya mazungumzo na Mh. Makamba ni pamoja na Balozi Abdulaziz Hamad Alasim (Saudi Arabia), Balozi Hussain Ahmad Al-Homaid (Qatar), Balozi Khalifa Abdulrahman M.A Almarzooqi (UAE), na Balozi Ahmed Djellal (Algeria).

Baadhi ya viongozi waliohudhuria mazungumzo hayo ni pamoja na Kamishna wa Petroli na Gesi Michael Mjinja, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Edward Sokoine na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Dkt. James Mataragio.

No comments :

Post a Comment